Mimi nilikuwa nyuma nyuma nikimuangalia huyu
mtu kwa mbali, taratibu akawa anatembea, na sasa akawa usawa wangu, na mimi
nilikuwa nimesimama, nia nimuone vizuri,…kiukweli ukiingia wodini, ukaona
wagonjwa, hasa wenye hali mbaya, moyo wangu unasawajika, huruma inakujaa, kibinadamu.
Lakini kila hatu, kila muda, nilipokuwa namuangali amutu huyu na kuvuta hisia
zangu kwa yaliyonitokea, hasira zilianza kunijaa!
Kiukweli,
sikuweza kuvumilia…
Tuendelee
na kisa chetu
************
Aliponikaribia
ina maana alikuwa sasa ananiangalia mimi moja kwa moja, akanitupia jicho, na
macho yetu yakakutana, na muda huo ndio hasira zinaanza kunijaa, akanipita,
kile kitendo cha kuniangalia na kutabasamu tabasamu la dharau kilitafsiriwa
akilini mwangu vingine.
Nilijua
dharau ile ni kuwa keshanizalilisha, kwahiyo sina maana tena kwake, na kile
kitendo cha kuniona na kushtuka, ina maana alishaniona kabla, kwahiyo ni kweli,
pale sikuweza kuvumilia zaidi,… sijui ilikuwaje, nilihisi hasira, nilihisi huyo
ndiye mbaya wangu, adui yangu mkubwa, na hapo alipo anajiona yeye ni mjanja,
hapana, sikubali , nikasahau usia wa mama yangu…nikasonga mbele kwani alihsnipa
mgongo..
Nikavuta
hatua, na kumpita mama mfadhili wangu wa kwanza, ..nikachomoka kwa hasira
kutaka kumvaa, na aliyeniwahi alikuwa huyo mama , sijui alijuaje na sijui
alivyoweza kunidaka kwa haraka kiasi hicho, akanishikilia kama mtu aliyedaka
mpira,..na hili tendo halikuonekana na wengine maana sisi tulikuwa nyuma.
Mimi
pale nilihisi mwili ukitetemeka, nataka
kujitoa kwa huyo mama, huku mwili unanitetemeka kwa hasira,lakini huyo mama
hakuniachia,...wale akina mama wawili walikuwa mbele walihisi nyuma kuna
purukushani, wakageuka na kuona nimeshikiliwa, na mmoja akauliza;
‘Vipi
huko, mbona hivyo..?’ akauliza
‘Naona
huyu binti anajisikia vibaya…’akasema huyo mama mfadhili.
‘Mhh,
kama hataweza kuvumilia,hali ya humu ndani bora akakae nje tukimuhitaji,
tutamuita…’akasema mama mwingine.
Huyu
mama aliyenishika, sasa akaniangalia machoni na kusema;
‘Hivi
wewe unataka kufanya nini, hujui utatuharibia, kama huwezi kuvumilia kakae nje,
mimi mwenyewe hapa nina hasira naye, lakini hatuendi hivyo, tutafukuzwa na
kilichotuleta tusikipate…’akasema na mimi nikatulia, lakini bado nilihisi damu
ikichemka, na baadae nikaanza kulia, huku natembea, huku namuwaza mama yangu, …angelikuwawepo,
usiombe kumkosa mama…!
Tuliingia
kwenye kile chumba, ni chumba cha huyo docta, yeye alijitolea tukitumie chumba
chake kwa muda.., naona huyo mama aliyeongea, wanafahamiana, au mumewe
anajulikana sana hapo..au kuna jinsi alivyofanya kumshawishi huyo docta, hakuna
aliyelijua hilo kwa muda huo.
Baadae
docta akasema;
‘Sasa mimi
nawaacheni humu na mtu wenu, jaribu kupunguza sauti, na sizani kama kuna tatizo
la kutokuelewa.., sawa, haya ongeeni, mkijali muda...’akasema docta.
‘Docta
usiwe na wasiwasi, sisi ni ndugu zake nia ni kutaka kumsaidia …’akasema yule
mama aliyenipeleka hospitalini.
‘Sawa
itakwua ni vyema, …’akasema akaanza kuondoka, lakini mama mwingine akauliza
swali kabla huyo docta hajatoka nje
‘Docta
lakini samahani tukuulize tatizo la huyu jamaa ni nini hasa..?’ mmoja akauliza
‘Hayo
ni siri ya mgonjwa na docta, na mtu wake wa karibu, kama ni lazima, na huyo mtu
atatuambia yeye mwenyewe mgonjwa kuwa huyu ndiye mtu wangu wa karibu, lakini
kwa vile yeye mwenyewe anajielewa, haina haja, sisi hatuwezi kuliongelea hili tatizo
lake hapa…’akasema docta.
