Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, April 20, 2010

Hekima na Busara wapo wapi?



Siku ileusiku nilisitaajabu sana, kwani kawaida ya kuku zangu nikawafungulia usiku kwenda kwenye banda lao la kulala, hawaachani. Iweje leo kuku huyo ninayemsikia njea akilia kubaki peke yake. Nikatoka nje kumsikiliza huyo kuku anayelia, ili kuhakikisha kuwa ni wa kwangu au ni kuku wa mtu mwingine. Ajabu kila nilipomsogelea akawa anazidi kukimbilia kwenye vichaka vilivyopo jirani na nyumba ninamoishi.

Nilimfuatilia na kujikuta nimefika nyumba zilizopo mbali kidogo na kwangu. Na bahati mabaya akavuka ukuta wa michongoma na kuingia maeneo ya nyumba iliyozungukwa na michongoma hiyo, na majirani wa nyumba hiyo walipoona hilo tukio wakasema leo umeukwaa ugomvi, na kama hutaishia kwa mjumbe ni bahati. yangu.

Sikujali maneno yao, nikamfuatilia Yule kuku na kumkamata. Nilimuona kabisa anafanana na kuku wangu nikasema huenda yeye alisahaulika nje. Wakati naruka ule ukuta wa michongoma kurudi nilipotoka nikasikia sauti ya hasira ikiniambia;

‘Wewe unafikiri unafanya nini hapo’ sauti mbili ya kike na yakiume zikaniuliza.

‘Samahani, nilikuwa namkamata kuku wangu kanitoroka nyumbani..’ nikajaribu kujitetea lakini hawa jamaaa hawakunielewa, walisema sio hilo lililonileta hapo nina langu jambo.

‘Iweje kuku wako atoke kule kote hadi aje kwenye nyumba yetu, utatueleza vizuri.’ Aksema Yule mama kwa ukali.

‘Samahanini jamani, kwa kuingia kwenye maeneo yenu bila hodi, lakini kisa ni huyu kuku, kama ningesubiri kuwapigia hodi angezidi kupotea,mnafikiri mimi nina makusudio gani, kwani kuku ndio huyu hapa…’ nilijitetea, lakini ikawa ndo napalilia ugomvi.

Nilimuwaza babu yangu wakati ananieleza kisa cha marafiki wawili; hekima na busara, babu alisema;

‘ Hekima na busara ni marafiki sana, kiasi kwamba maneno aliyokuwa akiongea Chuki juu yao hayakuwaingia akilini. Kazi ya chuki ilikuwa kwenda kwa Busara kuzumgumza hili kuhusu busara na kurudi kwa hekima na kuzungumza vingine kumhusu Busara. Busara alipopata taarifa kuwa rafiki yake mkubwa ana mpango wa kumharibia ukaribu wake na rafiki yao Maisha,  ilimbidi amuite Tafakari na Subira, na wote walishangaa kuhusiana na kauli hiyo. Busara akasema ngoja tumuachie Subira uwanja huu kwani sasa hivi Hekima kasafiri.

Chuki akiwa na Furaha aliondoka kwenye uwanja wa nyumba ile, na Furaha akasema mimi naona ulichosema hakina ukweli, lakini sipendi marafiki zangu wanikose miyoni mwao, awe mzuri au mbaya. Chuki akasema hilo sio jukumu lako, wewe kazi yako ni kuwa karibu na kila mtu. Chuki alipofika nyumbani kwa fitina akamkuta Hekima anataka kuondoka, akajua kazi waliyopeana yeye na fitina inafanyiwa kazi.

Ni ukweli usiofichika kuwa hekima na busara wanayeyuka vichwani mwatu, itafika mahali tutauliza `hekima na busara wapo wapi? Hali tunayokwenda nayo ni ya kuchukiana na tupo tayari kusikiliza maneno ya fitina na uzushi kulika kutafakari na kuweka subira. Wapo watu wanatafuta uchochoro wa chuki zilizotanda miyoni mwao na kuhalisha matamanio ya hisia zao. Hutaamini kuwa kwenye jiji hili wapo wanaoamini mambo ya kishirikina. Nilipozozana na jirani huyu nikasikia kuwa hiyo ndio tabia yake, kila anayeingia maeneo yake, huishia kusingiziwa kama sio mwizi ni mchawi! Na cha ajabu familia hii inajiita imetakasika mbele ya mungu! Ok, labda kwasababu huwezi kumhukumu mtu, lakini kama unamtegemea mungu, hutaogopa uchawi, au sivyo jamani?

Je hatuwataki marafiki zetu wapenzi, hekima na busara? Au Chuki na fitina ndio wanaofaa katika maisha yetu ya kila siku?

From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Nakupa heko mkuu