Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, June 22, 2010

Mwenzako akinyolewa sehemu ya pili

   Soma sehemu ya kwanza ya Mwezako akinyolea- halafu endela na sehemu hii ya pili, Usisahau kutoa maoni yako.

‘Baba mkwe Naomba tutoke kidogo, nina maongezi muhimu ambayo ningependa tukayafanyie faragha’ mume wa dada mlengwa alimfahamisha baba mkwe wake. Na baba mkwe hakufanya hiana akakubali na kufahamisha mkewe. Na mke mtu akasema kwanini na yeye aiwepo, na hatimaye naye akakubaliwa kwenda kwenye hayo maongezi, jama akisema kichwani mwake kama kweli mkewe kamsaliti basi wazazi wake wote watashuhudia hiyo talaka ikitolewa mbele yao.

Unajua katika penzi, ikitokea kusalitiana hasira na chuki hujijenga haraka sana, hata kama kulikuwa na mapenzi ya kuaminiana kwa muda lakini pindi shetani msaliti akiingia nyoyoni kitakachofuata ni majuto. Jamaa chuki ilimjaa aliposikia kuwa mkewe ana hiyo tabia, alisahau kabiosa tabia njema za mkewe, jinsi walivyopendana na kusaidiana kwa kila hali.

Basi masafara wa baba na mama mkwe na mume wa binti yao ulifanikiwa na wakapelekwa hadi kwenye hoteli moja maarufu ambapo ndipo sherehe za maasi zilipangwa kufanyika. Wao walikaa sehemu ya pembeni kidogo na iikuwa rahisi kwao kutambulikana. Lakini sehemu walipokaa walikuwa wakiiona ile sherehe inavyofanyika. Waliona watu wakijirusha, pombe zikinyewa na nyama za kila namna.

‘Baba nanihii, mbona nimemuona mtu kama binti yetu kwenye ile sherehe’ mama mtu akasema kwa shaka

‘Hapana hayo ni macho yako, mbona mumewe hajatuambia ‘ akasema baba mkwe bila wasiwasi.

Maongezi ya kifamilia yalianza, na jamaa alishapanga nini cha kuwaambia , kwahiyo wazazi wakawa wasikilizaji huku wakimsifia mkwe wao kuwa ni kichwa, na mbunifu mzuri wa maendeleo. Na wakati wanaendelea mara simu ikalia.

‘Tayari mdondwe umepelekwa chumba cha wageni chumba namba 104’ mume mtu akapokea simu kwa jamaa yake ambaye ndiye alimtonya kuhusina na sa kata hilo

‘Wazazi wangu Naomba twendeni kwneye ofisi niliyoiandaa, hiyo Ndiyo itakuwa ofisi ya mradi wetu, tukitoka hapo basi mtaamua kuwa mnaingia ubia au basi tena. Wazazi waksema wao wapo tayari, ila ni vyema waione hiyo ofisi.

Huku nyuma, Yule dada alishasuka wapambe na alishaongea na mhudumu wa ile hoteli, ingawaje kulitopkea kutokukubaliana na hilo swala kwani wao waliona ni kuwafukuza wateja wao. Mke wa Yule jamaa alishafika na Bahati nzuri alikuwa uopande ule waliokaa wakwe wa mke mlengwa, kwahiyo wakati wao wanaondoka na yeye alishapigiwa simu ya kuelekea huko kwenye chumba 104.

Jamani sitaki vurugu , Naomba mlimalize swala lenu kinidhamu’ akasema bosi wa ile hoteli na kuondoka kuelekea ofisini kwake.

Ishara waliyopkubaliana na kuwa jamaa akishachojoa nguo zote mke mtu azifiche na awapige simu wenzao nje na wakisikia hiyo simu wao wasukume mlango waingie ndani.

 Kilichotokea hapo ni mshikemshike, nitakuhadithia kwenye kesho mungu akipenda.Ngoja tuishie hapo kwanza nisikie maoni yenu, kama hakuna basi nitaleta mada nyingine.

From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Bwana hebu tumalizie hiki kisanga, manake kama ingekuwa mimi sijui ningesemaje. Mume wangu atafute mwanamke mwingine halafu niambiwe hivyo, kwanza nikifika huko guest huyo mwanamke atatoka na ngeu, halafu huyo mume nitampa vipande vyake, sijui kama nitaishi naye tena....