Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, July 25, 2017

DUWA LA KUKU...20


 Mimi nilikuwa nyuma nyuma nikimuangalia huyu mtu kwa mbali, taratibu akawa anatembea, na sasa akawa usawa wangu, na mimi nilikuwa nimesimama, nia nimuone vizuri,…kiukweli ukiingia wodini, ukaona wagonjwa, hasa wenye hali mbaya, moyo wangu unasawajika, huruma inakujaa, kibinadamu. Lakini kila hatu, kila muda, nilipokuwa namuangali amutu huyu na kuvuta hisia zangu kwa yaliyonitokea, hasira zilianza kunijaa!
Kiukweli, sikuweza kuvumilia…

Tuendelee na kisa chetu

************

Aliponikaribia ina maana alikuwa sasa ananiangalia mimi moja kwa moja, akanitupia jicho, na macho yetu yakakutana, na muda huo ndio hasira zinaanza kunijaa, akanipita, kile kitendo cha kuniangalia na kutabasamu tabasamu la dharau kilitafsiriwa akilini mwangu vingine.

Nilijua dharau ile ni kuwa keshanizalilisha, kwahiyo sina maana tena kwake, na kile kitendo cha kuniona na kushtuka, ina maana alishaniona kabla, kwahiyo ni kweli, pale sikuweza kuvumilia zaidi,… sijui ilikuwaje, nilihisi hasira, nilihisi huyo ndiye mbaya wangu, adui yangu mkubwa, na hapo alipo anajiona yeye ni mjanja, hapana, sikubali , nikasahau usia wa mama yangu…nikasonga mbele kwani alihsnipa mgongo..

Nikavuta hatua, na kumpita mama mfadhili wangu wa kwanza, ..nikachomoka kwa hasira kutaka kumvaa, na aliyeniwahi alikuwa huyo mama , sijui alijuaje na sijui alivyoweza kunidaka kwa haraka kiasi hicho, akanishikilia kama mtu aliyedaka mpira,..na hili tendo halikuonekana na wengine maana sisi tulikuwa nyuma.

Mimi pale  nilihisi mwili ukitetemeka, nataka kujitoa kwa huyo mama, huku mwili unanitetemeka kwa hasira,lakini huyo mama hakuniachia,...wale akina mama wawili walikuwa mbele walihisi nyuma kuna purukushani, wakageuka na kuona nimeshikiliwa, na mmoja akauliza;

‘Vipi huko, mbona hivyo..?’ akauliza

‘Naona huyu binti anajisikia vibaya…’akasema huyo mama mfadhili.

‘Mhh, kama hataweza kuvumilia,hali ya humu ndani bora akakae nje tukimuhitaji, tutamuita…’akasema mama mwingine.

Huyu mama aliyenishika, sasa akaniangalia machoni na kusema;

‘Hivi wewe unataka kufanya nini, hujui utatuharibia, kama huwezi kuvumilia kakae nje, mimi mwenyewe hapa nina hasira naye, lakini hatuendi hivyo, tutafukuzwa na kilichotuleta tusikipate…’akasema na mimi nikatulia, lakini bado nilihisi damu ikichemka, na baadae nikaanza kulia, huku natembea, huku namuwaza mama yangu, …angelikuwawepo, usiombe kumkosa mama…!

Tuliingia kwenye kile chumba, ni chumba cha huyo docta, yeye alijitolea tukitumie chumba chake kwa muda.., naona huyo mama aliyeongea, wanafahamiana, au mumewe anajulikana sana hapo..au kuna jinsi alivyofanya kumshawishi huyo docta, hakuna aliyelijua hilo kwa muda huo.
Baadae docta akasema;

‘Sasa mimi nawaacheni humu na mtu wenu, jaribu kupunguza sauti, na sizani kama kuna tatizo la kutokuelewa.., sawa, haya ongeeni, mkijali muda...’akasema docta.

‘Docta usiwe na wasiwasi, sisi ni ndugu zake nia ni kutaka kumsaidia …’akasema yule mama aliyenipeleka hospitalini.

