‘ Kila mtu hakuamini ,hata mimi mwenyewe sikuamini hilo, hadi
pale nilipopata ushidi wa waza kutoka kwa wahusika wakuu,….maana ilikuwa kama
mchezo wa kuigiza, au pwagu na pwaguzi,…mchezo uliochezwa ndani ya famila moja
kila mmoja akimtenda mwenzake bila ya mwenzake kujua,….lakini athari zake
zikawa zinawaumiza watu wengine ambao….kwa namna moja walikuwa na matatizo kama
hayo, wakaingizwa kama ngao …..’akasema wakili mwanadada, huku tukiwa na hamu kila mmoja alikuwa na
maswali mengi kichwani ambayo majibu yake tulitarajia kuyapata kutoka kwa huyu
wakili mwanadada.
‘Mimi hapo sielewi,matatizo ya familia yanakwenda
kuwahusisha watu wengine ….kwa vipi, kama mimi nahusika vipi na matatizo ya
familia nyingine, ambayo hata siijui vyema….?’ Nikauliza.
‘Jambo kubwa,ambalo nililigundua ambalo ndilo kiini cha hili
tatizo, ni swala la ndoa na mapenzi, ….’akasema
na wote tukabakia tukimwangalia huku tukiwa hatuelewi kabisa nini anachotaka kusema, iweje ndoa na mapenzi yazae vifo vya watu....!
.
‘Ndoa na mapenzi yalete maafa hadi kuuana, kwa vipi na ni nao hawo walisababisha hayo, usiniambia chanzo ni mimi, sikubali kabisa….?’ Nikauliza.
‘Ndoa na mapenzi ni swala nyeti, na tatzio hili limekuwa
likiathiri watu bila wenyewe kujua, na hata wanaolisababisha hilo,wanaweza wasijue kuwa chanzo na tatizo ni ndoa yao…..’akatulia na kuniangalia
mimi, nikawa kimiya kumskiliza.
‘Bosi anaweza akakorofishana na mkewe huko nyumbani,
kwasababu za kindoa, kwasababu za mahusiano ,hasira zile akazipeleka ofisini,
na mkamuoana bosi kabadilika, hasira tele, au ukimiya usio wa kawaida au ….hata
utendaji mbaya, kiini chake ni ndoa,….hili watu hawajui, na huenda wakataka
kujifanya kuwa sio sababu….’akatulia kidogo, na kuinama chini.
Hii ni kuonyesha kuwa wanawake niwatu muhimu sana,…katika
jamii, kutokana na wanawake tunaweza kuwa na taifa tulivu na la amani, kwani
ndoa ndio chimbuko la kizazi ambacho kinaweza kikawa chema au kibaya, kutokana
na malezi, kutokana na masikilizano ya wanandoa, kutokana na sintofahamu
inayoweza ikajijenga ndani ya ndoa….’akatulia an kutuangalia …
‘Mimi nazungumzahili baada ya utafiti wa kina, huwezi amini
hata viongozi wa nacho wanaathiriwa na hili,…ndio maana watafiti wanapendekeza
kuwa ili kiongozi awe bora, lazima nandoa yake iwe bora,…kama ndani ya ndoa
yake kunamsuguano, lolote linaweza likatokea…huko kwenye siasa sitaki
kupaendea, ila ninalotaka kusema ni kuwa tukio hili, limagubikwa na msuguano,
wa ndoa, ….ndoa mbayo iliwakutanisha mafahali wawili, wakawa wanapigana na
zinazoumia ni nyasi….’akasema wakili nakutulia.
‘Samahani,….mimi bado umeniacha njia panda….’nikaanza
kulalamika.
‘Nilitaka kuwaweka kwazi kuhusu hilo kwanza, kabla
sijawaelzea kazi nzimaya hili tukio,…tukio ambalo ni kielelezo kwa jamii, kuwa
ndoanimuhimili muhimu katika maisha ya jamii, …tujiribunii kuijua , kuiheshimu,
na wanadoa wasikubali tu kuitwa wanandoa, wawe wakiifanyia kazi,….waziboreshe
nda zao kwa kujifunza ….kamazilivyo Nyanja nyingine…’akatulia tena kidogo, na
mimi nikaoan akma anaipoteze muda nikauliza swali kwa haraka.
‘Tuambie ulivyogundua , maana hadi sasa mimi bado unanichanganya
tu, uligunduaje hayo yote maana ukiangalia ilivyo huwezi hata kukisia, wengi
walijua kuwa chimbuko la tukio hili zima ni kutoka kwangu, …kwasabbu ya damu
yangu moto…..maana kila jambo lililotokea limekuwa likinigusa mimi sio chanzo
cha yote, mimi ni kama mhanga mwingine wa ….ndoa za watu wengine.’nikasema na
hata mkuu akakubali kwa kichwa huku nikikosa neno sahihi la kumalizia.
‘Dunia hii ina mengi, na binadamu ni kiumbe wa ajabu sana,
kila mara anajaribu kuutumia ubongo wake,
akiona kuwa kuna upenyo wa kuutumia, bila kusahau kuwa na wenzake wana
ubongo huo huo na wanafikira hizo hizo,ila pengine kwa njia nyingine….na ndivyo
ilivyokuwa kwenye hili tukio zima,….tukio ambalo chanzo chake ni ndoa, hasira
zikazaa visasi, na visasi vikawa vinaumiza watu wengine, ambao nao wana
matatizo yao kama hayo, na hilo lilipikwa kitaalamu…...’akasema wakili
mwanadada akijaribu kutafuta njia ya kutuelewesha maana hadi hapo tulikuwa abado
hatujamuelewa vyema , licha ya kuwa mshukiwa wa tukio zima alishajulikana.
‘Ili muelewe hili tukio kwa undani, naona nielezee kwa
kupitia wahusika,nikianzia kwako wewe mtoto wa Msomali ,ambaye nitakuita
muhusika, ambaye kwa usoni mwa watu ulionekana kama mhusika mkuu, ….lakini kiundani wewe sio muhusika
mkuu, wewe ulikuwa kama tawi kwenye shina,….wapo wahusika wakuu wawili ambao ni
shina la tukio zima,…tutakuja kuwajua, ila nataka nianzie kwako wewe ili
kukuweka sawa…’akasema wakili mwanadada.
‘Nilishakuhoji sana, na katika kukuhoji huko nilgundua mengi
dhidi yako…..mambo haya yanaweza yakaanza mwanzoni tu mwa ndoa, watu hamkai
mkaongea, kila mmoja anajiona anajua zaidi ya mwenzake, na likitokea jambo,
kila mmoja anakuwa na maamuzi yake,…na hatimye lile pendo linageuka kuwa chuki,
wivu, usio na tija,…nakulipizana kisasi,….
Mimi nikakaa kimiya, nikisikiliza ,lakini kwa upande
mwingine akili yangu ikawa ikitamani kusikia mengi kwa wkati mmoja, hapo
nilikuwa na mawazo ya yule mgonjwa aliyekufa kule hospitalini, nilikuwa
nikitaka kwanza aniambie ukweli kuhusu huyo mgonjwa, kabla hajaongea kuhusu
mimi, kwahiyo wakati anaanza mimi akili yangu ikazama na kujiuliza,…
Hivi,…..huyo marehemu ...imekuwaje....mbona siambiwi lolote kuhusu yeye, maana kila nilipodadisi lini atazikwa nimekuwa nikipigwa danadana, na
kuambiwa hilo nitaambiwa baadaye……na hata ndani ya mahakama sikusiki hakimu
akiligusia,….kuna nini kinaendelea,…akili yangu ikasema `hapo kuna kitu
nafichwa..na kwanini nifichwe, hata hivyo huyo mtu mbona sijajua umuhimu wake
kwangu…’ sikuvumilia nikauliza;
‘Kabla hujaendelea nataka kujua jambo moja,kuhusu huyo
marehemu,…..kitu cha ajabu ni kwamba, sijasikia lolote mpaka sasa kuhusu yeye,
na maandalizi ya mazishi yake, …., jana nimewauliza mkasema hilo nitaambiwa
baadaye, sasa leo naona mnanipiga danadana, kwanza sijamjua ni nani, na kwanini
alikuwa akitaka kuongea na mimi, na alitaka kuniambia nini,hamuona mnanitesa mimi
kiakili…..’nikalalamika.
‘Ndio maana nawataka mtulie niwape tukio zima , huko kwa
huyo anayekutesa akili yako,tutafikia, kwani ni mmoja wa wahusika , sijui tumuiteje
, tiutamuita muhusika mashuhuri, kama ulivyo wewe…..maana huyo unayetaka kumjua
ni nani, yeye ndiye kiunganishi cha tukio zima, …sasa niwaulize mpo tayari
niwaambia nini kilitokea, au bado mna maswali mengine….’akauliza wakili
mwanadada na kutuangalia machoni kwazamu, na sisi tulibakia kimiya ….
*********.
Hiki ni kikao maalumu
ambacho tulijikuta tupo mimi, mkuu na wakili mwanadada, hapo tulikuwa kwenye chumba maalumu cha maongezi, baada ay
kutoka kwenye chumba cha mahakama ambapo
tulikutana na hakimu, ambaye alitaka kujua hatima ya kesi inayonikabili mimi,
…na baada ya maongezi na hakimu, ilionekana kuwa mimi sina hatia, ila
nilishikiliwa ikioanekanna kuwa mimi ndiye muhusika , lakini baada ya uchunguzi
, iligundulika kuwa mimi nilitegewa ionekane kuwa ndiye muhusika kiujanaj wa
huyo mhalifu, …
‘Sio kwa vile umeambiwa wewe huna makosa ndio uondoke hapa
jijini,hapana wewe ni shahidi muhimu sana katika kesi hii, usije ukaondoka, unahitajika
sana….’akasema wakili mwanadada.
‘Nimekusikia muheshimiwa ,….’nikasema nakumwanagalia hakimu
ambaye alikuwa akimsikiliza wakili mwanadada akiwa anatoa maelezo yake kuhusi
kesi niliyokuwa nimekamatwa nayo,…, na alipomaliza kutoa hayo maelezo hakimu
akaanza kumhoji wakili mwanadada akuliza swali,
‘Je huyo mshukiwa mumeshamkamata…?’akauliza hilo swali na
kumwangalia mkuu, mkuu ambaye kwa muda
mwingi alikuwa kimiya, akionekana mwingi wa mawao akasema;
‘Hajakamatwa muheshimiwa, ila tumeshagundua wapi alipo na
mtego umeshawekwa , …nia na lengo letu akamatwe bila umwagaji wa damu…’akasema
mkuu.
‘Kwahiyo mnataka kusemaje,maana nimewaita hapa kuwasikiliza
nyie,kutokana na kesi zenu ambazo zinakuwa haziishi, kila mnapoleta kesi izenu
zinakuwa hazijakamilika, …na hili halinifurahishi, kwanini msitafute ushahidi
wa kutosha kabla hamjazifikisha hizo kei zenu kwangu, msifanye kubahatisha, ….hilo
sitaki lijirudie tena,mnanielewa…?’akasema muheshimiwa hakimu.
‘Tumekuelewa muheshimiwa, imetokea hivyo kwasababu, kesi
hizi zimajisokota , ni watu wajanja walibuni mbinu zao, kwa kuichezea sheria,
na saikolojai za watu, wamekuwa wakitumia uzaifu wa wenzao na kujifanya
hawahusiki,…na matokeoa yake wakawa wanakamatwa watu wakijulikana wao ndio wahusika,
kumbe wahusika wamejificha kiujanja, na
jinsi walivyojipanga isingelikua rahisi kuwajua kuwa ni wao wahalifu,….lakini
ubaya hauna kwao wamepatikana…..’akasema wakili mwanadada.
‘Unatakiwa uliweke hilo wazi, na hakikisha kuwa unakuja na ushahid
uliokamilika, maana hapa tu umeongea kimafumbo, kitu ambacho sitakitaka kwenye
mahakama yangu, uweke uweke kila kitu wazi, ….na hakikisheni kuwa huyo mshukiwa
anakamatwa haraka iwezekanavyo, sitaki kusikia matendo macahafuyakitendeka
tena, na wakati mumesemamnaushaidi wa kutosha, mkameteni na haki itendeke
,….’akasema muheshimiwa na kuwaangalia wakili na mkuu kwa kila mmoja kwa wakati wake.
‘Sawa muheshimiwa, leo au kesho utapata taarifa kamili, na tunakuhakikishia
kuwa ushahidi wote umekamilika, ndio maana huyo mshukiwa akakimbia,….yeye
alichofanya ni kujaribu kuvuta muda ili azima yake ikamilike, lakini tutahakikisha kuwa hafanyi lolote
baya..’akasema mkuu.
