Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, December 27, 2013

Mkuki ni kwa Nguruwe-55 Shahidi rafiki yangu akawa anaendelea kutoa maelezo yake, maelezo yaliyonifanya nibakia nikiwa siamini, nilijikuta naweza kidole mdomoni, huku nikijuzia kulia, ....kwakweli inasikitisha sana, yasikie kwa wenzako, lakini usiombe yakutokea wewe...

Rafiki ayngu akasema;

'Nilipoongea na rafiki yangu yaani mke wa familia na yeye kunipa msimamo wake, msimamo  tofauti na nilivyofikiria mimi awali. Unafahamu unaweza uakatenda jambo ukiwa na matumaini mema kabisa, lakini wakati lile jambo linakamlika, mwenzako ambaye ulijua yupo nawe, kumbe hakupenda wewe ulifanye, japokuwa wakati unataka kulifanya alionyesha kuwa upo nawe, hapo utahisi nini, unaweza ukahisi kuwa huenda ni wivu.

Msimamo wa rafiki yangu, ulionekana tofauti na nilivyotarajia mimi, nilijikuta nikiyatafakari yale mawazo yake, ule ushauri wake, ambao nilijua kuwa ulikuwa na nia njema kwangu. Kumbe mawazo na ushauri wake ulikuwa ni mkuki kwa nguruwe, kuwa niwatendee wengine, ambao hawana uchungu na waume zao, lakini kwa mume wake, kwa vile ni binadamu nisimguse....

Kauli yake hiyo ilinifanya nianze kufikiria mara mbili, nakufahamu kuwa kuanzia sasa neno urafiki litakuwa ni kama nembo tu, lakini siku ukweli ukizihiri, neno hilo litabadilika haraka na kuitwa jina jingine, na sio siri, litakuwa ni `uadui’ .

Kwa mtizamo huo basi, hata ule ukweli niliotaka kumwambia kuhusu yaliyotokea nyumba, kuhusu tabia ya mume wake ya siri, ulinifanya nigeuze kibao, na kuficha hayo yote na kupanga uwongo,  ilibidi sasa nidanganye, lakini ilikuwa sio kazi rahisi kutunga uwongo, wakati ukweli upo dhahiri, na baya zaidi akaingia huyu mdudu mtu, akaniweka kubaya,..

Kwakweli, sikutegemea na sikupenda maisha yangu yawe hivyo, sikutaka kabisa , lakini hili lililotokea likanifanya na mimi nijunge kwenye kundi la watu wachafu duniani...,nilianza kuwaza mambo ambayo nilikuwa nayapiga vita, mambo ambayo mimi niliajiriwa kuyachunguza na kuhakikisha yanafikishwa kwenye vyombo husika, sikutemea kabisa..

Siku rafiki yangu ananitamkia kuwa siku akimgundua mtu anayetembea na mume wake atamkamatisha kwa wale wahuni hatjsli kuwa ni ndugu yake au ni rafiki yake nikajua sasa nimekwisha, nilichofanya ni kutuma maombo yangu haraka, niwahi kwenda kusoma, japokuwa mwanzoni, niliomba yasogezwe mbele kwa vile nimajifungua. Wakanikubalia, niwahi kwenda, na hili sikumfahamisha rafiki yangu ikawa kama kumshitukizia.

Nilipokubaliwa ombi langu la kuwa niaweza kwenda kusoma nafasi yangu bado ipo wazi,, nikaamua kuacha shughuli nyingine zote ikiwemo hiyo ya uchunguzi, wa kumgundua mpenzi wa mume wa familia, na pia kuacha shughuli zote alizonipa rafiki yangu ya kuchunguza ni nani anayemzuzua mume wake, nilitakiwa nijichunguze mwenyewe kwasabbu anayemzuzua mume wake ni mimi , japokuwa kuna huyo mpezi wake wa asil lakini kwa muda huo nilikuwa ni mimi ninayetafutwa, sasa ningechunguza kitu gani, wakati mtu ninayetafutwa ni mimi...

Kwahiyo wakati anondoka nilishapanaga mbinu kuwa ili kuendelea kujificha ni bora ni mtafute huyo mpenzi wa mume wa familia wa asili ili nije kumwambia mke wa familia kuwa huyu ndiye mtu unayemtafuta, huyu ndiiye anayemzuzua mume wako, .....lakini kazi ikawa kumjua huyo mtu, ...

