‘Kuna wataalamu wanasema mapenzi ya mwanzo, yana nguvu sana,
….macho na hisia za zinazomkuta mke au mume kwa mara ya kwanza, zinakuwa na
nguvu sana, inakuwa kama mtu amepata kitu ambacho ni kizuri kwa mara ya kwanza,
kama ujuavyo kuwa mapenzi ni jambo la kufurahisha na kupendezesha moyo, huitawala
hisia ya mwanadamu, ni mambo asilia katika mwili wa mwanadamu….ni kama vile
unapolamba asli kwa mara ya kwanza, utasema hakuna kitu kitamu kama asali duniani.Na hili halitawala hata hisia za kutenda tu, pia hutawala hisia za kuona na kusikia.
.
Kama unavyokumbuka Msomali, ukiwa mdogo, ulitokea kupendana
na binti, jirani yako huko kijijini, yule mchumba wako wa utotoni, na
unakumbuka mliwahi hata kufikia kufunga ndoa ya utotoni,…yale yalikuwa maswala
ya kitoto, lakini yalijijenga ahdi mlipokuwa vijana,…naunakumbuka kipindi hicho
cha uajanini, uliwahi kukufumaniwa,…ukumbuke kuwa mwenzako ule uchumba wa
utotoni, hadi ujanani, ulikuwa wa kweli na ulimkaa moyoni, kwasababu alikupenda
kiukweli, toka utotoni …. Hilo wewe huenda ulilichukulia kama mambo ya utotoni
au sio…...
‘Sitaki useme lolote, najua ulishaniambi kuwa bado ulikuwa unampenda, lakini upendo gani huo
wa namna hiyo, uwe na wasichana wengine,
na mwenzako aweanakuangalia akijua etu unampenda,..yeye alikuwa akikuona na
wasichana wengine, na mapaka siku hiyo akaja kukufumania, na kiukweli, siku ile
alipokufumania, mwenzko ilimuuma sana, na sikumuuma tu, kwa maneno, yeye
alikuja kuathirika kabisa kiakili, kisaikolojia, ingawaje baadaye wenzetu
walikuja kulitafsri vingine,…
Siku ile aliporudi kwao akawa kama mtu aliyekumbwa na mashetani,
kwani alipofika kwao alidondoka, na alipoinuka akawa anaongea lugha za ajabu,
anaweweseka,….kama ungelijua kipindi kile ungelimuendea na kumuomba msamaha,
huenda ingelisaidia,lakini sivyo ilivyokuwa, …na wao kamafamilia hawakuwa wanajua
undani wa mahusianoo yao, na hata hivyo bado mlikuwa vijana, kama wazazi
hawakujua jinsi gani binti alivyoathirika na tatizo hilo, wao walijua ni
matatizo mengine kabisa.
Kwa kipindi hicho wewe ukajifanya kama hujali, kwa lile
tendo la kufamaniwa, ulijiona wewe ni rijali, ni mwanaume,nahata hivyo ulisema
kuwa hamkuwa mumefunga ndoa, kwahiyo hana ruhusa ya kukufuatilia maisha yako,
hukuwa umeikumbuka ndoa yenu ya utotoni, kuwa mwenzako ilikuwa ni ndoa iliyokaa
akilini, na aliiona kuwa ni ya kweli,…ilehali mwenzako ilimtesa, na kule
kudondoka na kuweweseka, kukawa kuna mrudia mara kwa mara, wazazi hawakujua
chanzo ni nini, wakahangaika kwa matibabu ya kila namna.
Baadaye waliporudi huko Kenya ambapo walikuwa na masikani
yao pia, walitafuta wataalamu wa ushauri, madakitari bingwa ambao walijaribu
kumsadia,lakini kiukweli haikusaidia kitu, kwasababu dakitari na dawa yake ni
wewe, hakuna mwingine angeliweza kumtibia, lakini nani angelijua hilo, kwana
hata huyo mgonjwa mwenyewe hakuwa na hali ya kujielezea kuwa chanzo nini, kwani
hata yeye mwenyewe, hakuwa na ufahamu tena wakujua kuwa chanzo ni ile hali
iliyokuwa umejijenga akilini mwake, na iliyokuja kuathirika na yale
uliyomtendea wewe,,…
Binti akawa mgonjwa, mtu wa kuangaliwa na kuchungwa wakati
wote maana ukimuachia anakimbia., anakimbilia wapi ,mwenyewe anadai anakwena kumtafuta
mchumba wake,…..akawa anasoma kwashida, chini ya uangalizi wa karibu.
