Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, June 23, 2010

Mama mkwe!

 Mke wangu alikuwa masomoni, na mara ukaja msafara wa wakwe zangu bila kutegemea. Walifika waliposikia kuwa binti yao anarudi , kwahiyo walikuja kumpokea binti yao ambaye ni mke wangu baada yakukaa masomoni Ulaya miaka miwili. Ilikuwa raha kwangu na kwa wazazi pia, lakini safari yake ikaahirishwa bila kutegemea na ilibidi tusubiri mwezi mmoja, na tukaona haina haja kwa wazazi kuondoka halafu warudi tena.


Nilikuwa nimechukua likizo fupi kwa ajili ya mapokezi ya mke wangu na ukizingatia ni miaka miwili sijaonana naye, kwahiyo kwangu niliipanaga kama fungate jingine. Sasa ndiyo hiyo imeahirishwa mpaka mwezi ujao. Tukaona haina jinsi ni kuvuta subira, lakini hutaamini kipindi hicho nipo nyumbani na wakwe zangu ilikuwa mtihani. Wakwe zangu ni wale wenye mila za kuogopana, yaani mkwe kukutana na mkwe mwana wake ni kwa kuogopana hasa kwa mama Mkwe, kwa baba ilikuwa haina ugumu. Tulikuwa tunatoka naye tunabarizi huku na huko, kivumbi ukirudi nyumbani, mama anatafuta sehemuya kujificha.

‘Mzee hivi hizi mila zina maana gani manake mimi niliona ni furaha mama yupo hapa, tuongee, tule pamoja, na hata ikibidi wakati mwingine tutoke pamoja, lakini sasa naona hata shida kushinda hapa nyumbani’ nikamwambia baba mkwe.

‘Hawa wakina mama wa nyumbani siunawaelwa tena, bado wana zile imani za kizamani, hata mimi nimemshauri aachane nazo lakini anasema hataeleweka na ni vibaya kuwa karibu wewe na yeye’ akasema baba mkwe, na sikutaka kubishana naye zaidi.

Ikatokea siku baba mkwe ametoka kwenda Kimara kumuona mmoja wa Watoto wake na huko ikabidi alale, ilikuwa mtihani, kwani siku hiyo nilishikwa na tumbo la kuendesha, lilinishika kweli kweli, kiasi kwamba, nguvu zote zikaniishia. Sikuweza hata kutoka nje. Fikiria huo ugonjwa wenyewe, na vyoo ni vya nje, fikiria hali iliyonishika na nipo mimi na mama mkwe. Ikabidi uukwe uuishe mama afanya kazi za umama. Ilipofika usiku hali ikawa mbaya, hata kutembea nikashindwa, kwani hutaamanini mama ilibidi anisafishe kama mwanae. Sitasahau kisanga hicho na hata mke wangu alipokuja hakuamini kuwa mama ilibidi afanye kazi ambayo yeye mwenyewe hata haamini kuwa aliwezekanaje kwa jinsi anavyomjua mama yake.

Siku mama anaondoka ilibidi pamoja na kumshukuru kumwambia ukweli kuwa tukio hilo lilitokea ili iwe fundisho kwetu, kuwa mama mkwe hana tofauti na mama mzazi kwako, haina haja kuogopana. Nini umuhimu wa kuogopana kati ya mama na mkwe wake, labda zipo mila na miiko Hebu wanaoujua waniambie. Lakini toka siku hiyo mimi na mama mkwe wangu ni sawa na mama mzazi wangu.

Naombeni ushauri wenu na Yule anayejua kwanini mama mkwe anamuogopa mume wa mtoto wake atueleze.

From miram3

6 comments :

Anonymous said...

Wewe haya mambo yaache kama yalivyo, sio rahisi kuyatafsiri, na kama unataka kupoekenyua mambo ya kimila unaweza ukaota kibyongo. Mimi sijawahi kukaa meza moja na mama Mkwe wangu, sasa wewe umenawisha na mama mkwe wako, nenda kwenu ukaombe toba

Anonymous said...

Kuna dharura, na hiyo ni dharura, ikiisha umama mkwe upo palepale, hiyo ni mila na desturi. Ndio sisi wa mjini tunadharau hilo,lakini ukiwauliza wazee vizuri watakuambia.

Anonymous said...

Mimi ninawasiwasi wewe na mama mkwe wako, baba mkwe aliporudi alikaa kimya tu...mmmh, nafikiri nayeye ni mrembo kama mkeo..hahaha

Anonymous said...

Jamani kwani kuna ubaya kupenda tunda na mti wake...lakini haya yanasaidia nini, labda kuonea haya kuwa huyu ndiye anaye....hahaha , kwakweli haiji, anayejua nani atuambie

Anonymous said...

Mimi na baba mkwe wangu tunaongea tunapigana mabusu ya salamu, hakuna matatizo, unajua huo ni mtizamo wenu na sioni ubaya wa mama mkwe wako au baba mkwe wako, ila heshima lazima ichungwe

Anonymous said...

Ulishikwa na kipindupindu nini, msile ovyo, sasa unaona umeumbuka..