Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, November 4, 2014

DUNIA YANGU-58‘Kwanza sikujua kwa jinsi gani nitaweza kuyasomea hayo masomo mengine, kwani kwenye ule mkataba yalikuwa hayakutajwa kuwa ni masomo gani, au utaalamu gani..., lakini nilipofika huko nikakuta kila kitu kipo tayari, kwahiyo pamoja na masomo hayo ya udakitari bingwa wa magonjwa, lakini pia nikawa nasomea masomo hayo mengine ambayo hayakutajwa moja kwa moja ni magonjwa gani......’akakatiza.

‘Ni masomo gani hayo ya ziada uliyoambiwa uyasomee ulipofika huko..?’ akaulizwa na hakimu.

Tuendelee na kisa chetu....

**************

‘Ndugu muheshimiwa hakimu, nilipofika huko niliingia chuo nilichosajiliwa nacho nikabainishiwa kipi cha kusoma,…kulikuwa na kozi nyingi tu na zote mimi nilitaka kuzisomea,…lakini mimi nilitakiwa kuwa docta bingwa wa nyanja moja…’akatulia

‘Mimi nina akili ya ziada, nikataka kusomea zaidi ya Nyanja moja,  lakini kutokana na makubaliano ilibidi nianza na moja, na baadaye nikimaliza hiyo naweza kusomea nyingine, ni pesa yako tu. Mimi kwa swala la malipo, sikuwa na shaka nalo, mfadhili wangu alisema hilo ni jukumu lake,

Siku ya kwanza tu, tulipomaliza masomo, wakati nimepumzika, mara akaja huyo mdhamini wangu wa huko akanijia akaniambia nahitjika kwenda kuandikisha masomo mengine,nikauliza masomo gani hayo tena, huo ni muda wangu wa kupumzika, yeye akasema;

‘Uliona pale kwenye mkataba, kuwa kuna masomo mengine ya ziada, na wewe una akili ya ziada, huwezi kushindwa kusoma masomo zaidi ya moja, nasikia una kichwa cha ajabu sana wewe, hata mwenyewe umekubali kwenye huo mkataba, kuwa utaweza, au …?’ akaniuliza na kunisifia na mimi kwa kutamba nikamwambia;

Off course nitaweza, hamna shida ndio vizuri, akili yangu ipate mambo mengi,…nikibakia bila shughuli, akili inaniuma kulewa, na mimi kwa hivi sasa sitaki hiyo kitu, sasa hivi nataka kusoma kila kitu kuhusu udakitari kama nitapata nafasi hiyo…’nikasema

‘Usijali  utasoma kila kiu uanchotaka lakini ni muhimu twende na kataba wako, natakiwa nikupeleke huko, kwenye chuo kingine, huk utasome masomo kama hay ohayo, lakini kwa nji a nyingine,huko utapata masomo ya kuweza kujua mambo mengi ya dunia,..’ basi mimi nikakubali, tukaenda huko nikaanza kuelekezwa ni kitu gani natakiwa kujifunza, na hapo hapo nikaanza kuingiwa na wasiwasi, nikauliza;

‘Haya najifunza kwa madhumuni gani, hamuoni kuwa mambo haya ni maswala ya wapelelezi, n asana sana ni mambo ya ugaidi wa kimataifa, ambayo tunakatazwa duniani..’nikasema.

‘Dunia hii ina mambo mengi yanayokatazwa, lakini huko ndipo kwenu utajiri, wewe unasoma, ili uyajue hayo, na hata ukisikia utambue ni kitu gani, na kwa vile wewe utakuwa docta mkubwa sana, unatakiwa uyafahamu au sio, ili hata, akija mgonjwa wa namna hio hutasumbuka kumtibia…’nikaambiwa

‘Ni kweli kabisa, hapo nimewaelewa, kwanza itanipanua ubongo wangu wa ufahamu, kujua mengi ambayo hawa watu wanafanya, yes, I will do it…’nikasema kwa hamasa,

