Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, January 10, 2013

Uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi-46
‘Mama aliniambia kuwa siku aliyokutana na huyo mwanaume ambaye almuokoa ilikuwa kama pigo la pili katika maisha yake, maana hakutarajia kabisa kama itakuwa hivyo….’akaendelea kuongea huyo binti akisimulia kisa hiki.

*******

Turejee kidogo pale tulipoishia:

‘Haya sisi tunaondoka, tunashukuru sana kuwa mtoto amepatikana, na …safari ijayo tutakuja mimi na mume wangu,…’akasema malikia.

‘Na naomba mkija mje na huyo mwanaume aliyeniokoa….tafadhali mtafuteni popote alipo, …’akasema mama Maua.

‘Hilo usijali,..tutakuja naye….’akasema malikia huku akitabasamu,….na akafunua mdomo ili kumuelezea ukweli, ….

Lakini malikia alisita kumwambia ukweli je unafahamu ni kwanini, basi tuendelee na kisa hiki ili tujue ni kwanini malikia alisita kuelezea ukweli huo.

********

Wakati huo yule punda aliyempanda malikia akaanza kuondoka. Malikia aligeuka nyuma na kumwangalia yule mwanamke akiwa kasimama pale mlangoni huku akiwa kambeba mtoto wake, akatabasamu.

‘Mume wangu atafurahi sana kuwa hatimaye mtoto yupo mikononi mwa mama yake…’akasema na aliombea akifika huko kwao akute mambo yako shwari, ili safari ijayo warudi hapo pamoja, na kumtembea huyo mama, na ikiwezekana wamchuke wakaishi naye huko kwao msituni.

‘Lakini sheria hazimtaki…..’akasema na kuwaza

‘Sheria gani hizo za kubagua watu…kwani ana kosa gani, na kama ana kosa …hilo kosa hakulifanyia hapo, …hapana lazima hii hali iondolewe’akasema huku wakiendelea na safari ya kurudi kwao msituni. Na wakati wanaingia msituni, akakumbuka nyumbani kwao…..

‘Natamani sana nirudi niwaone ndugu zangu tena..lakinihaiwezekani, najua ipo siku nitarudi…’akasema huku machozi ya kimlenga lenga….

Wakati machozi yakimlenga , wakafika sehemu ambayo anaikumbuka sana, akasimamisha msafara, akaterema kwenye punda wake, na kuusogela ule mti. Akautizama na kuitafuta ile kamba ….huku akikumbuka tukio la siku ile….

Akakumbuka jinsi alivyomkimbia baba yake ….hebu turejee sehemu hiyo kidogo…..

Kauli ile ya baba ilinichefua, nikaona niondoke kabisa hapo nyumbani, sikuweza kuvumilia, nikalia sana huku nikikimbia, kuelekea nisipokujua nilikuwa nakimbilia tu, nilikimbia, hadi nikafika karibu na huu msitu, sehemu ambayo watu hutafutia kuni, na wakishakusanya hufika kwenye miti ambayo inatoa kamba. Na mimi nilifikia mti mmoja wa hizo kamba na kujikuta nachuna kamba na kuzikusanya hadi nikapata mzigo unaonifaa. Kamba hizi ni imara sana kwani hutumika pia kujengea.

Kamba hiyo ilikuwa ya nini?.....

Nilipohakikisha imekuwa vyema, nikapanda nayo juu ya mti , hadi kwenye tawi kubwa, nikaifunga ile kamba kwenye lile tawi upnde mmoja na upande mwingine niliokuwa nimetenegneza kitanzi, nikajivika shingoni, nikatulia huku nikiwaza jinsi mama yangu atakavyolia, lakini sikujali nikijua kuwa atalia kwa siku kadhaa na baadaye atanisahau na watu wote watakuja kunisahau na mimi nitakuwa nimeokoka na hayo mateso.

Nikasogea kwenye sehemu ambayo nilijua nikiachia tu ile kamba inanikaba halafu kitakachofuatia ni kupteza uhai. Nikamuomba mungu anisaidi nife kwa haraka, na kuomba kuwa  mama yangu asihuzunike sana, anishau kwani nampenda sana  ,lakini watu hawo wabaya hawanipendi ndio maana naona ni bora nikajipumzikie huko ahera,

Nikahesabu moja mbili tatu, nikajiachia, …nakweli kamba ikahikilia vyema shingoni na kunifanay niwe naelea hewani, pumzi ikaanza kuisha na shingo ikawa inauma kwa jisi ile kamba ilivyonikaba, jasho, likaanza kunitoka pumzi ikawa haitoki, nikajribu kuitoka ila kamba shingoni,lakini haikuwa kazi rahisi nikajaribu kupiga kelele ya kuomba msaada, lakini sauti haitoki, mkojo na hata haja,vikaanza kunitoka, 

Nikawa sasa nahangaika kwa kujipiga piga miguu ili kama ikiwezekana ile kamba ikatike, lakini ndio ikazidi kunikaba vyema, maumivu ya kichwa, kukosa pumzi, na hali ngumu ambayo sijawahi kuihi kabla, niliomba roho itoke haraka, lakini haikuwa hivyo, na giza likaanza kutanda kichwani, nikajua sasa muda umefika, na kabla sijapoteza fahamu  nikahisi nikipaa hewani ,nikajua ndio roho inasafiri, sikuweza kujua nini kilifuata baadaye...

Malikia lipowaza hayo, akikumbuka jinsi alivyotokea, na akikumbuka sehemu hiyo na jinsi alivyokuwa akimsimulia huyo manamama waliyemuacha huko nyuma, akapiga magoti ile sehemu na kutulia kwa muda; akiomba na kushukuru…..alikaa hivyo kwa muda na baaadaye akamkumbuka mume wake, kuwa yeye ndiye aliyemuokoa na kuikata ile kamba, hapo akasiamama kwa haraka, akitamani apae, ili afike kwa mume wake, amkumbatia na kumshukuru….….

**********
Ilikuwa ni siku nyingine ya kupokea ugeni wa watu kutoka msituni, ugeni huo  utafikia kwenye nyumba yao, sio ile nyumba ya muda ya majani ambayo walikimbilia kujificha kwani walishahakikishiwa kuwa hakuna tatizo tena.

`Msiwe na wasiwasi, utawala wa mzee hasimu, umeshaondoka, sasa hivi ni utawala mpya, utawala ambao jamii yote ya msituni ulikuwa ukiungojea,….usiwe na wasiwasi kabisa, rudini kwenye nyumba yenu muishi kwa amani…’ akaambiwa na malikia siku hiyo.

Na siku hiyo hiyo wakarudi kwenye nyumba yao, na kuikarabati, kwani walipata zawadi nyingi toka huko msituni, wakaziuza na kupata pesa, pesa ambazo walinunulia vifaa vya uujenzi, na nyumba ikapendeza.

Wakati mama Maua akiwa katulia ndani na mtoto wake mara mlango ukagongwa,  na haraka alimchukua mtoto wake na kumkimbiza ndani chumbani,…halafu akatoka na panga mkononi…
Mlangoni alikutana na mtu…kwanza alisita na kuanza kuogopa, lakini yule mtu akatoa tabasamu na kuinama kuonyesha heshima…..

‘Mimi ni mjumbe kutoka watu waishio msituni, nimetumwa na mfalme wetu kuwa atakuja kukutembelea wiki ijayo…’akaambiwa na mtu mmoja ambaye alijitambulisha kuwa anatokea huko msituni, na ni mmoja wa watumishi wa katibu wa mfalme.

‘Atakuja saa ngapi, na je atakuja na mkewe, na…..’hapo mama Maua akasita kuendelea, kwani licha ya kuwa alikuwa na hamu ya kumuona huyo mfalme, ambaye aliwahi kuishi naye, wakati akiwa mjamzito, lakini hakuwa na hamu naye kama alivyokuwa na hamu ya kumuona yule mtu aliyemuokoa.

‘Mtu huyo alinikaa akilini,….na kama kuna kupenda , basi kupenda hakuhitaji sura ya uso, maana huyo mtu sikuwahi kumuona sura yake, lakini cha ajabu akili yangu na moyo wangu ulikuwa ukitamani nimuone,….na sijui siku ya kumuona itakuwaje..’alisema mama Maua.

‘Muda wa kuja, sijaambiwa, na hilo huwezi kuambiwa kwasababu yule ni kiongozi wa jamii yetu, na usalama wake ni muhimu sana,..wewe jinadae kwa muda wowote anaweza kutokea, na kabla ya siku hiyo, kutakuwa na wageni wengine watatangulia, usiwe na wasiwasi nao, ….’akasema.

‘Hawoo wageni wengine ni akina nani, ….na alikuambia kuwa atakuja na nani mwingine?’ akauliza mama Maua akiwa na maana yake.

‘Huenda akafuatana na mtukufu malikia ambaye anakuja kwa ajili ya kumuona na kumbariki mtoto..ukumbuke kuwa mtoto, bado anatambulikana kuwa ni mtoto wa huko kwetu, na ….bado atapewa heshima na za watoto waliolelewa kwa ajili ya kuitumikia sehemu takatatifu….ana baraka na anastahili kubarikiwa’akaambiwa.

Mama alijiandaa siku hiyo, na kujiandaa kwake ilikuwa kwa huyo mtu mwingine, amabye hakuwa na uhakika kuwa atakuwepo kwenye huo msafara  lakini kutokana na maneno ya malikia ni kuwa mtu huyo atakuwepo. Mama Maua alijua kuwa mtu huyo anaweza akawa mmoja wa maasjari hodari, au kiongozi mashuhuri kwenye jeshi la huyo mfalme mpya.

Alimkumbuka jinsi alivyokuwa akimbeba kutoka sehemu moja hadi nyingine akiwa huko kwenye bonde la mauti. Japokuwa alikuwa katika hali mbaya,..ya kuumwa na kuchoka, lakini ile hali ya kuwa karibu na huyo mwanaume baada ya kumuokoa kutoka mdomono mwa mamba, na kuyajali maisha yake, …. ilimfanya amuone huyo mtu ni mwanaume  kipekee.

‘Wewe pumzika hapa, na utakula nyama hii…mimi nahitaji huko kwetu haraka, leo najua inawezekana ikawa siku ya mwisho, nimeota kuwa nahitaji haraka sana….na kama ulivyoona, hawa watu walikuja kuniua, lakini tumeweza kuokoka…..ngoja nifike huko nyumbani haraka, halafu nitarudi kuhakikisha kuwa upo mikono salama….’akasema.

Akayakumbuka hayo maneno na tabasamu likamjaa mdomoni, huku akiendelea kuweka nyumba katika hali ya usafi, baadaye akatulia kidogo, akijaribu kuikumbuka sura ya yule mtu,….ataikumbukaje sura yake , zaidi ya kuhisi kuwa huenda anafanana hivi…anachokumbuka na maumbile yake yaliyojaa ukakamavu, kuonyesha kuwa yeye ni jasiri…akatulia na kuangalia juu, na hapo akajiuliza;

‘Lakini kwanini huyu mwanaume hakutaka niione sura yake?’ akajiuliza.

‘Labda alikuwa na sababu zake za kiusalama, au ndivyo alivyoamrishwa na wakubwa zake waliomtuma,..’akahitimisha hivyo.

‘Kama atakuja, nitakuwa tayari ….hapana , nitamshawishi, tuishi naye huku, awe…ooh, lakini huenda ana mke , ..haiwezekani, mbona sikuwahi kusikia kuongelea kuhusu mke wake….atakuwa hana mke,….atakuwa hana mke…..’akawa anayarejea hayo maneno na mara akasikia sauti nje, sauti ambazo zilimfanya amchukue mtoto wake na kukimbilia chumbani….

NB: Kazi kweli kweli….muda hautoshi, ...hata hivyo tupo pamoja, tuweni pamoja.

WAZO LA LEO: Tenda wema angalau kidogo, bila kujali kuwa ni kidogo, kwani kidogo ni kwako, lakini kwa uliyemtendea wema ni kikubwa sana.

Ni mimi: emu-three

5 comments :

Anonymous said...

It's very effortless to find out any topic on net as compared to textbooks, as I found this article at this web page.
My page > bank lån

Anonymous said...

I have been browsing on-line greater than 3 hours
as of late, but I never found any fascinating article
like yours. It's lovely value enough for me.

In my opinion, if all webmasters and bloggers made excellent content material as you did, the internet will be a lot more helpful than ever before.


My weblog LavernHKliment

Anonymous said...

Hello it's me, I am also visiting this web site on a regular basis, this web
page is actually fastidious and the viewers are actually sharing nice thoughts.


Feel free to surf to my weblog :: BernadineSCurts

Anonymous said...

Its like you read my mind! You seem to grasp a lot approximately this,
such as you wrote the e-book in it or something. I feel that you just could
do with a few p.c. to power the message home a bit, however instead of that, that is
magnificent blog. A fantastic read. I'll definitely be back.Here is my webpage EleanoreQGluck

Anonymous said...

It's remarkable in favor of me to have a web page, which is valuable for my know-how.

thanks admin

Visit my blog ... EarlieMDies