Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, June 11, 2010

Bora liende

`Hivi bajeti imeongeza mshahara?' Jamaa mmoja akatuuliza wakati tumetulia kusikiliza bajeti jana jioni. Hakuna aliyegeuka kumsikiliza kwani kila mmoja alikuwa akisikilza ili ajue nini kimeongelewa, na kila mmoja alikuwa akisubiri sehemu anayoipendela. Wengine wanataka kusiliza mishara, wengine kodi, wengine bei za vitu, ilimradi kila mtu kalenga sehemu inayomgusa kiupendeleo wake.

Ni sawa kabisa, bajeti ni muhimu kwa kila mtu, lakini ninawaswasi kuwa wengi wetu hatujui umuhimu wa bajeti na kama unabisha zunguka mitaani uwaulize watu wa kawaida. Watakuambia aaah, hivyohivyo tu bora liende. Bajeti kama ilivyo demokrasia haipo akilini mwa Watanzania walio wengi, na hawana muda hata wa kuisikiliza. Kwanini, kwasababu ,bajeti ni nini na umuhimu wake kwao haijulikani, kinachosubiriwa ni matokeo yake na hapo ndipo utasikilia kilio na malalamiko.

Tunapenda sana kusubiri matokea, na kulalamika pindi matokea yakiwa mabavu.Lakini hatupendi

Angalia katika siasa watu hawajibidilishi kujua demokrasia ni nini na ina umuhimu gani kwao, utasikia watu wakisema siwezi kupoteza muda kwenda kupiga kura, kwasababu nikachagua nisipochagua atachaguliwa nisiyemtaka! Hivi fikiria huu usemi kwa huyu mtu anaelewa kweli nini maana ya kura yake!

Kuna haja ya kuelimishana kwa njia za ambazo mwananchi wa kawaida ataelewa hasa katika kipindi hiki kinachoendea uchaguzi,Ziwekwe semina, makongamano, hata nyumba kwa nyumba ili ikifikia kipindi cha kampeni wananchi wajitokeze kwa wingi, wekeni matangazo kwenye vipindi vya Tv hasa vile vinavyopendwa na wengi.Najua ni ghrama lakini gharama ya leo ni faida ya kesho.



Kwa watanzania wengi kuna kukata tamaa kuwa hakutawezekana kuwa na mageuzi katika demokrasia kwasababu nchi yetu bado ipo katika imani za chama kimoja, Na ndop maana wengi wanasema bora liende. Wengi wa wananchi hawajakubali vyama vya upinzani na sababu kubwa ni hiyo yakutokujua maana halisi ya demokrasia.Hili ni swala la kuwaelimisha wananchi kwa kuwaondoa hofu kuwa upinzani sio kama wanavyofikiria wao, upinzani ni chachu ya maendeleo na kusipokuwepo na ushindani mara nyingi kuna kudumaa kwa kuridhiki na kile kidogo ulicho nacho.

1 comment :

Anonymous said...

Sasa wewe fikiria utafanyanini ukijua nini bajeti imesema au imekosea wapi? Sanasana watakuona umechanganyikiwa kama utajitia kukosoa, labda tuongelee kijiweni yaishie kijiweni.
Swala la siasa mimi naona ni viini macho tu, hata ukipiga kura kama wana mtu wao ni mtu wao, sawa kupiga kura ni wajibu lakini...