Kama ningekuwa nimetulia vyema, isingelichukua muda kumtambua huyo mpenzi wake, ni nani, lakini nilikuwa na mambo mengi ya kufanya na moja ni kusoma, na hilo nikalipa kipaumbele nikijua kuwa ndilo litakalo kuja kunisaidia baadaye hata kama rafiki yangu atakuwa hanitaki tena, nitaweza kujiajiri au kuajiriwa sehemu nyingine,

Wakati nipo kwenye kitabu huku nalea huku kichwa kikifanya kazi ya ziada huku nikisumbuliwa na simu kuutoka kwa rafiki yangu, nikaona kuna umuhimu wa kumpa hii kazi mtu mwingine, mtu ambaye ninamuamini, na nikaanza kuwachuja rafiki wangu ninaowatumia kwenye kazi zangu, nikagungua kuwa kuna mtu wangu mmoja wa karibu sana ambaye nikimpa hiyo kazi anaweza kuifanya bila matatizo, lakini yeye alishaniambia kuwa anataka kuacha kazi , hataki tena kufanya kazi anayoifanya, kwa sababu zake za kifamilia, sikuweza kujua ni sababu gani, nay eye hakutaka kuniambia, kwa haraka nikahisi huenda mke wa familia keshanigundua na sasa anawazua watu wote walio karibu na mimi wasinifanyie kazi.

Unapofanya kazi kama ya kwangu unaweza ukawa na watu wako, hata muajiri wako asiwafahamu hata mume wake anaweza asijue kuwa mke wake anafanya kazi kama hiyo, na huyu mtu ninayekuambia, nina uhakika hata mume wake,alikuwa hajui kuwa anafanya kazi kama hiyo, hiyo ndio siri kubwa ya kazi yetu.

Aliponihakikishia kuwa yeye sasa hayupo na mimi, nikamwambia, kabla hatujaachana namuomba tena sana anisadia kazi moja kubwa, akaniuliza kazi gani, nikamwambia, kwanza nataka anichunguzie huyu mtu anayeitwa Makabrasha, nilipomtajia hilo jina, nilihisi jambo, kwani alihema kwa nguvu, nilihisi hivyo kwenye simu, maana nilikuwa nawasiliana naye kwenye simu, baadaye akaniuliza;

‘Kwanini unamtaka huyu shetani....’akasema, na alivyotamka hilo neno shetani, nikahisi kuna jambo kati yake na huyo Makabrasha. Mimi nikamwambia kwa kifupi;

‘Huyu mtu anataka kuniingila kwenye maisha yangu binafsi, na naona nikimuachia ataniharibia mpangilio wa maisha yangu..’nikamwambia.

‘Nilijua tu, ....huyu mtu anataka kumjaribu kila mtu, ili afanikiwe jambo lake, na kinachonishangaza ni kuwa hata polisi wanasindwa kumshika, ni mjanja kupita maelezo, lakini mimi naona hapo alipofikia kavuka mpaka, kuna haja ya kumuwahi kabla hajafika mbali...’akaniambia.

‘Kwahiyo unasemaje, upo tayari kuifanya hiyo kazi, ...au?’ nikamuuliza

‘Umesema kuna kazi mbili, hiyo ni ya kwanza , kazi gani ya pili unataka niifanye, lakini sio kwa mkataba, kama nitafanya kazi kwako, ni kazi ya kupita tu, ikiisha au hata kama hitaisha sima makubaliano na wewe....’akasema.

‘Huyo mume wa familia, mke wa bosi wetu, ana mpenzi wake wa zamani, na weni hatumjui, nakata unitafutie huyo mpenzi wake alikuwa ni nani,...hapo sikusema mume wa familia, nilimtaja kwa jina lake. Cha ajabu, simu ilikatika, nailionyesha kuwa haikukatika yenyewe, ni kuwa huyo mtu wangu aliamua kuikata, na hata nilipompigia simu, ikawa inaita tu, hapokei. Nilimpa muda, kama masaa mawili nikampigia tena..

Alipokea na nikamuuliza kwanini alikata simu, akaniambia kuna mtu alifika, na hakutaka asikie anaongea na mimi, lakini nilihisi sio kweli, alikata hiyo simu kwa jambo maalumu binafsi, nikamuuliza.

‘Mimi nahisi una jambo na hawa watu wawili, Makabrasha na huyo mume wa familia, naona kuna jambp linakugusa, nakufahamu sana...’nikamwambia.

