Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, June 22, 2010

Aliyekupa wewe ndiye aliyemnyima yule

`Unaua leo nilikuwa napata `heavy lunch'(chakula muhimu cha mchana) na wakuu wa nchi, siunajua ten ukiwa na watu kama lazima uijue nchi, nami sikusita kuwapa ndogondogo zetu...' huyu alikuwa jamaa mmoja ambaye alipenda sana kujiona, na kujiweka hali ya juu, kwa asiyemjua utasema kweli jamaa ni mtu wa watu, lakini mengi ya hayo alikuwa akituongopea.
'Sasa nemerudi ofisini, jioni dereva wangu akija, nitaenda kupata kinywaji na tajiri mmoja, ninamipango kabambe ya kufungua kampuni yangu' alisema huku anachokonoa meno kwa vijiti. Tulimwanagalia tukacheka, tulijua hizo ni miongoni mwa kamba zake. Hapo alikuwa akila mihogo ya kukaanga au mahindi, lakini anavyoigiza utafikiri kweli katoka kula nyama. Nilijiuliza kwanini atudanganye, kwanini aigize mambo yasiyo yake. Nikajua kuwa hii ni hulka ya binadamu, kujikweza. Kila mtu anapenda kuwa `mtu fulani wa hali juu' hata kama hana uwezo nawo.
 Binadamu kama tulivyo hatupendi uzalili. Hatupendi tuonekana hatuna, tutajitahidi kuficha aibu hii kila inapowezekana. Ndio maana tukaitwa binadamu, kutoka katika kundi la wanyama. wanyama wengine hawana utu ndio maana, wanaiba, wanatembea uchi na hata kufanya mambo ambayo sisi tunayaita ya aibu. Hii ndio tofauti kubwa na hawo wanyama wengine. Katika ubinadamu au tuseme `utu' wapo waliojaliwa kuwa katika hali nzuri, na wapo waliojaliwa kuwa duni, yote ni mapenzi ya mungu, kwani aliowajalia hawa wapate na wale wakose ni huyohuyo muumba, kwa kuigiza msomo usemao `aliyekupa wewe ndiye aliyeninyima mimi'
 Usione ajabu akatokea mtu kama jamaa yetu huyu, yeye yupo katika hali ya chini, lakini ndoto zake zote ni kuwa katika kundi la watu wa juu. Hana uwezo huo lakini anaigiza, ili watu wamdhanie kuwa yeye sio wa hali chini. Lakini wapo walio katika hali chini na hawana hata uwezo wa kuigiza, na wamefikia kuondoa utu wao wa aibu na wanatembea mabarabarani kuomba, sio kwamba wanapenda, inawauma lakini wafanyeje!
 Inapofikia binadamu anaondoa utu wake akapita mabarabarani kuomba, au akaja kwako kukuomba hela ya kula au shida fulani ujue kuwa inamuuma, hapendi lakini hana jinsi. Hawa ninaowazungumzia hapa sio wale wenye shida za upungufu wa viuongo. Nawazungumzia wale ambao wamekamilika, lakini hali ya kimaisha imewakwaza kupata ridhiki au kupambana na tatizo fulani.
           'Bwana huyu naye kazidi kuomba, hana ulemavu wowote lakini kila siku naomba, nauli,naomba hela ya kula' utasikia mtu akilalamika. Jiulize kweli hivi kuna binadamu anapenda kuzalilika. Sidhani kama kuna watu hawapendi kuwa watu miongoni mwa watu, sidhani kama kuna watu mawazo yao ni kuomba tu ili apate kuishi, nafikiri wanaofanya hivyo hali ya kimaisha imewakwaza. Mola kawapa mitihani, kwani yeye ndiye kakupa wewe na akamnyima huyo ili tupate majaribu. Sasa ukiwa nacho msaidie, na umshukuru mungu kuwa umepata na umewekeza kwa maisha yako ya baadaye, au hatuamini hili kuwa kila ukitoa kumsaidia mwenzako unawekeza kwa ajili ya maisha yatu ya baadaye!.
 Hili ndilo la wazo la leo likisema `aliyekupa wewe ndiye aliyemnyima mwezako'
 Ngoja niishie hapa na tusome sehemu ya pili ya mwenzako akinyolewa wewe tia maji
From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Aaaa bwana tupe stori za kufamania bwana, unatuletea hayo ya ombaomba, mtu mzima hana kilema anaomba kwanini asiende kijijini kulima. Usiwatete hawa watu bwana!