Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha
Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..
Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.
MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.
TUPO PAMOJA DAIMA
Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;
https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:
https://www.facebook.com/diaryyangu/
`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;
Saturday, April 24, 2010
Mwenzako akinyolewa wewe...
'Vipi ile kesi yenu iliishia wapi?' nikamuuliza
'Nayo kesi ile, mwanafunzi kampa mwanafunzi mwenzake mimba, sasa sisi wazazi tufanyeje, hiyoo ndio hoja ya muhimu, watu tunapelekana mahakamai utafikiri sio wazazi, kesi imerudishwa nyumbani!' akasema jamaa yangu. Katika maongezi yetu niligundua kuwa jamaa haikumuuma sana kwasababu mwanae ndiye aliyempa mtoto wa mwenzake mimba, na niligundua kuwa anakuwa sana upande wa mwanae na mara nyingi alikuwa akimlaumu huyo binti kuwa ni mhuni!
Kesi kama hizi zipo na nyingine hazifiki hata mahakamani, na mara nyingi anayeumia ni yule mwenye binti, kwani binti atafukuzwa shule, na nyie wazazi wa binti mtajutia gharama za kumsomesha, lakini mvulana anaendelea na masomo yake. Na hata wakikubaliana kuwa gharama zichangiwe bado yule mwenye binti anakuwa akibeba gharama nyingi zaidi.
Swala hapa linakuwa kwanini aumie mtoto wa kike zaidi? na Je tufanyeje ili kuweza kulikabili hili? Nhitaji mawazo kabla hatujatoa kisa kizuri kuhusiana na hili, kwani tukumbuke sote ni wazazi, mwenzako akinyolewa wewe tia maji
From miram3
No comments :
Post a Comment