‘Huyo mchumba wake anayemtafuta ni nani…..?’wakawa
wanaulizana wazazi mara kw amra bila jibu, maana wakimuuliza binti huyo mchumba
ni nani, anasema yeye hajui, na wala
hakumbuki kusema kitu kamahicho, fahamu na kumbukumbu zanyuma zilikuwa
hazijijengi,…zimejificha.
Waalipomuuliza mtaalamu mmoja wa mambo hayo ya mshetani,
akawaambia;
‘Huyu ana jinni mahaba, na anaposema kuwa anakwenda
kumtafuta mchumba wake, ni huyo jinni anamuita,….’akasema mtaalamu.
‘Sasa utamsaidieaje binti yangu, ukaliondoa hilo jinni
mahaba?’ akauliza mama.
‘Anatakiwa akatibiwe baharini usiku wa manane, na kuku
mwekundu, kitambaa cheusi,….’akaorozeshewa vitu vingi, ambavyo waliona wao wenyewe
hawataweza kuvipata, wakatoa pesa ili huyo mganga akavitafute mwenyewe, na
matibabu hayo yakafanyika, lakini haikusaidia kitu, ingelisaidiaje wakati
ugonjwa huo sio kama alivyosema huyo mtaalamu, ugonjwa huo chanzo chake ni wewe….’akasema
wakli mwanadadana huku akiniangalia mimi.
Walikaa sana Kenya bila kurejea nyumbani kwao, na akasoma
huko, licha ya matatizo hayo ya kiafya lakini akili yake darasaniilikuwa nzuri
tu akafaulu , kwenda masomo ya juu, na jinsi siku zilivyokwenda afya yake ikawa
inabadilika,ila ambacho kilishindikana kuondoka ni chuki,dhidi ya wanaume.
Pale karibu yao kulikuwa na kiliniki imefunguliwa, ilikuwa
kliniki ya matatizo ya akina mama, uzazi, ushauri nasaha na ndoa na mahusiano,
ilianzishwa na familia moja ilikaa nje kwa muda mrefu, na waliporejea hapo
Kenya waliamua kufungua kliniki hiyo, moja ya mambo waliyokuwa
wakiyashughulikia ni maswala mazima ya ndoa na mahusiano.
Kliniki hiyo ilikuwa pia ikitoa mafunzo kwa wale wanaotaka
kusomea mambo hayo, na pia ilikuwa ikitoa mafunzo kwa wale wanaotarajia kuingia
kwenye ndoa kabla wajafunga ndoa na baadaya kufunga ndoa, hili wenzetu waliosoma
wanalijua vyema, kuwa ndoa ni nusu ya maisha ya binadamu, kwahiyo inahitaji
kuilewa, ni hilo limekuwa ni tatizo katika jamii, kama ni tatizo kumbe basi mtu
anaweza akawekeza huko.
Familia hii ilikuwa inalijua hilo tatizo, kwani baba alikuwa
dakitari bingwa wa akina mama, na mama alikuwa matroni, aliyebobea katika maswala ya uzazi, wakiwa huko Ulaya, walisomea kiukamilifu hiyo
Nyanja na kumtafiti mwanadamu mwanaume na mwanamke jinsi alivyo, kisaikolojia
,kimaumbile na y ale yanayomkwaza husasani katika hisia za kimwili.
Familia hii ilibahatika kupata watoto wawili mapacha, na
watoto hawa walipokuwa wakubwa na kuingia mshuleni, na wao wakavutika na msomo
ya sayansi, na hatimaye maji yakafuata
mkondo na wao wakajikuta ni madakitari,….na mmoja wa mabinti hawa, akapata
ajira huku Tanzania kama dakitari,
….turejeeni kwanza kwa mwanadada wetu.
Huyu mwanadada tunayemzungumzia, baada ya kumaliza shule,
akawa anachukua mafunzo kwenye hiyo kliniki, ni katika kujiendeleza, na pia
alivutika na masomo hayo, yeye kwa muda wake wa ziada akawa anafika kwenye hiyo
kliniki kupata mafunzo, na kweli akavutika nayo sana, na hata akaona ni vyema,
akasomea kabisa mambo ya uzazi , na mataizo yake, na kujikita pia katika
mahusiano na matatizo yake.
Ile kliniki ikaamua kumchukua na kumuajiri. Katika masiha
lazima kuna kupendana, na huyo binti Ikatokea kupendana na mvulana mmoja huko
huko Kenya, walifikia hatua ya uchumba, na mwishowe wakaamua kuoana, na siku
wanapeleka posa ikatokea ajali mbaya sana….yule mvulana alipona, lakini alikaa
mwaka kitandani, hajiwezi.
Wazazi waile familia hawakurizika na hilo,mila na desturi
zetu hazikucheza mbali familia ile ya mwanaume ikaamua kulifuatilia kimila wakakutana
na hawa wataalamu wakimila, ambao hawakosi sababu, wakaambiwa huyo binti anamilikiwa
na shetani, au kama walivyoliita jinni mahaba, kwahiyo sio rahisi kuolewa, na
atakaye muoa atakumbana na matatizo makubwa.
Uchumba ule ukafa, haikuchukua muda akapata mchumba mwingine
na huyu walifika hadi hatua ya kufunga ndoa, wakiwa katika hilo tendo la
kufungishwa ndoa,yule binti akadondoka, na mara akaanza kuweweseka,na kusema
hataki kuolewa kwasababu yeye keshaolewa,…
.
‘Eti nini keshaolewa na nani…..’akaluliza mzazi mmojawapo.
‘Mumesikia wenyewe akisema, keshaolewa na hawezi kuolewa kwa
mara ya pili…..’akasema mume mtarajiwa.
NB: Leo nimechelewa kidogo kufika kijiweni, lakini nimeona siku isipite hivi hivi, tupate hicho kipnde kidogo,na nyie huku mkipata nafasi ya kutafakari na kama kuna
mwenye maoni au aliwahi kukutana na dhahama kama hiyo changia ili tuboroshe
hiki kisa…
WAZO LA LEO: Tujaribu kuwa karibu na watoto wetu, na kila
linalotokea kwa watoto, hasa wanapofikia umri wa udadisi, tuwe makini na kauli
zetu.
Na tukumbuke sasa ni dunia ya utandawazi, watoto wetu wanajua
mengi ambayo wewe kama mzazi huwezi amini kuwa wanaweza kuyajua, tuwe wadadisi wakuchnguza nyendo na mabdiliko ya watoto wetu, tusipende kuwaachia sana wafanyakazi wa nyumbani,…yote
hayo ni majukumu yetu kama wazazi, …tukumbuke kuwa samaki hukunja angali
mbichi.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
M3 bado tuko pamoja Mkuu nilipotea sana kutokana na majukumu na mihangaiko ya kimaisha niliacha hiki kisa kikiwa sehemu ya kumi 12 lakini nashukuru Mungu nimeweza kupitia kila ninapopata muda kwa ajili ya mwendelezo na nimefikia mpk hii sehemu ya Hitimisho yaani nimeshakuwa addicted na hii blog na ni vile napenda sana visa ambavyo vinasaidia changamoto ktk maisha yetu, nilipokuwa sina muda wa kuingia nilikuwa nakosa amani kabisa. M3 endelea kukaza buti ipo siku utafaidika na kazi ya mikono yako. Jioni Njema M3 na wadau wote.
Karibu tena Precious, hapa ni kwako,nilishaanza kuingiwa wasiwasi kuwa na wewe umekikimbia kijiwe. Tupo pamoja mpendwa,na ubarikiwe sana
Post a Comment