‘Sinimeshakuambia kuwa Makabrasha sio mtu mwema, ...’akasema kwa mkatao.

‘Kwahiyo utazifanya hizo kazi mbili nilizokupa, ni muhimu sana kwangu?’ nikamuuliza

‘Hapana, sitaki kufanya kazi kwa mtu mwingine yoyote kwa sasa, nataka kufanya mambo yangu binafsi, naomba unielewe hivyo, sijawahi kukutalia kazi yoyote, ...kwahiyo ukiona nafanya haivyo ujue kuna jambo kubwa,...’akasema

‘Na mimi ukiona ninakupa akzi hiyo wewe peke yako ujue ina umhimu sana, tafadhali, ..huwa wakati wote natoa amri kwako, lakini hii hii ninakuomba, ni muhimu sana kwangu..’nikamwambia.

‘Mhh,.... ama kwa Makabrasha, hiyo kazi ninaweza nikaifanya, lakini sio kwa hiyo kazi nyingine, hiyo nyingine siwezi kuifanya kabisa.

‘Kwanini , kwani huyo una hisa gani na yeye?’, nikamuuliza .

‘Naomba unielewe tu hivyo, sina sababu nyingine za msingi, ni maswala binafsi, hayamuhusu mtu...’akasema.

‘Sikuelewi, mpendwa, hiyo ni kazi maalumu, na ni muhimu sana, ndio maana nimekuomba wewe tu, na sio mtu mwingine...’nikajaribu kumsisitizia, na yeye akasema;

‘Ndio maana nimeamua kuacha kazi, kwani nafahamu hili litakuja na mengine mengi ambayo yataharibu mambo yangu binafsi, ni heri niache kazi mapema, ili niweze lufanikisha mambo yangu...’akasema.

‘Kwahiyo hiyo kazi kumuhusu Makabrasha , utaifanya , lakini kwa huyo mtu mwingine, ndio umesema hutaiweza, kwasababu zako binafsi,ehe?’ nikamuuliza, nay eye akasema.

‘Hiyo ya makabrasha nitaifanya tu kwa vile nimeona inaingilia na kazi zangu zingine binafsi,...japokuwa kwa ujumla sikutaka niifanye hiyo kazi kwa shinikizo la mtu mwingine, sikutaka kumshirikisha mtu, lakini kwa vile na wewe una muhitaji, basi tupo pamoja, ...’akasema.

‘Kwani kuna nini kikubwa zidi yako na Makabrasha ..?’nikamuuliza.

‘Unaona, ....sitaki mtu kuniingilia hayo mambo yangu, kama unataka niifanye hiyo kazi, sitaki kuniuliza maswala yangu mimi, nitakuambia yale unayoyataka, lakini usiniulize kuhusu mimi, ya kwangu niachie mimi mwenyewe...’akasema

‘Mhh, safari hii nakuona mwenzangu unaniacha njia panda, sijui kuna nini kinaendelea huko bongo, imafikia hatua hii, mnanipa wasiwasi sana...’nikasema.

‘Wewe maliza masomo yako, mengi unayafahamu, ...ila kwa kifupi, huyu jamaa, anayejiita mwanasheria, ni mtu mbaya sana, kuliko unavyofikiria wewe, hata hivyo, siwezi kukuambia lolote mpaka nimalize uchunguzi wangu, na sikutaka niyaongee haya kwenye simu na kwa mtu yoyote, mpaka nimalize kazi yangu...’akasema

‘Basi ukiwa tayari kuhusu huyo mtu tutaongea ili nijue tufanye nini, ni muhimu sana, nakuomba ulifanyie kazi hilo, na kwa huyo mtu mwingine nitajua nini cha kufanya, hata hivyo nina ombi moja kwako...’nikamwambia

‘Ombi gani...’akaniuliza

‘Ninakazi kubwa, nina mipanglio mingi ya kimaisha, nikimaliza elimu yangu huku nataka tuwe wabia,.kwahiyo ninakuomba usiache kazi yako kwangu  hadi nirudi kuna mengi nataka tuyafanye pamoja...’nikamuombia .

‘Hilo halitawezekana, hata hili la Makabrasha, nalifanya tu, lakini sio kwa ajili ya mkataba na wewe, mkataba wangu na wewe umeshafungwa, sitaki kujishughulisaha na mambo yako tena, kwa manufaa ya wengi, nakuheshimu sana kama bosi wangu,lakini kwa hili la sasa, sitamuheshimu mtu....’akasema.

