Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Thursday, May 20, 2010
Bodaboda na mwendo wa.....
‘Kipindi cha mvua barabara hii ya kutoka Mombasa hadi Kipunguni haisafiriki kwa mabasi ya kawaida, basi siku ile tulikuja kwa ajili ya harusi ya ndugu yetu mmoja. Tulipofika Mombasa, mvua ilikuwa imepungua na watu walikuwa wakitafuta usafiri, hata wa taxi lakini ni nani angekubali kupitisha gari lake kwenye hayo mahandaki.
‘ Tukatafakari tukaona tuchukue pikipiki, ambazo zilijazana pale kusubiri anayetaka kwenda. Tuligeuza shingo kuangalia upande ule mara pikipiki tano zikatujia.
‘Mama, ndugu mnataka kuneng’emuka…’ wakasema kwa pamoja.
‘Eti nini, …’nikajikuta nikiuliza
‘Hadi Moshi bar elifu mbili, hadi kwa Diwani utaongea mwenyewe, mwendo wa kuneng’emuka…chapuchapu umefika, simnajionea wenyewe hakuna gari wala taxi inayokwenda huko’ akasema mmoja wa madereva wa pikipiki, huku wakitupita huku na hko kwa mbwembwe’
Basi Yule mama akaendelea kuelezea kwa baadaye waliamua kupanda pikipiki moja kubwa, inayochukua watu watatu, au mishikaki kama walivyoitania. Wakajipanga, mama akaamua akae nyuma, shemeji yake katikati na mbele karibu na dereva akakaa mumewe.
‘Najuta kwanini niling’ang’ania kupanda nyuma, sikupenda kuwekwa kati , sikujisikia vyema, lakini sasa kama ikibidi kupanda nitang’ang’ania katikati’ akasema tena Yule mama huku kila mtu akitaka kusikai kilichomsibu Yule mama.
‘Safari ikaanza, pikipiki ile ikawa inakwepa maji, na mashimo, na kila mara nilikuwa nikihema kwa woga, siunajua jinsi gani unavyojisikia pale pikipiki ikishusha mlima, moyo wote unaelea hewani. Basi ilibaki kidogo niwaambie wenzangu nyuma sipawezi, kwasababu niliona kama wananisukuma nidondoke hasa pale pikipiki inapopandisha mlima.
‘Tulifika eneo lenye maji, mwili wangu ulishaanza kuisha nguvu, sijui ni presha au ni nini, miguu ikaanza kutetema. Shuka, panda, shuka panda, mara nikajisikia kama ninapaa hewani, na mara pwaaaa, kwenya dimbwi la maji…’ Yule mama akajiangalia kama vile anahakikisha kuwa nguo yake ni safi.
‘Wee fikiria, harusi hiyo nilivyojiandaa nayo, nguo za gharama, ….yaani nikikumbuka siku ile nilivyobadilika , hutaamini. Nguo yote ilijaa tope, na nilivyodondoka pale kichwa karibu kitangulie chini, nywele zangu nilivyokuwa nimeziseti zilibadilika kuwa uchafu wa tope…’ akajishika kichwa kuhakikisha tope la siku ile halipo!
‘ Jamani nilibaki pale chini hadi wasamaria wema walivyokuja kuniinua wakijuwa nimeumia sana. Sikuumia zaidi ya mshituko na kuchafuka. Lakini nguvu zilikuwa zimeniishia kiasi kwamba waliokuja kunisaidia ilibidi wafanye kazi ya ziada kunibeba, na kunibeba huko wakabeba na vito vyangu vua thamani nilivyokuwa nimevaa!’
Tangu siki ile nikisikia eti kuna pikipiki, najiuliza mara mbili. Ni heri heri nitumie TZ 11, huu ni usafiri wangu wa heri aliyonijalia mungu kuliko kuneng’emuka na bodaboda!’ akahitimisha kile kisa, huku tukiangua kicheko.
From miram3
2 comments :
Hivi kweli huko tunakokwenda tunarudi nyuma, au tunakwenda mbele manake wenzetu wanatumia usafiri wa umeme, anafanya kazi Mwanza anaishi Mtwara, fikiria, sisi leo tunakimbilia pikipiki! Haya tutaona
Hi, juѕt ωanted to say, Ӏ lоved
this post. It was funny. Keep on ρоsting!
Here is my blog post ; netbooks cheapest
Post a Comment