Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, June 1, 2010

mafao baada ya kifo

`Fao hilii litamsaidia mwanachama katika mazishi yake na gharama za mazishi...' hili nitangazo nililolisikia likitangazwa, wakati tumekaa barazani na mgeni aliyetutembelea, na mara watoto wakaanza kuliigiza, na mtotoo mmoja akasahau kulitamka vizuri, ikawa kichekesho.
`Kasemaje, eni-esi, esi, eti nini vile....'
 'Yule mgeni wetu akaanzisha mjadala kutokana na tangazo hilo. `Hivi kweli mnalielewaje tangazoo hili, mimi nahisi wanakariri hali halisi ya kimaisha kuwa `ukifa unapendwa zaidi ya ukiwa mzima...' akasema yule mgeni.
'Kwanini unasema hivyo, mimi nahisi wanatangaza fao mojawapo kati ya mengi wanayoyatoa...' nikasema
'Sawa, moja ya mengi, lakini kwanini wasitangaze yale yanayomsaidia mwanachama, akiwa hai, na nafikiri wangebuni mambo yatakayomsaidia mwanachama kuongeza maisha na sio fao la maisha baada ya kifo. Wewe kama mwanachama , ukifa sio fao kwako tena. Hivi kwanini watu tunasahau kuwa mtu akifa sio kitu tena, na jambo la muhimu ni kumjali akiwa hai, na hasa pale anapokuwa hana ajira tena, au akiwa mzee...' Akasema yule mgeni wetu kwa huzuni.
'Nakumbuka wakati nastaafu, baada ya kulitumikia shirika langu kwa miaka zaidi ya thelathini, hela nilizokuja kupata hazikunisaidi hata kununua baiskeli, niangalie sasa hivi nilivyochoka, ndio ingekuwa muda wa kupata manufaa ya michango niliyokuwa nikikatwa wakati nina nguvu zangu. Lakini kipindi nakatwa kwenye mshahara zilionekana nyingi kwangu, sasa siku zilivyokwenda na thamani ya hela ikawa inashuka, na kwahiyo kile kilichokuwepo kikawa sio kitu tena. Lakini kumbuka wao walizichukua zikiwa na thamani wakaziwekeza, na mwisho wa siku wanakupa kitu kisicho na thamani, na ndio maana wanakutangazia gharama za mazishi yako, kwanini, kwasababu hutaishi muda mrefu tena na hicho utakachokipata...' akasema huku anatabasamu.
 Mimi nilitafakari sana maneno yake, nikaona yana mantiki hasa katika thamani ya pesa, huenda imefika wakati shirika hili lingebadi muelekeo kwenda na wakati, hasa katika thamani ya pesa. Wajaribu kuziweka hela katika thamani ya pesa, yaani hata kama thamani ya pesa itashuka, mlengwa apate thamani sawa na kipindi alichakatwa katika mshahara wake!
 Pia, kuna haja ya kugundua njia za uzalishaji kwa wanachama, kuwa kuwe na mikataba ya uwekezaji, badala ya kusubiri mwisho wa siku unamlipa mwanachama hela ambayo haina thamani tena kwake. Mwanachama awe kama amewekeza hisa, ili mwisho wa siku naye afaidi kile kilichozalishwa na shirika, au awe naye muwekezaji!
 Hayo nio mawazo yangu kwani nahisi mwisho wa siku tutakuwa tukisubiri mafao ya baada ya kifo badala ya mafao wakati wa uzee au baada ya kuacha kaza na kujiajiri!



From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Eti mafao baada ya kufa, utanufaika vipi na wakati wewe ni marehemu. Mimi sijalifuatilia vyema hilo tangazo lao, nitasema chochote nikilisikia