‘Sawa itakwua ni vyema, …’akasema akaanza kuondoka, lakini mama mwingine akauliza swali kabla huyo docta hajatoka nje

‘Docta lakini samahani tukuulize tatizo la huyu jamaa ni nini hasa..?’ mmoja akauliza

‘Hayo ni siri ya mgonjwa na docta, na mtu wake wa karibu, kama ni lazima, na huyo mtu atatuambia yeye mwenyewe mgonjwa kuwa huyu ndiye mtu wangu wa karibu, lakini kwa vile yeye mwenyewe anajielewa, haina haja, sisi hatuwezi kuliongelea hili tatizo lake hapa…’akasema docta.

‘Sawa docta ngoja tuongee naye kwanza…’akasema na docta akaondoka.

Alipoondoka tu, yule mama mwenye nyumba wa mdada akaanza kwa jaziba…

‘Sikiliza wewe sijui tukuiteje, mchawi, …unajua kama tungelikuwa sehemu nyingine unegliona kuwa mimi ni nani,..nisingelijali cheo cha mume wangu…’akasema hivyo akimuangalia huyo mgonjwa kwa uso uliojaa hasira, mama  mdhamini wangu wa kwanza, akamshika begani huyo mwenzake, na kusema;

‘Subiri, niongee naye mimi…’ na hapo akasogea mbele akawa sasa anaangaliana na huyo mgonjwa uso kwa uso, akasema;

‘Ndugu, sisi ni wanadamu kama wewe, tuna hisia kama wewe, na tuna familia, hatujui wewe kama unayo, lakini kama unayo au huna wewe jaribu kujiweka kama mzazi, hawa mabinti wawili kwanza ni yatima pili walikuwa katika mazingira magumu, wanahitajia huruma za kibinadamu, sasa iweje wewe ufanyie hivyo, umekosa wanawake mitaani mpaka uwazalilishe hawa eeh..’ akaanza hivyo.

‘Ni nani kasema mimi nimewazalilisha hawa mabinti..?’ akauliza kwa jeuri fulani.

‘Kwahiyo hayo uliyomuambia mdada,… huyu,  ambaye anatokea huko kijijini kwenu sio kweli…?’akaulizwa

‘Yawezekana sio kweli..nyie mnasikiliza maneno ya mtu mmoja mmoja…, hiyo sio sahihi, watu wananisingizia ubaya. Niwaambie kitu, kama wao, hao watu wanaosema hivyo ni kweli basi, walete huo ushahidi wao. ‘akasema na hao akina mama wakaangaliana wakikonyezana.

‘Unajua niwaambie kitu....mimi nilitaka kuwasaidia nyie kama nilivyomsaidia huyo mdada, …maana mambo kama hayo mimi nayafahamu,…sio kwamba nataka kuwatapeli, hapana,… kama mtu kawekezewa mabaya, nina utaalamu huo …’akasema.

‘Utaalamu gani hasa..?’akaulizwa

‘Utaalamu wa kuondoa mazindiko ya uchawi…’akasema, na hao akina mama wakaangaliana tena.

‘Umejuaje kuwa sisi tumewekewa hayo mazindiko ya kichawi?’ akulizwa.

‘Kuna namna ya kuangalia mambo kama hayo…, ukipewa karama kama zangu, maana mimi nina kipaji hicho, cha kurithi, mimi naweza kukuangalia hivi nikasema wewe umelogwa, na dawa yake ni hii na hii…’akasema.

‘Kwahiyo ulipomuangalia huyo binti uliona kuwa kalogwa..?’ akaulizwa.

‘Kama alivyosema docta…, mambo mengine ni kati ya mgonjwa na mtaalamu wake, mimi siwezi kuyasema hayo, kuwa tuliongea nini na mgonjwa watu, hasa hapa mbele ya watu..niliongea naye huyo binti kwa siri tukiwa ofisini kwangu, ….’akasema.

‘Wao wanataka uyasema..ndio maana tumekuja nao, eti mabinti…muambieni…’akaambiwa, lakini kabla hao mabinti hawajasema kitu, huyo jamaa akasema;

‘Nyie mnaweza kuwalazimisha hivyo, kwa vile nyie ni mabosi wao, lakini kitaaluma yetu haturuhusiwi kuyasema hayo, ninachoweza kusema ni kuwa kwenye majumba yenu, kuna mazindiko mabaya, yanatakiwa kutolewa la sivyo, kunaweza kutokea mabaya zaidi,..sasa kwa vipi, na yapi, siwezi kusema mpaka tuingie kwenye makubaliano, mjini hapa, hakuna-cha-bure…’akasema akisisitiza kwa mkono na kichwa.

‘Unamfahamu huyu binti..?’ akaulizwa akionyeshewa mdada.

‘Ndio namfahamu nilikuja hata sehemu anayopofanyia kazi, tukaongea naye, na kabla ya hapo nilishawahi kuonana naye huko kijijini, hilo halina siri…’akasema.

‘Na yule..?’ akaulizwa na hapo akanigeukia na kunikagua kwa macho, halafu akabenua mdomo na kusema;
‘Mhhh, hiyo sura sio ngeni kwangu…, nahisi kama nilimuona mahali…’akasema

‘Wapi labda…?’ akaulizwa

‘Siwezi kujua,…nahisi hivyo tu…’akasema

‘Je yeye unaweza kumuangalia hivyo ukaona ana tatizo lolote…?’ akaulizwa , kwanza akanikagua tena, halafu akatabasamu na kusema;

‘Ama kwa kutaka kuonyesha promosheni, huyu mdada kwa jinsi nilivyomuangalia bila y akuwaita watu wangu..ana tatizo…’akasema

‘Watu wako..?’ akaulizwa

‘Yah, mizimu…’akasema

‘Ni hivi,…huyu mdada ana tatizo, tena tatizo kubwa, asipolifanyia kazi kwa haraka ..hata hivyo inavyoonyesha ameshachelewa, lakini hakuna kinachoshindikina , nikiongea na mizimu, wanaweza kunisaidia, tukapata njia mbadala, ni wao lakini wanaweza kusema hivyo…’akasema

‘Unaongea nao kwa vipi…?’ akaulizwa

‘Napandisha mambo yetu…nakuwa kama sio mimi..ukifika ofisini kwangu utaona…’akasema

‘Lakini niwaambie kitu kimoja, mambo haya yanahitajia imani hata huyu mdada, kama atanitaka mimi, nitaweza kumsaidia lakini iwe kwa haraka sana…hapo alipo ana kitu tumboni, na akienda hospitalini wakampima, watasema ana uja uzito,  lakini kiukweli sio mimba ya kawaida,..unabisha, kama umepima hujaambiwa una mimba..?’ akasema akinikagua mimi sehemu ya tumboni.

‘Nabisha..kwanza umesema mpaka uwaulize watu wako sijui, sasa hivi unaongea hivyo hata hujafanya hivyo, kuonyesha kuwa unalijua hilo kabla….au ni wewe unahusika nalo....’mimi nikasema kwa hasira.

‘Kama unabisha tumuite docta akupime tuone kama hawatasema wewe una ujauzito, ndio nilishaliangalia tatizo lako nilipokutana na huyu mwenzako,…siwezi kuficha hilo, alitaka kukusaidia, na ndipo nikakutizamia, unielewe hapo…’akasema.

‘Ujauzito wa nani…?’ nikamuuliza kwa hasira, na hapo akacheka kidogo, na kusema;
Unataka nikutajia huo uja uzito ni wa nani, upo tayari kwa hilo…?’ akauliza

‘Nipo tayari ndio..wewe si unamfahamu…’akasema

‘Hahaha, unajua huyu bado mdogo…hajui, haya mambo, anahisi natania, eti jamani huyu anataka nimtajia ni nani aliyempa huo ujauzito, lakini kumbukeni nilichowaambia awali..mimba hiyo sio ya kawaida, sasa iliingiaje, ndio anataka kujua,….sikiliza…’akatulia akawa anatikisa tikisa kichwa kwa muda..

Inaendelea……


WAZO LA LEO: Mambo ya shiriki yamegubikwa na uwongo mwingi…, asilimia kubwa ya watu hawa, hawaogopi kusema uwongo, hawaogopi kuzua jambo kwa ajili ya kufarakanisha watu wengine, bila kujali athari zake kwenye jamii, na dunia ya sasa watu kama hawa wapo wengi sana, wanawafarakanisha ndugu, jamaa, mataifa, nk..lengo lao ni kujenga chuki ili waweze kuweka hatamu zao za kishetani, tuweni makini sana, dunia ya leo sio ya jana, ulimi huu unaweza ukawa silaha ya kufanikisha malengo ya shetani,…Na tujiulize hatima ya haya yote ni nini basi,..vyovyote iwavyo, marejeo yetu ni kwa muumba wetu yule asiyedanganyika,, sasa kwanini tunayafanya haya…
Ni mimi: emu-three

No comments :