‘Kiujumla ndugu hakimu, mimi napenda sana kujifunza mambo mengi, hasa yanayohusu fani yangu, mimi ni mwanasayansi, na mwanasayansi wakati wote anataka kugundua jambo jipya, kusoma, kufanya uchunguzi na vitu kama hivyo, sia bla-bla ….’akatulia

‘Kwahiyo huko walitaka ujifunze nini hasa?’ akaulizwa

Kwa kifupi ni utaalamu wa kucheza na akili ya mwandamu, ufahamu wake…unajua ubongo ndio komputa ya mwanadamu, humo kuna mambo mengi sana,…sasa jinsi gani unafanya kazi katika maisha ya kila siku,..achilia mbali magonjwa, na matatizo yake, …sio rahisi kuelezea vyema, ila  ilitakuwa kujua jinsi gani mishipa ya ufahamu ilivyo, na  unaweza kucheza na mishipa hiyo ya akili ukamfanya mtu awe unavyotaka wewe, ni mambo ya kitelenjisia, kama ushushu katika udakitari nk..

‘Kuna mishipa ya ufaamu ya mwanadamu,  unaweza ukaiharibu , mtu akawa hajielewi, au kumtesa kwa kuiharibu hiyo mishipa ya ufahamu mtu huyo akawa kama zezeta, au akaongea yote yaliyo siri kwake na vitu kama hivyo, hasa wakati mtu akitaka kujua siri anayoitaka kutoka kwako, unaoneeh, ni mambo ya kipolisi kidogo….’akasema

‘Kwahiyo wewe ulisomea ili umfanyeje huyo mtu,  upasuaji au unatumia madawa?’ akaulizwa

‘Unaweza ukatumia madawa moja kwa moja, au ukamfanyia upasuaji, na kwa namna hiyo ilibidi pia nisomee  jinsi gani ya kutengeneza madawa yanayoendana na dhana hiyo, pia nikajifunza jinsi ya kutengeza sumu ambayo hata ikipimwa haiwezi kutambulikana kuwa huyo mtu kanywa sumu, ataonekana kafa kifo cha kawaida tu,, ..na hata kutengeneza madawa ambayo yakikutana na hewa hubadilika na kuwa mabomu ya hatari.....’akasema

‘Kwahiyo ulifundishwa ugaidi wa hali hiyo..?’ akaulizwa

‘Kiukweli mwanzoni sikuwa na ufahamu huo,kama nafundishwa ugaidi,na mimi kwa vile nilikuwa na hamasa ya kusomea mambo mengi, nilikubali, …..mmh, nilikubali nikijua yataishia huko huko, na kwa vile waliniambia kuwa ni mambo ya ziada tu ambayo yatanisaidia katika udakitari wangu mimi nikachukulia poa tu..’akasema

‘Je wakati unasoma huko , ulikuwa ukiwasiliana na mdhamini wako wa huku nchini?’ akaulizwa

‘Hapana, hata siku moja, mimi mara kwa mara nilikuwa na huyo mdhamini wa huko, ambaye tulikutana anye huko akajitambulisha kuwa yeye atakuwa mdhamini wangu nikiwa huko, na yeye akasema           kapewa maagizo yote,..kwa muda huo sikuwa na shaka naye, nikamfuata, akanielekeza nifanye nini na kwa ujumla nikiwa huko yeye ndiye alikuw a mwenyeji wangu, akawa ananipa kila kitu ninachohitajia, na hatimaye nikafanikiwa  ...’akasema

‘Ulifanikiwa nini hapo, udakitari au huko kujifunza ugaidi?’ akaulizwa

‘Nilifanikiwa Udakitari bwana,..hayo mengine, hayahusiani na  hicho kilichonipeleka huko, eleweni kuwa huko nilikwenda kusomea udakitari, ...kiukweli hayo mengine yalikuwa ni masomo ya ziada tu na hayakuwa yakitiliwa maanani sana, ila mimi kwa utundu wangu nilikuwa na hamasa ya kujua mengi, na wao wakawa wananifundisha mengi,..’akatulia

‘Nilifunza mengi sana, kuhusu silaha, utengenezaji mabomu,mada hatari, nk….yaani nikawa nataka nijue kila kitu, hata wao walinishanga jinsi gani nilivyoweza kufahamu mambo mengi na kufanya mengi, ambayo katika msimu wetu huo hakukuwa na mtu kama mimi,…kiasi kwamba waliata nibakia hapo kama mwalimu wao

‘Mdhamini wangu akaniambia huko sitakiwa kubakia muda mrefu ninachotakiwa ni kujifunza tu, nisikubaliane na wao, kwani wanaweza kuniingiza matatani, basi nikaona mdhamini wangu ananijali sana, na alinisisitiza kuwa  sitakiwi kuyaweka wazi kwa  mtu yoyote yule hayo masom o y a ziada....’akasema

‘Kwanini hukuuliza unayasoma masomo hayo kwa lengo gani au ulishaambiwa na wadhamini wako?’ akaulizwa

‘Mwanzoni niliuliza, mimi mwanasayansi bwana ni nahitajika kuwa mdadisi katika mambo ninayojifunza, lakini sikuwa na ufahamu kuwa nayasoma hayo kwa nia mbaya,..kabisa sikuwa nimefikiria hivyo, nikawa nayasoma tu, kama masomo ya kujistarehesha, au kitu cha ziada katika fani yangu, starehe tu, ukipenda kusoma, inakufanya utake kujua kila kitu, ni starehe kwa kweli...’akasema na watu wakacheka

‘Mnaona jinsi gani ugaidi unavyotengenezwa, mtu, anaambiwa  fanya hivi, utakuja kupata hiki, au soma tu kwa ziada, unakubali,..akili inakuwa haifikirii hatari yake,…na huwezi kujua malengo ya hao  wenzako wana nia gani kwako, hebu jiulize, wao watume gharama zao hivi hivi tu,…. haya hebu tuendee, ukasoma ukamaliza msomo yako ikawaje?..’akauliza muendesha mashitaka

‘Nilipomaliza masomo yangu tu, kwa vile nilishatambulikana kuwa nina kipaji cha ziada, wazungu wakataka nibakie huko huko,..ni kawaida yao ukiwa na akili sana, wengi wanabaki ahuko huko, hata pale chuoni walitaka bnibakie  niwe mkufunzi au niajiriwe kwenye mahospitali makubwa ya huko...,’akatulia

‘Nikaona …ni sawa, ni kweli napenda kubakia huko, lakini nina wadhamini, basi nikamuuliza mdhamini wangu, naye akasema;

‘Mhh, siwezi kukukataza, muhimu kwasasa wakubalie tu, lakini mimi nionavyo kabla hujaanza kazi na hao watu, kabla hujaingia mkataba wa ajira, ni vyema ukarudi nyumbani kwanza ili ujipange vyema, ujue ukianza kazi huku, hutakuwa na muda tena wa kurudi rudi nyumbani..’akaniambia

‘Kweli wewe ni rafiki wa kweli unanijali sana, hata mimi nilikuwa na wazo hilo, maana nataka nirudi nyumbani nikaweke mambo yangu sawa,nataka kwenda kuoa, na nina mipango mingi tu, ngoja nirudi nyumbani kwanza….’nikamwambia,

Nikafaya utafiti, ni hospiali gani kubwa huko inayolipa vyema, na hiyo ndiyo nikaingia mkataba nao, lakini kwanza wanikubalia nirudi nyumbani, nikikamilisha mambo yangu, nikirudi nitafanya kazi nao,…walikubali, na kwangu haikuwa shida sana…’akatulia

‘Muheshimiwa hakimu wazungu ni wajanja sana, wakikuona wewe ni kichwa, unajua vitu kama mimi, hawataki kukuachie, nikuambie ukweli, niliahidiwa mshahara mkubwa sana, marupurupu a hali ya juu…na wakanipa na mkopo wa kumalizia mambo yangu nikiwa huku nyumbani, mkopo usio na msharti….hebu fikiri….ni nani angelibakia hapa nchini tena, kama hakuna shininikizo la hali yajuu…’akatulia

‘Lakini  akilini mwangu  nilikuwa na hamu sana ya kuja nyumbani, ili niwaone wazazi wangu na jamaa zangu, maana sasa sio yule mtu wa hali ya chini wanayemfahamu, na ni vyema wanijue hivyo,… wale walioninyanyasa na kunidharau, wanione nilivyobadilika, ...lakini pia nilikuwa na ndoto ya kuanzisha hospitali yangu, ambayo hata nikiwa huko nje, bado itakuwa inajiendesha ...’akasema

‘Je kuanzisha hospitali yako ilikuwa ni wazo lako au wazo la mdhamini wako?’ akaulizwa

‘Nikuambie ukweli, nilikuja kugundua kuwa fani yangu inalipa….nyie hamjui tahamni yangu, thamani ya docta kama mimi, ..hapa nchini kuna wagonjwa wengi wanapata taabu kwenye hospitali zetu hizi kwa kukosa wataalmu wa namna yangu..ni kweli si kweli, , kwahiyo kama nikiwa na hospitali yangu, nitakuwa na wateja wengi tu, …hamna shida hapo kabisa, huhitaji kupiga debe, kwahiyo hilo lilikuwa wazo langu toka awali...’akasema

‘Wakati unarudi uliwasiliana na wafadhili wako wa huku na hukujua kuwa huenda mfadhili wako wa huko anawasiliana na, huyu  mfadhili wawa huko nchini?’ akaulizwa

‘Hapana….kuja kwangu nilitaka iwe kwa mshitukizo, na sikutaka kabisa huyo mdhamini wangu ajue,..’akatulia

‘Ni kweli ni lazima hao wafadhili watakuwa wakiwasiliana, hilo nilikuwa na shaka naloo na mara kwa mara nilijaribu kumuuliza mfadhili wa huko kuwa je anawasiliana na mfadhili wa huko nyumbani, yeye alisema, kazi yake ni kuniongoza nikiwa hapo, hana haja ya kuwasilina na huyo mdhamini wa huku nyumbani, kwanza hana mda huo, kwahiyo nisiwe na shaka, nilimuamini kwa kweli…’akasema

‘Huyu mdhamini wahuko ni mtu hapa nchini?’ akaulizwa

‘Ndio lakini yeye keshaukana uraia wa huku, anasema hataki hata kuitwa mbongo, yeye maisha yake na familia yake ni huko huko, na ameoa mtu wa huko, hata kuongea, maisha yake, yamekuwa ya kihuko huko….’akasema

‘Je wakati wewe unakwenda huko ulikuwa umeshaoa..?’ akaulizwa

‘Nilikuwa na mchumba niliyemuacha nyumbani, na matarajio yangu ilikuwa nikirudi tu tunafunga ndoa kwanza.. nilishajiona matawi ya juu, sibabaishwi tena na mtu, nilishazimia kuwa hata nikikutana na huyo mfadhili wa huko nyumbani, aaah, nitamwambia kuwa nitamlipa gharama zake tuachane, nilitaka niwe na uhuru, na isitoshe, nilishapata ajira huko Ulaya,nina wasiwasi gani, nilishasahau kabisa kuhusu masharti kwenye mkataba tulioandikishiana wakati nakuja kusoma. ....’akasema

‘Kwahiyo sasa ukafanyeje?’ akaulizwa

‘Nilipomaliza masomo yangu, nikarudi nchini, na nilifika bila kumuarifu mtu, nilikuwa nimepata pesa nyingi tu kutoka huko, pesa za kufanya vyema, na kuwa mwanafunzi bora, zawadi nyingi ….kiujumla nlikuwa na matji si haba, pia nilipewa na hiyo hospitali niliyoingia nayo mkataba, kama pesa ya kujikimu na mkopo kidogo kutoka hapo hapo , mkopo nafuu, wenyewe walisema wanaweza kuja kuufuta tu…’akatulia

‘Kwahiyo pesa hiyo ndio iliyoniwezesha kuanzisha hospitali hiyo kisiri, nikijua kuwa  hayo nayafanya kwa siri,  kumbe mwenzangu alikuwa akijua yote hayo, toka naingia nchini ananifuatilia kwa siri,  kila ninachokifanya alikuwa nacho kwenye kumbukumbu zaje akaacha hadi nikafungua hospitali, nikajulikana, na ndipo akanitumia ujumbe kuwa ananihitaji, siku ambayo kesho yake nilitakiwa kwenda kuanza kazi Ulaya..’akasema

‘Kwahiyo hukuonana naye uso kwa uso, yeye alikutumia ujumbe, kwanini usikate huo ujumbe, ukakubali kwenda kuonana naye?’ akaulizwa

‘Huyo jamaa alijiandaa vyema, alikuwa na kila njia za kunifanya nimfuate yeye, alikuwa na kumbukumbu zangu zote za nyuma, na alishawasiliana na polisi,, polisi wakampa  barua ya kunizuia mimi kutoka nje ya nchi,..mpaka mdhamini wangu akubali, je hebu niambie hapo ningelifanya nini, nikawa sina jinsi...nikaenda kuonana naye, na siku hiyo kumbe kulikuwa na watu kama mimi, waliopelekwa kusomeshwa kama mimi, tukajikuta tumekutana kwenye ukumbi maalumu.

‘Tulikumbushwa masharti na mikataba yetu, na huyo jamaa akasema nia yake sio kumkwaza yoyote, yeye anachotaka ni kupata msaada kutoka kwenye fani tulizosomea,  kwa kuingia ubia, hataki zaidi, yeye atawekeza kwenye vitega uchumi vyetu…’akatulia

‘Alisema yeye atawekeza hisa, asilimia fulani, kwenye kila kitega uchumi tulichoanzisha, ..na hutaaamini kila aliyerudi kutoka huko nje, alikuwa na wazo kama langu, la kuanzisha kitega uchumi, kujiajiri, na yoe hayo alikuwa akiyafahamu…..akasema nia ni kuendelea kutusaidia kwa kuongeza mtaji kwa kila mmoja wetu, ili kutuwezesha tuwe na vitega uchumi vikubwa vyenye faida, na atatupa wataalamu ambao watatuwezesha tufanye vizuri zaidi…’akatulia

‘Ni mjanja sana huyu jamaa, alitupika kisayansi, na tulijikuta tukikubaliana naye, tukawekeana mkataba kuwa ili kulipa fadhila na ili aweze kuendelea kutulinda , ni vyema tuwe na y eye, tufanya kazi na yeye, na anatoa mwaka mmoja tu, ukiisha kile mtu ataendelea na shuguli zake binfasi...’aksema

‘Ukakubali?’ akauliza

‘Hivi ingelikuwa wewe ungelifanya nini, ujue mdhamini wangu ndiye mwenye kibali cha kunifanya mimi nikafanye kazi nje, na kama ningelijua hayo yote mapema nikiwa huko ningelibakia huko huko, lakini sikujua hayo, ndio nikakumbuka kuwa kumbe hawa wadhamini wawili walikuwa wakiwasiliana na walifanya mbinu ili nirudi nchini, na nikirudi tu, nikutane na hichi kibano.

‘Kwahiyo ukajiunga na kundi hilo haramu kwa kazi yako hiyo ya ugaidi, au hukuambiwa moja kwa moja unatakiwa kulipa fadhila gani ....’akaambiwa.

‘Haikuwa hivyo moja kwa moja, mimi niliendelea na kazi zangu, na siku moja akaja mtaalamu ambaye niliambiwa atakuja kuonana na mimi, akaniambia;

‘Tunafahamu kuwa huko nje ulikuwa ukisomea mambo haya….akanionyesha kwenye laptop yake, jinsi ya kutengeneza sumu, ..ambayo akiwekewa mtu anatapatwa na shinikizo la damu, ..na baadaye anaweza kufa, na hata wakija kumpima wajue ni shinikizo tu la damu.

‘Ya nini hayo, …?’ nikamuuliza kwa mashaka

‘Tunahitaji vidonge kadha, kwa ajili ya majaribio…’akasema

‘Majaribio kwanani, huoni kuwa ni hatari..hapana mimi iswezi hilo’ nikamwambia, na mara akapiga simu kwa bwana mkubwa, na bwana mkubwa akajitokeza kwenye laptop yangu…’akatulia

‘Akajitokeza kwa vipi?’ akaulizwa

‘Yeye haonekani, kinachoonekana ni picha ya mtu akiangalia dunia, anayoiita ‘dunia yake’…alisema hiyo picha ndiyo inyomuwakilisha yeye, hataonekana kwa njia nyingine yoyote ile…’akasema

‘Kwahiyo hata uliporudi hukuwahi kuonana na huyo mtu uso kwa uso….?’ Akaulizwa

‘Sikuwahi hata mara moja,..akihitaji jambo anakuja kwa njia hiyo, kwanza anatuma mtu, halafu naambiwa niangalie kwenye laptop yangu, anajitokeza, kusadikisha huo ujumbe..’akasema

‘Lakini wewe utakuwa ukimfahamu kisura, na huenda una picha yake…’akaulizwa

‘Niwaambie ukweli, huyu jamaa ni mtu waajabu sana, mnakumbuka nilisema tulisoma naye, 
lakini mimi nilikuwa sipo karibu naye, hata sura yake ..haikuwa makini kwangu sana, hata siku ile tulipokutana naye akitaka mimi niende kwenda kusoma, alikuwa kavaa mawani meusi…ambayo yanaficha sura yake…hata akiyavua anakuwa anaangalia sehemu nyingine.

‘Kitu kingine cha ajabu nakumbuka katika kupenda kupiga picha tukiwa shule. Huyu jamaa alikuwa hapendi, na akipiga picha huharibika, ikafikia hatua hakuna aliyependa kupiga picha naye,..nakumbuka sana hilo tukio, na alikuwa na mtatizo ya macho kwahiyo siku zote anaishi na mawani machoni, toka utotoni,…kwahiyo sura yake, ilikuwa ni ya kujificha ficha….’akasema

‘Kwhiyo kwa ujumla huna picha yake, na sura yake haipo makini kichwani mwako?’ akaulizwa

‘Huo ndio ukweli wenyewe..ila kama nitaiona picha yake ninaweza kusema huyo ndiye mwenyewe, kwa vile namfahamu, lakini sijui, sina uhakika sana na hilo…’akasema

‘Je hiyo picha anayosema inamuwakilisha yeye ambayo hujitokeza akitaka kuongea na yeye, sio picha yake?’

‘Sio picha yake kabisa,…yeye anasema alivyokaa huyo jamaa, anawakilisha hisia zake…..’akasema.

‘Sasa hebu tuambie, kuhusu kifo chake….

WAZO ZA LEO: Dharau, kiburi sio jambo jema, tusipende kuwazarau watu kwa hali yoyote ile, inawezekana mtu akataka kukupa ushauri kwa nia njema tu,…wewe kwa dharau, ukakimbilia kuangalia hali ya huyo mtu, kuwa eti anatoka daraja la chini au wewe umemzidi kielimu, kiuchumi nakadhalika…hilo sio jambo jema.

Kiubinadamu, hata kama umesoma, huwezi ukawa unafahamu kila kitu, na huenda ushauri wa huyo mtu  ukaweza kukusaidia katika matatizo uliyo nayo, au hali unayokwenda nayo, ..

Muhimu,  katika maisha yako, kutokudharau jambo, hasa linahusu ushauri,.. usikimbilie kukataa wito au ushauri kutoka mtu, sikiliza kwanza, na wewe baadaye utakuja kuchuja, huenda katika maneno hayo, au ushauri huo,  ukajifunza jambo jipya, likaja kukusaidia au kukuokoa.

Ni mimi: emu-three

1 comment :

Mtanzania Halisi said...

Katika wazo la leo umezungumzia dharau. Naungana mkono na wewe tena kinachonikera ni kwamba kuna watu huwa wakiwe na vijifedha kidogo basi we mwenzangu na mimi ukimshauri jambo la maisha anakuona huna maana, pia vijana siku hizi wanaposhauriwa na wazazi wao kuhusu maisha huwa wanadharau wakiamini kuwa maisha yamebadilika hivyo wazazi wake hawana wanachojua kuhusiana na maisha ya sasa. Kibaya zaidi ni kuwa huwa WANAONYESHA dharau hiyo usoni