Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, May 6, 2010

Mfumo wa maisha ya kibata-bata

 Leo nakikumbuka sana kile kisa cha bata na kuku, kutoka kwa babu. Siku hiyo tulikuwa tumetoka kulinda ndege kwenye shamba la babu, lilikuwa shamba la mpunga! Babu kama kawaida yake alitukalisha chini na kutuuliza habari za shambani. Tukiwa tunajieleza mara bata akapita na Watoto wake, babu akawatupia chakula. Bata yule na watoto wake wakaanza kugombea, na bata-mama, akawa anawkanyaga watoto bila kujali huku akikila kile chakula karibu chote yeye mwenyewe! Tukabaki tunajiuliza, vipi huyu bata hana huruma na Watoto wake.


Mara akapita kuku akiwa na vifaranga vyake, na babu kwa kupenda mifugo yake akawatupia chakula, cha ajabu Yule kuku akawaita Watoto wake akawa anadonoa kidogokidogo huku akiwaita Watoto wake wale, na wakti mwingine akidonoa chakula mdomono na kumpa mmoja wa Watoto wake. Tukachekelea na kumsifu kuku, kuwa yeye angalau anawapenda watoto wake kuliko alivyofanya bata.

Babu akatuuliza , tumejifunza nini kutokana na kuku na bata. Tukaangalina na baadaye kila mmoja akasema kuwa kuku anawapenda Watoto wake lakini bata anajipenda mwenyewe. Tukabaki kimya kumsikilza babu atasema nini.

‘Huu ndio mfano halisi wa maisha yetu. Wajukuu zangu ni mfano halisi wa viongozi wetu, ni mfano halisi wa maisha yetu ya kila siku, hasa katika uongozi. Viongozi wengi wana tabia za bata, hasa wanaomilikia makumpuni. Angalieni wenyewe jinsi mishahara na mafao yanavyogawanywa. Katika pato ambalo nalilinganisha na mkate, nusu  ya huo mkate wanachukua viongozi ambao labda wanaweza wakawa watano tu na nusu wanagawana wafanyakazi tisini na tano waliobaki. Na katika kugawana huko, huenda wengine wakaumia, wanakanyagwa na viongozi wao, nani atawajali ilihali wote tunagombea huo mkate, kama pato la kampuni’ Babu akaasogea karibu yetu ili kutufundisha zaidi.

‘Vingozi wengi wanaangalia sana masilahi yao zaidi kuliko masilahi ya wanaowaongoza. Iweje leo huduma muhimu kama matibabu yanawaendea zaidi viongozi ambao bado wanaa pato kubwa, wanamaslahi mengi, lakini hawa watu wa chini wana pato dogo na bado huduma kama hizo kwao huenda hakuna au ni kwa mgawo.' Babu akainuka kuwatupia chakula wale bata, na sasa bata mama akawa kakaa pembeni akiwaangalia watoto wake wakila.
` Kama unabisha ni lini kiongozi alisema mimi sitaki marupurupu haya wageeni watu wangu. Labda awe kahiba, na sidhani katika maisha ya mishahara kuna kushiba. Kila kiongozi anataka zaidi, na hakuna hata mmoja atadai kuwa ametosheka. Lakini kama ataambiwa yeye kama kiongozi apate zaidi atasema hata hiyo zaidi hainioshi. Viongozi wetu wapo tayari kugombea hata kile kidogo kitakachopatikana bila kujali kuwa yeye ana zaidi hayo ni maisha ya Kibata-bata' akahitimisha babu.

Nilipoyakumbuka Maneno ya babu nikaoanisha na maisha yetu ya sasa. Nikakumbuka maisha ya ofisini ambapo wengi wa vingozi mishahara yao ni mara kumi ya mishahara ya kawaida, na bado wana marupurupu ya kila namna, tofauti na mfanyakazi wa kawaida, ambaye bado anatakiwa kulipia nauli, kujitibia yeye na fammilia yake na mambo kadha wa kadha. Angalia mshahara anaopata je unakidhi yote hayo? Haukidhi hata nusu yake, je ni kwanini huduma muhimu zisitolewe kwa huyu mfanyakazi wa chini, na huyu wa juu akazilipia kwasababu yeye ana mshahara mkubwa, utaambiwa yeye ni kutokana na wadhifa wake ndio maana anatakiwa kupata marupurupu hayo. Sasa huyu wa chini yeye sio binadamu, je hastahili maisha bora?

Sijui, lakini kwa uoni wangu, dhamira njema kwa wafanyakazi ni kuwajali katika huduma muhimu, ukiwatimizia hayo, mengine kama kutofautiana katika mshahara haitakuwa kero. Kero zinaanzia hapo, chakula, malazi, afya na elimue kwa familia. Acha niwaachie nyie mnaojua zaidi. Nyie ambao huenda mna mfumo wa kuku, sijui, ...

From miram3

No comments :