Shahidi rafiki yangu akawa anaendelea kutoa maelezo yake, maelezo yaliyonifanya nibakia nikiwa siamini, nilijikuta naweza kidole mdomoni, huku nikijuzia kulia, ....kwakweli inasikitisha sana, yasikie kwa wenzako, lakini usiombe yakutokea wewe...
Rafiki ayngu akasema;
'Nilipoongea na rafiki yangu yaani mke wa familia na yeye kunipa
msimamo wake, msimamo tofauti na
nilivyofikiria mimi awali. Unafahamu unaweza uakatenda jambo ukiwa na matumaini
mema kabisa, lakini wakati lile jambo linakamlika, mwenzako ambaye ulijua yupo
nawe, kumbe hakupenda wewe ulifanye, japokuwa wakati unataka kulifanya
alionyesha kuwa upo nawe, hapo utahisi nini, unaweza ukahisi kuwa huenda ni
wivu.
Msimamo wa rafiki yangu, ulionekana tofauti na nilivyotarajia
mimi, nilijikuta nikiyatafakari yale mawazo yake, ule ushauri wake, ambao
nilijua kuwa ulikuwa na nia njema kwangu. Kumbe mawazo na ushauri wake ulikuwa
ni mkuki kwa nguruwe, kuwa niwatendee wengine, ambao hawana uchungu na waume
zao, lakini kwa mume wake, kwa vile ni binadamu nisimguse....
Kauli yake hiyo ilinifanya nianze kufikiria mara mbili, nakufahamu
kuwa kuanzia sasa neno urafiki litakuwa ni kama nembo tu, lakini siku ukweli
ukizihiri, neno hilo litabadilika haraka na kuitwa jina jingine, na sio siri,
litakuwa ni `uadui’ .
Kwa mtizamo huo basi, hata ule ukweli
niliotaka kumwambia kuhusu yaliyotokea nyumba, kuhusu tabia ya mume wake ya
siri, ulinifanya nigeuze kibao, na kuficha hayo yote na kupanga uwongo, ilibidi sasa nidanganye, lakini ilikuwa sio kazi rahisi kutunga uwongo, wakati ukweli upo dhahiri, na baya zaidi akaingia huyu mdudu mtu, akaniweka kubaya,..
Kwakweli, sikutegemea na sikupenda maisha yangu yawe hivyo,
sikutaka kabisa , lakini hili lililotokea likanifanya na mimi nijunge kwenye
kundi la watu wachafu duniani...,nilianza kuwaza mambo ambayo nilikuwa nayapiga
vita, mambo ambayo mimi niliajiriwa kuyachunguza na kuhakikisha yanafikishwa
kwenye vyombo husika, sikutemea kabisa..
Siku rafiki yangu ananitamkia kuwa siku akimgundua mtu
anayetembea na mume wake atamkamatisha kwa wale wahuni hatjsli kuwa ni ndugu
yake au ni rafiki yake nikajua sasa nimekwisha, nilichofanya ni kutuma maombo
yangu haraka, niwahi kwenda kusoma, japokuwa mwanzoni, niliomba yasogezwe mbele
kwa vile nimajifungua. Wakanikubalia, niwahi kwenda, na hili sikumfahamisha rafiki
yangu ikawa kama kumshitukizia.
Nilipokubaliwa ombi langu la kuwa niaweza kwenda kusoma nafasi yangu bado ipo wazi,,
nikaamua kuacha shughuli nyingine zote ikiwemo hiyo ya uchunguzi, wa kumgundua
mpenzi wa mume wa familia, na pia kuacha shughuli zote alizonipa rafiki yangu
ya kuchunguza ni nani anayemzuzua mume wake, nilitakiwa nijichunguze mwenyewe
kwasabbu anayemzuzua mume wake ni mimi , japokuwa kuna huyo mpezi wake wa asil
lakini kwa muda huo nilikuwa ni mimi ninayetafutwa, sasa ningechunguza kitu
gani, wakati mtu ninayetafutwa ni mimi...
Kwahiyo wakati anondoka nilishapanaga mbinu kuwa ili
kuendelea kujificha ni bora ni mtafute huyo mpenzi wa mume wa familia wa asili
ili nije kumwambia mke wa familia kuwa huyu ndiye mtu unayemtafuta, huyu ndiiye
anayemzuzua mume wako, .....lakini kazi ikawa kumjua huyo mtu, ...
Kama ningekuwa nimetulia vyema, isingelichukua muda
kumtambua huyo mpenzi wake, ni nani, lakini nilikuwa na mambo mengi ya kufanya
na moja ni kusoma, na hilo nikalipa kipaumbele nikijua kuwa ndilo litakalo kuja
kunisaidia baadaye hata kama rafiki yangu atakuwa hanitaki tena, nitaweza
kujiajiri au kuajiriwa sehemu nyingine,
Wakati nipo kwenye kitabu huku nalea huku kichwa kikifanya
kazi ya ziada huku nikisumbuliwa na simu kuutoka kwa rafiki yangu, nikaona kuna
umuhimu wa kumpa hii kazi mtu mwingine, mtu ambaye ninamuamini, na nikaanza
kuwachuja rafiki wangu ninaowatumia kwenye kazi zangu, nikagungua kuwa kuna mtu
wangu mmoja wa karibu sana ambaye nikimpa hiyo kazi anaweza kuifanya bila
matatizo, lakini yeye alishaniambia kuwa anataka kuacha kazi , hataki tena
kufanya kazi anayoifanya, kwa sababu zake za kifamilia, sikuweza kujua ni
sababu gani, nay eye hakutaka kuniambia, kwa haraka nikahisi huenda mke wa
familia keshanigundua na sasa anawazua watu wote walio karibu na mimi wasinifanyie
kazi.
Unapofanya kazi kama ya kwangu unaweza ukawa na watu wako,
hata muajiri wako asiwafahamu hata mume wake anaweza asijue kuwa mke wake
anafanya kazi kama hiyo, na huyu mtu ninayekuambia, nina uhakika hata mume
wake,alikuwa hajui kuwa anafanya kazi kama hiyo, hiyo ndio siri kubwa ya kazi
yetu.
Aliponihakikishia kuwa yeye sasa hayupo na mimi,
nikamwambia, kabla hatujaachana namuomba tena sana anisadia kazi moja kubwa,
akaniuliza kazi gani, nikamwambia, kwanza nataka anichunguzie huyu mtu anayeitwa
Makabrasha, nilipomtajia hilo jina, nilihisi jambo, kwani alihema kwa nguvu, nilihisi
hivyo kwenye simu, maana nilikuwa nawasiliana naye kwenye simu, baadaye
akaniuliza;
‘Kwanini unamtaka huyu shetani....’akasema, na alivyotamka
hilo neno shetani, nikahisi kuna jambo kati yake na huyo Makabrasha. Mimi
nikamwambia kwa kifupi;
‘Huyu mtu anataka kuniingila kwenye maisha yangu binafsi, na
naona nikimuachia ataniharibia mpangilio wa maisha yangu..’nikamwambia.
‘Nilijua tu, ....huyu mtu anataka kumjaribu kila mtu, ili afanikiwe
jambo lake, na kinachonishangaza ni kuwa hata polisi wanasindwa kumshika, ni
mjanja kupita maelezo, lakini mimi naona hapo alipofikia kavuka mpaka, kuna
haja ya kumuwahi kabla hajafika mbali...’akaniambia.
‘Kwahiyo unasemaje, upo tayari kuifanya hiyo kazi, ...au?’
nikamuuliza
‘Umesema kuna kazi mbili, hiyo ni ya kwanza , kazi gani ya
pili unataka niifanye, lakini sio kwa mkataba, kama nitafanya kazi kwako, ni
kazi ya kupita tu, ikiisha au hata kama hitaisha sima makubaliano na
wewe....’akasema.
‘Huyo mume wa familia, mke wa bosi wetu, ana mpenzi wake wa
zamani, na weni hatumjui, nakata unitafutie huyo mpenzi wake alikuwa ni
nani,...hapo sikusema mume wa familia, nilimtaja kwa jina lake. Cha ajabu, simu
ilikatika, nailionyesha kuwa haikukatika yenyewe, ni kuwa huyo mtu wangu
aliamua kuikata, na hata nilipompigia simu, ikawa inaita tu, hapokei. Nilimpa
muda, kama masaa mawili nikampigia tena..
Alipokea na nikamuuliza kwanini alikata simu, akaniambia
kuna mtu alifika, na hakutaka asikie anaongea na mimi, lakini nilihisi sio
kweli, alikata hiyo simu kwa jambo maalumu binafsi, nikamuuliza.
‘Mimi nahisi una jambo na hawa watu wawili, Makabrasha na
huyo mume wa familia, naona kuna jambp linakugusa, nakufahamu
sana...’nikamwambia.
‘Sinimeshakuambia kuwa Makabrasha sio mtu mwema, ...’akasema
kwa mkatao.
‘Kwahiyo utazifanya hizo kazi mbili nilizokupa, ni muhimu
sana kwangu?’ nikamuuliza
‘Hapana, sitaki kufanya kazi kwa mtu mwingine yoyote kwa
sasa, nataka kufanya mambo yangu binafsi, naomba unielewe hivyo, sijawahi
kukutalia kazi yoyote, ...kwahiyo ukiona nafanya haivyo ujue kuna jambo
kubwa,...’akasema
‘Na mimi ukiona ninakupa akzi hiyo wewe peke yako ujue ina
umhimu sana, tafadhali, ..huwa wakati wote natoa amri kwako, lakini hii hii
ninakuomba, ni muhimu sana kwangu..’nikamwambia.
‘Mhh,.... ama kwa Makabrasha, hiyo kazi ninaweza nikaifanya,
lakini sio kwa hiyo kazi nyingine, hiyo nyingine siwezi kuifanya kabisa.
‘Kwanini , kwani huyo una hisa gani na yeye?’, nikamuuliza .
‘Naomba unielewe tu hivyo, sina sababu nyingine za msingi,
ni maswala binafsi, hayamuhusu mtu...’akasema.
‘Sikuelewi, mpendwa, hiyo ni kazi maalumu, na ni muhimu
sana, ndio maana nimekuomba wewe tu, na sio mtu mwingine...’nikajaribu
kumsisitizia, na yeye akasema;
‘Ndio maana nimeamua kuacha kazi, kwani nafahamu hili
litakuja na mengine mengi ambayo yataharibu mambo yangu binafsi, ni heri niache
kazi mapema, ili niweze lufanikisha mambo yangu...’akasema.
‘Kwahiyo hiyo kazi kumuhusu Makabrasha , utaifanya , lakini
kwa huyo mtu mwingine, ndio umesema hutaiweza, kwasababu zako binafsi,ehe?’
nikamuuliza, nay eye akasema.
‘Hiyo ya makabrasha nitaifanya tu kwa vile nimeona
inaingilia na kazi zangu zingine binafsi,...japokuwa kwa ujumla sikutaka
niifanye hiyo kazi kwa shinikizo la mtu mwingine, sikutaka kumshirikisha mtu,
lakini kwa vile na wewe una muhitaji, basi tupo pamoja, ...’akasema.
‘Kwani kuna nini kikubwa zidi yako na Makabrasha ..?’nikamuuliza.
‘Unaona, ....sitaki mtu kuniingilia hayo mambo yangu, kama
unataka niifanye hiyo kazi, sitaki kuniuliza maswala yangu mimi, nitakuambia
yale unayoyataka, lakini usiniulize kuhusu mimi, ya kwangu niachie mimi
mwenyewe...’akasema
‘Mhh, safari hii nakuona mwenzangu unaniacha njia panda,
sijui kuna nini kinaendelea huko bongo, imafikia hatua hii, mnanipa wasiwasi
sana...’nikasema.
‘Wewe maliza masomo yako, mengi unayafahamu, ...ila kwa
kifupi, huyu jamaa, anayejiita mwanasheria, ni mtu mbaya sana, kuliko
unavyofikiria wewe, hata hivyo, siwezi kukuambia lolote mpaka nimalize
uchunguzi wangu, na sikutaka niyaongee haya kwenye simu na kwa mtu yoyote,
mpaka nimalize kazi yangu...’akasema
‘Basi ukiwa tayari kuhusu huyo mtu tutaongea ili nijue
tufanye nini, ni muhimu sana, nakuomba ulifanyie kazi hilo, na kwa huyo mtu
mwingine nitajua nini cha kufanya, hata hivyo nina ombi moja
kwako...’nikamwambia
‘Ombi gani...’akaniuliza
‘Ninakazi kubwa, nina mipanglio mingi ya kimaisha,
nikimaliza elimu yangu huku nataka tuwe wabia,.kwahiyo ninakuomba usiache kazi
yako kwangu hadi nirudi kuna mengi
nataka tuyafanye pamoja...’nikamuombia .
‘Hilo halitawezekana, hata hili la Makabrasha, nalifanya tu,
lakini sio kwa ajili ya mkataba na wewe, mkataba wangu na wewe umeshafungwa,
sitaki kujishughulisaha na mambo yako tena, kwa manufaa ya wengi, nakuheshimu
sana kama bosi wangu,lakini kwa hili la sasa, sitamuheshimu mtu....’akasema.
‘Sawa nimekuelewa, lakini mimi nina imani kuwa tupo pamoja,
hata kama kuna mambo yametokea ya kukwaza, bado tuna mafungamano ya kikazi,
unafahamu kazi zetu hizi zilivyo, unaweza ukasema humuhitaji mtu, baadaye iaktokea
jambo ukamuhitajia sana mtu wako wa zamani, usitupe mti na jongoo wake..’nikamwambia
‘Kwa hayo yaliyotokea, sizani kama kuna mshikamano tena,
naomba tuishie hapo ,na ni vyema usitake kujua mengi zaidi....nafahamu mengi
yametokea, kwa vile kulikuwa hakuna njia nyingine, lakini hata hivyo,kuna
sehemu unafika unaona kuwa usiposimama kwa mguu wako mwenyewe, itafika muda
wenzako watachoka, watakuachia, na unaweza ukadondoka, nimechoka kutumiwa,
..nataka kujituma mwenyewe..’akasema
Kwakweli sikumuelewa, na nikaona nimuache kwanza, ili nije
niongee naye baadaye, na wakati natafakari hilo, mara nikapokea simu,na ujumbe mnzito,
ukiniambia nahitajiwa Dar haraka,
nikasaini mkataba wa hiari, dhidi yangu na mzazi mwenzangu, na kwa
msisitizo, ule ujumbe ukaambatishwa na picha, mojawapo ya picha mbaya, ambazo
zilionyesha yale niliyokuwa nikifanya na mume wa familia, hiyo ikiashiria
vitisho, kuwa nisipofanya hivyo, picha hiyo itafikishwa kwa walengwa.
Nilipopata huo ujumbe nikampigia simu huyu mtu wangu wa
karibu, nikamwambia anifanyie uchunguzi, ni kitu gani kinaendelea kati ya Mume
wa familia na mkataba wake, ...n a hapo mtu wangu huyo, akaniambia hilo
ameshalifanyia kazi, na kusema;
‘Mume wa familia kaingia kwenye mtego na adui yetu, kwahiyo
inabidi afanye kila anachotaka huyo adui yetu, ikiwemo kukubali kuingia na adui
yetu kwenye mkataba unaoidhinisha adui yetu kupata hisa kwenye makampuni ya
bosi..’akaniambia.
‘Haiwezekani...’nikasema kwa mshituko mkubwa.
‘Ndio hivyo, kuna mengi yamefanyika, na mshika usukani ni
huyo adui yetu, inavyoonekana ni kuwa huyu adui yetu kaingilia mambo mengi,
lakini nia na lengo lake ilikuwa kuingiza makucha yake kwenye mali za bosi
wako, hasa kwenye makampuni yake, na ukumbuke kuwa bosi wako na mume wake
hawapo kwenye mahusiano mazuri, japokuwa kuna hali ya kibinadamu inayowafanya
waendelee kuitwa mume na mke...’akasema.
‘Hali gani hiyo ya kibinadamu?’ nikamuuliza.
‘Ya ugonjwa wa mume wa familia, nahisi kama isngelikuwa huo
ugonjwa wa mume wa familia, hiyo nd isingelikuwepo tena...’akasema.
‘Kuna nini kikubwa ulichokigundua, kilichosababisha hadi hiyo ndoa iingiwe na tatizo kubwa kiasi
hicho, ni mambo yao ya ndani kwa ndani au kuna msukumo mwingine kutoka nje...?’
nikamuuliza.
‘Hayo unayafahamu sana wewe, sioni haja ya mimi kukuambia, japokuwa
kuna mbinu zilizotoka nje, zilizojengwa kitaalamu sana na wajnja, ili ionekane
hivyo ilivyo, kwa muda niliofanya uchunguzi wangu, nimegundua mengi, kumbe hata
wewe upo kwenye mchakato huo, sikutegemea, ....imeniuma sana, kuwa kumbe
nafanya kazi kwa mtu ambaye ni mmoja wa watu wanaonichoma kisu moyoni
mwangu...’akasema akiongea kwa sauti yenye huzuni.
‘Una maana gani,kwanini huniambii ukweli...nimekufanyia nini
mimi kibaya , niambie ukweli, kama kuna jambo nimekukosea, ni bora uniambie,
huenda kuna sababu ya msingi ya mimi kufanya hivyo, ila wewe hufahamu’
nikamuuliza na kujaribu kumuelezea, ili nifahamu ni jambo gani hilo,
nililolifanya hadi mwenzangu afikie kuumia kiasi hicho.
‘Ukweli unaoufahamu wewe unatosha, na nakushauri ufanye
walivyotaka hawa watu, fika huku nyumbani, ufanye wanavyotaka wao, baada ya
hapo, mengine yatafuata, kwa hivi sasa wameshikilia mpini, ukikosea kidogo utakuja
kujuta,..’akaniambia.
‘Ina maana hata wewe upo kundi moja na hawo watu,unavyoongea
ni kama unashirikiana nao?’ nikamuuliza
‘Hata siku moja siwezi kama huyu kushirikiana na hawa
mashetani, hili ninalokushauri ni kutokana na uchunguzi wangu, ndio wengi
wanaona nipo na huyu jamaa lakini ni kwa ajili ya kazi zetu. Siku nikimaliza
hii kazi, kila kitu kitakuwa hadharani, na nitahakikisha kuwa kama kuna kundi,
kama kuna njama, basi zitafikia kikomo chake...kama ni kundi, nikitoka kwa huyu
nitakwena kwa mwingine, mpaka nihakikishe nimemaliza kazi...’akaniambia
‘Unaposema kundi, au watu wengine ni akina nani, inaonyesha
umeshawagundua?’ nikamuuliza
‘Mhh, hayo ni mambo binafsi, siwezi kukuambia zaidi ya hapo,
lakini cha muhimu ni kuhakikisha kuwa hili jambo nimeliweka sawa, nataka
kuhakikisha kuwa hawa wananitesa moyo wangu, wanasambaratika, na hakuna kitu
kama hicho tena, na kama ni njama, zinazofungamana na mwenza wangu,
nitahakikisha nazifahamu, na kama yeye anahusika, ataumbuka, na atanikumbuka
milele..’akasema
‘Mhh, sasa hapo unazidi kunichanganya, na huyo mwenza wako ndio
nani tena ?’ nikamuuliza
‘Ni moyo wangu.....ni, ni....’ simu ikakatika, na ilikatika
kama vile mtu kapatwa na tatizo, ikanibidi nipige simu, kwa mtu wangu mwingine,
yeye ni msaidizi wake, katika mambo yetu ya utendaji, nikamhoji, kuna nini
kinaendelea akaniambia ni kweli huyo mtu wangu kaamua kuacha kazi kwasababu
zisizojulikana na hajamwambia yoyote ni sababu gani, ni siri yake kubwa sana.
‘Kwahiyo hana kazi yoyote yupo nyumbani tu, au ana kazi gani
maalumu anaifanya kwa sasa...?’ nikamuuliza
‘Nimemuona kama anafanya kazi kwa mtu, lakini sio kwa muda
wote, ni mara chache sana, mara nyingi anaonekana yupo peke yake, kuna jambo
linamtatiza, anakuwa kama kachanganyikiwa..’akasema.
‘Kwa mtu gani huyo anapoonekana akifanya kazi
...unamfahamu?’ nikamuuliza
‘Ndio namfahamu,huyo mtu anafahamika sana...’akasema
‘Ni kwa nani hapo anapofanya kazi, nipe taarifa kamili, sio
unanipa taarifa kama unaogopa, ni kwa mtu gani anapofanya kazi kwa sasa?’
nikamuuliza kwa hasira
‘Ni kwa Makabrasha, ...mara nyingi anaonekana ofisini kwa
Makabrasha, inaonekana kaajiriwa na Makabrasha, au kuna kazi maalumu
anamfanyia...’akasema na hapo hapo nikakata simu.
Sikupoteza muda nikapanda ndege na kuja Dar,ndivyo
ilivyokuwa kuja kwangu Dar, kwa ghafla ....
WAZO LA LEO:
Mambo yanayohusu imani za watu , hisia za watu, upendo, nk ni nyeti sana, ni
vyema, ukikutana na vitu kama hivi uwe makini sana kuviingilia. Mtu akiamini,
akapenda, huona vingine vyote havina maana, anaweza hata akafumbia macho elimu
yake, na akafanya mambo ambayo kwa elimu yake, hastahili kuyafanya hayo. Ndio
maana wanasema, mwenye kupenda haoni, hata akiona kibaya kwake, ni kizuri,
akiona chongo ataita ni kengeza.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment