Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, May 4, 2012

Hujafa hujaumbika-31Ilipita muda nikiwa peke yangu, nikimsubiri huyo mke ambaye aliagiza nije nionane naye aliyedai kuwa ni mke wangu. Na kila muda ulivyopita ndivyo nilivyozidi kuwaza hili na lile, na kujaribu kumfikiria huyo mke ni nani, na kwanini aliagiza nije nionane naye…ndio kama ni mke wangu angelihitaji msaadawangu,lakini mke ninayemtambua ni Kimwana…ingawaje nilishampa talaka kirohoni.

Mara nikahisi dalili ya kuwemo mtu, lakini sikujua yupo upande gani, nikageuza uso kuangalia  huku na kule sikuona mtu,.... na mara baadaye mlangoni wa nje ukafunguka, na pale mlangoni akawa kasimama yule mwanadada wakili, ambaye ndio alikuwa kafika,toka huko alipokuwa, kwani aliponifikisha maeneo ya magereza aliniambi mimi nitangulie chumba cha wageni yeye ana mambo mengina anayafutailia humo gerezani
.
‘Mumeshaongea….?’ Lilikuwa swali lake la kwanza, nikashangaa,na kumwangalia kwa mshangao.

‘Yupo wapi mtu wa kuongea naye,….?’ Nikamuuliza, naye akageuka bila kusema kitu kurudi huko alipotoka, nikabakia nikiwa nimeduwaa.

Haikupita muda, mara nikasikia sauti ya mlango wa ndani, ambapo wafungwa wanatokea ukifunguliwa na akatokeza mlinzi mwanamke, na ilionekana dhahiri kuwa kuna mtu mwingine yupo naye, nikasema moyoni, huyo sasa anakuja,…nikatulia kumsubiri kwa haumu huyo mke wangu.

Mara akatokea mwanadada mmoja,….mmh, sio yeye, labda ni huyo wakwangu bado,….yule mwanadadamafungwa, akasogea hadi kati kati ya chumba, huku akiwa kanikazia macho mimi, alikuwa akiniangalia mimi bila kupepesa macho, alikuwa kabisa habandui macho yake kwangu. Nikashikwa na mshangao, maana simjui, sikumbuki kabisa kumuona,….kwa vile sikuwa namjua nikawa sina habari naye, nikageuza kichwa changu na  kuangalia mlangoni kama atatokezea mtu mwingine….

Mwanadada wakili alikuwa kasimama, akituangalia sisi, …niliona usoni mwake kumejaa tabasamu, nikamwangalia, halafu nikataka kusema kitu...,lakini nikasita, nikasubiri, na baadaye nikageuka kumwangali yule mfungwa mwanadada ambaye kwa muda ule alikuwa kakaa kwenye kiti huku kaweka mguu mmoja juu, na kuushikilia kwa mkono, bado akiwa kaduwaa, na macho yake bado yananiangalia mimi kwa woga,ulionekena dhahiri usoni.
.
Haraka nikageuza kichwa changu pembeni kumkwepa tusiangaliane, na baadaye nikamgeukia yule wakili mwanadada nikitaka kumuuliza huyo mke wangu aliyeniita yupo wapi,….na kabla sijamuulizia nikaona nimuangalie tena vizuri huyo mwanadada anayeniangalia kwa uwoga, labda namfahamu...
.
Nilipogeuka kwa mara ya pili  kumwagalia, macho yetu yalipokutana, mara, akaafunua mcho yake kama vile kaona kitu cha kuogofya, akazidi kuyafunua macho yake na hata niliona akifunua mdomo wake kutaka kupiga ukulele, nikabakia nimeduwaa, nilipoona hivyo, nikainuka….nikitaka kuondoka humo ndani, …

Kama ningelijua nisingelifanya hivyo, maana kilichotokea hapo ilikuwa ni maajabu.
Yule mwanadada mfungwa, alirudi kinyume nyuma, pale aliponiaona nimesimama, akageuka, na kuanza kutimua mbio, akawa anaelekea ulemlango wa kutokea nje, na bahati nzuri mlinzi hakuwa mbali akamkimbilia na kumdaka, kabla hajaishie huko nje, akaanza kumwida kwa hasira;

‘Wewe unakimbilia wapi, mbona sikuelewi,nini kinachokukimbiza, unataka kwenda wapi, huyo si ndio mgeni uliyeagiza aletwe kwako, mbona unaonyesha vituko hapa,….’akasema kwa ukali huku akimweka yule mwanadadachini ya ulinzi wake.

'Ndiyo yeye, lakini....'akasema huku anaonyeseha kidole kwangu,....akiwa hataki hata kuniangalia vyema, ananianglia kwa kujiiba huku kama anafunika uso wake, asinione.....

Yule wakili mwanadada, naye akiwa kashikwa na mshangao, akamsogelea yule mwanadada mfungwa na kumwangalia machoni, akamuashiria yule askari amuachie, na yule askari kwa mashaka akafanya hivyo, na baadaye akasogea pembeni, huku akiwa tayarii kuwajibika kama lolote litatokea.

‘Sikiliza dada yangu, huyo uliyemuona hapo ndio huyo uliyeagiza alatwe, au sio yeye….?’akamuuliza.

‘Ndio yeye, lakini kuna mtu mwingine nyuma yake, …..’akasema huku akigeuka kuniangalia kwa woga,na mimi nikageuka nyuma yangu kuangalia kuwa kweli kuna mtu nyuma yangu,...hata yule askari akawa ananiangalia na kuangalia kwa nyuma yangu,...huku akionyesha uso wa mshangao,  nahata huyo wakili mwanadada akafanya hivyo hivyo.

‘Hakuna mtu mwingine, hizo ni hisia zako, …yupo wapi huyo mtu mwingine mbona hatumuoni sisi,hebu tuonyeshe..?’ akasema huyo wakili mwanadada.

Yule mfungwa mwanadada,akanyosha mkono kuonyesha pale nilipokaa, nami nikageuka nyuma tena kuhakikisha, lakini sikuona mtu, nikawa nusu nimekaa, na nusu nataka kuinuka, lakini sikuweza hata kusogeza mguu, na yule mwanadada, alrudisha mkono wake haraka, kama vile kaogopa kuunyosha, au kaambiwa usifanye hivyo, akageuka na kuangalia mlangoni, alipokuwa kasimama yule askari.

‘Nikuulize tena, huyoo hapo ndiye mtu uliyetaka aje muongee naye au sio yeye,….?’ Akauliza yule wakili mwanadada.

‘Ndio yeye, lakini….kwanini nawaona wapo wawili…?’akasema  huku akionyesha kuchanganyikiwa, na baadaye akamwangalia yule wakili mwandada, akitaka kusema kitu, na yule wakili mwanadada akamshika yule mwanadada mfungwa mkono, na kumvuta kuja mbele yangu.Ilikuwa kazi kubwa, mpaka walipofika pale miliposimama, yule mwanadada mfungwa, alikuwa akitetemeka na hata kulowana jasho.

‘Niacheni, niacheni, nyie mnataka niuwawe hamuoni hayo majitu yanayotisha ...sasa…ooh, jamani nimekoma..nimekoma sirudii tena, nimekoma nimekoma,sitamfanyai lolote tena.…..’akasema huku anapiga ukulele.

Mimi niliona sasa imekuwa taabu, nikaona nitamke lolote,ilimradi mambo yaishe, nikasema kwa sauti ya upole,sijui ni kwasababu ya ile sauti, au ni ninii kilitokea, maana sauti yangu ilipotoka yule mwanadada mafungwa alishtuka na kutulia,akageuka kuniangalia alifanya hivyo kwa muda,halafu taratibu akanisogelea.

‘Mbona mimi nipo peke yangu hapa,…una nini wewe mwanadada…’ndivyo nilivyosema.

Yule mwanadada aliponikaribia,...ghafla akasimama, na kufanya kama alivyofanya mwanzoni, kwanza alitoa macho ya uwoga, halafu akapanua mdomo kamavile anataka kupiga ukulele, na hapo hapo akageuka kwa haraka sana, na kwa vile aligeuka kwa kasi bila kutegemewa kuwa atafanya hivyo, alimpiga kikumbo yule wakili mwanadada.Na yule wakili mwanadada kwavile hakutegemea hilo akajikuta akidondoka chini, na yule askari alikuwa keshajua mambo yameenda vyema, kwahiyo hakuwa kaangalia kwa makini upande wetu.

Yule mwanadada mfungwa alitoka mle ndani na kumpita yule askari kama upepo,na yule askari, alirukakutaka kumdaka, lakini alikuw akachelewa, mwenzako akatoka huyooo, mbio sijui huko nje itakwuaje. ….

Yule askari hakupoteza muda, akatoa filimbi yake nakuipuliza, kilikuwa kitendo cha sekunde chache wenzake walishafika an kupata maagizo kuwa yule mfungwa mwanadada katoroka wahakikishe kuwa hatoki getini, lakini walishachelewa,….

Yule mwadada mbio alizotoka nazo hapo, hakuna aliyeweza kumkamata, kwani hata askari wa getini ambao hawakuwa an mashaka, maana haijawahi kutokea wafungwa kutoroka,na muda kamahuo waliachia geti wazi kwa wageni kuingia,...yule aliyekuwa karibu na mlango, alishitukia tu huyo mwanadada akimpita kwa mwendo wa kasi, na hata alipojaribu kumzuia akajikuta akila mwereka.
.
‘Wewe mbona umeacha geti wazi,huoni huyo mfungwa kuwa anatoroka..’sauti ya ukali ikasema na mimi kwa wakati huo nilikuwa nafuatilia kwakaribu hayo matukio. Ilikuwa kama picha ya aina yake....

‘Mbona mimi sielewi ….!’ Nikasema kwa mshngao.

‘Hakuna anayejua, hatujui kuw ailikuwani mbinu yake,au kuna kitu kingine…lakini tutampata tu…..’akasemaaskari mmojawapo.

‘Aaah, sasa unaona kunileta huku ,matokeao yake ndio hayo,….’nikawa namlaumu yule wakili mwanadada.

‘Kwani sisi tumefanya makosa gani,yeye ndiye aliyeagiza kuwa uuitwe, na hakuniagiza mimi moja kwa moja, aliomba kupitia ngazi husika, na wao wakanipa ujumbe nikufikishie, wakijua nitakupata,haya yaliyotokea sasa hivi hakuna aliyetarajia….’akasema huyo wakili mwanadada.

‘Hata hivyo itabidi mukahojiwe , tunahitaji maelezo yenu,..huku tukiendelea na uchunguzi, atatafutwa na ataonekana, ...wapo watu wanamfuatilia kwa karibu, atakamatwa tu,hawezi kwenda mbali….’akasema huyo askari. Na tukakubali wito wake, na kuelekea huko sehemu ya mahojiano, nilishukuru kuwa nilikuwa na wakili ambaye alijua nini cha kuongea, na mimi sikuwa na kazi kubwa sana.

‘Hebu niambie wewe una nini katika maisha yako ambacho siocha kawaida, maana kwanza uliniambi kuwa ndugu yoyote anayekujua akikuona nakukimbia, na hilo sikuwa na uhakika nalo,mpakanilivyomuona huyo, na kwanini iwe kwa walewanaokujua tu….?’ Akaniuliza

‘Ni kweli,lakini huyu mwanadadambona mimi simjui..sikumbuki kabsa kumona kabla….’nikajitetea.

‘Yeye mbona ansema anakujau, na sio kukujua tu, anadai kuwa yeye ni mke wako,..’akasema wakili mwanadada. Na kamaulivyosikia alivyosema yule afande,kuwa aliomba kuwa akutane na mumewe,kabla hakijafanyika chochote, na wao kwa vile wanaheshimu mambo ya mke na mume,wakafanya hivyo, na walipoelezwa ni nani,na wapi unaweza kupatikana, …..’akasita hapo kidogo.

‘Wao ndio walijua wapi naweza kupatikana,au yeye ndiye aliwaelekeza….?’ Nikasuliza.

‘Hapo kuna kitu….kuna kitu natakiwa nikifanyie kazi, ….maana askari wanasema yeye ndiye aliyewaelekeza wapi unaweza kupatikana,ina maana huyo mwanadada anakujau vyema….hadi msiha yako….’akasemahuyo wakili mwanadada.

‘Atanijuaje na mimi simjui?’ nikauliza.

‘Hilo nitalifanyia kazi,nahisi kuna kitu kimejificha hapa, lakini ni kazi ndogo kuigundua, kwanza nikuulizie kuhusu maisha yako mengine huna mambo mengine ambayo yaliwahi kukutokea kabla, au kuhisiwa au kuambiwa, maana hayo yaliyotokea sidhani kuwa ni mpango, nahisi kweli yule mwanadada atakuwa anaona kitu,…. au anatokewa na kitu kinachomuonyesha hivyo…kinachomugofya…..’akasema huyo wakili mwanadada.

Aliposema hivyo, nikaumbuka maisha yangu ya utotoni wakati babu akiwa bado hai, nilikuwa nimesahau kabisa maisha yangu na babu, ….sikuwa nimeliwaza hilo kabla , na huenda haya yanayotokea kwasabaabu ya yale aliyonifanyai babu, lakini hata hivyo sikuamini hayo, ……………

**********

‘Mjukuu wangu, kama utakuwa hivi ,karibu na mimi nitakupa zawadi moja nzuri sana, zawadi ambayo hitolewi ovyo, maana nimekuependa sana, ….’akaniambia babu yangu tkusaidiana kupukuchua mahindi.

‘Zawadi gani babu,…?’ nikauliza nikifurahia, maana nilishamuambia babu anitafutie manati, kwa ajili yakuwindia ndege, na mimi hiyo ndiyo niliona kuwa ni zawadi nzuri kwangu,….’nikasema.

‘Wewe zawadi nzuri ni manati, …Hapanamimi siwezi kukupa manati, maana sipendi hiyo tabia ya kuwaua wadudu wadogo kama ndege, ….na hiyo zawadi nikikupa hutakiwi kuwaua ndege tena. Unanielewa kama hutaweza kufuata hayo masharti, nimpa mtu mwingine hiyo zawadina hautakuwa rafiki yangu tena…’akasema babu.

‘Mimi napenda zawadi ya manati,….nikiwapiga hawo ndege nawachukua kuwafuga, akiumia nitamtibia…’nikasema. Akanishika kichwa na kusema;

‘Mjukuu wangu, hiyo zawadi kama nilivyokuambia nikikupa, unatakiwa usiwaue ndege, au kuua wanyama wasio na hatia,ili hata ukiwa mkubwa, usije ukawaua watu, ukiua mtu na wewe utauliwa, …sasa hiyo dawa itakusaidia wewe watu wasikuzuru, na atakayejaribu kukufanyia ubaya, yatamkuta makubwa,unasikia…?.’akanimbia na mimi nikakubali maana nilikuwa mtoto a sikujua nini anachoniambia zaidi ya kuitikia tu.

Kila siku babau akawa ananimbi jambo hilo hilo, na wakati mwingine ananichukua matembezini kwenye shamba lake, na sehemu ambazo aliniambia ni sehemu anapoweka dawa au kutengeneza dawa zake.Babu yangu alikuwa mganga wa kienyeji. Na ukumbuke yote hayo yalitendeka kipindi nikiwa hata darasa la kwanza  sijaanza.

Nilipofika umri wa kuanza darasa la kwanza, siku moja, babu akanichukua tukasafiri naye mbali sana, huko alinimabi ndipo familia za mababu zetu zilipoanzaia, na hata akanionyesha mafuvu ya hawo mababu wa mababu. Na pale alianza kumwaga mwaag unga huku akiongea maneno ambayo sikuyajua,.. baadaye akakoka moto na kuweka chungu jikoni.

Katika moja ya yale mafuvu, alitoa unga mweupe, akauchukua na kuchanganya na mfuta ambayo alisema ni ya simba….akavichangaya vyote hivyo kwenye damu, aliyoichukua toka kwenye mbuzi aliyemchinja siku hiyo ,kabla hatujaanza safari ya kuja huku mashambani. Halafu alichukau wembe akanichanja mwilini na kunipaka huo mchanganyiko, .akanifukiza na na moshi uliotoka kwenye mjani ambayo aliyachoma na kutoa harufu kali…

Nakumbuka baada ya kufukizwa huo moshi wenye harufu kali, nilisikia kizunguzungu, na usingizi mzito ulinichukua, sikumbuki ilikuwaje maana nilipoamuka nilijikuta nipo nyumbani. Sikuweza kukumbuka nini kilitokea hata wazazi wangu sikuwahi kuwaambia, ….na hata nilipoanza kupata mambo ya ajabu ajabu, sikuwa nakumbuka mambo hayo aliyoniafanyia babu.

Nilianza kutokewa na mambo ya ajabu ajabu, kipindi babu ameshafariki, na sikumbuki kama abu aliwahi kumwambi baba kuwa alinifanyia hayo aliyoniafanyia,mimi mwenyewe sikuwahi kukumbuka hadi nilipofika ukubwani, ndipo nikakumbuka hilo tukio,…..na wala sikujua kuwa lina uahusiano wowote na hayo yaliyokuwa yakitokea.

Nakumbuka nikiwa mdogo kuna mambo mengi yalikua yakinitokea, kwa mfano niliweza kuwaona watu ambao watu wengine walikuwa hawawaoni, hasa kipindi cha usiku,…na watu wengine wakasema nina karamaya unajimu, lakini mimi nilikuwa sitaki kabisa  mambo hayo,na wakati mwingine nilikuwa kama napandisha hayo wanayoyaita mashetani, na hali hiyo iliwafanya wazazi wangu wahangaike kwa waganga na wataalamu mmoja alisema;

‘Mwanenu anatembea na wahenga wake,….na sisi hatuwezi kufanya lolote kuhusu hilo, na kama kuna mtu anatasema kuwa anaweza kufanya lolote kwakwe, anawadanganya.Kwanza wahenga wake, sio watu wabaya, wao kazi yaokubwa ni kumlinda huyu mwanenu. Na inafanyika hivyo kwasababu ni mteule katika ukoo wenu.,…

‘Sasa mbona anatokewa na mambo ya ajabu.. kama kuchanganyikiwa…..?’ akauliza baba.
‘Inatokea hivyo kwa sababu ni mara ya kwanza, lakini baadaye atawazoe, na hata kama hatawazoea ,hawo watu watakuwa karibu yake, na wabaya wake wanaweza wakawaona kama mijitu ya kutisha….’alisema huyo mtaalamu.

‘Kwahiyo mtoto wetu ataonekana kama mchawi…?’ akauliza mama.

‘Hapana ….mchawi ni mtu anayewangia watu na kuwazuru, lakini huyu atakuwa na hawo whenga kwa ajili ya kumlinda tu, …hawatakuwa na kazi nyingine kwake, na hawatamuingilia katika mambo yake,ila tu,sije akaua,…..’akasema huyo mtaalamu.

Wazee hawakukomea hapo, walihangaika we mpaka wakachoka,wakoona waniache na mambo yangu, na nikawa nimekuwa, ila kila aliyejaribu kunifanyia ubaya alikipata cha moto,…mimi sikuwa nafuatilia nini wanakipata, ila nilichokuwa nikiona nahawo watu kukimbia sana, na kwa vile sikufuatilia niliishia kucheka, kwasababu sikujua ni kwanini walikuwa wakifanya hivyo, au waliona nini kwangu. Baaaye nilianza kuna wasi wasi,maana kuna watu walianza kuninyoshea kidole.Baadaye yakawa kama yameisha,….

Huyo wakili mwanadada akaniangalia kwa muda na baadaye akaniuliza;

‘Je wewe kama ulivyodai walisema usimwage damu ya watu au wanyama wasio kuwa na hatia,ina maana haijawahi kutokea hivyo,kuwadhulumu watu,au kuwafanyia ubaya….kama hivyo ulivyokamatishwa na hilo kundi,huoni damu ya watu ilimwagika…?’ akaniuliza huyo mwanadada.

‘Sikuwahi kumwaga damu ya mtu, na kama ilitokea hvyo, sio kwamkono wangu,na mambo mengine nilijikuta nikiingizwa bila ya hisari yangu, kama ujuavyo,… na nahisi hawo watu walikuwa na niambaya kwangu ndio maana yametokea hayo yaliyotokea….;nikatulia na kukumbuka jambo.

‘Unajua Nimefikia hatua nakudhania kuwahuenda hata hawo watu ninaokutana nao halafu  wananikimbia,…inawezekana walikuwa na lengo baya kwangu au huenda walikuwa ni washirika wa watu wenye lengo baya kwangu, nafikiri itakuwa hivyo, ingawaje kwakweli sina uhakika na sihitaji kuwa na uhakika….’nikasema.

‘Kwahiyo unayaamini hayo ….kuwa kweli unayo mwilini mwako, na yanafanyika hivyo kwasababu ya mambo yaliyopo mwilini mwako…?’ akaniuliza huyo mwanadada,

‘Niamini nisimiani,…kwa sasa nitasemaje…hebu niambie kama wewe ungelikuwa katika nafasi yangu ungelisemaje, ….?’ Nikamwangalia kwa muda nay eye hakujibu kitu, akawana kanitizama tu mahoni.

‘Mimi sijui kuwa ni kweli au sio kweli,na wala sijali….ndivyo nilivyo siwezi kujidai kuwa labda najisifia au labda napendaiwe hivyo,…..hapana kabisa, na nimeyaongea haya kwasababu umeniuliza na kunisistizia kuwa nikuambie ukweli kwa ajili ya utafiti wako huo, …insingekuwa hivyo, nisingeliongea lolote, kuhusu hayo…’nikasema huku nikikunja uso kwa kuwaza mbali;

‘Ni kweli nitashukuru sana kama utakuwa mkweli kwangu na kuniambia kila jambo, …na ina maana hata baada ya mtukio yote hayo, nafsi yako haijaguswa na kitu, kuwa una jambo ambalo sio la kawaida…?’ akaniuliza na huku kidole chake kikiwa kimeshikilia kichwani karibu na jicho.

‘Sijawahi kufikiria hayo kwa undani, maana hayo ni mambo ya imani…na mimi sina imani nayo …ila kwa ujumla yanapotokea, ukaona watu wanavyobadilika,….inashangaza, na hata wakati mwingine nakuwa kama siamini, maana mimi sioni hivyo wanavyoviona kwangu….’nikasemana kutulia kwa muda.

‘Ina maana hayo yanayowatokea hawo watu wewe huyaoni, na hujawahi kuwaona watu wa ajabu ajabu ?’ akauliza na kuniangalai kwa mashaka.

‘Huwa ilikuwa ikitokea hivyo, hasa nilipokuwa kijijini, nawaona watu kamili, na wengine nawafahamu kabisa ni watu walio hai, lakini wamekuja kimazingara, ambayo watu wengine hawawezi kuwaona ,mimi nawaona kabisa kwa macho yangu,…..’ niaksema huku naonyeshea macho yangu kwa kidole.

‘Hayo yalitokea kipindi nikiwa mdogo, na sikumbuki kutoka hayo  nilipokuwa mkubwa, sikumbuki ….sin uhakika na kwa vile sifuatilii, naona kama hayo yalikuwa ya utotoni,..ila wakati mwingine ,huwa nahisi tu, kama kuna mtu yupo karibu, lakinii simuoni, au nahisi naambiwa jambo, labda nenda huku, usifanye hiki, lakini sioni mtu, au kitu cha kutisha….’nikatulia kidogo nikiwaza.

‘Unaju amwanzoni nilidhania kuwa hawo watu au sijui mizimu, wapo kwa ajili ya kukusaidia kwa kila hali, nilitaka nikuulize kuw a kwanini hawakusaidii atika hali ya kimaisha kama sasa hivi huna kazi,…..”akasema na kuangalai nje.

‘Hilo sijui, lakini kama sikose, yule mtaalamu alisema hawo, aliowaita wahenga, kazi yao ni kunilinda tu na mabaya,sio kunipatia utajiri…..hawahusiki, labda na wao wana mashsrti yao,mimi sijui….’nikasema.

‘Je hali kama hiyo haikusumbui, hujisikii vibaya kiafya au kujiona kuwa katika jamii unaonekana mtu waajabu, hujisikii lolote, …na uliwahi kusema kuwa kuna muda watu wa huko kijijini walifikia hatua ya kukunyoshea kidolena kwa hayo au ni kwasababu ya utundu wako mwingine…?’ akaniuliza.

‘Najiskia vibaya pale tukio linapotokea, lakini baadaye nazarau,na wakati mwingine napotezea tu kinamna, kwasababu siamini,…sijui kama unanielewa,…’nikasema na kutulia kwa muda,halafu nikasema tena;

‘Mimi sitilii maanani hayo matukio,…lakini kama binadamu lazima inipe mawazo fulani, hasa pale unapoona watu wananikimbia,….kwakweli hainipi raha,na kama kungelikuwa na njia ya kuliondoa hilo wazazi wangu wangeshafanikiwa kuliondoa, lakini kila walipokwenda waliambiwa hilo haliwezekani…..’nikawa nimetulia na kuwaza kwa muda, halafu nikasema ;

‘Unajua  hata mimi kama ningelikuwa najali au kuyaamini hayo ningelikuwa nimeshalifanyia kazi hilo,…lakini hayo siyaamini na wala sijapoteza muda wangu kuwazia hilo…huwezi amini hilo, lakini kama ungelifunua moyo wangu ungeligundua hilo, kuwa mini siamini kabisa mambo hayo ya nguvu za giza, ushirikina au…’nikasema.

***********

‘Hebu nikuulize swali kuhusu huyo mwadada tuliyemkuta huko gerezani, huna kumbukumbu yoyote kumuon mahali, maana hata askari wanatlia mashaka kuwa huenda unamfahau, lkini kwasababu ya kuogopa unajifanya humfahamu?’ akaniuliza.

‘Nikuambie ukweli, simfahamu,….siwezi kukuficha wewe…..na kwanini nifiche, hata mimi najaribu kuvuta kumbukumbu ,lakini haiji akilini, na kwanini aniite mimi mume wake, au alidanganya tu, au alikuwa na maana ya mtu mwingine nyinyi mkazania kuwa ni mimi….’ Nikasema.

‘Hilo la kukosea , …haipo, kiujumla alikutaja wewe kwa jina na kwa sifa, na kusema uliwahi kushikiliwa kwa muda mrefu kwa kesi hiyo uliyokuwa nayo….alitoa vielekezo vya maneno ambavyo kila mtu aliyesikia na anakufahamu angeubali kuwa wewe ni mke wake, lakini mke kwa vipi maana wake zako tunwajua..’akasema na kutulia kidogo.

‘Kwani Kimwana hamjajua yupo wapi,…?’ nikauliza.

‘Hajulikani kabisa alipo…kila kons ya nchi na kila mahali kunapojulikana kumetafutwa hajapatikana na wala hakuna anayejua habari zake…’akasemahuyo wakili mwanadada, na kuniangalia kwamuda halafua akniuliza;

‘Kwanini umemuulizia yeye kwa sasa?’ akanitimzama machoni.

‘Maana nilitaka kusema huenda huyo mwanadada wanajuana na huyo Kimwana na amemtumia au amejifanya kama yeye, ….kwahiyo pengine alishaambiwa mengi kuhusu mimi,na wakatumia hiyo mbinu ili nifike huko magereza,…’nikasema.

‘Ili iweje….?’ Akauliza.

‘Hapo sijui,labda ili apate mwanya wa kutoroka…labda ili niingie hatiani, maana itaonekana kuwa mimi nimeshiriki kumtorosha…nashukuru mlikuwepo hapo, kama msingelikuwepo, unafikiri ingelikuwaje…’nikasema na kutulia.

‘Hilo halina mantiki,kuna kitu…nitakigundua tu, ngoja nipate mudawakulifanyia kazi, lakini bado nina maswali ya kukuuliza,…’akatulia na kuwakama anawaza jambo.

‘Uliza tu,mimi na wewe tena…’nikasema na kumwangalia, nilimtizama kwa muda na hata akili ikawa inaanza kumfikiria yeye, na hata kutaka kuulizia kuhusu maisha yake na mume wake amabye simjui na wala hataki kuliongelea kwa sasa, nakaribu nimuulizie hilo swali, lakini yeye akaniwahi kwa swali jingine.

‘Sasa tutafanyeje,maana huyo mwanadada alikuwa mtu muhimu sana kwa huu utafiti wangu, na …na huenda tungeligundua jambo hapo,…na ikibid itabidi nitasafiri hadi huko Kenya, nataka kutafuta wapi huyo mke wako wa utotoni yupo,….’akasema na kuniangalia kwa makini.

‘Mimi sioni kamakuna umuhimu wowote, lakini ni vyema, kamautakuwa na uhakika wapi alipo,na mimi kama itakuwepo nauli tutaongozana….’nikasema.

‘Hiyo naweka kama akiba,..lakini huenda mambo yote yakaishia hapa hapa, ….cha muhimu ni wewe kutoa ushirikiano wa kuniambiakila kitu unachokijua kuhusu hawo waliowahi kuwa wake na zako, na kama utakutana nao, nipe taarifa haraka….’akasema .

‘Haina shida,kwangu mimi na wewe tena, haina shaka,….lakini fanya ufanyalo, ila naomba msinirudishe tena huko mageerzani..sitaki kufika huko gerezani,na kama inawezekana, nisingelipenda kuonana na huyo mwanadada,maana nahisi hana jema na mimi, ….sitaki kushirikiana na watu wa namna hiyo, mtu simjui, halafu anadai mimi mi mume wake,haiingii akilini…..’nikasema.

‘Haya tutayaangalia baadaye kwa kina,… maana dunia hii ina mambo, unaweza ukasema haiwezekani, ukaja kuona tofauti ikawezekana, usihukumu jambo kablahuajlithibitisha,….leo unaamuka hivi kesho vile, huwezi ona ajabu kamaulivuyosema hujafa hujaumbika….au sio?’ akasema huyo mwanadada na mwishoni akaniuliza kiujanja, huku anatabasamu.

‘Yaah, ni kweli hujafa hujaumbika maana matukio yanayoniandama hata mimi sikujua kuwa ninaweza kuwa hivi leo hii, ila ninachotaka kwa sasa ni kukwepa mambo ambayo yatanitia kwenye misuko suko, nimepata mafundisho….na ili kukwepa hayo ni kuwakwepa watu wenye nia mbaya, hasa Kimwana na huyo mwanadada, nitajaribu kuwakwepa kwa nguvu zote…’nikasema na yule mwanadada wakili akaniangali kwamakini nakusema;

‘Mimi katika maisha yangu , huwa sipendi kukata tamaa, na huwa napenda kudadisi mambo ya ajabu ajabu, ndio maana napenda kupekenyua undani wa matatizo ya kina mama, ukiyachunguza sana unapata hadithi za ajabu ajabu walizokumbana nazo. Na sasa hili lililotokea kwako,linanipa hamasa ya kulijua undani wake, nataka nilichunguze nigundue kuna nini kimejificha ndani yake,….na huenda ikawa na msaada mkubwa …hasa kwa aina mama, naomba tushirikiane…’akasema.

‘Mimi sipendi hayo….sipendi kuchunguza chunguza watu,naogopa sana kufanya hilo, ila nitakusaidia pale utakapohitaji msaada wangu, lakini nisichopenda ni huko kwenda magerezani,….kama uliwahi kuingizwa huko sizani kama utatamani tena itokee hivyo,labda wewe sio mtu kamili,…na naona ili niweze kuyashinda hayo majaribu,…naona ni vyema nisikutane na hawa watu wanaonikimbia….’nikasema.

‘Hakuna shida tutaangalia itakavyokuwa….’akasema huyo mwanadada wakili, na kuniacha niondoke kwenda kuhangaika, kwani alishaniahidi kuwa atanipatia kazi kwenye ofisi yake, lakini mwakani, …kwasasa nihangaike kivyangu….

NB. Je ni nini huyu mwanadada atakigundua…na kitanihusu nini mimi,na je kweli hiyo miiko ya kutokukutana na hawo wanadada au kwenda magereza  itafanikiwa,..tuzidi kuwemo hata kwa KIMIYA KIMIYA, HAINA SHIDA.

WAZO LA LEO:Katika maisha yetu tujaribu kukwepa dhana mbaya kwa wengine,…tusipende kuwadhani wengine kuwa wapo hivi au vile , kwa ubaya, ….hebu tujaribi kujenga dhanazilizo njema, ili tukwepe chuki, na uhasama, maana Ubaya hauna kwao.

Ni mimi: emu-three

2 comments :

Rachel siwa Isaac said...

Ndugu wa mimi upo juuuuu juuu zaidi,Mungu azidi kukufunulia, yaani zaidii.

Mmmmhh!! kweli ndugu yangu ubaya hauna kwao.

Pamoja Daima!!

emu-three said...

Ndugu wa mm kweli ubaya hauna neema na mwisho wake ni fedheha.
Nakushukuru sana kuwa nami wakati wote. Ubarikiwe sana