Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Wednesday, May 30, 2012

Hujafa hujaumbika-44 hitimisho-2



‘Kuna wataalamu wanasema mapenzi ya mwanzo, yana nguvu sana, ….macho na hisia za zinazomkuta mke au mume kwa mara ya kwanza, zinakuwa na nguvu sana, inakuwa kama mtu amepata kitu ambacho ni kizuri kwa mara ya kwanza, kama ujuavyo kuwa mapenzi ni jambo la kufurahisha na kupendezesha moyo, huitawala hisia ya mwanadamu, ni mambo asilia katika mwili wa mwanadamu….ni kama vile unapolamba asli kwa mara ya kwanza, utasema hakuna kitu kitamu kama asali duniani.Na hili halitawala hata hisia za kutenda tu, pia hutawala hisia za kuona na kusikia.
.
Kama unavyokumbuka Msomali, ukiwa mdogo, ulitokea kupendana na binti, jirani yako huko kijijini, yule mchumba wako wa utotoni, na unakumbuka mliwahi hata kufikia kufunga ndoa ya utotoni,…yale yalikuwa maswala ya kitoto, lakini yalijijenga ahdi mlipokuwa vijana,…naunakumbuka kipindi hicho cha uajanini, uliwahi kukufumaniwa,…ukumbuke kuwa mwenzako ule uchumba wa utotoni, hadi ujanani, ulikuwa wa kweli na ulimkaa moyoni, kwasababu alikupenda kiukweli, toka utotoni …. Hilo wewe huenda ulilichukulia kama mambo ya utotoni au sio…...

‘Sitaki useme lolote, najua ulishaniambi kuwa  bado ulikuwa unampenda, lakini upendo gani huo wa  namna hiyo, uwe na wasichana wengine, na mwenzako aweanakuangalia akijua etu unampenda,..yeye alikuwa akikuona na wasichana wengine, na mapaka siku hiyo akaja kukufumania, na kiukweli, siku ile alipokufumania, mwenzko ilimuuma sana, na sikumuuma tu, kwa maneno, yeye alikuja kuathirika kabisa kiakili, kisaikolojia, ingawaje baadaye wenzetu walikuja kulitafsri vingine,…

Siku ile aliporudi kwao akawa kama mtu aliyekumbwa na mashetani, kwani alipofika kwao alidondoka, na alipoinuka akawa anaongea lugha za ajabu, anaweweseka,….kama ungelijua kipindi kile ungelimuendea na kumuomba msamaha, huenda ingelisaidia,lakini sivyo ilivyokuwa, …na wao kamafamilia hawakuwa wanajua undani wa mahusianoo yao, na hata hivyo bado mlikuwa vijana, kama wazazi hawakujua jinsi gani binti alivyoathirika na tatizo hilo, wao walijua ni matatizo mengine kabisa.

Kwa kipindi hicho wewe ukajifanya kama hujali, kwa lile tendo la kufamaniwa, ulijiona wewe ni rijali, ni mwanaume,nahata hivyo ulisema kuwa hamkuwa mumefunga ndoa, kwahiyo hana ruhusa ya kukufuatilia maisha yako, hukuwa umeikumbuka ndoa yenu ya utotoni, kuwa mwenzako ilikuwa ni ndoa iliyokaa akilini, na aliiona kuwa ni ya kweli,…ilehali mwenzako ilimtesa, na kule kudondoka na kuweweseka, kukawa kuna mrudia mara kwa mara, wazazi hawakujua chanzo ni nini, wakahangaika kwa matibabu ya kila namna.

Baadaye waliporudi huko Kenya ambapo walikuwa na masikani yao pia, walitafuta wataalamu wa ushauri, madakitari bingwa ambao walijaribu kumsadia,lakini kiukweli haikusaidia kitu, kwasababu dakitari na dawa yake ni wewe, hakuna mwingine angeliweza kumtibia, lakini nani angelijua hilo, kwana hata huyo mgonjwa mwenyewe hakuwa na hali ya kujielezea kuwa chanzo nini, kwani hata yeye mwenyewe, hakuwa na ufahamu tena wakujua kuwa chanzo ni ile hali iliyokuwa umejijenga akilini mwake, na iliyokuja kuathirika na yale uliyomtendea wewe,,…

Binti akawa mgonjwa, mtu wa kuangaliwa na kuchungwa wakati wote maana ukimuachia anakimbia., anakimbilia wapi ,mwenyewe anadai anakwena kumtafuta mchumba wake,…..akawa anasoma kwashida, chini ya uangalizi wa karibu.

‘Huyo mchumba wake anayemtafuta ni nani…..?’wakawa wanaulizana wazazi mara kw amra bila jibu, maana wakimuuliza binti huyo mchumba ni nani, anasema  yeye hajui, na wala hakumbuki kusema kitu kamahicho, fahamu na kumbukumbu zanyuma zilikuwa hazijijengi,…zimejificha.

Waalipomuuliza mtaalamu mmoja wa mambo hayo ya mshetani, akawaambia;

‘Huyu ana jinni mahaba, na anaposema kuwa anakwenda kumtafuta mchumba wake, ni huyo jinni anamuita,….’akasema mtaalamu.

‘Sasa utamsaidieaje binti yangu, ukaliondoa hilo jinni mahaba?’ akauliza mama.

‘Anatakiwa akatibiwe baharini usiku wa manane, na kuku mwekundu, kitambaa cheusi,….’akaorozeshewa vitu vingi, ambavyo waliona wao wenyewe hawataweza kuvipata, wakatoa pesa ili huyo mganga akavitafute mwenyewe, na matibabu hayo yakafanyika, lakini haikusaidia kitu, ingelisaidiaje wakati ugonjwa huo sio kama alivyosema huyo mtaalamu, ugonjwa huo chanzo chake ni wewe….’akasema wakli mwanadadana huku akiniangalia mimi.

Walikaa sana Kenya bila kurejea nyumbani kwao, na akasoma huko, licha ya matatizo hayo ya kiafya lakini akili yake darasaniilikuwa nzuri tu akafaulu , kwenda masomo ya juu, na jinsi siku zilivyokwenda afya yake ikawa inabadilika,ila ambacho kilishindikana kuondoka ni chuki,dhidi ya wanaume.

Pale karibu yao kulikuwa na kiliniki imefunguliwa, ilikuwa kliniki ya matatizo ya akina mama, uzazi, ushauri nasaha na ndoa na mahusiano, ilianzishwa na familia moja ilikaa nje kwa muda mrefu, na waliporejea hapo 

Kenya waliamua kufungua kliniki hiyo, moja ya mambo waliyokuwa wakiyashughulikia ni maswala mazima ya ndoa na mahusiano.


Kliniki hiyo ilikuwa pia ikitoa mafunzo kwa wale wanaotaka kusomea mambo hayo, na pia ilikuwa ikitoa mafunzo kwa wale wanaotarajia kuingia kwenye ndoa kabla wajafunga ndoa na baadaya kufunga ndoa, hili wenzetu waliosoma wanalijua vyema, kuwa ndoa ni nusu ya maisha ya binadamu, kwahiyo inahitaji kuilewa, ni hilo limekuwa ni tatizo katika jamii, kama ni tatizo kumbe basi mtu anaweza akawekeza huko.

Familia hii ilikuwa inalijua hilo tatizo, kwani baba alikuwa dakitari bingwa wa akina mama, na mama alikuwa matroni, aliyebobea katika  maswala ya uzazi,  wakiwa huko Ulaya, walisomea kiukamilifu hiyo Nyanja na kumtafiti mwanadamu mwanaume na mwanamke jinsi alivyo, kisaikolojia ,kimaumbile na y ale yanayomkwaza husasani katika hisia za kimwili.

Familia hii ilibahatika kupata watoto wawili mapacha, na watoto hawa walipokuwa wakubwa na kuingia mshuleni, na wao wakavutika na msomo ya sayansi, na  hatimaye maji yakafuata mkondo na wao wakajikuta ni madakitari,….na mmoja wa mabinti hawa, akapata ajira huku Tanzania kama dakitari,
….turejeeni kwanza kwa mwanadada wetu.

Huyu mwanadada tunayemzungumzia, baada ya kumaliza shule, akawa anachukua mafunzo kwenye hiyo kliniki, ni katika kujiendeleza, na pia alivutika na masomo hayo, yeye kwa muda wake wa ziada akawa anafika kwenye hiyo kliniki kupata mafunzo, na kweli akavutika nayo sana, na hata akaona ni vyema, akasomea kabisa mambo ya uzazi , na mataizo yake, na kujikita pia katika mahusiano na matatizo yake.

Ile kliniki ikaamua kumchukua na kumuajiri. Katika masiha lazima kuna kupendana, na huyo binti Ikatokea kupendana na mvulana mmoja huko huko Kenya, walifikia hatua ya uchumba, na mwishowe wakaamua kuoana, na siku wanapeleka posa ikatokea ajali mbaya sana….yule mvulana alipona, lakini alikaa mwaka kitandani, hajiwezi.

Wazazi waile familia hawakurizika na hilo,mila na desturi zetu hazikucheza mbali familia ile ya mwanaume ikaamua kulifuatilia kimila wakakutana na hawa wataalamu wakimila, ambao hawakosi sababu, wakaambiwa huyo binti anamilikiwa na shetani, au kama walivyoliita jinni mahaba, kwahiyo sio rahisi kuolewa, na atakaye muoa atakumbana na matatizo makubwa.

Uchumba ule ukafa, haikuchukua muda akapata mchumba mwingine na huyu walifika hadi hatua ya kufunga ndoa, wakiwa katika hilo tendo la kufungishwa ndoa,yule binti akadondoka, na mara akaanza kuweweseka,na kusema hataki kuolewa kwasababu yeye keshaolewa,…
.
‘Eti nini keshaolewa na nani…..’akaluliza mzazi mmojawapo.

‘Mumesikia wenyewe akisema, keshaolewa na hawezi kuolewa kwa mara ya pili…..’akasema mume mtarajiwa.

NB: Leo nimechelewa kidogo kufika kijiweni, lakini nimeona siku isipite hivi hivi, tupate hicho kipnde kidogo,na nyie huku mkipata nafasi ya kutafakari na kama kuna mwenye maoni au aliwahi kukutana na dhahama kama hiyo changia ili tuboroshe hiki kisa…

WAZO LA LEO: Tujaribu kuwa karibu na watoto wetu, na kila linalotokea kwa watoto, hasa wanapofikia umri wa udadisi, tuwe makini na kauli zetu.  
Na tukumbuke sasa ni dunia ya utandawazi, watoto wetu wanajua mengi ambayo wewe kama mzazi huwezi amini kuwa wanaweza kuyajua, tuwe wadadisi wakuchnguza nyendo na mabdiliko ya watoto wetu, tusipende kuwaachia sana wafanyakazi wa nyumbani,…yote hayo ni majukumu yetu kama wazazi, …tukumbuke kuwa samaki hukunja angali mbichi.


Ni mimi: emu-three

2 comments :

Precious said...

M3 bado tuko pamoja Mkuu nilipotea sana kutokana na majukumu na mihangaiko ya kimaisha niliacha hiki kisa kikiwa sehemu ya kumi 12 lakini nashukuru Mungu nimeweza kupitia kila ninapopata muda kwa ajili ya mwendelezo na nimefikia mpk hii sehemu ya Hitimisho yaani nimeshakuwa addicted na hii blog na ni vile napenda sana visa ambavyo vinasaidia changamoto ktk maisha yetu, nilipokuwa sina muda wa kuingia nilikuwa nakosa amani kabisa. M3 endelea kukaza buti ipo siku utafaidika na kazi ya mikono yako. Jioni Njema M3 na wadau wote.

emuthree said...

Karibu tena Precious, hapa ni kwako,nilishaanza kuingiwa wasiwasi kuwa na wewe umekikimbia kijiwe. Tupo pamoja mpendwa,na ubarikiwe sana