Mama Maua alifungua mlango taratibu, na alipopata upenyo wa
kutosha akachungulia kwa kupitia kwenye
ule upenyo mdogo, kuangalia nje, …akaona watu wamesimama, walikuwa maaskari wa
msituni, aliwatambua kwa mavazi yao, akajua ndio huo ugeni
umeshafika,….akaufunga ule mlango kwa haraka. na moyo ukawa unamwenda mbio,
akatulia, na kupangusha macho yake , …halafu akajiangali alivyovaa,
alipohakikisha kuwa yupo tayari, akashika mlango, akaufungua kwa mapana.
Na askari wawili wakapiga hatua tatu mbele hadi wakawa
karibu na ule mlango, wakainamisha vichwa vyao…na kutulia , na walikaa hivyo
kwa muda hadi Mama Maua aliposema;
‘Karibuni wageni….’akajitahidi kutoa sauti, lakini sauti
iliyotoka hapo ilikuwa kama sio yake.
Wale askari wawili wakasogea pembeni, na kuonyesha ishara kwa
wenzao, ambao walikwua wamesimama kwa mbali wakiwa na silaha zao. Wale askari
waliokuwa kwa mbali wasogea hadi sehemu iliyopo wazi …walipafika pale
wakasimama, na wakaja wengine wane wakiwa wamebeba vifaa vyao, ilikuwa ngozi ya
chui, na viti vya kienyeji, vilivyopambwa kwa ngozi za wanyama,wakaviweka,
sehemu ambayo huenda kiongozi wao atakaa, …halafu wakageuka kumwangalia mama
Maua.
‘Huko ndani yupo nani ?’ akaulizwa, na kabla hajajibu,
askari wawili wakawa wamesogea hadi pale mlangoni aliposimama Mama Maua.
‘Nipo peke….peke….yangu’akasema akisita hakutaka kusema yupo
na mtoto, na kusita kwake kule kukawapa wasiwasi wale maaskari, ….mmoja
akasogea mlangoni na kusema;
‘Samahani mama, sisi tunahitaji usalama, hatuna nia mbaya,
naomba niingie ndani nihakikisha unayoongea maana kauli yako
hainirizishi’akasema yule askari na hata kabla mama Maua hajamaliza yule askari
akawa keshaingia ndani.
Baadaye alitoka na kumpa mwenzake ishara….na mwenzako akatoa
sauti Fulani, ambayo ilikuwa ya kuashiria jambo, kwani baadaye kulianza
kuwasili kikosi kingine, na kati yao kulikuwa na mmoja kapanda juu ya punda,
alikuwa ni malikia…..
Maua akawa anamwangalia malikia anavyokuja akiwa juu ya yule
punda, aliyewekewa ngozi nyingine iliyotengenezwa na kuwa na kiti kizuri cha
kukalia,..akasema kimoyo kimoyo,;
‘Ndio malikia kaja
peke yake tena….ina maana kaamua kuja yeye badala ya mfalme wao?’ akajiuliza,
na akatupa jicho la kujiiba, na kuangali huku na kule kama atamuona mtu wake
anayemtafuta, lakini hakuona dalili yake,..moyo haukutulia, na akaona
akiendelea kuvumilia anaweza kupata shinikizo la damu, akamsogelea yule askari
na kumuuliza …
‘Mfalme wenu yupo wapi?’ akaumuuliza yule mlinzi, yule
mlinzi alimwangalia tu bila kusema neno, na Mama Maua akasogea mbele, kwani
aliishiriwa kufanya hivyo, na yule mtu askari aliyekuwa akliongoza hupo msafara
akatoa ishara na mara malikia akasonge mbele na kikosi chake.
Ule msafara wa malikia ulisogea hadi karibu na mlangon na
malikia akateremka, na kumkabili mama Maua, na mama Maua kwa vile alishajua
taratibu zao, alipiga magoti mbele ya malikia na kuinamisha kichwa, na malikia
akamshika kichwani kama ada yao akambariki, na baadaye akaambiwa ainuke,…
‘Kamachukue mtoto ndani….’akasema malikia kumuamrisha mmoja
wa watu wake, na kweli akaingia na kumchukua mtoto. Hawakuongea kwanza, kwani
kulikuwa na taraibu za kumhudumia mtoto, na hizo zilitakiwa kufanyika mbele ya
mama malikia, ikiwemo kumuogesha, kumpaka aina Fulani ya mafuta ya msituni,
ambayo wao wanaamini kuwa yanaondoa magonjwa, nuksi na mengineyo.
Baada ya taratibu hizo, …walimchukua yule mtoto na kukaa
naye pembeni, na malikia akamsogelea mama Maua na kumsalimia, na wakaingia
ndani na kuanza kuongea mambo mbali mbali,….
