‘Mama aliniambia kuwa
siku aliyokutana na huyo mwanaume ambaye almuokoa ilikuwa kama pigo la pili
katika maisha yake, maana hakutarajia kabisa kama itakuwa hivyo….’akaendelea
kuongea huyo binti akisimulia kisa hiki.
*******
Turejee kidogo pale tulipoishia:
‘Haya sisi tunaondoka,
tunashukuru sana kuwa mtoto amepatikana, na …safari ijayo tutakuja mimi na mume
wangu,…’akasema malikia.
‘Na naomba mkija mje
na huyo mwanaume aliyeniokoa….tafadhali mtafuteni popote alipo, …’akasema mama Maua.
‘Hilo
usijali,..tutakuja naye….’akasema malikia huku akitabasamu,….na akafunua mdomo
ili kumuelezea ukweli, ….
Lakini malikia alisita kumwambia ukweli je unafahamu ni kwanini, basi tuendelee na kisa hiki ili tujue ni kwanini malikia alisita kuelezea ukweli huo.
********
Wakati huo yule punda aliyempanda malikia akaanza
kuondoka. Malikia aligeuka nyuma na kumwangalia yule mwanamke akiwa kasimama
pale mlangoni huku akiwa kambeba mtoto wake, akatabasamu.
‘Mume wangu atafurahi sana kuwa hatimaye mtoto yupo mikononi
mwa mama yake…’akasema na aliombea akifika huko kwao akute mambo yako shwari,
ili safari ijayo warudi hapo pamoja, na kumtembea huyo mama, na ikiwezekana
wamchuke wakaishi naye huko kwao msituni.
‘Lakini sheria hazimtaki…..’akasema na kuwaza
‘Sheria gani hizo za kubagua watu…kwani ana kosa gani, na
kama ana kosa …hilo kosa hakulifanyia hapo, …hapana lazima hii hali
iondolewe’akasema huku wakiendelea na safari ya kurudi kwao msituni. Na wakati
wanaingia msituni, akakumbuka nyumbani kwao…..
‘Natamani sana nirudi niwaone ndugu zangu
tena..lakinihaiwezekani, najua ipo siku nitarudi…’akasema huku machozi ya
kimlenga lenga….
Wakati machozi yakimlenga , wakafika sehemu ambayo
anaikumbuka sana, akasimamisha msafara, akaterema kwenye punda wake, na
kuusogela ule mti. Akautizama na kuitafuta ile kamba ….huku akikumbuka tukio la
siku ile….
Akakumbuka jinsi alivyomkimbia baba yake ….hebu turejee sehemu
hiyo kidogo…..
Kauli ile ya baba
ilinichefua, nikaona niondoke kabisa hapo nyumbani, sikuweza kuvumilia, nikalia
sana huku nikikimbia, kuelekea nisipokujua nilikuwa nakimbilia tu, nilikimbia,
hadi nikafika karibu na huu msitu, sehemu ambayo watu hutafutia kuni, na
wakishakusanya hufika kwenye miti ambayo inatoa kamba. Na mimi nilifikia mti
mmoja wa hizo kamba na kujikuta nachuna kamba na kuzikusanya hadi nikapata
mzigo unaonifaa. Kamba hizi ni imara sana kwani hutumika pia kujengea.
Kamba hiyo ilikuwa ya nini?.....
Nilipohakikisha
imekuwa vyema, nikapanda nayo juu ya mti , hadi kwenye tawi kubwa, nikaifunga
ile kamba kwenye lile tawi upnde mmoja na upande mwingine niliokuwa
nimetenegneza kitanzi, nikajivika shingoni, nikatulia huku nikiwaza jinsi mama
yangu atakavyolia, lakini sikujali nikijua kuwa atalia kwa siku kadhaa na
baadaye atanisahau na watu wote watakuja kunisahau na mimi nitakuwa nimeokoka
na hayo mateso.
Nikasogea kwenye
sehemu ambayo nilijua nikiachia tu ile kamba inanikaba halafu kitakachofuatia
ni kupteza uhai. Nikamuomba mungu anisaidi nife kwa haraka, na kuomba kuwa mama yangu asihuzunike sana, anishau kwani
nampenda sana ,lakini watu hawo wabaya
hawanipendi ndio maana naona ni bora nikajipumzikie huko ahera,
Nikahesabu moja mbili
tatu, nikajiachia, …nakweli kamba ikahikilia vyema shingoni na kunifanay niwe
naelea hewani, pumzi ikaanza kuisha na shingo ikawa inauma kwa jisi ile kamba
ilivyonikaba, jasho, likaanza kunitoka pumzi ikawa haitoki, nikajribu kuitoka
ila kamba shingoni,lakini haikuwa kazi rahisi nikajaribu kupiga kelele ya
kuomba msaada, lakini sauti haitoki, mkojo na hata haja,vikaanza kunitoka,
Nikawa sasa nahangaika
kwa kujipiga piga miguu ili kama ikiwezekana ile kamba ikatike, lakini ndio
ikazidi kunikaba vyema, maumivu ya kichwa, kukosa pumzi, na hali ngumu ambayo
sijawahi kuihi kabla, niliomba roho itoke haraka, lakini haikuwa hivyo, na giza
likaanza kutanda kichwani, nikajua sasa muda umefika, na kabla sijapoteza
fahamu nikahisi nikipaa hewani ,nikajua
ndio roho inasafiri, sikuweza kujua nini kilifuata baadaye...
Malikia lipowaza hayo, akikumbuka jinsi alivyotokea, na
akikumbuka sehemu hiyo na jinsi alivyokuwa akimsimulia huyo manamama
waliyemuacha huko nyuma, akapiga magoti ile sehemu na kutulia kwa muda; akiomba
na kushukuru…..alikaa hivyo kwa muda na baaadaye akamkumbuka mume wake, kuwa
yeye ndiye aliyemuokoa na kuikata ile kamba, hapo akasiamama kwa haraka,
akitamani apae, ili afike kwa mume wake, amkumbatia na kumshukuru….….
**********
Ilikuwa ni siku nyingine ya kupokea ugeni wa watu kutoka
msituni, ugeni huo utafikia kwenye
nyumba yao, sio ile nyumba ya muda ya majani ambayo walikimbilia kujificha
kwani walishahakikishiwa kuwa hakuna tatizo tena.
`Msiwe na wasiwasi, utawala wa mzee hasimu, umeshaondoka,
sasa hivi ni utawala mpya, utawala ambao jamii yote ya msituni ulikuwa
ukiungojea,….usiwe na wasiwasi kabisa, rudini kwenye nyumba yenu muishi kwa
amani…’ akaambiwa na malikia siku hiyo.
Na siku hiyo hiyo wakarudi kwenye nyumba yao, na
kuikarabati, kwani walipata zawadi nyingi toka huko msituni, wakaziuza na
kupata pesa, pesa ambazo walinunulia vifaa vya uujenzi, na nyumba ikapendeza.
Wakati mama Maua akiwa katulia ndani na mtoto wake mara
mlango ukagongwa, na haraka alimchukua
mtoto wake na kumkimbiza ndani chumbani,…halafu akatoka na panga mkononi…
Mlangoni alikutana na mtu…kwanza alisita na kuanza kuogopa,
lakini yule mtu akatoa tabasamu na kuinama kuonyesha heshima…..
‘Mimi ni mjumbe kutoka watu waishio msituni, nimetumwa na
mfalme wetu kuwa atakuja kukutembelea wiki ijayo…’akaambiwa na mtu mmoja ambaye
alijitambulisha kuwa anatokea huko msituni, na ni mmoja wa watumishi wa katibu
wa mfalme.
‘Atakuja saa ngapi, na je atakuja na mkewe, na…..’hapo mama
Maua akasita kuendelea, kwani licha ya kuwa alikuwa na hamu ya kumuona huyo
mfalme, ambaye aliwahi kuishi naye, wakati akiwa mjamzito, lakini hakuwa na
hamu naye kama alivyokuwa na hamu ya kumuona yule mtu aliyemuokoa.
‘Mtu huyo alinikaa akilini,….na kama kuna kupenda , basi
kupenda hakuhitaji sura ya uso, maana huyo mtu sikuwahi kumuona sura yake,
lakini cha ajabu akili yangu na moyo wangu ulikuwa ukitamani nimuone,….na sijui
siku ya kumuona itakuwaje..’alisema mama Maua.
‘Muda wa kuja, sijaambiwa, na hilo huwezi kuambiwa kwasababu
yule ni kiongozi wa jamii yetu, na usalama wake ni muhimu sana,..wewe jinadae
kwa muda wowote anaweza kutokea, na kabla ya siku hiyo, kutakuwa na wageni
wengine watatangulia, usiwe na wasiwasi nao, ….’akasema.
‘Hawoo wageni wengine ni akina nani, ….na alikuambia kuwa
atakuja na nani mwingine?’ akauliza mama Maua akiwa na maana yake.
‘Huenda akafuatana na mtukufu malikia ambaye anakuja kwa
ajili ya kumuona na kumbariki mtoto..ukumbuke kuwa mtoto, bado anatambulikana
kuwa ni mtoto wa huko kwetu, na ….bado atapewa heshima na za watoto waliolelewa
kwa ajili ya kuitumikia sehemu takatatifu….ana baraka na anastahili
kubarikiwa’akaambiwa.
Mama alijiandaa siku hiyo, na kujiandaa kwake ilikuwa kwa
huyo mtu mwingine, amabye hakuwa na uhakika kuwa atakuwepo kwenye huo msafara lakini kutokana na maneno ya malikia ni kuwa
mtu huyo atakuwepo. Mama Maua alijua kuwa mtu huyo anaweza akawa mmoja wa
maasjari hodari, au kiongozi mashuhuri kwenye jeshi la huyo mfalme mpya.
Alimkumbuka jinsi alivyokuwa akimbeba kutoka sehemu moja
hadi nyingine akiwa huko kwenye bonde la mauti. Japokuwa alikuwa katika hali
mbaya,..ya kuumwa na kuchoka, lakini ile hali ya kuwa karibu na huyo mwanaume
baada ya kumuokoa kutoka mdomono mwa mamba, na kuyajali maisha yake, ….
ilimfanya amuone huyo mtu ni mwanaume kipekee.
‘Wewe pumzika hapa, na
utakula nyama hii…mimi nahitaji huko kwetu haraka, leo najua inawezekana ikawa
siku ya mwisho, nimeota kuwa nahitaji haraka sana….na kama ulivyoona, hawa watu
walikuja kuniua, lakini tumeweza kuokoka…..ngoja nifike huko nyumbani haraka,
halafu nitarudi kuhakikisha kuwa upo mikono salama….’akasema.
Akayakumbuka hayo maneno na tabasamu likamjaa mdomoni, huku
akiendelea kuweka nyumba katika hali ya usafi, baadaye akatulia kidogo,
akijaribu kuikumbuka sura ya yule mtu,….ataikumbukaje sura yake , zaidi ya
kuhisi kuwa huenda anafanana hivi…anachokumbuka na maumbile yake yaliyojaa
ukakamavu, kuonyesha kuwa yeye ni jasiri…akatulia na kuangalia juu, na hapo
akajiuliza;
‘Lakini kwanini huyu mwanaume hakutaka niione sura yake?’
akajiuliza.
‘Labda alikuwa na sababu zake za kiusalama, au ndivyo
alivyoamrishwa na wakubwa zake waliomtuma,..’akahitimisha hivyo.
‘Kama atakuja, nitakuwa tayari ….hapana , nitamshawishi,
tuishi naye huku, awe…ooh, lakini huenda ana mke , ..haiwezekani, mbona sikuwahi
kusikia kuongelea kuhusu mke wake….atakuwa hana mke,….atakuwa hana mke…..’akawa
anayarejea hayo maneno na mara akasikia sauti nje, sauti ambazo zilimfanya
amchukue mtoto wake na kukimbilia chumbani….
NB: Kazi kweli kweli….muda hautoshi, ...hata hivyo tupo pamoja, tuweni pamoja.
WAZO LA LEO:
Tenda wema angalau kidogo, bila kujali kuwa ni kidogo, kwani kidogo ni kwako,
lakini kwa uliyemtendea wema ni kikubwa sana.
Ni mimi:
emu-three
5 comments :
It's very effortless to find out any topic on net as compared to textbooks, as I found this article at this web page.
My page > bank lĂ¥n
I have been browsing on-line greater than 3 hours
as of late, but I never found any fascinating article
like yours. It's lovely value enough for me.
In my opinion, if all webmasters and bloggers made excellent content material as you did, the internet will be a lot more helpful than ever before.
My weblog LavernHKliment
Hello it's me, I am also visiting this web site on a regular basis, this web
page is actually fastidious and the viewers are actually sharing nice thoughts.
Feel free to surf to my weblog :: BernadineSCurts
Its like you read my mind! You seem to grasp a lot approximately this,
such as you wrote the e-book in it or something. I feel that you just could
do with a few p.c. to power the message home a bit, however instead of that, that is
magnificent blog. A fantastic read. I'll definitely be back.
Here is my webpage EleanoreQGluck
It's remarkable in favor of me to have a web page, which is valuable for my know-how.
thanks admin
Visit my blog ... EarlieMDies
Post a Comment