Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, April 21, 2010

Taswira ya maisha na giza

Tulikuwa ndani ya chumba cha giza(dark-roam), humo kuna vitu vya ajabu, nilimuamini rafiki yangu kuwa kweli ameiva kwa utaalamu huo, usafishaji wa picha, utengenezaji wa filamu, na mambo kadhaa. Tukiwa tunasubiri jambo mara umeme ukakatika. Fikiria giza tulilolipata humo ndani, huwezi kuona chochote.
`Haya Tanesco wamefanya vitu vyao, siwezi kuamini kuwa tatizo hili litaisha, ngoja mipango ya generator yangu ikamilike nitaachana kabisa na huyu jamaa' akasema rafiki yangu, nami nilimuunga mkono.
Mara akainuka kuzima baadhi ya vifaa ili kama umeme ukirudi asije akapata hasara, kwani wakati mwingine umeme hurudi kwa nguvu kubwa na kuunguza vitu. Akiwa anafanya hivyo akasema jambo lililonipa mawazo kidogo.
'Unajua nimefanya kazi hii karibu miaka mitano, huko nyuma nilikuwa nimeajiriwa, na mmoja wa walimu wangu alinifundisha jambo. Ukiwa katika dark-roam, au sehemu yoyote ya giza, huhitaji kufungua macho yako. Fumba macho yako kwa usalama wake, kwasababu ukilazimisha kuona, baada ya muda utapofuka...' akasema huku anarudi kukaa kwenye meza yake.
'Hapo mimi sikuelewei, mimi najua baada ya muda ukiwa kwenye giza macho huona angalau kwa shida sasa wewe unasema ufumbe macho, hii hainiingii akilini' nikasema
'Hebu niambie muda wote uliokaa humu ndani umeshaweza kuona, unaona tu kwa hisia, na jinsi unavyojilazimisha kuangalia ndivyo unavyotumia nguvu za macho yako, na nakumabia ukiendela hivyo utaniambia' akasema nikawa natafakari, lakini nikasema ipo siku nitamuuliza dakitari kuhusiana na hili.
'Hata katika maisha yetu ya Kibongo, huhitajiki kutunia nguvu nyingi, kwasababu tupo katika dark-roam. Maisha yetu nayafananisha na kuishi kwenye giza nene. Unajua hali zetu ni duni hata kama utasema ujitume sana, utaishia kuzeeka kabla muda sio wako. Nilipokuwa katika ajira nilijifunza mengi. Wewe unafanya kazi masaa nane hadi tisa mshahara ni ule ule, uwe umefanya kazi kwa bidiii au umelala, ni kweli  au si kweli?' akaniuliza swali rafiki yangu na kabla sijamjibu akasema
'Kwahiyo hali hii ya giza tuliyo nayo hapa ndani ni sawa na maisha ya kibongo. Ukifumba macho au ukifumbua haina tofauti. Umtumikie bwana wako mkubwa kwa bidii au ufanye kwa kawaida mshahara ni uleule, faida ni kwake. Ni heri ufumbe macho ili uwekeze nguvu za macho yako kwa baadaye kuliko kufumbua, na hali kadhalika, ni heri ukiwa katika ajira usijitume sana na uwekeze nguvu zako katika kujiajiri kwasababu ukifanya kazi kwa bidii, bwana mkubwa ataishia kukusifu, lakini mwili na taswira yako vinakwisha mwisho wa siku umezeeka huna kitu, lakini kama uliweza kuwekeza nguvu zako za baadaye katika kujiajiri ungekuwa huna wasiwasi.
 Niliwaza hadi umeme uliporudi bila kumuulewa huyu jamaa analenga nini hasa!
 Je wewe mwenzangu ukiwa kwenye giza unafumba macho au unafumbua?  Je umemuelewa huyu jamaa?
From miram3

No comments :