Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Monday, May 3, 2010
Mvua njoo, katerina usije
‘Jamani sasa haya magari yameacha barabara yao yanakuja huku kwa watembea kwa miguu, sisi tutapita wapi?’ mmoja aliuliza kwa hasira
‘Basi tunaomba aje muongoza magari ili atusaidie tupite kwa zamu’ akasema mwingine kwa mzaha
‘Trafiki yeye huongoza magari barabarani,sidhani kazi yake ni kuongoza magari na wapiti njia ehemu isiyo barabara’ mmoja akaongezea.
Hivi ni baadhi ya visa vilivyotokana na mvua hii ambayo wengi tulikuwa tukiiomba, hatukudhani kuwa itafikia watu wataanza kulalamika, kuwa imekuwa kero badala ya faraja. Hii ni hulka yetu binadamu, ikiwa jua tutataka baridi, na ikiwa baridi tutataka joto, vyote sio heri kwetu!
Nakumbuka niliwahi kutoa wazo kuwa vu vyema watu wautabiri wa hali ya hewa wakawa karibu na watu wa jiji, kuwatahadharisha kuwa sasa mvua zinakuja, kwahiyo, mitaro isafishwe na wale wanaoishi mabondeni wapewe taarifa rasmi, na iwe katika vyombo vya habari kama tahadhari rasmi, kuwa kila eneo linalotuama maji liwekwe vizuri ili mvua zikianza kusilete kizaazaa!
‘Wakifanya hivyo wengine watakula wapi?’ mmoja akasema na kuongezea kuwa mvua kama hizi wapo wameneemeka kwayo, kuna ambao wamefanya kazi ya kuwabeba wale waliotka kuvushwa kwenye maji machafu, hutaamini kuna kuvushwa kunakoitwa `chagua bega’ huyu anaombea mvua kama hizi ziendelee.
Vyovyote itakavyokuwa mvua kama hizi ziwe changamoto kwa jiji, na wahusika wa barabara, kwani kama mitaro ikijaa sio kero kwa wenye magari tu, ila hata sisi watembea kwa miguu, kwani magari yanashindwa kupita barabarani, kwasababu ya makorongo na kujaa maji, yanakimbilia njia ambazo sisi watembea kwa miguu ndio nafasi zetu.
Tuombee mvua za heri huku tukiimba Mvua njoo, katerina usije, na kwa wakulima mazao yawe ya heri kwani mvua za heri ni Baraka kwa kila mtu!
From miram3
No comments :
Post a Comment