‘Samahanii kwa kukuingilia, lakini naomba uelewe kuwa sasa
hivi nalelewa kama mama malikia, kuna taratibu nyingi ambazo hata mimi zinanipa
shida sana, kwani siwezi kujifanyia baadhi ya mambo mwenyewe,…na kiusalama
siwezi kuwaingilia, kwani wao wanajua zaidi..inabidi niwasubiri mpaka wamalize
kazi zao, …halafu ndio….’akasema malikia na kukatisha kwani alionyeshwa ishara
Fulani na watu wake.
‘Mume wako ndio huyo anakuja ?’ akauliza malikia, na mama
Mua akaangalia kwe mbele, na kumuona yule mwanaume akija akiwa kavaliwa nguo na
tai…huwa mara nyingine anajipenda sana, lakini hakujua wapi kazipatia nguo
nzuri ….
‘Sio mume wangu, jamani…ninaishi naye tu humu ndani,….mimi
siwezi kuwa na mume mwingine tena, baada ya huyo aliyenipa mimba, ambaye
tulipendana sana sikuwahi kufikiria kuwa ninaweza kuachana naye….lakini ndio
dunia, na …’akasema mama Maua akitabasamu.
‘Na…na vipi mbona humalizii, usiniambie kuwa uliwahi
kukutana na mwanaume mwingine akakuingia akilini, zaidi ya huyo aliyekupa
mtoto, …hebu niambie rafiki yangu’akasema malikia huku akitabasamu.
‘Aaah, sio hivyo, unajua kuna hali unaweza ukaipitia na
ukazoeana na mtu , ukafikia kusema kuwa huyu anafaa kuwa mume wangu…lakini je
huyo mwanaume naye ana mawazo kama yako…na sijui kama kweli ninaweza kumuona
tena…’akasema huku akiangalia nje.
‘Unasema kuhusu yule mwanaume aliyekuoakoa…nimekupata, sasa
nimejua kwanini ulikuwa ukihitaji uonane neye tena..hilo lipo, nakubaliana
nalo, kuwa unaweza ukajiukuta kwenye shida, matatizo na akatokea mtu anakujali
na kuwa tayari kukusaidia..ukawa na ye hadi ukamzoea na hata kutamani kuwa naye
milele……’akatulia malikia kwa muda.
‘Ni kweli….mimi nakubaliana na wewe,na hayo ni
maumbile,….nikuulize mfano akatokea huyo aliyekuapa mtoto na huyo aliyekusaidia
ukaambia uchague mmojawapo utamchagua nani?’ akauliza malikia.
‘Sijui….na wala sikuwa nawazia hivyo, mimi nijuavyo, kila
kitu huja kwa wakati wake…na kama ikitokea hivyo, basi nitasema mwenye kisu
kikali ndiye atakayekula nyama….’akasema mama Maau huku akitabasamu,
Hiyo ilikuwa kwa mara ya kwanza kumuona mama Maua
alitabasmu, maana muda wote uso wake ulitawaliwa na huzuni,….hana raha,…na hapo
malikia akamwangalia kwa makini na huruma , upendo ukamjaa moyoni, akasema;
‘Hebu nikuulize, mfano huyo mtu aliyekuokoa akaja na
kukuambia kuwa yupo tayari kukuoa,. ..lakini ni lazima mkaishi naye msituni
utakubali?’ akauliza.
‘Maswali yako ni magumu sana…jibu la swali hilo ni kama
swali la mwanamke anayetaka kuolewa, sizani kama ana hiari ya kuchagua wapi pa
kwenda, lakini kwanza kuwa na hali hiyo ya kuolewa, kimoja ndio hufauata
kingine….’akasema mama Maua.
‘Nimekuelewa mpenda, na natumai…mambo yatakwenda vyema,
tusubiri kimoja ili kifuate kingine, au sio?’ akasema malikia.
‘Kwani huyo mfalme atakuja ?’ akauliza.
‘Kimoja ndio kifuate kingine, kwanza tunahitaji kumuona huyo
mtu wako, au sio..natumai moyo wako upo radhi kumuona huyo mtu aliyekuokoa
zaidi ya mfalme,…au sio?’ akauliza malikia na kabla hajajibu akamuona yule
mwanaume anayeishi na mama Maua akipita na kukaa sehemu ambayo kulikuwa na
walinzi, hakutaka kuingia ndani.
Malikia alimwangali yule mwanaume kwa nje, halafu akamgeukia
mama Maua na kusema;
‘Wengi wanasema huyo ni mume wako,…. lakini hayo hayatuhusu
kwa sasa, au sio, kimoja kwanza kingina kitafuattia..’akasema na kutabsamu,
lengo lake ni kumfanya mama Maua naye atabasamu, lakini ilikuwa sivyo, mwenzake
akaonekana kuingia na ile hali ya huzuni.
‘Mimi nakuona huruma sana naona kama unaishi maisha ya
taabu, kwani huyo mwanaume, anajulikana sana kuwa ni mlevi, na muuza pombe kali…na akilewa huwa
mkorofi sana, na hili tumaliogopa hasa kwa mtoto…’akasema malikia.
‘Ndio yeye mwanaume aliyeamua kuishi name, kwa kipindi hiki
cha shida, siwezi kumtupa, ….pamoja na mapungufu yake namshukuru sana kwa
kunijali,…kwani kuna wakati nazidiwa, mwanaume wa watiu anahangaika huku na
kule ninitafutia dawa, japokuwa si lolote, anahotegemea ni kipato kidogo kwa
kuuza hizo pombe....’akasema mama Maua akionyesha uso wa huzuni.
‘Lakini ….mama Maua, nakuomba ufikirie sana ombi letu,…kama
ulivyosema, umeguswa sana na huyo mwanaume aliyekuokoa, sasa kama je huyo
mwanaume akaja na wazo la kukuoa,…utakubali. Hata kama hilo halikuwezekana, sisi pia tulishafikia maamuzi ya kukukuchukua
ukaishi pamoja nasi huko msituni, ..najua unayoaona maisha ya huko kuwa sio ya
kawaida, lakini mbona mimi nimeyazoea, …..ni maisha mazuri tu ukiyajulia, …’akasema
malikia.
‘Hapana, nashukuru kwa ombi hilo, lakini sitaweza tena
kuishi huko, ….mengi yaliyotokea huko, ni machungu sana, sitaweza kutazamana na
watu wa huko…..’akatulia kidogo huku akikimbuka yaliyotokea nyuma; jinsi
alivyojifungua na baadaye akachukuliwa kwenda kutupwa ziwani ili aliwe na
mamba,..je ataweza kuishi na watu
waliomtambua kama mkosi wa jamii zao,….hapana huko sio pa kwenda tena.
‘Nashukuru sana kwa kunijali hivyo, lakini sitaweza kwenda
kuishi huko tena ….’akasema huku akiangalia nje, maana kulikuwa na sauti
zikiongezeka.
‘Najua utakubali tu, hasa akija huyo mwanaume aliyekuokoa,
….’akasema malikia huku naye akiangalia nje, na kweli nje kukawa na kikosi
kingine kinaingia na mama Maua
alipoangalia akaona huo msafara unaoingia kwenye eneo lao,…akawaona punda wawili,
ambao waliokuwa wakikokota gari kwa nyuma yao, na ndani ya hilo gari
linalokokotwa, ….kulikuwa na watu wawili..
Mama Maua akainua kichwa vizuri kuwaangalia wale watu
wawili, mmojawapo alikuwa ni mzee….akamkumbuka, yule mzee, …mzee mteule, mzee
aliyemuheshimu sana kwa busara zake, alikuwa kajaa mvi kichwa kizima, lakini
kilichomvutia sana na kumfanya moyo wake usitulie ni yule aliyekuwa pembeni
mwake….
‘Oooh ndiyo yeye…’akajikuta akisema kwa sauti.
‘Ndio ndio yeye….’akasema malikia akitabasamu.
Yule mtu alikuwa kavalia kiaskari, na kichwani kavalia kofia,
kofia ambalo lilimfunika kichwa kizima…kama vile vile….akatabasamu na akageka
kumwangali malikia, na malikia akatabsamu pia. Malikia akainuka na kumshika
mkono mama Maua na kumwambia.
‘Haya twenda ukampokee…’
‘Lakini, …mfalme yupo wapi?’ akauliza mama Maua.
‘Kimoja kwanza, ndio kifuate kingine…au sio ’akasema malikia
huku akitabasamu, na mama Maua akatabasamu….lile tabasamu la uhakika, tabasamu ambalo
malikia hakuwahi kuliona kwa huyu mama kabla, …wakaondoka wote wawili kwenda
kuwapokea hawo wageni maalumu….
NB: Kulikuwa na muendelezo wa sehemu hii lakini muda, jamani
muda…unakimbia kama nini..
WAZO LA LEO: Sisi
sote ni wana wa Adam, hatuna haja ya kuzarauliana, kama umejaliwa kipato, hali
nzuri, sura nzuri, nk, usijione sana na kuwadharau wenzi wako. Ukumbuke sura
nzuri, kipato ulicho nacho, maisha bora, uongozi nk ni wa kupita tu, kuna leo
na kesho, kuna kupanda na kushuka, …shukuru mungu kwa majaliwa hayo, na
watendee wema wenzako, ili upate baraka kutoka kwa mwenyezimungu.
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment