Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, May 15, 2012

Tutafika kweli?


 Leo kanitembelea mjomba wangu, akanihadithia kisa kilichomtokea, nilicheka, …sikucheka kwasababu ya yaliyomtokea ila nikikumbuka mambo kamahayo yaliyowahi kunitokea hata mimi, mjini hapa hakuna mjinga kila mtu anaibiwa kinamna ambayo hakutegemea.


‘Sasa mjomba unanicheka nini,wakati uozo mnaufuga wenyewe, unafikiri hapa tutafanikiwa kweli, kama tupo kwenye mashindano ya makasia, na siri ya kushinda ni wote tupige makasia kwa pamoja, kwa mdundo mmoja, lakini sisi tunapiga makasia kila mtu kivyake, ndio maana mtumbwi wetu unayumba, hausongi mbele..’ mjomba akasimama, nikifikiri amekasirika anataka kuondoka, kumbe ndio anageuka mwalimu wa vitendo.

‘Unajua nilipofika pale Ubungo kituoni, umati wa watu na magari na vuruguvurugu za pale, nikafurahi nikisema hapa tupo wengi, kwahiyo usalama ni mkubwa, ni nani anaweza kuiba katika umati kama huu. Niliacha begi langu pale dukani, na muuzaji duka aliniona, akajifanya haniangalii, lakii nikasema, ilimradi kaniona, haijalishi, ngoja ninunue vocha duka la pili yake, kwasababu yeye haiuzi vocha. Niliporudi, begi langu halipo, nilipomuuliza akasema yeye hakuwa mwanagalizi wa begi langu, na aliona mtu analibeba, lakini alijua ni jamaa yangu.

‘Mzozo niliounzisha pale nilionekana mimi ni mshamba wakuja, watu badala ya kunisaidia wakawa wananicheka na kunizihaki kuwa nimeingizwa mjini.

 Haya, nikaingia kwenye daladala, fikiria ndani ya daladala tupo abiria wengi, na nje wapo watu wengi wanasubiri magari, wakati naongea na jamaa yangu kwenye simu kumhadithia yaliyotokea, nikawa nimetokeza kichwa nje, siunajua tena kelele ndani ya daladala sauti husikiki vyema. Niligutuka ghafla mtu kanigonga mkono, paaa! Simu haipo, natizama nje na gari hilooo linapamba moto kuondoka.

Kwa nje, nilimuona yule mwizi akiwa ameishikilia simu yangu anakatisha barabara, taratibu, hana wasiwasi, utafikiri simu yake,anakatisha kueleeka sehemu ya pili ya barabara, wapo watu waliopo nje,waliliona lile tukio lakini hawakujali wala kumshika huyo mwizi. Nilipiga kelele za mwizi , lakini sikupata msaada wowote, hata daladala nililopanda halikutaka hata kusimama…

‘Sasa mjomba, wingi wetu unasaidia nini? Kama hata wewe mjomba, ndugu yangu wa damu nakuhadithia unaishia kunicheka, je watu baki..itakuwaje’

‘Unajua mjomba, sio kwamba nakucheka, kukudhihaki, lakini matukio kama hayo yametukuta wengi, hayana ujanja, nacheka kutokana na kumbukumbu zinazonijia kichwani, niliwahi kuuziwa viatu, nilipofiak nyumbani nikakuta ni kipande cha sabuni,....na vitu kama hivyo, nikikumbuka na jinsi ulivyonihadithia ndio maana nacheka, siunajua tena, kumbukumbu kwetu ni jadi, na tunazifanya kama dhihaka, ili kujisahaulisha, licha ya kuwa inauma…’

‘Etii nin, unasemahakuna ujanja, !?, Katu, sikubaliani na hillo, Ni sisi wenyewe hatutaki kuliondoa hilo tatizo kwa umoja, nahisi kila mmoja anataka kupiga kasia kivyakevyake, kwa mpangilio wake, na nina wasiwasi kuwa chombo chetu hakiwezi kufika ufukweni salama…kama kila mtu atajali ubinafsi wake’ alikatishwa na kukatika kwa umeme.

Ndio, umeme maeneo yetu kila ikifika saa moja lazima ukatike, kurudi ni majaliwa!.....akaangali juu kwenye taa ta umeme na kucheka.

‘Haya ni yale yale,kitu muhimu kama umeme, ni kwa mgawo, tuna-dhamira ya kweli ya maendeleo, angalia barabara zenu mbovu, sikutegemea jiji kama hili kuna sehemu barabara mbovu kuliko hata kule kijijini kwetu, na hata maji ya shida, wote tunasema `sawa, bora liende…tutafika kweli?.

'Wakati nakuja tuliambiwa tulipe shilingi mia tano badala ya shilingi mia tatu, watu wanakubali kirahisi, mimi nikagoma kulipa, utashangaa badala ya watu kuniunga mkono wananiona eti nina njaa, na mmoja akajitolea kunikipia....ni ajabu kabisa,....haki yako unaiachia eti kwasababu unaogopa utaonekana una njaa,,,,nyie watu wa Dar niliona labda mumepambazukiwa lakini kumbe ni bure kabisa...'akasema na kutema mate chini.

'Mjomba ipo siku...kwasababu mabadiliko huanzia hivyo, leo shida ya usafiri, foleni, wizi ukizidi utakuta sasa wananchi wanachukua sheria mikononi mwao, kesho watageukiwa na hawo wezi waliopewa majukumu ya uongozi badala ya kutimiza majukumu yao wanahujumu kodi wa wavuja jasho,...vitu vinapanda bei,...umeme shida, kesho maji hakuna, mahospitalini hakuna dawa....unafikiri nini kitafuata baadaye. Binadamu sip punda bwana, inafika mahali anasema basi...liwalo na liwe....

'Haya tutaona....maana hayo niliyasikia nikiwa kijana na leo nimezeeka....hakuna mabadiliko,,labda ...labda,lakini niwaambia mabadiliko yanatakiwa kuanzia kutoka kwenu nyie wenyewe, kwanza shirikianeni,....saidianeni,....na msikubali kuvunja sheria ndogondogo, ...na hata akisimama kiongozi mbovu itakuwa rahisi kwenu kumuondoa,...lakini nyie wenyewe mumegawanyika,...hamtashinda.....hutatufika huko tuendapo...kamwe .'kasema mjomba

Nimeidondoa hii toka katika diary ya mwaka 2010

From emu-three

5 comments :

Anonymous said...

Jamani mi nimeingia kwa furaha nkijua kisa cha Jana kinaendelea anyway subra yavuta kheri,tuko pamoja kaka

emuthree said...

Kweli subira yavuta heri mpendwa, leo nilichelewa kufika ofisini, shida ya usafairi, ninapokaa ni magongo kuinamana mvua zikinyesha usafiri taabu,bei wanapandisha kiholela,ndio nikakumbukia hili tukio...na muda wa kukiandika hicho kisa ikawa sina,tuombe mungu kesho nikiwahi, tutakuwa pamoja.

Yaani huko ninapokaa ,sasa hivi barabara haitamaniki na mbunge hatumuoni...siunajua tena kila tatizo kwa mbunge. hapa nilipo najiuliza nitafikaje nyumbani...

samira said...

mungu yupo nawe dear ,sisi wafuatiliaji wako tupo na subra wewe ni binadamu .usijali cha muhimi kuomba mungu ufike nyumbani salama .maana mvua nasikia mpaka zanzibar ni nyingi.
kuhusu hao wabunge tusahau mpaka 2015 watatuhitaji tena haaa inatia uchungu
any way m3 mungu yupo nawe my dear
tupo pamoja

Yasinta Ngonyani said...

Nimekipenda hiki kisa kimenikumbusha mwaka jana nilipokuwa nyumbani hivyohivyo nauli ya daladala imepanda na baba yangu hakujua na wengine wakasema ww mzee nini lipa bwana ili tuondoka na baba yangu akasema silipi na mwisho akasema watu bwana kwa nini wanakubali tu kirahisi?

emuthree said...

Maisha ndivo yalivyo