Tuendelee na mama wa kambo ambaye alishaamua kulala ukumbini, lakini tuliona sio jambo jema. Pia ukumbuke kuwa kinafsi nilishaingiwa na huruma, na kutaka kumruhusu aingie alale ndani na mengine tumuachie Mungu. Isingekuwa busara za mama watoto, Na kisa cha msamaria mwema ambacho ni fundisho kwetu sote, niilishamua vinginevyo. Mama watoto akacheza karata yake, na kumuinamia Yule mama yetu ambaye ni mama wa kambo wa jirani yangu.
‘Naomba utusikilize mama yetu, naomba utuonee huruma na sisi, unaona jinsi mwanao alivyotutega, kasema tuamue wenyewe kukulaza hapa kwetu au tukufukuze na yeye hahusiki na lolote lile. Hatuaombei mabaya, lakini kuna leo na kesho, ni vyema tuakajihami kibinadamu. Sisi tulikuwa na nia njema kabisa, kuwa twende kwa mjumbe huko atatupa kibali cha kisheria cha kukulaza humu ndani kwetu, ili huyu mtoto wako asije akatugeuka. Na isitoshe inaweza ikakusaidia na wewe, kuweka ushahidi kuwa mwanao kakufukuza’.
Yule mama akatingisha kichwa, sikumuelewa mwanzoni alikuwa na maana ya kukubali au kukataa, ila kauli yake ikadhihirisha ukweli akasema;
‘Mimi nakubaliana na nyie kuwa twende huko lakini sio kwa mimi kwenda kulala, ila tupate hicho kibali mnachokitaka, sielewi kwanini inafikia hatua hiyo. Mimi kulala kwa leo tu iwe namasharti kiasi hicho, jamani huu ndio ubinadamu wa mji huu. Mbona mji huu kila kukicha kuna vituko. Kama ingekuwa huko kwetu mgani akija hukaribishwa , hula na hupewa kitanda, nah ii ni Baraka, lakini…haya’’ akasema Yule mama huku akisita kuamuka pale aliposimama.
Mimi kichwani nilikuwa na mengi ya hayo, niliomba ikiwezekana tukifika kwa mjumbe, mjumbe amlazimishe alale huko, kwasababu kisa cha msamaria mwema kilishanikaa kichwani na matokeo yake yalianza kunipa fundisho. Hebu tuendelee nacho huenda na wewe ukaliona hilo fundisho:-
Mjumbe alipangusa macho yake, na kuchunguza mwanzo wa kitanda hadi mwisho kwa macho yake yake, na alipohakikisha kuwa anachokiaona ndio sahihi akamgeukia mwenzake, ambaye kwa muda huo aliyekuwa karibu yake ni Yule nesi, mhudumu wa huduma ya kwanza ya eneo lake. Alitaka kumuuliza kitu lakini akasita, akaona yeye sio sahihi yake, akageuka nyuma, na kukutana na macho ya watu waliokuwa wakihakiki kile walichokiona. Aliwapa muda ili wasije wakasema kinyume na ushahidi. Halafu akapanua mdomo wake na kusema
‘Mwenye nyumba hebu sogea huku na mkuu wa usalama nawe usogee hapa, na pia msaidizi wangu nawe nakuomba. Hii sasa ni utata, hebu mwenye nyumba ongea ilikuwaje kabla hatujatoka humu.
‘Mjumbe nilichosema ni hichohicho, nilitoka mapema na kumuacha mke wangu, huku nikimuagiza kuwa amuamushe mgeni wetu, siunajua tena akina mama, wanahitaji muda wa maandalizi na hivyo ndivyonilivyoongea na mwenzangu, sasa sijui kilichotokea huku nyuma, au kilichotokea usiku…’
‘Sawa nimekuelewa, hebu mama mwenye nyumba tueleze ilikuwake ulipoachiwa hayo maagizo, ulipogonga mlango ilikuwaje, ulisikia sauti, ulienda wapi baada ya hapo alikuwa ulikuwa hapo mlangoni muda wote?’ akauliza mjumbe.
‘Mimi niligonga mara nyingi bila jibu, nikaamua niache kidogo, huenda mwenzangu alikuwa akijiweka vizuri. Nilioona kimya nikarejea tena kugonga, lakini kulikuwa kimya. Mwishowe nilimpigia simu mume wangu ili anipe ushauri, ndio aksema nisubiri mnakuja’ aksema Yule mama
‘Je hukujaribu kuufungua kwa kuzungusha kitasa, au kuusukuma?’ akauliza mjumba
‘Hapana, sikujaribu hivyo, kwasababu mlango huu tunaujua, kama ukiufungua, unakwenda moja kwa moja, na kwahiyo kama mgeni alikuwa kaamuka, na hajajiandaa itakuwa ni karaha kwake, sikufungua kitasa wala kuusukuma’ akasema Yule mama.
Mjumbe alikuna kichwa na kumgeukia msaidizi wkusikia kama ana cha kuuliza. Msaidizi wake akasema hana, lakini baadaye akasema;
‘Mimi naona kiusalama tukawahoji vizuri wahusika, sio mbele ya kadamnasi, na kila watakachoongea kiwe kwenye maandishi kwani ushahidi wa wazi tumeuona, lakini hatujui nini kilitokea, mapaka ikawa hivi’ Mumbe akakubali kwa kichwa.
Mjumbe alitoa amri kuwa Yule fundi wa mlango aurudishie vizuri, na kuhakikisha kuwa mlango na chumba hicho hakitumiki, ili ushahidi usiharibiwe. Na kwa muda huo wazo la kumpigia mjomba wake likamjia kichwani, lakini akaona ngoja kwanza watimize wajibu wao kama viongozi. Akapitia kwa macho kuhakikisha kweli kile chumba hakina zaidi ya hicho walichoona, na kusogea nje. Na hapo nje alihakikisha Yule fundi anauruidishia ule mlango vizuri na kukabidhiwa ufunguo.
Haya vipi tena, Oooh, muda umekwisha, tuonane baadaye
From miram3
1 comment :
Halloh, mbona inachelewa kutoka, manake ni movie ya Kinageria. Au Chase....keep it up
Post a Comment