Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, June 1, 2010

kwenda na wakati

`Hivi unaweza kukumbuka kwa siku moja umepewa au umetoa shukrani ya ahsante mara ngpi?' Alituuliza babu yetu wakati tumejipumzisha jioni. Kila mmoja alitafakari na wengi tulikumbuka kuwa kila tukimaliiza kula lazima tuseme ahsante kwa mama, kwahiyo tulikadiria kutoa ahsante kwa milo mitatu, na pia tukakumbuka njiani tuliwasaidia wazazi kubeba mizigo, tukapata ahsante. Lakini hata tulivyojitahidi kuhesabu hatukufikia kumi, tukakaa kimya kumsikiliza babu anataka kusema nini.
 `Ni vyema ukajitahidi angalau kupata ahsante kumi kwa siku, hiyo ni moja ya hazina yako. Unajua ukifa, huko mbele utakuwa na kitabu cha hazina yako, na ulichotenda leo kinahifadhiw huko kama unavyoweka akiba benki, sasa hebu fikiria unafika huko kitabu chako kina madeni tu, yaani umetenda maasai, manake ukitenda maasi ni madeni, ukiwa mjeuri kwa wazazi ni madeni...' babauu kasimama kidogo, akitafakari kitu.
 Mimi nilipokumbuka haya nilijaribu kutafakari kizazi chetu hiki cha leo, jinsi gani tunakilea. Hivii wewe kama mzazi umewahii kukaa na watoto wako mara ngapi kuwakumbusha mambo muhimu kama haya. Nafikiri mara nyingi tunakumbuka kuwakanya watoto wetu wasifanye mabaya pale wanapokosea. Lakini kuna njia nyingine kama hizi kuwapa changamoto watoto kuwa wajitahidi kufanya mema kwa siku ili jioni wakupe idadi ya wema wliofanya, wakizoea hivi mara mbili basi inakuwa kawaida yao.
 Hebu jiulizeni, leo hii unaweza kumkuta mtoto akimsaidia mtu mzima kubeba mzigo? Sidhani, sisi tulifundishwa hiyo. Au mnapotembea njiani unaweza kumkuta mtoto kweli akimpisha mzazi apite kwanza? sidhani. Yote haya ni kile kinachoitwa kwenda na wakati! Lakini kwenda na wakati huko tunakudekeza sisi wenyewe, kwasababu kama utakuwa na jitihada za kuwaweka watoto wako chini na kuwapa semina za maneno hata vitendo, tunaweza tukapunguza hili tatizo. OOh, jamaa mmoja akasema `hivi unakumbuka moja ya haki za watoto, ukimchapa umekiuka haki zao? ' Ni kweli lakini tujiuliza je mtoto akifanya mabaya mara nyingi, ukakanya kihekima, hakusikia, akarudia mara nyingi, utafanyaje, umuachie tu? Je haya mabaya anayofanya hayakiuki haki ya maisha yake ya baadaye.
 Hebu tutafakari haya, na tunaweza kujadili wenyewe kama tutaona uzito kuweka mawazo yetu hapa hewani

From miram3

No comments :