Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, May 12, 2010

'Usikojoe hapa' amri

`Usikojoe hapa’ Ni maandishi makubwa yaliyokolezwa, na hata asiyeona vizuri angeliweza kuyaona, lakini cha ajabu, konda wa gari letu katika kusubiri foleni ya magari akachepuka na kuanza kukojoa huku anayangaalia yale Maneno mbele yake. Nafikiri alikuwa akiyasoma kwa dharau, au alikuwa hakuyaona kabla hajaanza kukojoa. Sisi tuliokuwepo ndani ya gari tukaanza kucheka. Tulicheka kwasababu ya maandishi na wengine walicheka kwasababu ya jamaa kukojoa ili hali watu wengi wanamuona.


‘Usikojoe hapa, nikakojoe wapi na hali mkojo umenibana, eti abiria wangu nisaidieni, nikakojoe wapi na mimi mkojo umenibana?’ Konda aliingia ndani ya gari huku bado anafunga vifungo vya suruali yake ya kibluu, sare ya mokondakta.

‘Acha mzaha una maana hukuona yale maneno na hata hivyo pale sio chooni, utakojoa aje hadharani’ mama mmoja akasema kwa hasira.

‘Sawa mama yangu sio chooni, na nimeyaona yale Maneno, sasa nimebanwa na mkojo nikakojoe wapi, nijikojolee, simtanishambulia kwa Maneno ya hasira, nakuniita kichaa, au?’ Yule konda akajitetea.

Mimi kwa tafakari zangu nikajiuliza hivi kweli katika foleni hizi za jiji la Dar, kutoka Msasani hadi Gongolamboto unachukua masaa matatu hata manne, na umebanwa na haja utajisaidiaje? Heri anayeenda Morogoro anaweza akafika hata wewe hujafika, na njiani kuna kuchimba dawa, sie tutachimba dawa wapi?.

‘Mnatakiwa msinywe chai asubuhi, ili msikojoe ovyo, simnaona tangu tusimame hapa kusubiri turuhusiwe na trafiki imepita masaa mawili, hebu fikirieni, hawa matrafiki wana ubinadamu kweli, wengine tumesimama na mguu mmoja, tumebanana, na bado hataki kuruhusu upande wetu…’ akalalamika mzee mmoja.

Nikakumbuka siku moja nilitoka na rafiki yangu, saa kumi na moja na nusu za asubuhi, kama kawaida yetu kuwahi kibaruani, yeye alikuwa akienda Morogoro siku hiyo, na tulipofika Mombasa, akapata mabasi ya Ubungo, kirahisi mie ninayeenda Msasani nikabaki nasota, kupata magari ya Msasani inabidi ujue kudandia kwani wao ni mwendo wa juu kwa juu, wanakwepa wanafunzi. Kimzaha mwenzangu akaniambia atafika Morogoro mimi bado sijaiona Msasani.

Na kweli siku hiyo kulikuwa na foleni ya kufa mtu. Banana, tukasoteshwa, kufika Magomeni , ikawa ni kambi ya muda, masaa yanakatika, tulipofika njia ya kuingia Karume ikawa kama vile wanajua tupo watu wakusota, tulikaa mpaka abiria wakaanza kumtukana Yule trafiki anayeongoza magari. Baadaye alituruhuru, tukasogea kidogo tukakutana na foleni ya kutoka Buguruni, tulisota hapo na baadaye hawo tukafika Magaomeni, hapo ndio usiombe tulikaa, mpaka akina mama wengine wakaanza kudondoka.

Tuliruhusiwa na nilipoangalia saa ilikuwa saa tatu na nusu, nikambipu mwenzangu kuwa kafika wapi, alinipigia haraharaka akisema anakaribia kuingia Moro. Sikuamini, na tulipofika Morocco, hapo napo kulikuwa na msafara gani sijui tukasota. Ilibidi nipige simu ofisni kuwaeleza hali halisi ya barabarani.

Tulipofika Namanga jamaa akanipigia simu kuwa anakunywa chai hotelini Morogoro. Nilibaki nimeduwaa, hivi kweli nchi hii tutafika, mnataka tufanye kazi au tushinde mabarabarani. Na heri tungekuwa ndani ya magari yenye viyoyozi, lakini adha ya majasho, hewa ndogo na kusimama kwa msangamonao ndio maisha yetu maisha bora haya. Najua wengine mtasema kwanini nisingepanda bodaboda. Mhh, kuna kisa cha bodaboda nitakupa baadaye

. Ahsanteni

From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Lakinii watu wengine bwana utakojoaje mbele ya kadamnasi! Ni sawa mkojo umekubana, lakini mmmh, mkojo unauma jamani