‘Sawa nimekuelewa, lakini mimi nina imani kuwa tupo pamoja, hata kama kuna mambo yametokea ya kukwaza, bado tuna mafungamano ya kikazi, unafahamu kazi zetu hizi zilivyo, unaweza ukasema humuhitaji mtu, baadaye iaktokea jambo ukamuhitajia sana mtu wako wa zamani, usitupe mti na jongoo wake..’nikamwambia

‘Kwa hayo yaliyotokea, sizani kama kuna mshikamano tena, naomba tuishie hapo ,na ni vyema usitake kujua mengi zaidi....nafahamu mengi yametokea, kwa vile kulikuwa hakuna njia nyingine, lakini hata hivyo,kuna sehemu unafika unaona kuwa usiposimama kwa mguu wako mwenyewe, itafika muda wenzako watachoka, watakuachia, na unaweza ukadondoka, nimechoka kutumiwa, ..nataka kujituma mwenyewe..’akasema

Kwakweli sikumuelewa, na nikaona nimuache kwanza, ili nije niongee naye baadaye, na wakati natafakari  hilo, mara nikapokea simu,na ujumbe mnzito, ukiniambia nahitajiwa Dar haraka, nikasaini mkataba wa hiari, dhidi yangu na mzazi mwenzangu, na kwa msisitizo, ule ujumbe ukaambatishwa na picha, mojawapo ya picha mbaya, ambazo zilionyesha yale niliyokuwa nikifanya na mume wa familia, hiyo ikiashiria vitisho, kuwa nisipofanya hivyo, picha hiyo itafikishwa kwa walengwa.

Nilipopata huo ujumbe nikampigia simu huyu mtu wangu wa karibu, nikamwambia anifanyie uchunguzi, ni kitu gani kinaendelea kati ya Mume wa familia na mkataba wake, ...n a hapo mtu wangu huyo, akaniambia hilo ameshalifanyia kazi, na kusema;

‘Mume wa familia kaingia kwenye mtego na adui yetu, kwahiyo inabidi afanye kila anachotaka huyo adui yetu, ikiwemo kukubali kuingia na adui yetu kwenye mkataba unaoidhinisha adui yetu kupata hisa kwenye makampuni ya bosi..’akaniambia.

‘Haiwezekani...’nikasema kwa mshituko mkubwa.

‘Ndio hivyo, kuna mengi yamefanyika, na mshika usukani ni huyo adui yetu, inavyoonekana ni kuwa huyu adui yetu kaingilia mambo mengi, lakini nia na lengo lake ilikuwa kuingiza makucha yake kwenye mali za bosi wako, hasa kwenye makampuni yake, na ukumbuke kuwa bosi wako na mume wake hawapo kwenye mahusiano mazuri, japokuwa kuna hali ya kibinadamu inayowafanya waendelee kuitwa mume na mke...’akasema.

‘Hali gani hiyo ya kibinadamu?’ nikamuuliza.

‘Ya ugonjwa wa mume wa familia, nahisi kama isngelikuwa huo ugonjwa wa mume wa familia, hiyo nd isingelikuwepo tena...’akasema.

‘Kuna nini kikubwa ulichokigundua, kilichosababisha  hadi hiyo ndoa iingiwe na tatizo kubwa kiasi hicho, ni mambo yao ya ndani kwa ndani au kuna msukumo mwingine kutoka nje...?’ nikamuuliza.

‘Hayo unayafahamu sana wewe, sioni haja ya mimi kukuambia, japokuwa kuna mbinu zilizotoka nje, zilizojengwa kitaalamu sana na wajnja, ili ionekane hivyo ilivyo, kwa muda niliofanya uchunguzi wangu, nimegundua mengi, kumbe hata wewe upo kwenye mchakato huo, sikutegemea, ....imeniuma sana, kuwa kumbe nafanya kazi kwa mtu ambaye ni mmoja wa watu wanaonichoma kisu moyoni mwangu...’akasema akiongea kwa sauti yenye huzuni.

‘Una maana gani,kwanini huniambii ukweli...nimekufanyia nini mimi kibaya , niambie ukweli, kama kuna jambo nimekukosea, ni bora uniambie, huenda kuna sababu ya msingi ya mimi kufanya hivyo, ila wewe hufahamu’ nikamuuliza na kujaribu kumuelezea, ili nifahamu ni jambo gani hilo, nililolifanya hadi mwenzangu afikie kuumia kiasi hicho.

