Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Thursday, April 29, 2010

Uongozi ni dhamana

 Huyu jamaa nitamkata na panga, haiwezekani kabisa, yeye anaona mpaka wa shamba ndio huu, bado kaupita na zaidi kaingia mpaka eneo langu, huyu ni mwizi na dawa ya mwizi ni moja tu,kukatwa mkono..' jamaa akiwa na hasira huku anainua panga lake juu bila kujali mjumbe na jamaa waliofika kuamua ugomvi huo akawa anamsogelea mgomvi wake!
'Aaah, huko sasa unafika mbali, mimi sio mwizi, na huwezi kunikata mkono mimi, kama unataka vita sema tu, mimi naviweza sana, lakini namheshimu  sana mjumbe wetu, wewe wakati nauziwa hili eneo hukuwepo, wakumuuliza ni mjumbe aliyepita na huyo aliyeniuzia..' akasema jamaa ambaye alishachafuka kwa mchanga, nafikiri ni kutokana na mapigano waliyokuwa nayo na mhasimu wake.
 Tatizo lilikuwa mpaka wa eneo, jamaa hawa walifikia hatua ya kupigana, sababu ya eneo dogo tu. Mwanzoni kuikuwa na barabara iliyoachwa na wahusika wa pande mbili za viwanja. Mhusika wa kwanza akaamua kuuza eneo lake kwa kulikata vipande vipande. Waliouziwa wakawa hawatambui eneo lililoacha kwa ajili ya barabara. Ugomvi ukazuka, kwa yule ambaye aliendelea kulimiliki eneo lake, kwani waliouziwa hawakuishia kuingia eneo la barabara tu bali walienda hadi kuingilia eneo la yule ambaye hakupenda kuuza eneo lake.
 Mjumbe aliyeuza maeneo hayupo, fununu za kusikia zinasema kuwa alikimbia baada ya kuuzia watu maeneo mara mbili. Na huyo mjumbe ndiye aliyesimamia awali kuwa kila eneo liache mita kadhaa kwa ajili ya barabara, iweje baadaye akiuke utaratibu wa awali.
'Tunamtaka mjumbe wa awalii awepo hapo' akasema jamaa mmoja
'Utampata wapi naye kakimbia' akasema mwanamama mmoja
 Hali hii ilitokea kilele cha muungano, nami nikajaribu kutafakari mengi nikioanisha kadhia hii na muungano wetu. Nilioanisha nikijua kuwa uhusiano mwema huanzia kwa raia mmoja mmoja! Kama raia ambao ndio walengwa watakuwa hawaelewani, bado kutakuwa na kazi kubwa ya kujenga mahusiano. Na ili kuelewana inatakuwa kuwe na utaratibu uliokubalika, na kuwe na haki kwa pande zote. Utaratibu huo ueleweke, na uwe wazi kwa kila mtu, na kama haupo wazi basi kuwepo na tafsiri sahihi. Utaratibu mwem! Na sheria hii hulindwa na wale waliokabaidhiiwa dhamana kama viongozi. Swali linakuja kama hawa waliokabidhiwa dhamana watakuwa sio makini ni nini tunataraji kitokee!
 Wewe wasemaje

From miram3

No comments :