Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, June 17, 2010

wahenga wasema mficha uchi....

Binti mrembo alipita mbele ya nyumba yetu, tulikuwa tumekaa na wageni mbalimbali waliotutembelea, na kama kawaida ya binadamu minong'ono na kusengenya kukaanza. Mara wengine wakasema huyo binti pamoja na uzuri wake ana kasoro kubwa ndio maana mpaka leo hajaolewa, wengine wakasema mwenyewe hataki wengine wkasema inatokana na familia yao, wengine wakafikia kusema mvuto wake ni usoni tu, ilimradi kila mmoja akasema yake anayohisi moyoni.
 Bahati nzuri nikapata upenyo wa kwenda kukutana na huyu binti mwenyewe nikaona heri nikate mzizi wa fitina nimuulize yale yasemwayo yana ukweli ndani yake. mmmh, kwanza kukutana naye ilikuwa mbinde, manake sijui ndio huko wanakosema kuringa, dharau...vikwazo kedekede!
'Naona na wewe sasa unataka kunichefua, yanawahusu nini maisha yangu, kwani ni lazima niolewe, kwani nakula kwao ...' akasema kwa hasira, lakini kwa vile ananiheshimu hakuweza kuvuka mipaka.
'Sahamani kwa hilo, ila wahenga walisema `mficha uchi hazai, au sio na sina nia mbaya ila ni kutaka kuelewa tu, huenda katika hilo nikajifunza mengi kutoka kwako, huenda yana heri kwangu na pia huenda nikakupa neno lenye busara' nikajiumauma ili angalau nipunguze hasira zake.
 Katika maongezi yetu niligundua mengi na mojawapo ni msigishano wa mawazo, hasa ya wanaomtaka kuwa na mtizamo hasi na wa kwake. Yeye ana mapendeleo yake na msimamo wake hataki kuuvunja, na imefikia hatua wanaomtaka kutamka kuwa anaringa.
 'Mimi sidanganyiki na wao, siku nikitaka kuolewa nitaolewa, kama hapatatokea wa kunioa basi kwani nakosa nini' akahitimisha usemi wake.
 Alipoondoka mawazo yangu yakavuka mpaka na kuichungulia nchi yangu katika taswira hii, niliiona kama huyu binti mrembo. Nchi yangu ina kila kitu, imejaliwa urembo wa sili, masha-Allah. Maliasili, madini mito , maziwa bahari, na hata kuitwa kusiwa cha amani, lakini kuna walakini. Nasikia katika orodha ya nchi masikini yumo katika nafasi za juu, nikajiuliza hivi kweli tumekosa nini? Kwanini tuwe masikini, ilihali tuna kila sababu ya kuwa matajiri. Ooooh, isije ikawa sie ndio tunaosababisha, matokeo yake tunasingizia hili au lile.
 Kwa mtizamo wangu, kwanza labda tungehakikisha miundo mbinu inaboreshwa kwa hali inayovutia wawekezaji, kwani kila tunalofanya wenyewe tunaishia kugonga ukuta, hatutaki kuwa wakweli kuwa tumeshindwa, basi tuwavutie hawo tunaosema wanaweza, wanaotutaka manake, ili wakija wafike hata kijijini bila shida. Au tunaogopa huko watagundua umasiki wetu uliokisiri.
 Unajua sisi tunahangaika na uso, kuuremba, wakati huku kwingine kunakasoro, uso wa nchi yetu ni Dar-es-salaam, tunasahau kuwa mali asili na utajiri mwingi upo vijijini, huko tungepaboresha kimiundo mbinu kama vile usafiri, umeme nk, ili wawekezaji wajenge viwanda huko, hata sie tusingelijazana hapa Dar!
 Oh, ngoja niishie hapa nisije nikavuka mipaka, lakini hilo ndilo wazo langu la leo
From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Mimi nimekuelewa, lakini jamaa watakuelewa saa hizi. Siunajua tena sasa hivi ni mwendo wa kimuhemuhe, je nitasemaje kwa wananchi, nitawadanganyaje sasa hivi...