Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, November 12, 2013

Mkuki ni kwa Nguruwe-26Nikiwa jela, walinitembelea wazazi wangu, bila kutegemea, sikupenda waje, lakini kama wazazi isIngelikuwa rahisi kwao kutokufika,...nilipoambiwa ni wazazi wangu wamefika, nilishindwa kujizuia kulia, na sikupenda wanione katika hiyo hali, mtu niliyekuwa nikijiamini, nina kila kitu, leo nipo mahali hapo, nikajikuta nikitamani, nizame ardhini nisionane nao, lakini ile hali ya utoto kwa mzazi ikaniingia ..nikalia tena na tena, hadi nilipoona hiyo hali imekwisha ndio nikaenda kuonana nao..

Mama aliponiona alishindwa kujizuia, akanivamia na kunikumbatia, alitamani anibebe, akalia na mimi hapo sikuweza kujuzuia tena, nikajikuta ninalia,.. mama akawa ananishika shavuni mwilini, kama kuhakikisha hakuna sehemu nilyoumia, halafu akasema;

‘Mwanangu kwanini hutaki kutuelewa sisi wazazi wako, ujue mzazi anaona mbali, tulishakuamba huyo mume wako hakufai, unaona sasa...’akasema.

‘Mimi sitaki hata kukumbushia hilo, cha muhimu, ni jisni gani ya kukusaidia utoke hapa...’akasema baba.

‘Wazazi wangu msihangaike, hilo linafanyiwa kazi, wakili wangu yupo huko, na taarifa za awali ni kuwa dhamana imeshakubaliwa, iliyobakia ni taratibu ndogo ndogo...’nikasema.

‘Tatizo lako ni hilo la kujiamini kupita kiasi, una uhakika kweli kuwa dhamana imekubaliwa?’ akaniuliza.

‘Sasa mimi baba ningekudanganya , ili iweje, dhamana imeshakubaliwa,....msiwe na wasiwasi...’nikasema.

‘Lakini umeonaaeeh, tuliyokuambia kuwa tabia ya mtu huwa haijifichi, sasa unaanza kuonja joto ya jiwe, na kama hutakubaliana na sisi, utaone mengi zaidi, hatukuombei hivyo, na hatutafurahia iwe hivyo, ila muonja asali huwa haonji mara moja, ...kaa fikiria na chukua hatua kabla mambo hayajawa makubwa zaidi...’akasema baba.

‘Baba kwanini unakimbilia huko, una uhakika gani kuwa hayo yote ni kwasababu ya mume wangu?’ nikamuuliza.

‘Mimi sio mtoto mdogo, usione nimekaa kimiya ukafikiria sifuatilii nyendo za maisha yako, hata kama unajimudu, hata kama una kila kitu, bado mimi kama mzazi wako nina wajibu wa kutafirti, ili nijue mtoto wangu anaishi vipi, jpokuwa sio kwa saana, lakini siku moja moja naulizia,..’akasema.

‘Binti yetu sio tunafanya hayo kwa kutokupenda fuaraha yako, ..hatuna nia ya kuvuruga ndoa yako,lakini tunaangalia mbali, furaha ya muda, au furaha ya kudumu, haya yanayotokea hayafurahishi, na hujui wenzako wamepanag nini, huenda ukakumbana a makubwa zaidi ya hayo, sasa upo tayari kuishi maisha kama hayo hadi unashuka akburini...?’ akaniuliza mama.

‘Lakini wazazi wangu haya yanaweza kumpata yoyote, hata awe na mume kipenzi cha wazazi, bado, mitihani kama hii inaweza kumpata. Na sioni kwanini nikate tamaa na mume wangu kwa kufikiria kuwa kuna makubwa yanakuja, sijachunguza na kuamini kuwa hayo yaliyotokea ni kutokana na yeye, je kama sio yeye, na je, kama kuna shinikizo jingine lililomsukuma akashindwa kuvumilia, mimi kama mke wake natakiwa nifenyeje?’ nikawa kama nawauliza.

‘Tatizo lako ndio hilo, ubishi, unataka mpaka yakukuta makubwa ndio uamini, hili la kukuweka jela hujaamini, sisi tunafahamu kuwa mume wako, akishirikiana na huyo marehemu, walipanga haya, na lengo lao ni mali yako....sasa uwe makini, kama bado hujaamini, basi subiri...lakini onyo, hayo yaendelee kwako, lakini yasije yakagusa familia yetu, hatutavumilia,...sitajali kama wewe ni mtoto wangu,...’akasema baba kwa sauti ninayoijua , huwa akiongea hivyo hatanii.

‘Sawa baba nimekuelewa, ....’nikasema na mama akasema;

‘Hebu tuambie, ukweli, ...rafiki yako, kazaa nani?’ akaniuliza mama.

‘Mama, mimi sijui, kwasababu hajawahi kuniambia...’nikasema.

‘Haya hilo tunakuachia kama homework, ukigundua, utakuja kutuambia,..’akasema mama na mazungumzo yakabadilika tukaongea mengine, na wakati wanaondoka wakasema;

‘Kama unaona unahitaji msaada wetu tuambie, mimi nitafuatilia nihakikishe unapata dhamana, nina wakili wangu ....lakini hawezi kuingilia taratibu zako maana wewe una wakili wako, tusije tukaonekana watu wa ajabu, sio unajua taratibu zilivyo...’akasema baba.

‘Msiwe na wasiwasi wazazi wangu, dhamana ilishakubaliwa, hapa nasubiria tu kuondoka...’nikawaambia  nikiwa na uhakika,....sikujua kuwa mambo yatakuja kuabdilika.

Saa zikawa zinakwenda, simuoni wakili au rafiki wa mume wangu,...hata wale maaskari nilizoeana nao, wanaonipa taarifa za mambo yangu sikuweza kuwaona, na mchana ukapita, ikawa inaingia jioni, simuoni mtu
Nikijipa moyo, nikizania kuwa huenda kuna mambo bado yanafuatiliwa na watu wangu hao, hasa wakili, .

Ni wakati nimeshakata tamaa kabisa, nikiwa nahangaika kumtafuta mlinzi ili nimtume kwa wahusika ili angalau nijue ni nini kinachoendelea , mara nikasikia nikiitwa, na hapo nikajau ni muda wa kuondoka, dhamana imeshakubaliwa, japokuwa wamenichelewesha lakini sasa naondoka, nikajaribu kujiweka sawa, kwani sikutaka kurudi hapo tena, nilipokuwa tayari, nikatoka hadi chumba cha kupokea wageni.

Nilimkuta wakili wangu akiwa amekaa kwenye kiti, na aliponiona kama kawaida yake akasimama na kuja kunisalimia, nikamuitikia, lakini kwa jinsi nilivyomwangalia, nilimuona kama hana raha, kanyong’onyea, nikahisi mambo hayapo shwari, nikaona nikianza kuongea mimi nitapasuka kwa hasira, nikatulia, na yeye akaanza kuongea, akisema;

‘Yaani hapa nilipo naogopa hata kusema kitu, maana huyo mkuu wa kituo, na mkuu wa upelelezi wa kituo ulichokamatiwa,  sijui wana dhamira gani,...ni aheri wangelianiambia mapema, lakini walichofanya ni kuchelewesha muda, na baadaye waakniambia kuwa mambo hayajawa safi....’akasema.

‘Unataka kusema nini?’ nikamuuliza nikiwa nimeshitushwa kwa kauli yake hiyo.

‘Wamakataa kukupa dhamana,...na walioweka pingamizi hilo ni  mkuu wa kituo na mkuu wa upelelezi..wa eneo lilipotokea tukio, wao ndio wana dhamana ya uchunguzi kwa vile tukio limetokea sehemu yao....’akasema

‘Wanatoa sababu gani za msingi, za kuweka pingamizi la dhamaan yangu...?’ nikauliza

‘Wanasema kuwa, kupewa kwako dhamana kunaweza kukaharaibu baadhi ya mambo wanayoyafuatilia, wakasema wewe kwa jinsi wanavyodai, ...kuwa unaweza kutumia pesa zako, na watu wako, kuharibu ushahidi,..’akasema.

‘Mhhh, mimi sielewi, kwa vipi, jamani hivi hiyo ni hoja ya kukubalika kisheria, haya niambie .....,halafu ikawaje..?’ nikamuuliza huku nikicheka kwa huzuni.

‘Baadaye tukaona twende ngazi za juu, ndio tukajipanga, Rafiki wa mume wako, na yule ofisa wa polisi, wao wakasema wanakwenda kwaona viongozi wa usalama wa ngazi za juu na mimi nikawa naendelea kufuatlia mambo ay kisheria , tuligawana hivyo, ili kuona kuwa hakuna lolote jingine linaloweza kuleta pingamizi, lakini wenzangu tangu waende huko, hawajawasiliana na mimi, na cha ajabu kila nikipiga simu zao, hawapokei, zinaita tu..’akasema.

‘Mimi bado sijawaelewa, kwanini  mlipoona hivyo, hamkuja kuniambia mapema, mumesubiri hadi saa hizi, unafikiri mimi nitachukua hatua gani kwa sasa, kama mngelijuwa hilo limeshindikana mungekuja kuniambia mapema, mimi ningejua ni nini cha kufanya, sasa muda kama huu, mnafikiria nitafanya nini, ....au mnataka niendelee kusota huku jela au...?’nikasema kwa hasira.

‘Sio kusudio letu, bosi, kila kitu kilikuwa kinakwenda vyema, na hatukutarajia kabisa kuwa kutatokea pingamizi kama hilo, mwanzoni tulijua kuwa wanafanya kupoteza muda tu, lakini dhamana ilishakubaliwa, ..taarifa ya kukataliwa imekuja baadaye sana..jioni hii, kwahiyo tukaona tukimbilie ngazi za juu, na kiukweli dhamana ipo, lakini kwa leo...itakuwa vigumu, maana hawo viongozi wawili hawapatikani kabisa...’akasema.

‘Kwahiyo nyie mnataka nilale hapa tena, na huenda hata hiyo kesho ikashindikana, maana kama wameweka pingamizi, hata huko ngazi za juu watafanya nini, hawawezi kuwahini watendaji wao, au sio?’ nikauliza

‘Nimeona nije nikufaahmishe hivyo, halafu mimi mwenyewe nitaende  huko ngazi za juu nionane na mwanasheria wao, kwasababu waliokwenda huko hawapokei simu, na hawajaweza kunipa yaliyotokea huko, na sheria inaona una haki ya dhamana, kwasababu hawana ushahidi wa moja kwa moja kuwa wewe unahusika na hayo mauaji....nashindwa kufahamu kuna tatizo gani,   kama ningelifahamu ni kitu gani kimekwamisha, ningelijua ni nini cha kufanya, aheri ningelifuatana nao...’akasema.

‘Mimi nahisi huko walipokwenda wamekwama, ndio maana hawataki kupokea simu yako...wanachofanya na wao,  ni kupoteza muda tu, ili wakija hapa, wasipate hata muda wa kuongea na mimi, hamna shida, nitasota tena hapa leo, lakini kesho nataka kuwasiliana na hizo ngazi za juu, nisikie kwanini wananisotesha hapa, wakati sina kosa....mimi nina kosa gani, sijaua, ...wao ni kazi yao kumtafuta muuaji, sio kunikamata mimi mtu nisye na hatia, ...’nikasema na kuinuka kuondoka.

‘Kulikuwa na jambo jingine nataka kukuulizia...’akasema.

‘Sitaki kuongea lolote na nyie tena, ninachotaka kusikia ni dhamana yangu imekubaliwa, basi, kama hakuna jibu kama hilo, sitaki kuongea na nyie, mumeshanivuruga akili yangu, wamefika wazazi wangu hapa wananiona mimi kama mtoto mdogo, ...halafu nitakuja kuwaambia nini, wakati nilishawaambia kuwa dhamani imekubalika, wataniona mimi nawadanganya, ...’nikasema huku nikiendelea kuondoka, na yeye akauliza juu kwa juu.

‘Wazazi wako nimeongea nao, na wao wakasema kama kesho itashindikana watafuatailia na wao waone tatizo lipo wapi, ...lakini nina uhakika kesho dhaman itapatikana....’akasema.

‘Hata kama umeonga na wazazi wangu,  haina maana tena kwangu, tumeshathibitisha kwao, kuwa hatuwezi kujitatulia mambo yetu wenyewe, mpaka wao wahusike, kitu ambacho sikutaka kabisa kitokee, ina maana wewe umeshindwa kazi, na wao watamuweka wakili wao, je unakubali hilo, mimi ninakulipa gharama zako za nini,kama kazi imekushinda....’nikasema.

‘Kazi haijashikana, usiwe na wasiwasi, ...ni mbinu zao za kupoteza muda tu, wazazi wako wamenielewa, na sio kwamba watamuweka wakili wao, ...nitaendelea kufanya hii kazi, kama wakili wako, na hata kama wakili wao akifika hawezi kufanya miujiza, taratibu ni zile zile....hata hivyo, ... ‘nikamkatisha na kusema;

‘Ulitaka kuniuliza nini mwanzoni nisamehe maana akili yangu haipo sawa...’nikauliza huku nimesimama, nikiwa simuangalii, nimempa mgongo, niliona nimeongea kwa jaziba,na huyu ni wakili wangu natakiwa kumuheshimu.

‘Nilitaka kukuuliza je Mume wako alifika hapa leo kukuona?’ akauliza

‘Mume wangu, ...!!’ nikasema kwa kushangaga, ‘Hapana, mbona nasikia hali yake sio nzuri, ..?’ nikauliza

‘Kuna muda alilazimsiha kuja kukuona, na alipokataliwa akatoroka, na wakajua kuwa amekuja huku kukuona....’akasema.

‘Katoroka,!!..una maana hani kusema hivyo, kwani kashikiliwa kama mfungwa, mimi ninavyojua yupo hapo hospitalini kwa rizaa yake mwenyewe, ...’nikasema huku nikimgeukiwa kumwangalia.

‘Ndivyo ilivyo, lakini kama mgonjwa akitaka kutoka nje,au kuondoka hospitalini kwa muda, ilibidi aondoke kwa kibali maalumu, kama ni lazima, na alipomuomba hivyo docta, akamkataliwa kutokana na hali yake ilivyokuwa, yeye akaondoka kwa siri, huko ni kutoroka, kavunja masharti ya hospitalini..’akasema.

‘Mimi nilishawaambia msimwambie huyo mtu, ni nani alimwambia, hamuoni sasa mnaweza kusababisha matatizo mengine, na kunifanya niwe mtu wa mawazo, ....sijui watu wana akili gani...sasa karudi?’nikasema nikiwa nimekunja uso.

‘Kesharudi, na hata mimi sijui ni nani alimwambia, nahisi, ni wazazi wako walipopata taarifa, walipiga simu yako na walipoona hupokei, wakajaribu kupiga simu yake, na hapo ndipo akajua kuwa umeshikiliwa...’akasema.

‘Na wazazi wangu aliwaambia nani?’ nikauliza.

‘Sijui...labda rafiki ya mume wako, ....’akasema.

‘Hapana rafiki wa mume wangu tulikubalina naye kuwa wazazi wangu na mume wangu wasijue lolote hadi hapo muda muafaka utakapofika, na nilitarajia kuwaambai nikipata dhamana, kama ni lazima,..nahisi kuna kitu kimejificha,  na nahisi hawo watu wamewaambia  wazazi wangu kwa kussuio maalumu....’nikasema.

‘Mimi sioni kama kuna kusudio maalumu hapo, ni watu waliona kufanya hivyo, wanatenda wema, ...cha muhimu kwa sasa ni kutuliza akili zetu tuone ni jinsi gani tutalimaliza hili, na mimi nataka kuongea na mume wako, nina imani kuwa ninaweza kupata taarifa muhimu kwake, zitakazo tusaidia kwenye hii kesi,.....’akasema.

‘Kwa vipi wakati yeye ni mgonjwa?’ nikauliza

‘Kwa jinsi ilivyo, inabidi tuongee naye, hata kama ni mgonjwa, maana kila ukiangalia ni nani angeliweza  kuingia ndani kwako na kufungua  kabati, ...na kama ulivyosema hata ufungua wako, unao, na kule ofisini uliuficha mahali pa siri, hapa inaleta mashaka, maana kama ulivyosema wanaofahamu wapi unapoweka hata hiyo bastola yako ni wewe na mume wako tu, .....’akasema.

‘Kwahiyo unataka kusema nini?’ nikauliza

‘Inawezekana mume wako aliwahi kumwambia mtu mwingine, na huyo mtu mwingine akatumia mwanya huo kuingia na kuchukua hiyo bastola,...maana yeye ni mgonjwa, hatuwezi kusema kuwa yeye ndiye aliyefanya hivyo...’akasema.

‘Mimi bado sioni umuhimu wa kumuuliza mume wangu, tunaweza kufanya uchunguzi mwingine na kugundua ukweli hata bila kumgusa mume wangu,..tatizo nipo hapa jela, siwezi kufanya lolote kwa sasa, lakini kama ningelikuwa nje, ningelishagundua kitu...je kuna mtu kawasiliana na rafiki yangu,?’ akauliza.

‘Ndio , mimi mwenyewe nilitaka kuongea naye, lakini muda niliompigia alikuwa yupo darasani, ufahamu aliondoka wakati wenzake wanaendelea na masomo, kwahiyo alipofika tu, akaingia darasani, ...bila hata kupumzika...baadaye aliongea na rafiki wa mume wako, sijamuuliza waliongea nini zaidi maana tulikuwa tuankimbizana na muda.’akasema.

‘Namfahamu sana rafiki yangu huyo ni mtu mwenye bidii sana, na akiamua kitu chake ni lazima akipate, na hayo masomo kwake ni muhimu sana, lakini ninachomshangaa ni kutokunijali mimi, hafahamu kuwa hayo yote yasingelipatikana kama isingelikuwa ni mimi....nina hamu sana ya kuongea na yeye, na safari hii nataka anijibu maswali yangu yote kwa uwazi...’nikasema.

‘Mimi nahisi rafiki yako huyo, kaingia huko, kwenye matatizo bila kupenda, kwani ninavyomfahamu ni mtu anayekuheshimu sana, isingelikuwa rahisi kuvunja uaminifu wake kwako, ukizingatia kuwa wewe umemchukua kama ndugu yake...’akasema

‘Kunaswa kwa vipi?’ nikamuuliza.

‘Kwa jinsi marehemu anavyojulikana, tunahisi, huyo jamaa alikuwa kwenye kazi zake za kitapeli, na huyo rafiki yako alikamatika kwenye jambo fulani, akapewa masharti kufanya hivi, usipofanya hivi, nitakuharibia, ni tabia yake ya kucheza na mlungula, ‘ blackmail.’.na hilo polisi wanalifanyia uchunguzi....’akasema.

‘Na kwanini tusubiri mpaka polisi waingilie undani wetu, nataka tufahamu ni nini kilitokea kabla polisi hawajagundua, je hilo linaweza kufanyika?’ nikamuuliza.

‘Linaweza kufanyika kama wahusika watatoa ushirikiano, akiwemo mume wako, na rafiki yako,...nahisi hawo wanaweza wakawa ufungua muhimu wa kulijua tatizo hili , chanzo chake na hatima yake...na nahisi kwasasa itakuwa ni rahisi kwao kuongea kila kitu, maana yule mtu walyekuwa wakimuogopa, keshafariki...’akasema.

‘Kwahiyo unahitajia msaada gani kutoka kwangu?’ nikamuuliza

‘Msaada wako mkubwa ni kujua kuwa nataka kuongea na mume wako, na ikibidi nifanya uchunguzi nyumbani kwako...’akasema.

‘Kwa hivi sasa nakuruhusu, lakini hebu subiria mpaka kesho kama nikitoka humu, mimi mwenyewe nitaifanya hiyo kazi, nikisaidiwa na wewe...kuna mambo nahitaji mwenyewe niyafanyie uchunguzi, sitaki yatoke nje, ....kesho hiyo nitakuambia ufanye nini, kwahivi sasa fuatilia mambo ya dhamana yangu, na natumai kesho itapatikana , kama itakosekana, sitaki nikuone...’nikasema na kuanza kuondoka.

‘Kuna jambo jingine muhimu , unahitajika kulifahamu...’akasema

‘Hilo jambo lisubiri kesho tafadhali...’nikasema.

‘Ni muhimu ulijue, ...mtoto wa marehemu aliyekuwa nje, ameshafika, na alitaka kuongea na wewe....’akasema

‘Kuhusu nini, mimi ninaongea naye kwa kazi gani, mimi sio ndugu yake hatuna mahusiano naye au anafikiri mimi ndiye niliyemuua baba yake..au mimi nitamshauri  mambo ya mirathi....hapana sina haja ya kuongea na yeye’nikasema.

‘Anasema kwenye mkataba aliomuachia baba yake, ...yeye ana hisa kwenye kampuni zako, kwa mume wako na kwako pia..ipo kwenye mirathi ya baba yake.’akasema

‘Eti nini?’ nikasimama kama mu aliyegusa umeme.

‘Lakini hilo niachie mimi nitapambana naye nahisi ni kutokana na ule ubadhirifu wa ule mkataba wa awali, na sasa mkataba wao mpya unataka kuanza kuleta chokochoko, ..hilo niachie mimi hiyo kwangu ni kazi ndogo tu...’akasema.

This...oh,.... I can’t believe this,  its too much,....sitaki kusikia hayo maneno,...mwambie huyo mtu, asimchokonoe nyoka mwenye sumu shimoni, kama wanaishi kwa njia ya ulaghai, kama yeye ni sawa na baba yake, wasijidanganye kuwa wanaweza kufanya hivyo kila mahali...hakikisha unalimazliza hilo bila ya mimi kukutana na huyo mtu, sijui mtoto wa umri gani...’nikasema huku nikishika kichwa change na kuvuruga nywele kwa hasira.

‘Huyo ni mtoto wake wa kwanza, ni mkubwa tu, alizaliwa mapema sana, akiwa bado anasoma, alimpa uja uzito, mke wake, akiwa bado shuleni, ...na baadaye ndio akaja kumuuoa,...kwahiyo ni mkubwa,. Mimi nilishamwambia kuwa kama ni maswala ya mikataba, anatakiwa kuongea na mimi, kwani mimi ndiye wakili wako, lolote linalohusiana na hiyo mikataba nalifahamu mimi, lakini kasisitizia kuwa anataak kuonana na wewe ili muelewane....’akasema

‘Sitaki kumuona huyo mtu...naogopa kuwa ,nitafanya kitu ambacho sitapenda kukifanya, ...okey, tutaona hiyo kesho, ...fanyeni haraka nipate hiyo dhamana...sitweza kuvumilia kubakia hapa ndani tena, ..siwezi kukubali , ikishindikana nitatoka humu kwa nguvu..na wewe kazi hakuna...hii ni ahadi....sijui kama nitaweza kuvumilia tena, si...ooh’nikasema huku natembea kuondoka kuelekea huko jela...na sijui ni kitu gani kilitokea, ila nilisikia kitu kikigonga kichwani, na giza likatanda,.....nikadondoka, na kupoteza fahamu.

NB:Ni nini tena hiki....


WAZO LA LEO: Siku hizi kuna watu wanaishi kwa njia za ulaghai, utapeli, na wizi wa kutumia maandishi na mitandao, ...hili ni changamoto kwetu, wakati huu jamii, zetu zinapojiunga kwenye kijiji kimoja cha utandawazi. Ni muhimu tukawa makini katika kutoa taarifa zetu, majina, anuani, namba za akiba zetu na maneno ya siri kwa watu, kwani huwezi kujua ni lini bahati mbaya itakuangukia. 
Ni mimi: emu-three

No comments :