Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, February 10, 2017

FUPA LILOMSHINDA FISI….ni NANI ataliwezaNi mbiu ya mgambo, na mbiu ya mgambo ikilia ina jambo, na hasa ikiwa inapigwa na tan-tan-lila mpiga mbiu mashuhuri ambaye mitaani wamempa jina la ‘Tantalila…’

‘Ndugu wa kazi wa nchi hii ya ‘Boraliende..’ akaanza mpiga mbiu, na wakati huo wakazi wengi walishatega masikio, na akina mama walishatoka nje na wengine kusimama milangoni kusikia mbiu hiyo ya mgambo...., maana mpiga mbiu huyo ni mtaalamu na mara nyingi , yeye akipewa hiyo kazi ujue kuna ujumbe muhimu sana...

Lakini sio tu kwa ujumbe muhimu, lakini pia na mbwembwe zake za utangazaji.., kila akiongea jambo huwaacha wakazi wengi kwenye teta-teta nyingi na gumzo la siku, hata wenzetu wauza magazeti na vyombo vya habari soko lao hupanda maradufu.

‘Wana Boraliende, mtege masikio vyema, na yule asiye na sikio akaazime sikio kwa  jirani yake, kwani ujumbe huu unamuhusu kila mkazi wa N-NCHI..ya bora liende… na hata yule asiye mkazi,…unawahusu pia, ilimradi ana uhai…hata mifugo ifungulieni milango isikie maana litawagusa hata wao,….’akaanza mbwembwe zake.

‘Ndugu zanguni tumeingiliwa…’hapo akapiga tantalila lake kidogo….

‘Tanta –ta-ta-rararara… Tanta –ta-ta-rararara….’

‘Tumeingiliwa majumbani mwetu,..tumeingiliwa mpaka chumbani, ….maisha yetu yamewekwa rehani, na tusipoangalia tutaishia kuzimu…’ akatulia.

‘Huo ndio ukweli….lakini niwaulize jamani, hivi jamani hamlioni hili,…’ akatulia

‘Jamani…tunalima,…tunafuga, ni nani asiyeijua nchi hii, toka zama za mababu, kulima na kufuga ndio jadi yetu,…pia tunafanya kazii kwa bidi tu…tunazalisha sana tu….’akatulia

‘Lakini cha ajabu mauzo, mazao hatuyavuni, na hata tukivuna hatuuzi, na hata tukiuza hatupati, na hata tukipata hatujui kina kwenda wapi…sababu ni nini…au  nadanganya…?’

‘Kipato chetu kimekuwa ni duni…umasikini umekithiri…hivi hili jamani hamlioni….’akawa kama anauliza na wakazi wale wale waliokuwa karibu karibu wakawa wanaangaliana na kutikisa kichwa kukubali.


‘Kuna mdudu anapekenyua maisha yenu, amavuruga akili zetu, za vizazi vyetu maisha yetu, huyu mdudu ni hatari maana anaweza kuingia hadi kwenye akili zetu, atatughilibu, na kufanya kile anachokitaka, huyu mtu lakini ni mdudu…’akatulia

‘Ukweli ni kuwa tumeingiliwa…na hili ni janga, tumeingiliwa na ‘MDUDU-MTU…’akatamka maneno hayo ya mwisho kwa sauti kubwa na mbwembwe

‘Huyu mdudu mtu ni mchawi mkubwa duniani, ..huyu kazi yake ni kusubiria, ulime, uvune uuze, halafu kwa ulaini anazichukua pesa zetu,….hamulioni hilo jamani, mkuu anauliza hamlioni hili,..hali sasa zimekuwa sio nzuri, njaa, hali ngumu, ndoa zina migogoro,….tumekondeana kama tunaumwa nanihino…’hapa wenye kucheka wakacheka.

‘Hatuumwi nanihino kabisa kabisa mkuu kasema hakuna huo ugonjwa,….kwani keshaligundua hilo tatizo….’akatulia

‘Mkuu kasema keshampata huyo mdudu mtu, na keshaipata dawa yake…..kampata mtaalamu kutoka milimani, mganga mwenye siha, mwenye nguvu, mwenye utaalamu, mganga anayeona mbali….yeye ataimaliza hii kazi mara moja, hiyo ni ahadi yake….’hapo akakohoa.

‘Jamani ni nani asiye na shida…?’ akauliza kama vile anahutubia, lakini anapita mitaani, na tantalila lake, wakazi kila mmoja akasema, ‘tuna shida,..kila mtu ana shida, mimi nina shida…ni kweli tuna shida…’ japokuwa wengine walisema kimoyo.

‘Sasa tunataka kumtoa huyu mdudu mtu, …tunataka kumtoa majumbani kwetu, kwa udi na uvumba, tunajua wapi alipo, tunajua wapi anafanyia shughuli zake tunawafahamu na washirika wake…na yeye ni wakala tu, wenzake wakubwa wapo, tunaishi nao tunakula nao…lakini kwa vile …hatuna ufahamu wa kuwajua, …hatuwajui…sisi hatuna utani,…kazi ni moja tu, utekelezaji, si mnatufahamu jamani…kazi ni moja tu…’akapuliza tantarira…..

‘Wengine ni ndugu zetu, jamaa zetu, marafiki zetu….tutawataja hatutaogopa…’akatulia,

‘Sasa ndugu zanguni, mjumbe hauwawi….wakati umefika,..wakati wa kumfichua huyo mdudu-mtu, na mawakala zake….je huyu mdudu mtu ni nani, na anafanya nini, mhh, huo ni mzigo mzito kwangu,…….’akasema mpiga mbiu

‘Huo ni mzigo wa Mkuu wa nchi ……’

‘Huyu mdudu mtu alikuwa kajificha, kava ngozi ya kondoo, mawani ya giza,…ana walinzi wa juu na chini, ana ….kila kitu, anajua kujibadili kama kinyonga,… lakini sasa keshapatikana….mnasikia mkuu wa nchi keshampata huyu mdudu mtu, na washirika zake….’akasema na kulipuliza tantarira lake.

‘Huyu mdudu mtu kawafanya vibaya watoto wetu,,….watoto wetu , kizazi cha leo na kesho, hata kazi hawawezi sasan, watoto wetu wamelegea hawana nguvu tena, wanatoa maudenda tu…..inasikitisha…’akatulia

‘Jamani hili janga hamlioni ….ni nani asiye na uchungu wa mwanae,..eeh, niambie,..sasa wakati umefika,….tushirikiane, na kushirikiana huku ni kusaidia kumtoa, kumfichua, mkuu anawafahamu lakini nyie ndio mnaishi nao…toeni ushirikiani tuharakishe hii kazi….’akatulia

‘La mgambo ndio hilo mwenye macho atizame, mwenye masikio asikie, ukimaliza kusikia kama uliazima sikio  kwa jirani usisahau kulirejesha kwa mwenyewe…mkuu katoa siku saba tu, hao watu wajisalimishe, la sivyo, ataingia nyumba hadi nyumba… ’akamaliza kwa kupiga tanta-rira lake

Wakazi wa Bora liende wakabakia wanaulizana..ni nani,..ni yupi…, ikawa ni soga ya siku, magazeti yakapambwa kwa vichwa vikubwa, mdudu mtu keshapatikana, mkuu anataka kumtaja mdudu mtu....na wauza gumzo ikawa ndio kazi yao…..wambeya, watesi….wakapata cha kuongea…mdudu mtu mdudu mtu……sasa fupa limepata mtafunaji…

‘Mhh…haya jamani, fupa lilomshinda fisi ni nani wa kulitafuna..

Tutaona sehemu ya pili

‘Huyu mdudu –mtu ni nani?’


Wakatabahu mzee wa Busara.
emu-three

No comments :