‘Ukweli unaoufahamu wewe unatosha, na nakushauri ufanye walivyotaka hawa watu, fika huku nyumbani, ufanye wanavyotaka wao, baada ya hapo, mengine yatafuata, kwa hivi sasa wameshikilia mpini, ukikosea kidogo utakuja kujuta,..’akaniambia.

‘Ina maana hata wewe upo kundi moja na hawo watu,unavyoongea ni kama unashirikiana nao?’ nikamuuliza

‘Hata siku moja siwezi kama huyu kushirikiana na hawa mashetani, hili ninalokushauri ni kutokana na uchunguzi wangu, ndio wengi wanaona nipo na huyu jamaa lakini ni kwa ajili ya kazi zetu. Siku nikimaliza hii kazi, kila kitu kitakuwa hadharani, na nitahakikisha kuwa kama kuna kundi, kama kuna njama, basi zitafikia kikomo chake...kama ni kundi, nikitoka kwa huyu nitakwena kwa mwingine, mpaka nihakikishe nimemaliza kazi...’akaniambia

‘Unaposema kundi, au watu wengine ni akina nani, inaonyesha umeshawagundua?’ nikamuuliza

‘Mhh, hayo ni mambo binafsi, siwezi kukuambia zaidi ya hapo, lakini cha muhimu ni kuhakikisha kuwa hili jambo nimeliweka sawa, nataka kuhakikisha kuwa hawa wananitesa moyo wangu, wanasambaratika, na hakuna kitu kama hicho tena, na kama ni njama, zinazofungamana na mwenza wangu, nitahakikisha nazifahamu, na kama yeye anahusika, ataumbuka, na atanikumbuka milele..’akasema

‘Mhh, sasa hapo unazidi kunichanganya, na huyo mwenza wako ndio nani tena ?’ nikamuuliza

‘Ni moyo wangu.....ni, ni....’ simu ikakatika, na ilikatika kama vile mtu kapatwa na tatizo, ikanibidi nipige simu, kwa mtu wangu mwingine, yeye ni msaidizi wake, katika mambo yetu ya utendaji, nikamhoji, kuna nini kinaendelea akaniambia ni kweli huyo mtu wangu kaamua kuacha kazi kwasababu zisizojulikana na hajamwambia yoyote ni sababu gani, ni siri yake kubwa sana.

‘Kwahiyo hana kazi yoyote yupo nyumbani tu, au ana kazi gani maalumu anaifanya kwa sasa...?’ nikamuuliza

‘Nimemuona kama anafanya kazi kwa mtu, lakini sio kwa muda wote, ni mara chache sana, mara nyingi anaonekana yupo peke yake, kuna jambo linamtatiza, anakuwa kama kachanganyikiwa..’akasema.

‘Kwa mtu gani huyo anapoonekana akifanya kazi ...unamfahamu?’ nikamuuliza

‘Ndio namfahamu,huyo mtu anafahamika sana...’akasema

‘Ni kwa nani hapo anapofanya kazi, nipe taarifa kamili, sio unanipa taarifa kama unaogopa, ni kwa mtu gani anapofanya kazi kwa sasa?’ nikamuuliza kwa hasira

‘Ni kwa Makabrasha, ...mara nyingi anaonekana ofisini kwa Makabrasha, inaonekana kaajiriwa na Makabrasha, au kuna kazi maalumu anamfanyia...’akasema na hapo hapo nikakata simu.
Sikupoteza muda nikapanda ndege na kuja Dar,ndivyo ilivyokuwa kuja kwangu Dar, kwa ghafla ....


WAZO LA LEO: Mambo yanayohusu imani za watu , hisia za watu, upendo, nk ni nyeti sana, ni vyema, ukikutana na vitu kama hivi uwe makini sana kuviingilia. Mtu akiamini, akapenda, huona vingine vyote havina maana, anaweza hata akafumbia macho elimu yake, na akafanya mambo ambayo kwa elimu yake, hastahili kuyafanya hayo. Ndio maana wanasema, mwenye kupenda haoni, hata akiona kibaya kwake, ni kizuri, akiona chongo ataita ni kengeza.
Ni mimi: emu-three

No comments :