Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Thursday, June 10, 2010
Nashuka au Nateremka?
'Hi-yo, ime-ime kaa sawa, kusema na-shu-ka' akauliza yule mzungu.
Nilimtizama yule mzungu, nikaona aibu, kwasababu lugha ni yetu na huyu ni mgeni anayetaka kujifunza lugha, na mbele ya uso wake anakuta watu wanazungumza tofauti na alivyojifunza. Ikabidi nimueleze kuwa, lugha yetu ina maneno mengine yanaweza kutumika kwa maana tofautitofauti kwa neno moja, ikitegemeana na mtumiaji anavyolenga hoja yake.
'Hiyo sawa njua, kuwa unaweza kusema paa la nyumba au paa juu, au paa mnyama. Lakini mimi sioni eeeeh, manti-ki ya eeh, neno `shu-ka' kutumika mahala hapo.Nafikiri, eeh, sijui kama nime-kosea au la, alitakiwa aseme `na-te-re-mka, sawa...' Akaniangalia nakuwaangalia watu wengine mle ndani.
Hapa nilijifunza kitu kimoja kuwa sisi Watanzania hatukabali kushindwa, hata kama tumekosea, hapa ilibidi nikubali wazi kuwa hapo kuna makosa, lakini siunajua tena hulka yetu, nikaanza longolongo. Na matokeo yake tunakifanya kiswahili chetu kisieleweke vyema kwa wageni wetu! Mara siku hizi unasikia kiswa-engilish.
'Sawa kabisa, hilo ndilo neno sahihi, lakini kuna kitu mazoea, watu wakizoea neno wanalifanya litumike hata pasipostahili, ila kwa sababu ya mazoea watu wanaelewana. Kuna maneno mengine watu wamefikia kuogopa kuyatamka kwasababu ya tafsiri potofu. Lakini ndipo mahali pake. Mfano kuna mmoja alichekesha hapo wakati tunatoa hoja. Akasema ukiwa na chungwa zima na unataka umpe mwenzako kipande utasema nini...sikumuelewa, lakini watu walicheka, kwanini, sijui!
Sasa waungwana ni vyema tukajenga hulka ya kupenda lugha yetu, tujitahidi kuioboresha kwa kuongea usahihi, tusipende kuzungumza lugha kwa nia ya kuichafua. Nakumbuka kuna neno `onyesha na onesha' alipolizungumza mzee wetu Mwinyi kuwa linapotoshwa watu walianza kiijisahihisha. Hii inatujulisha kuwa viongozi wetu wakiamua, lugha hii inaweza hata ikawa ya kimataifa. Kwa mfano viongozi wetu wakitembelea nchi za nje waamue kutayarisha hotuba zao kwa lugha ya Kiswahili, ni lazima wajumbe na vyombo husika vitatafuta tafsiri na hapo ndipo itakuwa chanzo cha kukiweka kiswahili kwenye uwanja wa kimataifa. Mbona Wajerumani, Warusi, hata Waarabu wanaongea lugha zo kwenye ulingo wa kimataifa. Walianza vipi kama sio hivyo. Tatizo hatujiamini, tatizo hata lugha yetu wenyewe hatuithamini, tatizo hata lugha hii bado ni changa masikioni mwetu.
Na tukumbuke kuwa mkataa utumaduni wake ni mtumwa, au!
From miram3
1 comment :
Yaah, utumwa wa minyororo tunaulaani, lakini utumwa huu wa ki-akili tunaukumbatia, ambao ni mbaya zaidi kam tungelikuwa na ufahamu huo
Post a Comment