‘Sawa
docta ngoja tuongee naye kwanza…’akasema na docta akaondoka.
Alipoondoka
tu, yule mama mwenye nyumba wa mdada akaanza kwa jaziba…
‘Sikiliza
wewe sijui tukuiteje, mchawi, …unajua kama tungelikuwa sehemu nyingine
unegliona kuwa mimi ni nani,..nisingelijali cheo cha mume wangu…’akasema hivyo
akimuangalia huyo mgonjwa kwa uso uliojaa hasira, mama mdhamini wangu wa kwanza, akamshika begani huyo
mwenzake, na kusema;
‘Subiri,
niongee naye mimi…’ na hapo akasogea mbele akawa sasa anaangaliana na huyo
mgonjwa uso kwa uso, akasema;
‘Ndugu,
sisi ni wanadamu kama wewe, tuna hisia kama wewe, na tuna familia, hatujui wewe
kama unayo, lakini kama unayo au huna wewe jaribu kujiweka kama mzazi, hawa
mabinti wawili kwanza ni yatima pili walikuwa katika mazingira magumu,
wanahitajia huruma za kibinadamu, sasa iweje wewe ufanyie hivyo, umekosa
wanawake mitaani mpaka uwazalilishe hawa eeh..’ akaanza hivyo.
‘Ni
nani kasema mimi nimewazalilisha hawa mabinti..?’ akauliza kwa jeuri fulani.
‘Kwahiyo
hayo uliyomuambia mdada,… huyu, ambaye
anatokea huko kijijini kwenu sio kweli…?’akaulizwa
‘Yawezekana
sio kweli..nyie mnasikiliza maneno ya mtu mmoja mmoja…, hiyo sio sahihi, watu
wananisingizia ubaya. Niwaambie kitu, kama wao, hao watu wanaosema hivyo ni
kweli basi, walete huo ushahidi wao. ‘akasema na hao akina mama wakaangaliana
wakikonyezana.
‘Unajua
niwaambie kitu....mimi nilitaka kuwasaidia nyie kama nilivyomsaidia huyo mdada,
…maana mambo kama hayo mimi nayafahamu,…sio kwamba nataka kuwatapeli, hapana,…
kama mtu kawekezewa mabaya, nina utaalamu huo …’akasema.
‘Utaalamu
gani hasa..?’akaulizwa
‘Utaalamu
wa kuondoa mazindiko ya uchawi…’akasema, na hao akina mama wakaangaliana tena.
‘Umejuaje
kuwa sisi tumewekewa hayo mazindiko ya kichawi?’ akulizwa.
‘Kuna
namna ya kuangalia mambo kama hayo…, ukipewa karama kama zangu, maana mimi nina
kipaji hicho, cha kurithi, mimi naweza kukuangalia hivi nikasema wewe umelogwa,
na dawa yake ni hii na hii…’akasema.
‘Kwahiyo
ulipomuangalia huyo binti uliona kuwa kalogwa..?’ akaulizwa.
‘Kama
alivyosema docta…, mambo mengine ni kati ya mgonjwa na mtaalamu wake, mimi
siwezi kuyasema hayo, kuwa tuliongea nini na mgonjwa watu, hasa hapa mbele ya
watu..niliongea naye huyo binti kwa siri tukiwa ofisini kwangu, ….’akasema.
‘Wao
wanataka uyasema..ndio maana tumekuja nao, eti mabinti…muambieni…’akaambiwa,
lakini kabla hao mabinti hawajasema kitu, huyo jamaa akasema;
‘Nyie
mnaweza kuwalazimisha hivyo, kwa vile nyie ni mabosi wao, lakini kitaaluma yetu
haturuhusiwi kuyasema hayo, ninachoweza kusema ni kuwa kwenye majumba yenu,
kuna mazindiko mabaya, yanatakiwa kutolewa la sivyo, kunaweza kutokea mabaya
zaidi,..sasa kwa vipi, na yapi, siwezi kusema mpaka tuingie kwenye makubaliano,
mjini hapa, hakuna-cha-bure…’akasema akisisitiza kwa mkono na kichwa.
