Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, January 21, 2014

Mkuki ni kwa Nguruwe-imefika mwishoniManeno kutoka kwa mtunzi.

Kisa chetu cha mkuki kwa nguruwe kimefika mwisho, na nafahamu kila mtu ana maoni na mtizamo wake, lakini tukumbuke kuwa kisa hiki ni cha kweli kilichomtokea mwenzetu mwanadada, utaona hata jina lake sikupenda kulitaja, kwa nia njema kabisa. ...mimi kama mtunzi nimejaribu kutia madoido tu,....

Kuna watu wengi wanasema kwanini sipendi kutumia majina ya watu,..natumai kila mtu ana mtindo wake wa kuandika visa kama hivi, na mimi nimeona niwe na namna yangu, ya kuandika visa hivi, kwahiyo tujaribu kuutizama mtindo huu wa aina yangu, ...na wale waliodai wanahitajia picha yangu, mmh, nawaomba mkubali mtindo wangu huo, kuwa picha yangu ni hayo ninayowatolea. Maelezo, visa na maneno ya hekima na busara yanatosha kabisa kuwa picha yangu.

Sasa kabla sijaweka hitimisho hilo, ambalo lipo tayari, limeshakamilika, nilikuwa napenda kidogo kusikia maoni ya watu, je wewe kama wewe ulihitajia mwanadada atoe maamuzi gani, maana ndoa na maamuzi ya ndoa sio rahisi kihivyo, kila mtu ana mtizamo wake....nitashukuru kila aliyekipitia kisa hiki akasema lolote, tuwe pamoja, ...

Bado natafakari ni kisa gani kifuate, kuna kuna visa viwili vipo jikoni, na vyote ni matukio halisi yaliyowakuta wanzetu ambao bila uchoyo wameamua kuyatoa hadharani ili kila mwenye hekima ajifunze, ..kwahiyo mwisho wa kisa hiki ni mwanzo wa kisa kingine. Wewe kama mdau muhimu unawajibu wa kuchangia mawazo na vyovyote vile uinavyo,..ili mtunzi emu-three naye ajione yupo na watu wanaojali kazi yake.


Nawashukuruni sana, na karibuni kwa maoni...

Ni mimi: emu-three

4 comments :

NUSHRI J KADUSI said...

HONGERA KWA KAZI NZURI.MI NASUBIRI UYO MWICHO

Iddi said...

Ni kisa kizuri nakushauri uandae tamthilia yake ni hakika kama itaonehswa katika TV itasisimua zaidi na kuwavutia wengi.
Na kuhusu mke wa familia nahisi ataendelea kuishi na mumewe.Na kuyasahau yaliyopita.

Liz said...

Kama mimi mume akikubali kuwa amekosa na kuomba msamaha wa dhati nitamsamehe, ila akiendelea kukataa siwezi msamehe coz hataki kuwa mkweli kwangu.

mama brenda said...

Dah kisa kizuri na kinasikitisha pia kinafundisha tuwe makini tunapotoa ushauri cha muhimu ni kumsamehe mumewake maisha yaendelee no way out but mapenzi hayatakuwa kama mwanzo hasa kwa mwanamke ameumia sana jipe moyo dada kwavile kaumbuka labda anaweza kuwa mumebora ila sina uhakika coz kunguru ni kunguru tu hafugiki.wanaume badilikeni mnatuumiza jamani nasisi wanawake tuwe tunasikiliza wazazi wanaona mbali tabia za kiasili nyingine ngumu kumbadili mtu.