Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Wednesday, May 12, 2010
Mgawanyo wa keki
Tulipoarifu watu watangaziwe ikawa tumeharibu, kwani kila aliyesikia aliamua kuja, sijui kwa mapenzi ya waliohusika au ni hali halisi ya kimaisha kuwa shughulini angalau utajazia bajeti yako na siku hiyo itapita bila kugusa mfuko wako. Kila dakika iliyopita watu wakawa wanakuja, na hata sehemu za kukaa zikawa hazitoshi. Ikabidi kamati ndogo iundwe na wanandugu tuitane pembeni.
‘sasa jamani tufanyeje na hali mumeiona, cha msingi watu tuingie mfukoni tuongeze chochote’ mwenyekiti akatoa rai, na watu wakajipapasa, lakini kilachopatikana kikawa hakikidhi haja. Tukakabidhiwa majukumu kamati ya chakula, tufanye vyovyote iwavyo angalau watu wajilambe.
Wazo likatolewa kuwa, kwanza tuwaridhishe wageni mashuhuri, viongozi wa dini ambao walialikwa rasmi na wazee waheshimiwa ambao walitambulika kama `meza ya waheshimiwa’ na mgawo wao ukawa wa kuridhisha wakala wakaondoka, ikabakai watu wa kawaida. Na mgawo huo wa meza ya juu, ukawa umeondoa nusu ya chakula tulichokuwa nacho, hatuakumaini, ina maana waheshimiwa walikuwa wengi kiasi hicho.
‘Sasa tufanyeje’ mgawaji akauliza
‘Mimi kwa ushauri, tusitumie sahani ya mmoja mmoja, tutumie sahani hizi kubwa tuwapange kimakunndi, atakaye bahatika basi, lakini tuwe wakweli kwa hili’ mmoja akasema na akajitolea kwenda kuwatangazia watu.
Ukweli ukatuokoa, kwani wale walioelewa wakaondoka huku wakisema shughuli sio lazima kula, lakini wapo waliolalamika kuwa kama tulijua kuwa hatujiwezi kwanini tukatangazia watu.
Kwenye shughuli hiyo kulikuwa na mjadala wa keki ya taifa au pato kama mshahara, mjadala huo ulizuka kabla kama sehemu ya kupoteza muda, tukisubiriana. Swali lilikuwa kwanini mshahara hautoshi. Na hapo niliweza kuokoteza baadhi ya hoja muhimu .
`Mimi nawashangaa sana wanasema kwanini watu wanadai mishahara haiwatoshi, hivi kweli gari linaweza kwenda bila petrol au dizeli kama linatumia kimojawapo! Tunasahau kuwa mtu kama binadamu ana mahitaji muhimu, mahitaji hayo ni sawa na petrol au dizeli kwenye gari’ Haya yalikuwa Maneno ya mzee wa hekima..
‘Kiutafiti na hali halisi ya kimaisha mtu na familia yake ili aishi anahitaji kupata mahitaji muhimu, tunasema mahitaji muhimu, kama chakula, malazi, maji,, usafiri wa kumfikisha kazini na yale yanayoitwa mahitaji muhimu anatakiwa apate shilingi lakini nne kwa mwezi. Haya tunaita mahitaji muhimu. Hebu fikiria mtu huyu analipwa lakini moja, je ataishije? Je unategemea utendaji wake wa kazi utakuwaje? Atakuwa anafanya kazi huku akili yake yote haipo kazini, atakuwa anafanya kazi lakini haithamini kazi yake! Na hapa kwavyovyote tutakuwa tunafungua mianya ya rushwa’ Hii ni hoja ya mtafiti mmoja
‘Mimi nawashangaa wakisema keki iliyopo haitishi , lakini hebu tuiangalie hiyo keki inavyogawanywa'. Hoja hii nilioanisha na chakula cha shughuli hii. Nilijionea mwenye jinsi gani keki inavyogawanywa kivitendo. Hebu tulijadili hili kila mtu katika sehemu yake!
From miram3
No comments :
Post a Comment