‘Unamfahamu
huyu binti..?’ akaulizwa akionyeshewa mdada.
‘Ndio
namfahamu nilikuja hata sehemu anayopofanyia kazi, tukaongea naye, na kabla ya
hapo nilishawahi kuonana naye huko kijijini, hilo halina siri…’akasema.
‘Na
yule..?’ akaulizwa na hapo akanigeukia na kunikagua kwa macho, halafu akabenua
mdomo na kusema;
‘Mhhh,
hiyo sura sio ngeni kwangu…, nahisi kama nilimuona mahali…’akasema
‘Wapi
labda…?’ akaulizwa
‘Siwezi
kujua,…nahisi hivyo tu…’akasema
‘Je yeye
unaweza kumuangalia hivyo ukaona ana tatizo lolote…?’ akaulizwa , kwanza
akanikagua tena, halafu akatabasamu na kusema;
‘Ama
kwa kutaka kuonyesha promosheni, huyu mdada kwa jinsi nilivyomuangalia bila y
akuwaita watu wangu..ana tatizo…’akasema
‘Watu
wako..?’ akaulizwa
‘Yah,
mizimu…’akasema
‘Ni
hivi,…huyu mdada ana tatizo, tena tatizo kubwa, asipolifanyia kazi kwa haraka
..hata hivyo inavyoonyesha ameshachelewa, lakini hakuna kinachoshindikina ,
nikiongea na mizimu, wanaweza kunisaidia, tukapata njia mbadala, ni wao lakini
wanaweza kusema hivyo…’akasema
‘Unaongea
nao kwa vipi…?’ akaulizwa
‘Napandisha
mambo yetu…nakuwa kama sio mimi..ukifika ofisini kwangu utaona…’akasema
‘Lakini
niwaambie kitu kimoja, mambo haya yanahitajia imani hata huyu mdada, kama
atanitaka mimi, nitaweza kumsaidia lakini iwe kwa haraka sana…hapo alipo ana
kitu tumboni, na akienda hospitalini wakampima, watasema ana uja uzito, lakini kiukweli sio mimba ya
kawaida,..unabisha, kama umepima hujaambiwa una mimba..?’ akasema akinikagua mimi
sehemu ya tumboni.
‘Nabisha..kwanza
umesema mpaka uwaulize watu wako sijui, sasa hivi unaongea hivyo hata hujafanya
hivyo, kuonyesha kuwa unalijua hilo kabla….au ni wewe unahusika nalo....’mimi
nikasema kwa hasira.
‘Kama
unabisha tumuite docta akupime tuone kama hawatasema wewe una ujauzito, ndio
nilishaliangalia tatizo lako nilipokutana na huyu mwenzako,…siwezi kuficha
hilo, alitaka kukusaidia, na ndipo nikakutizamia, unielewe hapo…’akasema.
‘Ujauzito
wa nani…?’ nikamuuliza kwa hasira, na hapo akacheka kidogo, na kusema;
Unataka
nikutajia huo uja uzito ni wa nani, upo tayari kwa hilo…?’ akauliza
‘Nipo
tayari ndio..wewe si unamfahamu…’akasema
‘Hahaha,
unajua huyu bado mdogo…hajui, haya mambo, anahisi natania, eti jamani huyu
anataka nimtajia ni nani aliyempa huo ujauzito, lakini kumbukeni nilichowaambia
awali..mimba hiyo sio ya kawaida, sasa iliingiaje, ndio anataka kujua,….sikiliza…’akatulia
akawa anatikisa tikisa kichwa kwa muda..
Inaendelea……
WAZO LA LEO: Mambo ya shiriki yamegubikwa na uwongo
mwingi…, asilimia kubwa ya watu hawa, hawaogopi kusema uwongo, hawaogopi kuzua
jambo kwa ajili ya kufarakanisha watu wengine, bila kujali athari zake kwenye
jamii, na dunia ya sasa watu kama hawa wapo wengi sana, wanawafarakanisha
ndugu, jamaa, mataifa, nk..lengo lao ni kujenga chuki ili waweze kuweka hatamu
zao za kishetani, tuweni makini sana, dunia ya leo sio ya jana, ulimi huu
unaweza ukawa silaha ya kufanikisha malengo ya shetani,…Na tujiulize hatima ya
haya yote ni nini basi,..vyovyote iwavyo, marejeo yetu ni kwa muumba wetu yule
asiyedanganyika,, sasa kwanini tunayafanya haya…
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment