Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Tuesday, June 8, 2010
Kimuhemuhe na meseji ya mume wangu
'Ndio maana nimekununua simu yako..' akasisistiza mume wangu
Mume wangu alikuwa bafuni akioga, nilitazama kuhakikisha kuwa bado anaoga, au keshamaliza, nakagundua kuwa bado kajipaka sabuni, kwa tahadhari nikaichukua ile simu na kufungua ile meseji. Mwili ulikuwa ukinicheza kwa woga nikiogopa je akitoka ghafla na kunikuta sio ndio itakuwa dhahama. Sio kificho mume wangu ni mkali na kweli akiangusha kipigo ni kipigo kweli, nakumbuka siku alipompiga mdogo wake wote nyumba nzima tulitetemeka. Na hata hivyo, sina mazoea ya kuchunguza chunguza vitu vya watu, tabia hii nimeijenga toka kwa wazazi wangu.
Ukiniuliza kwanini siku ile siwezi hata kukupa simu kubwa muhimu, sijui hata mimi, kwanini hamu ya kuisoma meseji hiyo ilinijia, na kwaweli najuta, huenda maisha yetu yangeliendelea kuwepo, huenda kilichoandikwa humo, ilikuwa sio kweli, huenda, huenda ni ....kwahiyo huenda zinaniandama kila siku nikifikiria maisha yangu ni mume wangu.
Mume wangu alikuwa mpole, na mkarimu hutaamini, na hatukuwahi kuogombanagombana ovyo, kwani nilishamjulia nini anakitaka na nini hakitaki. Hii ndio hulka njema ya kuishi na watu, ukitaka msikosane jifunze nini mwenzako anapenda na nini hakipenda, kile asichokipenda jaribu kujihadharii nacho. Na mume wangu naye alijaribu kufanya hivyohivyo, ila niligundua kuwa ana usiri fulani, na huo usiri ndio ulionipa kimuhemuhe cha kutaka kugundua siri iliyopo, nahisi ndio sababu kubwa ya kutaka kuisoma ile meseji, sijui na sina uhakika kwa hilo. Nisema moyoni, huenda nikigundua hiyo siri itanisaidia kujenga penzi letu na mume wangu, lakini ...
Niliifungua ile meseji na mara ikatokea picha na maandishi...mmmh, mungu wangu, nilishikwa na butwaa. Mwili mzima ulizizima, na giza likatanda usoni ghafla. Mimi sina ugonjwa wa shinikizo la damu, lakini kwa muda ule nilihisi kupatwa na tatizo hilo. Niliishiwa nguvu , kiajabu kabisa, sikuweza kujimudu na mara nikadondokea kitandani, na ndicho kilichoniokoa, vinginevyo kama ningedondokea chini huenda ningeliumia vibaya. Na kwa mbali nikasikia mlango ukifunguliwa, na fahamu zikanipotea.
Je mshikaji unaweza kukisia huyu mama aliona nini?
Kabla sijaendelea na kisa hiki chenye mafundisho fulani, niwaulizeni wajumbe, ni hivi ni vyema tukachangia simu na wapendwa wetu, hapa nikiwa na maana waume na wake zao kuna ubaya gani wa kuchangia simu, kwanini tufichane simu wakati sie ni kitu kimoja. Nahisi wale wanaofichana simu kuna lao jambo! Hilo ni wazo langu sijui wewe unasemaje?
From miram3
5 comments :
NI kweli kabisa wanaume wengi wanamataizo hayo, hawataki wake zao waguse simu zao, pia wapo baadhi wa wanawake. Na ukiona hivyo jue kuwa ni kweli kuna KITU si cha kawaida (anamaovu yake) ndio maana wanakuwa wakali sana wakiona unashika simu yao. Na akiona vipi basi akiingia tu home anazima simu kwa vile anajua ana vimeo vyake, vitamsumbua na kwako anajifanya kuwa yeye ni mtakatifu. Kwa kweli usiombe yakukute kama hayo, ni kweli yapo. na unaweza usiwe na tabia ya kuchunguza simu ya mmeo lakini kutokana na ishala fulanifulani ukajikuta unajiuliza kulikoni? ndio maana unaamua kuchunguza, ndio matokeo yake ndio hivyo. Na mara nyingi simu huvunja nyumba za watu au kutokuwa na maelewano ndani ya nyumba. KWA KWELI HATA MIMI KINANIUMA SANA KWA WATU WA AINA HIYO.
mtu ambaye hataki cm yake iguswe na mwenzake naniwanandoa basi ujue huyo sio mwaminifu kwa nini hataki iguswe wakati mnashirikiana kila kitu?
Ahsante sana mjumbe kwa hoja zako, najua wapo wengi yamewasibu haya na wanamengi ya kuongea, lakini wanaogopa kuwekwa hewani.
Sio lazima utaje jina lako, kama hutaki au e-mail yako, ingia kwenye sehemu ya comment, , ukishaiandika acha sehemu ya Google account, acha sehemu ya open ID, acha sehemu ya Name nenda kwenye Anyonymous(manake asiyejulikana) unaclick hapo, basi hoja yako itaonekana na haitajulikana imetoka kwa nani!
Changieni hili ili tujue ukweli wa nafsi zetu, je simu zetu ziwe huru kwa mume na mke au kila mtu chake!
Jamani mnashindwa kuelewa maana ya simu za mkononi, hizi ni kwa ajili ya meseji, au mawasiliano ya mtu binafsi. Kama mnataka simu ya kuchangiana ipo hiyo ya mezani, lakini sio simu ya kiganjani.
Hiyo kusema labda mtu ana lake jambo, anaweza akawa nalo hata kama hana simu.
Kwangu mimi simu yangu ni yangu na ya mke wangu ni yake, kupekenyuana ndio huko kunaleta presha kupanda presha kushuka, matokeo yake mtakufa, au mtavunja ndoa zenu bure, kwa vitu ambavyo sio kweli.
Hayo ndio yangu
baba nanihii
Duuh! yaani mdau umenigusa kweli simu ya kiganjani ni kwa ajili ya private issues lakini lakujiuliza baina ya wewe na mwandani wako kuna cha usiri zaidi yenu?. ukiona pana mashaka hapo kwanza ujue uaminifu una potea kwa nini mfichane ndoa ni uaminifu, hakuna jambo la siri zaidi baina ya wana ndoa, chake chako changu chake ukiona tu pana kijificho ficho ujue kushaliwa mdau tena uanze tahadhari au utaharibikiwa.uaminifu ndio silaha kwa wana ndoa.simu ya mkononi isiwe sababu. tudumishe uaminifu hii ndio silaha ya kumshinda shetani.nawatakia uvumilivu.
Post a Comment