‘Kama wewe ni mtaalamu, na ulinitizamia, na kama unavyodai wewe unafahamu mambo aliyo nayo mtu, sasa niambie, huu uja uzito ni wa nani…?’ nilimuulizaa
‘Unataka
nikutajie ni wa nani…hahaha, eti jamani nimtajie…?’ akauliza akionyesha kama
mzaha
‘Kasema
umtajie, wewe si unajua ni wa nani au…?’ akaambiwa kama anaulizwa
Tuendelee
na kisa chetu
************
‘Unajua
nyie ni wajanja sana..nyie mnataka niwaambie kila kitu, wakati na mimi hiyo
ndio kazi yangu, nikiwaambia kila kitu, malipo yangu nitapata wapi…eti
jamani..?’ akawauliza
‘Hili
hapa sio swala la malipo, ni swala la wewe kujibu shutuma, mdada anahisi wewe
unahusika na hayo yaliyomtokea sasa mjibu swali lake…’akaambiwa.
‘Aaah,
kumbe…unajua mimi sikujua, nilijua mnataka niwaambie kazi zangu ili muwe wateja
zangu, au sio..?’ akauliza
‘Pamoja
na hayo, waganga ni wachawi pia,..tunataka ulikane hilo, je ni kweli au sio
kweli kwako wewe.?’ akaulizwa
‘Yategemea,
sasa…wewe binti, ukitaka nikuelezee hayo yote, matatizo yako, unatakiwa tuwe
wawili, unanielewa, hapa sipo ofisini kwangu…tutaongea, usijali kuhusu malipo
wala nini…halefu eti jamani wewe ndiye una mimba, na mimba inakujaje, wewe
ndiye utakuwa unamfahamu aliyekupa hiyo mimba ni nani..’akatulia akisubiria mtu
kama ataongea
‘Ndio mimi
nakubali kuwa mimi nina kipaji, urithi wa uganga, ni-naweza kukuambia hiyo ni mimba
ya nani., lakini hilo ni la ndani zaidi, siwezi kukuambia hapa, nitakuambia
tukiwa wawili, tukishakubaliana malipo, labda niweke wazi hivyo…’akasema
‘Hapo
hapo…umesema hiyo mimba sio ya kawaida,…kwahiyo hata kupatkana kwake sio kwa
kawaida, ndio maana hiyo mimba iliingia isivyo kawaida, iweje tena uniambie
kuwa mimi namfahamu huyo mtu, kwa vipi sasa...’nikasema
‘Unajua
wewe una nidodosa, ili nikuambie kila kitu, lakini siwezi kukuambia hilo kwa
sasa …hayo niliyokuambia yanatosha, kama huamini, kaa na hiyo mimba yako,
utakuja kunitafuta mwenyewe…’akasema
‘Kama
ni tatizo linahitajia matibabu , kwanini mpaka nikutafute wewe…kwani hakuna
wengine wanaoweza kunitibia…?’ nikamuuliza
‘Nimeshasema
mimi siwezi kuliongelea swala lako zaidi ya hayo niliyokusaidia kukufafanulia,
zaidi ya hapo, unanitaka na mimi nisipate ujira wangu….au jamani nakosea…?’
akawauliza wale akina mama.
‘Sasa
ni hivi, unasema yeye akipimwa ataonekana ana uja uzito, lakini sio mimba ya
kawaida…, kama sio mimba ya kawaida ni
mimba gani, hapo unatuchanganya…?’ akaulizwa na akina mama .
‘Wewe
unauliza maswali vizuri sana, wewe ni mwanasheria nini, au…mwalimu…au….aah,
nimeshakugundua wewe ni mwalimu…’akacheka.
‘Tujibu
swali…’akasema mama mwingine.
‘Huo
uja uzito sio mimba ya kawaida, umeelewa hapo…, akichelewa itaendelea kukua
kama mimba ya kawaida tu…, lakini kilichopo tumboni sio kiumbe cha kawaida, na
anaweza akafikia muda wa kuzaa na kuzaa kama kawaida, ila atazaa nini sasa,
hapo ndio tatizo,..wakati huu wa miezi kwenda tisa..kuna dalili atazipata kabla
ya kuzaa, kama nilivyosema awali…’akasema.
‘Atazaa
nini mtoto au kitu gani…?’ akaulizwa, sasa akanigeukia na kuniangalia akasema;
‘Upo
tayari nisema hayo maana ni mambo yako, unaweza ukaogopa, ndio maana nilitaka tuongee
mimi na wewe, ngoja nfanye hivi, hili nilitoe kama promosheni, sitakuchaji
kitu, navutia biashara, maana huyu mama nimependa anajua kuuliza maswali
kihekima, hana jaziba, jaziba za nini..mimi nina kosa gani eeh,…?’ akauliza.
‘Sio
jaziba, ni kweli, wewe sema ulichonifanyia, usijifanye kutabiri hapa..mimi
nimeshakujua,….wewe ’nikasema na huyo mama akaniashiria ninyamaze, na jamaa
akaniangalia halafu akatabasamu kidharau fulani hivi, akazidi kunichefua, …unajua
mtu kama alikuzalilisha, akawa anaonyesha hivyo, ni kama anakuona wewe ni nani
hasa nimeshakuona ilivyo, kiukweli nilihis vibaya, hasira…
‘Wewe
hapo ulipo una mimba na ukiiachia itakua tu…, utakuja kuzaa mtoto…mwanadamu
kama kawaida, atakuwa na umbile la mwanadamu, lakini tofauti yake itakuja
kwenye matendo, hulka, utachoka kwa jinsi atakavyokuwa, watu wanazaa na
hawataki kujisafisha na mauchafu ya mwilini,…sawa kama ana imani ya dini,
anaweza kuhudumiwa huko, lakini sisi tunajua mambo yetu ya kimila,…’akatulia
kama anawaza jambo.
‘Niwaambie
kitu, kuna watu wanazaa, wanataka watoto, wanakwenda kwa wataalamu,
wanafanikishiwa, haajui wamewekewa nini…acha hao, kuna watu wanatembea ovyo
ovyo, wanakuja kujifungua,, lakini wanakuja kusumbuliwa kweli na walichokizaa,
mara unasikia mtoto sio rikizi,…kwanini asiwe riziki, mtoto jambazi, mtoto hasikii, hashikiki,
..unaona hiyo ni mifano tu, sasa hayo nimekutolea mfano, ila wewe utakuja kuzaa
zaidi ya hiyo, sikuambii zaidi ya hapo…’akasema
‘Hapo
bado unatuchanganya, ina maana atakuwa kazaa nini, …kama sio mwanadamu, na
utamtofautishaje na watu wengine..?’ akaulizwa.
‘Kwa
ufupi,..unajua shetani, ibilisi, sio lazima awe huyo tusiyemuona, mnakubaliana
na mimi…?’ akauliza
‘Utuambie
wewe, maana hata wachawi, …kwa imani zetu ni mashetani…’akasema mama mmojawapo.
‘Umeonaeeh,..sasa
huyu atazaa mtoto zaidi ya huyo…kitabia, na matendo yake, atakupa shida sana,
lakini unaweza kuwapata watu kama sisi tukakusafishia njia, tukakisafisha hicho
kiumbe, tukaondoa hayo mazindiko, maana sio mipango ya mungu, ni watu
wamekufanyia hivyo…’akasema
Wale
akina mama wakaangaliana, na kutikisa kichwa.
‘Mimi
nawaonea huruma sana,..mtasumbuliwa sana na mambo haya, lakini kwanini
msihangaike, mkawaona watu kama sisi, tukawaondolea hayo matatizo, nyie tatizo
mnajali sana mali, mali ni nini, mali zina fadia gani, kama watoto wanakuwa
hivyo, wanaumwa, wanakuwa na tabia mbaya,..ina faida gani sasa…’akawa kama
anauliza
‘Sawa
wewe mdada, binti, nimekupa hilo kama angalizo, na sio wewe hata nyie sote,
hangaikeni,..utazaa mtoto awe jambazi, awe muaji, na mwisho atakuambi anahitajia
damu za watu…’akasema na mimi pale nilipo nilihisi mwili ukiniishia nguvu,
nikajikaza, ilichukua muda hadi hali ikawa sawa, nashukuru nilikuwa nimeegemea
ukuta.
‘Umejuaje
hayo, na kwanini ni iwe hivyo na huku hospitalini wanasema ni mimba, ya kawaida
na haina tatizo..?’ akaulizwa
‘Nimewaambia
mimi nina karama za mambo hayo kujua mambo ya mtu yaliyojificha, kwa kutumia
watu wangu, lakini kwa anayeamini siwezi kuwalazimisha watu wote waniamini,
unaelewa hapo…, mtu kama haamini hawezi kuwa muumini wa kile kitu…si ndio
hivyo…swali jingine, hilo tumalimaliza, kwa huyu tuyaachie hapo…’akasema.
‘Kwa
utaalamu wako, unahisi matatizo hayo yametokana na nini, au na nani hasa, maana
unasema ana mimba ya lakini sio mimba ya kawaida, sasa imeingiaje mwilini mwake..?’
akaulizwa.
‘Hapo
sasa unaingia kwenye sehemu ya ndani ya kazi zangu, hapo kunahitajika makubaliano,
promosheni hiyo haiwezi kwenda kiundani ki-hivyo…, hapo sasa ni nipe nikupe,
siwezi kutoa utaalamu wangu wote bure , kama anataka nimsaidie basi tukubaliane
kwa malipo stahiki, najua yeye ana hali mbaya, hata mshahara wake hataweza
kunilipa, na mimi nitaangalia ahueni fulani….’akasema.
‘Bei
gani..?’ akaulizwa
‘Mhh..umekwenda
mbali, ..kwanini wewe unamuulizia.., wakati mwenyewe yupo, kama unataka kumlipia sawa, lakini nilitakiwa
nikae naye nifanye mambo yangu yaniambie ni kitu gani kinahitajia,…lakini kwa
vile nilishalifanyia kazi kabla, naweza kumtajia vifaa kwa ufupi…’akasema .
‘Sisi
ndio tumechukua dhamana kama wazazi wake tunataka umtibie, tuambie gharama
zake, ili tuwezi kujipiga, tuone kama tutaweza , la sivyo tuta-tafuta mganga
mwingine…, au mnaitwaje nyie watu, wataalamu,…tuambie ukweli pamoja na mengine,
dhumuni letu mojawapo ni kumsaidia huyu mdada, na wewe umesema unaweza kuifanya
hiyo kazi, ulimuambia huyo mdada mwingine si ndio hivyo…’akaambiwa, na
akaniangalia mimi kwa muda, halafu akasema;
‘Kwa
haraka, ..yaweza ikawa juu au chini, ndio maana sitaki kukadria, lakini kwa
uzoefu, ili kuliondoa hilo tatizo, na kumweka huru na hayo mazindiko yaliyotokana
na watu,..kuna makafara ya damu ya kimizumu, ili yafanyike kunahitajika ng’ombe
mwekundu dume lislo na tatizo lolote,,na pia..mbuzi au kondooo wa rangi mchanganyiko.
Kuku wawili, mtetea,…kuna viti vingine vidogo vidogo, madawa ya kufuza…eeh, kwa
hivi sasa siwezi kuvitaja mpaka niongee na watu wangu, ila muhimu kunahitajika
damu ya kafara, hayo ni mambo yetu ya kitaalamu zaidi….sasa ukipiga gharama hapo
utaniambia…’akasema
‘Duuh,
ndivyo mnavyofanyia watu hivyo, mbona gharama kubwa sana..?’ akaulizwa
‘Hapo
nimemsaidia tu kwa vile ni mtu wa shida, …, la sivyo,..’akatabasamu tabasamu
lake la dharau akiniangalia usoni, halafu akatikisa kichwa kama kusikitika.
‘Kiukweli
binti huyu ana matatizo makubwa namuonea sana huruma..yeye hajijui tu, sasa kama
haamini, yeye abakie hivyo hivyo tu…, kuwa ana mimba, itafikia sehemu ataanza
kupata shida sana, atahisi vitu vinatembea tumboni, vinamchoma choma, si unajua
shetani lina makucha, lina…sasa siwezi kumtisha, lakini ndio hivyo, haraka
afanyiwe hivyo ili asije kuzurika..anaweza akavumilia, akazaa lakini kwa shida
pia…’akasema.
‘Jamani
sasa mnielewe kwa huyu siwezi kuongea zaidi ya hayo, nimemalizana naye…’akasema
akiangalia pembeni
**************
‘Sawa…lakini yupo huyu mwingine pia, kabla
hutujamalizana, tunataka tujue gharana zako kwa wote wawili maana wote wana
matatizo yanayofanana, je huyu mdada mwingine naye ana tatizo gani..?’
akaulizwa
Aligeuka
na kumuangalia mdada, lakini akawa hamuangalii kama alivyokuwa akiniangalia
mimi, ni kama anamuogopa kumuangalia moja kwa moja usoni, ….akasema
‘Huyu
bwana, nakumbuka alikuja kwangu ndio,… ila tulikuwa hatukuelewani kidogo, akaenda
kwa wataalamu wengine wakamfanyia walichomfanyia,…siwapuuzi hao wataalmu..
nawaamini, sio haba.., ..na kwa vile alikwenda huko mimi sitakiwi kuwaingilia,
yeye mwenyewe kama hajarizika nako basi anione mimi ..’akasema
‘Unasema
alikuja kwako mkawa hamukuelewana kidogo…ni kwanini hamuekelewana na huyu
mdada, wakati alikuja kwako akiwa na tatizo ina maana mgonjwa akija kwako kama
hamtaelewana huwezi kumuhudumia…?’ akaulizwa.
‘Kwanini
hatukuelewana, hayo ni kati yangu mimi na yeye ni mambo binafsi kwa kweli..’akasema
‘Lakini
sisi tunataka umuangalie na yeye matatizo yake,..bila kujali hayo ya huko
nyuma,.. kama matatizo yake yamekwisha au la, sisi tutakulipa, lakini tuwe na
uhakika wa kupona kweli, uhakika wa kazi yako,..?’ akaulizwa.
‘Yeye
tumeshaongea naye sana, na kwa vile hatujaelewana kwa mabo fulani fulani,
siwezi kumlazimisha zaidi, kama atanihitajia sawa, atanitafuta, yeye,
ananifahamu , anajua mpaka nyumbani kwangu huko jijini…’akasema.
‘Mhh,
unataka kusema nini ina maana matibabu yako yanagusa hata maswala mengine,
unavyoongea ni kuwa kuna mambo binafsi kati yako na wewe, hayo yanazuiaje
matibabu yake..?’ akaulizwa
Hapo
akamuangalia mdada, halafu akasema;
‘Unajua
pamoja na hayo, sio kwamba nilikataa kumtibia, ila yeye mwenyewe alipoona
nimegusia maswala mengine akajenga chuki,…akawa haniamini tena, na kazi yetu
hii ni ya kuaminiana…kwahiyo nikaona aheri aende kwa wengine…’akasema
‘Ni
wewe ulisema au yeye mwenyewe ndio aliamua hivyo..?’ akaulizwa
‘Yeye
mwenyewe…na mimi sikumfuatilia sana, nilijua ipo siku atanitafuta tu…’akasema
‘Kwanini,
akutafute wewe tena, wakati hamukuelewana…?’ akaulizwa
‘Haya
mambo yanazidiana, mimi sio kwamba nitamba, lakini waulizeni wote huko
kijijini, wanajua kuwa mimi ni mtaalamu zaidi yao,…sio siri, utaalamu wangu unasifika…’akasema
‘Wewe
una mke?’ akaulizwa
‘Swali
gani hilo jamani, mbona haliendani na haya, kwanini umeniuliza hivyo, mimi
naona kuwa, hayo ni mambo yangu binafsi, …?’ akauliza na kabla hajajibiwa
akasema
‘Lakini
nikujibu tu, nilikuwa naye,..nilikuwa na mke,.. lakini kwa bahati mbaya,
tukaaachana naye ..’akasema
‘Kwanini
mliachana naye..?’ akaulizwa, na hapo akamuangalia huyo mama, sasa kwa uso wa
kushangaa zaidi.
‘Ohh,
unataka kujua na maisha yangu,…?’ akauliza
‘Nitakuaminije
kuwa unayoyasema ni ya ukweli, …ni lazima nikupime kwanza kabla sijajiingiza
kwenye matibabu yako, au una wasiwasi na maisha yako kuwa hayana ukweli..?’
akaulizwa
‘Oh,
sawa,..usiwe na shaka nitakujibu tu..ni hivi,…hatukuelewana naye, watu
wanaachana kihivyo, au sio..? mimi sio wa kwanza kuacha mke.., au sio….’akasema.
‘Kwanini
hamukuelewana naye, kwasabau hapo kutakuwa na maswali ya kuuliza, ni kwanini, kwa mtu kama mimi ninayekutaka uwe mganga
wangu…?’ akaulizwa.
‘Maisha
tu ndugu yangu…, sio kila mtu mtaelewana naye, unajua tena ndoa zingine zina
mitihani yake..’akasema
‘Ukashindwa
kuhimili mitihani ya ndoa, lakini wewe unawaambia watu waje kwako unaweza
kuwatengenezea ndoa zao,…hapo huoniunanitia mimi mashaka…?’ akaulizwa
‘Mganga
hajigangi, hilo liamini hivyo…ilifikia mahali niliona ni bora kuachana, hata
watu wakija kwangu nikiona ndoa zao hazitadumu, kuna tatizo haliwezi kutatuliwa
nawashauri hivyo, hata mimi ilifikia hapo…’akasema
‘Kwanini
sasa hujaona kwa muda huo wote,….unaishije, au una namna nyingine ya
kukuwezesha usiwe na hamu yakuoa..?’ akaulizwa na hapo akacheka na kutikisa kichwa.
‘Wewe
mjanja sana…’akasema
'Jibu swali...auunaogopa kujibu kwa kuwa litafichua ukweli wa ulivyo...?' akaulizwa , hapo akacheka, na akageuka kumuangalia mdada, na mdada alipomuangalia na yeye, akageuka kwa haraka kuangalia pembeni, na kabla hajasema neno huyo mama akamuuliza swali jingine.
‘Halafu
ndio ukataka kumuoa huyo mdada, au sio, alipokuja kwako ukampenda,
nikurahisishie hivyo maana unaogpa kujibu hilo swali kwa vile muhusika yupo huwezi kudanganya,…, au sio..?’
akaulizwa
NB:
Msichoke na maswali na majibu kuna kitu kinatafutwa na mwisho wake jamaa
ataingia kwenyewe bila kujua, tukumbuke kisa chetu ni swali, je duwa la kuku
kweli halimpati mwewe,
WAZO LA LEO: Tunapokuwa kwenye fani zetu, ziwe za
kitaalamu, za kiimani, au za kipaji ulichojaliwa nacho, jaribu kuwa mkweli,
hata kama ndio fani yako hiyo ndio njia ya kukuwezesha kupata riziki yako,
usiingize uwongo, udanganyifu na ujanja ujanja wa kitapeli,…UKWELI, ndio
utakuongezea kipato chako kwani utajenga uaminifu kwa wateja wako, lakini ukiwa
muongo, ipo siku uongo wako utagundulikana, na wateja wako watakuona wewe sio
mkweli na ndio itakuwa mwanzo wa kukimbia.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment