Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, November 5, 2013

Mkuki ni kwa Nguruwe-22


‘Ni kweli unayoyasema, naanza kuamini hivyo,..na hao wanaojifanya ni marafiki zangu kumbe ni maadui zangu nimeshaanza kuwagundua mmoja mmoja,.....

Maneno haya niliyasema nilipoanza kuwashuku watu niliokuwa nikiwaamini japokuwa moyoni mwangu nilikuwa sijathibitisha hivyo, ilikuwa kazi ngumu kwangu, kumshuku rafiki yangu ubaya, lakini kutokana na matukio yanajitokeza nilianza kuwatilia mashaka rafiki zangu, japokuwa sikujua ni yupi wa kumtilia mashaka...na kwa hali hiyo, nikawa nashindwa kufahamu ni nani rafiki wa kweli na ninani rafiki wa uwongo.

‘Hata wewe wewe mwenyewe sikuamini, ....’nilisema moyoni pale nilipomtamkia huyu rafiki wa mume wangu maneno haya;

Katika watu waliokuwa marafiki zangu wakubwa, wewe ulikuwa mmoja wapo, nikakuamini kupita kiasi, lakini kutokana na yanayotokea hivi sasa, hata wewe mwenyewe sikuamini tena, usijifanye kuwa wewe haupo kwenye hilo kundi la watu wanajifanya marafiki kumbe ni wanafiki, maana nimekugundua kuwa wewe unauma na kupulizia,...upande mmoja unajifanya rafiki upande mwingine, upo kwenye maadui zangu,...’

Nilimwambia hivyo kwasababu kubwa, kwamba yeye anafahamu ukweli, lakini hataki kuniambia huo ukweli, kuna mambo mengi anayafahamu dhidi yangu, lakini kwasababu zake binafsi aliamua kunificha,sasa ni urafiki gani huo, na nidio maana nikamwambia:

Yeye nimeshafahamu kuwa ana ajenda zake za siri na ya kuwa, kuna jambo analitafuta kwangu, ..'

Ili kumvunja nguvu kabisa nilimwambia;

'Nyie siwajli, na wala siwaogopi,  nitapambana nanyi, mmoja baada ya mwingine....hilo nawathibitishia...’ Niliongea kwa kujiamini, na yeye ananifahamu kuwa sitanii,...

Sasa je kweli nitaweza kutimiza hayo kivyangu vyangu....

Tuendelee na kisa chetu....

                                    ***********

Nilipotoka pale hospitali, niliendesha gari huku akili yangu haijawa sawa, kitu ambacho nilikuwa sikipendelei, hasa baada ya kuona ajali ya mume wangu, ambayo kwa wengi ilionekana kuwa aliipata kwa kuchanganyikiwa,...na sio kwasababu ya ulevi, hakuonekana amelewa, baada ya hiyo ajali. Na siku ile hata mimi ningejikuta kwenye ajali, kwa jinsi nilivyoendesha gari.

Kwa hali kama hiyo, ikanibidi niwe na tahadhari,nilishaamua kuwa makini sana nikiwa barabarani. Na hata 
hivyo, japokuwa nilijitahidi kuendesha kwa tahadhari, lakini bado akili yangu ilikuwa kwenye mawimbi ya mawazi, na hata wakati naingie kwenye barabara kuu, nilikuwa sijapangai nielekee waoi kwanza.

Nilitakiwa nifike nyumbani, maana kulikuwa na mambo nilihitajika kuyachunguza, lakini pia nilihitajika kwenda kuonana na rafiki yangu, ambaye tangu afike kutoka huko masomoni, nilikuwa sijaonana, naye, na nilitumaini kuwa yeye, anaweza kunisaidia kwa haya yanayotokea,...sikufahamu kwanini karudi haraak hivyo,

Nikaona bora nifika hapo anapoishi huyo rafiki yangu, kwani sehemu ile ya mwanzo, alishahama, na baadhi ya vitu vyake vipo kwangu, kuna chumba alichukua kwa dharura, na kuweka baadhi ya vitu vyake, ni kwa ndugu yake, na niliwaza hivyo nikaongeza mwendo wa gari hadi nikafika hapo anapoishi.

Nlipofika hapo niliambiwa hayupo, walisema rafiki yangu huyo aliaga kuwa anakwenda hospitalini kumuona mgonjwa, na aliondoka muda,nikashangaa, kwani kama likuja kumuona mgonjwa, ambaye ninahisi ni mume wangu, basi tungelikutana huko.

‘Na mtoto yupo wapi?’ nikauliza.

‘Mhh, hayo utamuuliza mwenyewe, hatujui....’akasema huyo ndugu yake.

Basi nikaona hakuna haja ya kupoteza muda, nikaamua kurejea nyumbani kwangu, nilipofika nyumbani kwangu nikaanza kuwahoji, watu kuanzia mlinzi hadi wafanyakazi wa ndani, kama kuna mtu yoyote aliwahi kufika hapo, kabla, ambaye walimtilia mashaka, au kunitafuta mimi au mume wangu, nikaambiwa hakuna, nikaona nifanye jambo moja kwa haraka, sikupendelea kufanya hivyo, lakini nikaona ndio muda pekee ninaoweza kufanya jambo kama hilo,

Nikaanza kupekua vitu vya mume wangu, sehemu zote nyumba, au kile chumba alichokuwa akipendelea kulala, kwenye nguo zake,kama ninaweza kupata kitu chochote cha kunisaidia,lakini sikuweza kupata kitu chochote cha maana, mwishowe nikaona nirejee kwenye maktaba niangalie vyema.

Nikafungua tena lile kabati langu, safari hii kwa uangalifu kidogo, na cha ajabu niliona ile nakala ya mkataba wangu na mume wangu, ukiwa umewekwa pale pale nilipopendelea kuuweka,...kwanza sikuugusa, nikachuka kitu cha kuzuia alama za vidole mkononi, nikaanza sasa kuukagua huo mkataba, kwa haraka nikagundua kuwa sio ile nakala yangu, maana ile lama niliyokuwa nimeweka haikuwepo,

‘Hii nakala imewekwa baadaye....sio ile nakala yangu.’nikasema ,

Nilichukua ile nakala na kuanza kuipitia kwa haraka haraka, sikuweza kugundua mabadiliko, sijui kwa vile muda huo sikuwa nimetuliza kichwa,...nikaona nipumzike kwanza, na wakati napumzika nikagundua kitu, kwenye sehemu ya kipengele cha watoto, ....nikaanza kuisoma sehemu hiyo kwa makini, ilikuwa sio kazi rahisi, ila niligundua sehemu moja, inasema hivi;

‘Watoto wote wana haki sawa, na mali ya urithi , itagawiwa sawa, kama wazazi watakuwa wamefariki,...’hili neno `wote’ sikumbuki kama ilikuwa hivyo mwanzoni, nakumbuka tulitumia neno `wetu’ na hili neno wetu kwenye ufafanuzi tuliandika, kuwa linasimama badala ya wanandoa mimi na mume wangu kwa kutaja majina. Nikafungua kwenye ufafanuzi, sehemu ya huo ufafanuzi, ilikuwa imeondolewa....’

‘Kwanini wafanye hivyo, na ni nani huyu, ni mume wangu na wakili wake....mmh, nahisi kuna jambo, nimewapata sasa....’nikasema kwa kujipa moyo.

Hapo nikaanza kuingiwa na mashaka, kumbe nia yao ilikuwa kubadili huo mkataba, nikaanza kusoma tena sehemu nyingine kuna sehemu zimeondolewa na kuongezwa maneno mengine ili kuleta maana fulani, sikuelewa ni kwanini walifanya hivyo.

Nikafungua sehemu nyingine lakini sikuweza kugundua mabadiliko mengine, japokuwa nilihisi kuwa kuna sehem fulani fulani zimebadilika, lakini kiutalaamu zaidi, na hapo nikaona niwasiliane na wakili wangu, nikampigia simu.

Simu iliita kwa muda bila kupokelwa, na baadaye akaipokea, na kusema alikuwa akimsaidia mgonjwa, maana alikuwa kwao, akimuuguza mzazi wake, nikamwambia hayo yaliyotokea, na akasema;

‘Kuna mtu ana nia mbaya, maana mimi nilipoondoka tu, nilipata taarifa kuwa kunawatu waliingia ofisini kwangu wakaiba baadhi ya vitu, sasa sina uhakika kama ni pamoja na hiyo nakala ya huo mkataba, ni mpaka nikirudi huko.....’akasema.

‘Kumbe lengo lao ni kuhakikisha kuwa wameiba nakala zote, je kwenye mtandao hukuhidhi chochote?’ nikamuuliza.

‘Katika vitu ambavyo nasikia wameiba, ni pamoja na komputa yangu ambayo nimehifadhia mambo yote, na sikumbuki kuhifadhi sehemu nyingine zaidi, maana sikuwa na mashaka kuwa hali kama hiyo inaweza kutokea, hii ni changamoto kwangu, kazi zote sasa nitaziweka kwenye mtandao ya kudumu...japokuwa napo kuna matatizo yake, huwezi kuwa na uhakika wa usiri’akasema.

‘Sasa kama nakala ya huo mkataba imechukuliwa huko kwako na komputa imeibiwa, tunawezaje kuipata nakala nyingine wapi, maana nahisi wamebadili huu mkataba kwa makusudi maalumu, na cha ajabu wameweza kutumia sahihi yangu kama ilivyo,..ina maana huyu mtu ni mtaalamu kweli wa kunakili sahihi za watu....’nikasema.

‘Kama wameamua kufanya hivyo, basi nina imani kuwa hata huko serikalini watakuwa wameshafanya hivyo hivyo,watakuwa wameshabadili huo mkataba na kuweka huo wanaoutaka wao,....’akasema.

‘Kwa vipi sasa, ?’ nikauliza

‘Unafahamu hali ilivyo, kama una pesa lolote linaweza kufanyika, sina uhakika sana, wanaweza hata wasitumie pesa, wakatumia ujanja ujanja....cha muhimu nataka niipate hiyo nakala mpya waliyoitengeneza wao, ili na mimi niupitie upya,mimi nitagundua ni sehemu gani wamebadili, na kwanini...fanya kila juhudi unitumie hiyo nakala, haraka iwezekanavyo?’ akaniuliza.

‘Kwanza nitakutumia kwa mtandao..nitainakili kwenye mtandao na kukutumia kwa njia hiyo, halfu nitatoa nakala nyingine, na kukutmia kwa njia ya DHL, huko kuna ofisi zao, kama hakuna nitakutumia kwa njia ya mabasi, ......’nikasema,

‘Itakuwa vizuri, kama hatujachelewa....’akasema na kauli yake hiyo ilinikatisha tamaa.

***********

Wakati nataka kuondoka nyumbani, nikakumbuka jambo, nikarudi kule kwenye maktaba yetu na kufungua kabati sehemu ninapohifadhia silaha, yangu, niliikuta ipo pale pale, lilinijia wazo la kuichukua niwe natembea 
nayo, kwa usalama wangu, lakini nikaona kwa vile ni mchana, hakuna umuhimu nayo, nikaondoka hadi ofisini kwangu, na nilipofungua kabati langu, nikakuta nakala ya mkataba, nikaichunguza na kugundua kuwa sio ile nakala yangu ya awali, hakuna alama niliyokuwa nimeweka,

Nikaifungua na kuanza kuisoma, ni kama ile ile niliyoikuta nyumbani kwangu, na safari hii nilitulia kidogo, nikagundua sehemu kubwa ya vipengele vya umiliki wa mali, vimbebadilishwa, hapo nikaanza kuingiwa na wasiwasi, kuwa hawa watu hawana nia njema kwangu, wameingilia hata mali yangu,...na kwahiyo, kuna mambo mengi yamebadilishwa kitaalamu,....na hapo nikaanza kumshuku mume wangu vibaya;

Kuna sehemu iliandikwa hivi;

‘Mume ndiye atakayekuwa muangalizi wa mali yote na mwenye mamlaka ya mali zote, na atakuwa na uhuru wa kumuingiza mtu yoyote katika umiliki wa mali kama atakavyoona yeye inafaa, hata bila ya idhini ya mke wake...’nikashangaa sehemu hiyo imetoka wapi, mbona haikuwepo, na kwanini mume wangu akubali sehemu hiyo iongezwe ni ili aweze kufanya lolote kwenye mali zetu, haiwezekani, sikubali,...

Nikasoma maelezo mengine, lakini akili yangu ilikuwa imechafuka, hasira zilianza kunipanda, hapo hapo nikampigia simu, tena wakili wangu kumuulizia hicho kipengele, mbona hakikuwepo, ndipo akaniambia kuwa hawo watu wamefanya hivyo makusudi, huenda kuna mtu wanataka kumuingiza kwenye umiliki wa mali...

‘Kumuingiza kwa vipi?’ nikamuuliza.

‘Kwenye maelezo ya mwanzo, ilikuwa imesema kuwa hakuna mtu atakayeruhusiwa kuingizwa kwemue umiliki wa mali, kampuni , zaidi ya wewe na mume wako na watoto wenu. Nyie wawili mnamiliki mali kutokana na mitaji yenu na hakuna anayeruhusiwa kumuingiza mtu yoyote kama mwekezaji kwenye mali zakifamilia....’ sasa hicho kipengele kimeondolewa, na wameweka hicho kipengele ili kumruhusu mume wako kufanya atakavyo..’akasema wakili.

‘Kwa mtizamo huu, mume wangu ndiye yupo nyuma ya haya?’ nikamuuliza.

‘Kwa jinsi ilivyo inaonyesha hivyo....lakini huwezi kumshika moja kwa moja, nahisi anafanya hivyo kwa shinikizo fulani, ....’akasema.

‘Kwa ushauri wako nifanye nini, nitoe taarifa polisi....?’ nikamuuliza.

‘Ukitoa taarifa polisi kwa sasa moja kwa moja, atakayekamtwa ni mume wako, na kutokana na hali yake unaweza ukammaliza kabisa, ...’akasema.

‘Sasa nifanyeje?’ nikamuuliza.

‘Ngoja kwanza niupitie huo mkataba wote, halafu nitakuwa na nafasi ya kusema lolote,...usijali hawo wamechukulia kienyeji sana, huwezi ukafanya hayo waliyoyafanya kirahisi hivyo, labda wawe na mtu fulani kwenye sehemu za uandikishaji wa mikataba hiyo , vinginevyo, kuna kitu kibaya kinaendelea ujaribu kuwa makini, huo ni ukiukwaji wa sheria, na huyu aliyefanya hivyo anaonekana ni mtu anayefahamu sana kazi hii ya kubadili badili maandiko ya kisheria...’akasema.

‘Nahisi anaweza kuwa huyo wakili wa mume wangu...’nikasema.

‘Wakili gani tena huyo wa mume wako, kaamua kuchukua wakili mwingine zaidi yangu...?’ akaniuliza

‘Ni wakili Makabrasha.....’nikasema.

‘Oh, balaa, huyo mtu tena, nakumbuka nilishawaonya kuhusu huyo mtu, ...’akasema.

‘Mume wangu sijui kaingiwa na wazimu gani, nahisi kuna tatizo kubwa kwa mume wangu, sio yeye, sio mume wangu ninayemfahamu,  sasa wewe, utarudi lini?’ nikamuuliza.

‘Kiukweli sijui, maana hali ya mzazi wangu sio nzuri, na siwezi kumuacha katika hali kama hii, kama hali yake itakuwa hivi, nitachelewa sana, na ikibidi nitakuja naye huko kwa ajili ya matibabu zaidi japokuwa yeye mwenyewe kakataa, ningelishamchukua, nije naye huko, lakini hakubali, kabisa, yeye anasema anataka afie nyumbani kwake, kwahiyo kwa hivi sasa siwezi kusema lolote, ....’akasema.

Nilipoona hiyo nakala imeweka hapo, nikaona nimuhoji huyu mtu anayehifadhi funguo, nikamuita huyo mfanyakazi , Safari hii nikawa mkali, nikamuuliza anieleze ukweli, kama kweli hakuna mtu analiyewahi kuingia kwenye hiyo ofisi yangu;

‘Niambie ukweli ni nani ambaye aliingia ofisini kwangu, maana nina ushahidi kuwa kuna mtu aliingia wakati mimi sipo kazini, na kuchukua vitu vyangu muhimu kwenye kabati langu?’ nikamuuliza.

‘Bosi hakuna mtu aliyeingia,mimi nina uhakika, maana ufungua ninao mimi, na sijawahi kuuacha popote, kama ulivyoniagiza,....’akalalamika akionyesha wasiwasi.

‘Sasa sikiliza, kama nitakuja kugundua kuwa kuna mtu aliyeweza kuingia ofisini kwangu, na wewe unafahamu ujue ndio mwisho wa ajira yako, na nitahakikisha unakwenda jela...’nikasema kwa ukali na yeye akaniangalia kwa mashaka, lakini aliendelea kukataa kuwa hakuna mtu aliyewahi kuingia, au  yeye kumruhusu mtu yoyote kuingia kama nilivyomuagizia.

‘Sawa nitaiarifu polisi, na watafanya uchunguzi , na ujue wewe ndie uliyekuwa na mamlaka ya ufunguo kwahiyo wewe ndiye utakayekuwa mshukukiiwa mkuu, utalala jela hadi hapo huyo mtu aliyeinga kwenye ofisi yangu na kuchukua vitu akapopatikana..,kama sio wewe uliyefanya hivyo’nikasema.

‘Bosi, mimi sijui lolote, na kama polisi watanikamata, watakuwa wakinionea bure, maana sijui, na sijawahi kumruhusu mtu kuingia ofisini kwako..nakuomba bosi, unisaidie, nasema ukweli sijawahi hata siku moja kufanya hayo .......’akasema kwa uchungu, huku akipiga magoti, kitu nisichokipenda mtu kunifanyia hivyo, mimi ikabidi nimwamini tu, ila nikamwambia kuwa nifanya uchunguzi kama nitagundua kuwa anafahamu sitakuwa na msamaha na yeye.

Akilini mwangu nilijiuliza maswali mengi ni nani huyo angeliweza kuingia ofisini kwangu na kujua wapi nimeweka vitu vyangu vya siri, na kuweka kila kitu, kama kilivyokuwa na aliingia muda gani maana kama aliingia kwa uficho, basi itakuwa ni usiku , na kama ni usiku, walinzi walikuwa wapi. Hapo nikaona niwahoji walinzi.

Niliwaendea walinzi na kuwahoji, na wote walikana kabisa kuwa hakuna mtu angeweza kuingia usiku bila ya wao kumuona,wakasema kama ni kuingia hko ofisi, basi itakuwa imefanyika mchana sio usiku....nikajikuta nikikosa ushahidi wa kuwabana hawa walinzi, lakini nilihisi kwa vyovyote vile ni lazima kuna mtu wa ndani anayehusika,hakuna mtu angeliweza kuingia hadi ofisini kwangu, kama sio mtu anayenifahamu, na kufahamu taratibu zangu.

Sikutaka kuwahoji wale wote ninaowahisi, kama katibu muhutasi wangu, ambaye sizani kama angelifanya hivyo,...niliona hilo swala niende nalo kimiya kimiya, na ikibidi nitatafuta mpelelezi wa kujitegemea.

Nilimpigia jamaa yangu wa mambo ya komputa, nikamuomba aniwekee vifaa vya kunasa matukioa ili kama huyo mtu ataingia tena aweze kuonekana, japokuwa nilikuwa na uhakika kuwa huyo mtu hakuwa na sababu ya kuingia tena kwani walichokitaka wamekipaa, sasa ataingia ofisi kwangu kufanya nini....

Hapo nikamkumbuka rafiki yangu , kuwa angelikuwepo kazini ingelikuwa ni rahisi kuyagundua hayo yote, na nilipomkumbuka nikaona nimpigie simu, na akaipokea kama vile alikuwa akisubiria simu kutoka kwangu;
‘Nilikuwa na maongezi na wewe, tunaweza kukutana wapi?’ nikamuuliza.

‘Hata mimi nimekuwa nikikutafuta sana, ...kuna mambo nilitaka kukuweka wazi, kuhusu ile kazi uliyonipa kabla sijaenda kusoma,...na nimejitahidi ili tuonane, lakini imeshindikana....’akasema.

‘Kwanini ishindikane, kwangu unakufahamu, ofisini unakufahamu, kwanini usinifuatilie huko kote?’ nikamuuliza.

‘Nilifanya hivyo, lakini ni kama vile imepangwa tusionane, maana nilifika kwako kwa mara ya kwanza nikaambiwa haupo, mara ya pili nikaambiwa umekwenda hospitalini niliwafuata huko, na bahati mbaya nilipofika nikaambiwa umetoka muda huo huo,nikakufuatilia nikijua upo nyumbani,...nilipofika kwako sikukuta,nikahisi umekuja kwangu, na nafika kwangu nikaambiwa ulifika...umetoka, sasa nina mambo mengi yakufuatilia, na muda ni mchache sana, ...’akasema.

‘Unaonaje nikafika kwako, ...nije tuongee huko kwako, au?.’nikasema.

‘Mimi kwa sasa nipo uwanja wa ndege kwa jamaa yangu, maana natarajia kuondoka leo usiku, nikaona nikakae kwake, ili iwe rahisi kuwahi kuondoka , ninaondoka leo usiku, na ndege ya usiku kurudi masomoni...’akasema na kuniacha hoi.

‘Ina maana ulikuja mara moja tu, ,..?’ nikauliza.

‘Ndio nilikuja mara moja, kwa dharura,....’akasema.

‘Dharura gani?’ nikauliza.

‘Kuna mkataba nilihitajika kuja kuweka sahihi yangu, ni muhimu sana kwa ajili ya mtoto na mimi mwenyewe, na kutokana na wakili alisema mimi ni muhimu nije mwenyewe ....’akasema.

‘Mkataba gani huo?’ nikauliza nikihisi kichwa kikizunguka.

‘Ni mkataba wangu na huyu mtu....aliyenibebesha mimba, naona kang’ang’ania niingie mkataba naye, kwa ajili ya mtoto, sikupendelea nilitaka mambo ya mtoto yasimuhusishe yoyote, lakini naona kang’ang’ania na hata kunitishia kunishitaki, nikaona isiwe taabu kama ndivyo anavyotaka, mimi sina shida ilimradi tu mtoto wangu asichukuliwe....’akasema.

‘Huyo mtu ni nani?’ nikauliza kwa ukali.

‘Kwa hivi sasa siwezi kukuambia, maana naona hali imeharibika...nikirudi kutoka kwenye masomo nitakuambia kila kitu, maana haitakuwa na haja ya kukuficha, ila kwasasa kwa vile kuna mambo ya kisheria yanayofuataliwa na wakili wangu, sistahili kukuambia lolote...’akasema.

‘Na mtoto wako yupo wapi?’ nikamuuliza.

‘Natarajia kuletewa leo......’akasema

‘Sijakuelewa, kwanini unasema unatarajia kuletewa leo, kwani alikuwa wapi?’ nikamuuliza.

‘Alichukuliwa kama dhamana,....waliponiita, kwa ajili ya kuweka sahihi ya huo mkataba, sikufahamu kama itakuwa hivyo, na nilifahamu kuwa lengo lao ni jema tu, siku nilipofika nikiwa nyumbani kwangu, wakati nipo bafuni naoga, walifika watu nisiowafahamu, wakamchukua mtoto wangu..nilichanganyikiwa, maana kwa muda huo sikuwa na mfanyakazi wa ndani, ...mtoto nilimuacha kalala chumbani,lakini baadaye wakanipigia simu, kuwa kama namtaka mtoto wangu, akiwa hai basi nifanye wanavyotaka wao, nikawaulize nifanye nini......’akatulia.

‘Kuna mambo mengi walitaka niwafanyie, sitaweza kukuambia yote kwa sasa, ila moja wapo ikawa kuweka sahihi kwenye huo mkataba, ...’akasema.

‘Mkataba gani huo, na una nini ndani yake?’ nikamuuliza.

‘Una mambo mengi sana, lakini muhimu ni kuwa mtoto huyo, atakuwa na haki sawa na watoto wengine..maana huyo mtu ana watoto wengine..na yeye  kutokana na huo mkataba kwasasa atatambulikana kama baba yake halali, ina maana mtoto wangu kwasasa ni mtoto wake halali,, na ana haki sawa ya kurithi mali ya baba yake, .....'akatulia kidogo, na moyoni nilimpongeza kwa hilo

'..na kwa vile ni mtoto wa kiume, yeye atapewa kipaumbele cha kusimamia mali yote, hapo umri wake ukifika,.... lakini kwa vile bado ni mdogo, mimi mama yake, nimepewa uhalali wa kusimamia mali zake..'akatulia kidogo, halafu akakohoa na kusema;

'Mimi sikuona ugumu wa hilo, na sikuona kwanini nisitie sahihi yangu kwa ajili ya makubaliano, hayo, lakini sikupenda kufanya hivyo,ila ni kwa shinikizo,....maana sio halali, sio mali iliyotokana na jasho langu, ..ooh.’akasema.

'Sasa kwanini ukatae, na ni kwa masilahi ya mtoto wako?' nikamuuliza
'Hebu nikuulize wewe, kama ingelikuwa wewe, unasikia mwanamke, anakuja kurithi mali yako ya jasho lako kihivyo ungelikubali?' akaniuliza.

'Mali yangu mimi, thubutu...usiongelee mali yangu, hayo ni yenu, na wewe hujataka kunishirikisha, ila nakuuliza hivi, tena na tena..'nikatulia kidogo

‘Ni nani huyo baba wa mtoto wako, mbona inakuwa siri, au ....’nikamuuliza na mara simu ikakatika,ilionekana kama kakatishwa na mtu, ...nilijaribu kupiga tena , lakini ikawa haipatikani,...nikaona nitafute ndugu wa huyu rafiki yangu anayeishi huko uwanja wa ndege, lakini sikuweza kumpata ndugu kama huyo, ila nikaona niende huko huko maeneo ya uwanja wa ndege huenda nikaonana naye, lakini haikuwa kazi rahisi.

Moyoni nilihisi huyu rafiki yangu yupo matatani, ni kama mtu kamnyang'anya simu, ili asiendelee kuongea, na sikujua nifanye nini, niliogopa kabisa kuwahusisha polisi, maana sikujua niwaambie nini...na wakati nawaza mara simu yangu ikalia,...nilipoangalia ni nani anayenipigia nikagundua kuwa ni rafiki wa mume wangu;

'Upo wapi wewe, nakutafuta sana.....'akasema.

'Unanitafutia nini?' nikamuuliza kwa sauti ya chuki.

'Kuna mambo muhimu sana, nataka kuongea na wewe....'akasema

‘Mambo gani?’ nikamuuliza kwa mkato,niliona kama ananipotezea muda wangu.

‘Kuhusu huyo wakili wa mume wako.....’akasema

‘Ana nini huyo wakili wa mume wangu..hebu ongea moja kwa moja?’ nikauliza

‘Huyu mtu ni hatari sana, kama tusipofanya haraka, utakuja kujijutia, nimegundua mambo mengi sana juu yake, na sipendi niyaongelee kwenye simu, tuonane tuongee tuone tutafanya nini, ni muhimu sana, kabla hujachelewa...’akasema na sauti yake ilinitia mashaka, inaonyesha msisitizo ...’nikasema;

‘Nitakuja nyumbani kwako....’nikasema.

‘Hapana, njoo ofisini kwangu....’akasema

‘Sawa vyovyote utakavyo, nipo njiani, nakuja....’nikasema na kuingia kwenye gari , sikujali tena mambo ya rafiki yangu.

NB: Sehemu hii ina mambo mengi sana yalitokea, ngoja kwa leo tuishie hapa


WAZO LA HEKIMA:Usalama wa majumbani kwetu, usalama wa watoto wetu, au usalama wa maofisini, ni muhimu sana, na ni vyema, vitu kama ufunguo, ulinzi, na usafi, vikapewa kwa watu wanaoaminika, kwa mkataba maalumu. Tatizo kubwa lililopo, ni kuwa watu hawo hawalipwi vizuri, na kutokana na hali ngumu za kimaisha, ni rahisi kwao kushawishiwa na kurubuniwa kwa pesa ndogo tu. Cha muhimu ni kuwajli sana hawa watu, na kuwatimizia mahitaji yao muhimu, ili waione hiyo kazi kama yao.

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Anonymous said...

Hello, i believe that i noticed you visited my weblog thus i got here to go back the want?.I'm attempting to in finding issues to
improve my website!I guess its ok to make use of a few of your ideas!!

Anonymous said...

Howdy very cool web site!! Man .. Beautiful .. Amazing .. I will bookmark your
blog and take the feeds additionally? I'm satisfied to search out a lot of useful information here in the post, we want work out more techniques in this
regard, thank you for sharing. . . . . .