‘Sawa hilo tumemaliza, na nini mnataa kusema kuhusu huyu
mshukiwa Msomali, maana leo mlisema mtakuja na kauli sahihi, kuwa yeye ndiye mshitakiwa
na tunze kusikiliza kesi yake, na kama ndio hivyo ni nani wakili wake, …..?’
akauliza muheshimiwa Hakimu.
‘Kama nilivyosema awali, muheshimiwa, kesi hizi
zilijisokota, na hawa watu walikuwa wakitumia mbinu, ambazo zimetufanya
tuwakamate watu, tukijua wao ndio wahalafu, kumbe, wao wamejikuta wakiwa kwenye
tukioo kama chambo tu, …..’akasema wakili mwanadada.
‘Kwahiyo hapa unataka kusema nini, kuwa kesi dhidi ya
Msomali tuifute….nawaonya tena, mjue kwa mtindo huu mnatupoteze amuda wetu,
kuna kesi nyingi za kusikiliza, na isiwe kila tukipanga muda wa kesi yenu,
mnadai hili halijakamilika na sasa mnadai huyu mshukiwa sio yeye, ni yupi basi
mshitakiwa, ili,tuyamalize haya matatizo…?’ akauliza muheshimiwa hakimu
akimwangalia wakili Mwanadada, na wakili mwanadada akamgeukiwa mkuu,akiwa
anataka yeye aliongelea hilo, na hakimu alipoona wanatupiana macho, akasema;.
‘Kwahiyo mnachotaka kusema hapa ni kuwa kesi dhidi ya
Msomali, ifutwe, kwa masharti kuwa, muda wowote atahitajika kama shahidi, ila
sasa yupo huru,….sawa?’akasema muheshimwa hakimu na wakili mwanadada akasema;
‘Ndio Muheshimwa, tunaomba kesi hiyo ifutwe dhidi yake,….hana hatia,
ila atahitajika kama shahidi…
‘Sawa, mshitakiwa Msomali, kuanzia sasa upo huru,… ila kama
ulivyoarifiwa utahitajika kama shahidi, hilo mtaliongelea wenyewe huko, naona
hatuna zaidi, …nasubiri mumulete huyo mshitakiwa anayehusika…...’akasema muheshimiwa
Hakimu na akawatizama kwa muda wakili na mkuu na alipona wote wapo kimiya
akainuka kwenye kiti chake nakuondoka.
Mimi na wakili mwanadada na mkuu, tukatoka na kuingia kwenye
chumba cha maongezi, ambapo mimi nilikuwa na mengi ya kujua, na hapo ndipo
wakili mwanadada akaanza kuelezea jinsii ilivyokuwa kwenye kisa hiki hatua kwa
hatua…..akianzia kwangu,na malezo yake yalijifanya nijijue …. na hapo akili
yangu ikama kama mtu aliyezibuliwa,,…ni kama mtu aliyekuwa kaingiwa na maji
masikioni, na yale maji yakatolewa……
NB: Haya wapenzi wa blog hii, naanza hitimisho la hiki kisa…..zipo
njia nyingi za kuandika visambalimbali, unaweza ukaandika kisa ukikianzia kwenye shina
au aukakianzia mwishoni,ukakianzia kwenye matawi yake,….kisa hiki ni mtindo mwingine
ambao tumeaniza kwenye matawi, na sasa
tunaingia kwenye shina…mpo hapo…
WAZO LA LEO:
Dunia ni starehe, na starehe iliyo bora ni maisha ya mume na mke ndani ya ndoa.
Na ili starehe hiyo ikamilike na kuleta
matunda bora na mema, matunda ambayo nikiini cha amani na upendo duniani, ni
bora wewe unayatarajia kuingia kwenye ndoa ukatafuta mke au mume mwema, na pia
ni muhimu ukaijua ndoa na misingi yake vyema.
Ni mimi:
emu-three
1 comment :
Ndoa ni mawasiliamo, masikilizano, utulivu= UPENDO WA NDOA...nasubiri hitimisho la kisa hiki kwa hamu kwelikweli...Kazi nzuri na nakutakia nguvu na kheri.
Post a Comment