Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, March 10, 2010

mama wa kambo-5

                                          Na kisa cha msamaria mwema

Kabla ya kusoma hii rejea sehemu iliyopita.

Au anza mwanzo wa kisa hiki, mama wa kambo

  Wakati kisa hiki cha msamaria mwema kikiendelea kichwani, huyu mama yetu mgeni alishaamua kuondoka, huku akilalamika kuwa hatuna huruma, na mimi huruma zilinishika, ikabidi nimuulize mwenzangu kuwa tulichofanya ni sawa. Kabla hajanijibu nikawa nimeshainuka pale nilipokuwa nimekaa, na kufuatilia njia aliyoondokea yule mama. Tulipofika eneo la kibaraza cha nje ya nyumba yangu tukasikia mtu akiguna na kutoa sauti ya kama mtu anayelia. Kulikuwa na giza kwahiyo ilikuwa sio rahisi kuona vyema.


Kumbe Yule mama kama alivyosema kuwa talala ukumbini au hata chooni, hakuwa ameondoka na alikuwa kakusudia kulala pale kwenye kibaraza cha nje, tulimkuta akiwa kajiinamia huku analia. Mama nanihii akamuinamia kumbembeleza huku akijaribu kumuelezea kwanini sisi tumeamua kuwa hili swala lipelekwe kwa mjumbe kwanza.

‘Swala la kwenda kulala kwa mjumbe siliafiki kwani mimi ningetaka siningeenda huko. Halafu niende kwa mjumbe kwani nimeiba, nyie nendeni mkalale , mimi nitajisitiri hapa barazani hadi asubuhi..’ alisema Yule mama. Mimi niliona bado hilo sio suluhisho, hapa barazani kuna usalama gani, na pia ni maeneo ya nyumba yangu likitokea tatizo nitawajibika mimi.Akilini nikafikiria kumruhusu aingie ndani alale, tumuachie mungu, lakini kile kisa cha msamaria mwema kilivyonijia kichwani nikasita. hebu tuendelee pale tulipoachia.

Mjumbe alimuacha Yule jamaa, nakumsihi amsubiri hapo nje. Na alipofika varandani na kukikabili kile chumba ambacho mlango ulishafungulia kitasa, kilichobaki ni kuusukuma ufunguke pawe wai, ili kuonekane ndani, na kuona kilichomo. Mjumba akasita kwanza , ikabidi aiite kamati yake ya ulinzi, na msaidizi wake pamoja na dakitari wa huduma ya kwanza. Ilibidi kwanza awape somo, kuwa hakuhitajiki kushikashika vitu ovyo, na kama inawezekana kila mtu afunge mkono wake.

‘Mjumbe vipi wewe, mbona una wasiwasi sana, kwanza unapoteza muda, huenda huyo mtu kazidiwa anahitaji msaada na jinsi tunavyochelewa kuingia humo ndani , ndivyo tunavyohatarisha maisha ya huyo mgeni, tunaweza kumkuta kafa, kwasababu ya uzembe wetu, hayo ya vitambaa, sijui nini, ni kazi ya polisi, sisi tuwahi tumuoke huyo mtu…’ akasema mmoja wa jamaa aliyekuwepo pembeni.

‘Sawa, lakini lazima tuwe na tahadhari zote kwanza’ akasem mjumbe huku akiusukuma mlango ili ufunguke. Na kabla mlango haujafunguka simu ikaita. Na alaiyepiga hiyo simu ni mjomba mtu alitaka kujua nini kinaendelea.

‘Ndio Mjomba sema,…ndio mlango umefunguka, sasa tunataka kuingia, nahisi ukimya wa ajabu…ngoja tufungue tuangalie’ akasema mjumbe

‘Hakikisheni hamshikishiki vitu ovyo, na kama mnahisi kuna tatizo ngoja sie tuje kwanza; akasema mjomba-polisi.

‘Hapana, subiri tuhakikishe, nitakuarifu kama kuna tatizo’ akasema na kukata simu.

‘Haya nasukuma mlango, na naomba nesi achungulie kwanza kama huyo mtu yupo safi, tusije kumkuta yupo uchi, na narudia mtu asishike kitu na msiwe na papara ya kuingia. Nitaingia kwanza mwenyewe na mtu wa huduma ya kwanza, nyie wengine msubiri hapo varandani’ akasema huku akiusukuma mlango ambao ulikuwa ukigoma-goma. Na punde ukafunguka…

Mlango ule ulijifungua wote kiasi kwamba kila aliyekuwepo kwenye kivaranda kile aliweza kuona kila kitu kilichopo ndani, haikuwezekana kuuzua jinsi ulivyojifungua wote ha kugonga ukutani. Na kile aliyekuwepo hapo varandani alishikwa na hamu ya kuona ni nani na yupoje huyo mgeni, kwahiyo watu wakajisogeza karibu na mlango, kinyume na amri ya mjumbe!

Ndani ya kile chumba, kulikuwa na meza ya chai, stuli ndogo nne, na pembeni kulikuwa na kabati kubwa la nguo, lilotoka upende wa chumba hadi upande mwingine. Lakini wote waliokuwemo humo hawakutaka kuangali vitu vingine vilivyokuwemo humo ndani, zaidi ya yote mawazo yao yalikuwa kwenye kitanda.

Kitanda kilikuwa kikubwa cha futi tano kwa sita, na chandarua kubwa iliyotundikwa na kuninginia toka darini ilikuwa imeshushwa upande mmoja, wa dirishani, ila upande wa huku, kunakotazamana na mlango, kulikuwa kumefuniliwa, na kuachwa wazi , na hii iliwasaidia watu kuona vyema ni nani aliyelala humo kitandani.

Kila mtu ilibidi apikiche macho yake kuhakikisha kuwa wanachokiona ni sawa au ni ndoto. Hata mjumbe ilibidi agune, na wengine yaliwatoka pima macho yao kuangalia na kupepesa-pepesa huku yakizunguka kama gololi kutoka mwanzo wa kitanda hadi mwisho wake. Na wakati wanahakiki walichoona, mara ikasikika vurugu toka nje , ilikuwa vurugu ya walinzi wakijaribu kumzuia Yule mume mtu aliyetaka kuingia ndani ili aonane namjumbe, kwani alikuwa akichelewa kwenye shughuli zake.

‘Mjumbe mbona mnaniwekea kiwingu, mimi nina mishemishe zangu, na isitoshe mama watoto wangu sijawasiliana naye aliondoka usiku sasa mnanichelewesha bwana, kwani kuna nini cha ziada humu ndani…akasema Yule mume mtu akiwa keshapenya na yupo karibu na mjumbe, naye akabakia mdomo wazi akijaribu kupangusha macho yake ili aone vizuri wanachoangalia wenzao!

Je kulikoni?
From miram3

1 comment :

Anonymous said...

Mhh hii ni movie au kwa waliosoma Chase, jamaa anajaribu kuwa Hadley chase.Hongera let we see another chapter