Ilipita muda nikiwa peke yangu, nikimsubiri huyo mke ambaye
aliagiza nije nionane naye aliyedai kuwa ni mke wangu. Na kila muda ulivyopita
ndivyo nilivyozidi kuwaza hili na lile, na kujaribu kumfikiria huyo mke ni
nani, na kwanini aliagiza nije nionane naye…ndio kama ni mke wangu angelihitaji
msaadawangu,lakini mke ninayemtambua ni Kimwana…ingawaje nilishampa talaka
kirohoni.
Mara nikahisi dalili ya kuwemo mtu, lakini sikujua yupo
upande gani, nikageuza uso kuangalia huku na kule sikuona mtu,.... na mara baadaye mlangoni
wa nje ukafunguka, na pale mlangoni akawa kasimama yule mwanadada wakili,
ambaye ndio alikuwa kafika,toka huko alipokuwa, kwani aliponifikisha maeneo ya
magereza aliniambi mimi nitangulie chumba cha wageni yeye ana mambo mengina
anayafutailia humo gerezani
.
‘Mumeshaongea….?’ Lilikuwa swali lake la kwanza,
nikashangaa,na kumwangalia kwa mshangao.
‘Yupo wapi mtu wa kuongea naye,….?’ Nikamuuliza, naye
akageuka bila kusema kitu kurudi huko alipotoka, nikabakia nikiwa nimeduwaa.
Haikupita muda, mara nikasikia sauti ya mlango wa ndani,
ambapo wafungwa wanatokea ukifunguliwa na akatokeza mlinzi mwanamke, na ilionekana dhahiri kuwa kuna
mtu mwingine yupo naye, nikasema moyoni, huyo sasa anakuja,…nikatulia
kumsubiri kwa haumu huyo mke wangu.
Mara akatokea mwanadada mmoja,….mmh, sio yeye, labda ni huyo
wakwangu bado,….yule mwanadadamafungwa, akasogea hadi kati kati ya chumba, huku
akiwa kanikazia macho mimi, alikuwa akiniangalia mimi bila kupepesa macho,
alikuwa kabisa habandui macho yake kwangu. Nikashikwa na mshangao, maana
simjui, sikumbuki kabisa kumuona,….kwa vile sikuwa namjua nikawa sina habari
naye, nikageuza kichwa changu na
kuangalia mlangoni kama atatokezea mtu mwingine….
Mwanadada wakili alikuwa kasimama, akituangalia sisi,
…niliona usoni mwake kumejaa tabasamu, nikamwangalia, halafu nikataka kusema
kitu...,lakini nikasita, nikasubiri, na baadaye nikageuka kumwangali yule mfungwa
mwanadada ambaye kwa muda ule alikuwa kakaa kwenye kiti huku kaweka mguu mmoja
juu, na kuushikilia kwa mkono, bado akiwa kaduwaa, na macho yake bado
yananiangalia mimi kwa woga,ulionekena dhahiri usoni.
.
Haraka nikageuza kichwa changu pembeni kumkwepa tusiangaliane, na baadaye nikamgeukia
yule wakili mwanadada nikitaka kumuuliza huyo mke wangu aliyeniita yupo wapi,….na
kabla sijamuulizia nikaona nimuangalie tena vizuri huyo mwanadada anayeniangalia kwa
uwoga, labda namfahamu...
.
Nilipogeuka kwa mara ya pili kumwagalia, macho yetu yalipokutana, mara,
akaafunua mcho yake kama vile kaona kitu cha kuogofya, akazidi kuyafunua macho
yake na hata niliona akifunua mdomo wake kutaka kupiga ukulele, nikabakia
nimeduwaa, nilipoona hivyo, nikainuka….nikitaka kuondoka humo ndani, …
Kama ningelijua
nisingelifanya hivyo, maana kilichotokea hapo ilikuwa ni maajabu.
Yule mwanadada mfungwa, alirudi kinyume nyuma, pale aliponiaona nimesimama, akageuka, na kuanza kutimua mbio, akawa anaelekea ulemlango wa kutokea nje, na bahati nzuri mlinzi hakuwa mbali akamkimbilia na kumdaka, kabla hajaishie huko nje, akaanza kumwida kwa hasira;
‘Wewe unakimbilia wapi, mbona sikuelewi,nini kinachokukimbiza, unataka kwenda wapi, huyo si ndio mgeni
uliyeagiza aletwe kwako, mbona unaonyesha vituko hapa,….’akasema kwa ukali huku
akimweka yule mwanadadachini ya ulinzi wake.
'Ndiyo yeye, lakini....'akasema huku anaonyeseha kidole kwangu,....akiwa hataki hata kuniangalia vyema, ananianglia kwa kujiiba huku kama anafunika uso wake, asinione.....
Yule wakili mwanadada, naye akiwa kashikwa na mshangao,
akamsogelea yule mwanadada mfungwa na kumwangalia machoni, akamuashiria yule
askari amuachie, na yule askari kwa mashaka akafanya hivyo, na baadaye akasogea
pembeni, huku akiwa tayarii kuwajibika kama lolote litatokea.
‘Sikiliza dada yangu, huyo uliyemuona hapo ndio huyo
uliyeagiza alatwe, au sio yeye….?’akamuuliza.
‘Ndio yeye, lakini kuna mtu mwingine nyuma yake,
…..’akasema huku akigeuka kuniangalia kwa woga,na mimi nikageuka nyuma yangu
kuangalia kuwa kweli kuna mtu nyuma yangu,...hata yule askari akawa ananiangalia na
kuangalia kwa nyuma yangu,...huku akionyesha uso wa mshangao, nahata huyo wakili mwanadada akafanya hivyo hivyo.
‘Hakuna mtu mwingine, hizo ni hisia zako, …yupo wapi huyo mtu
mwingine mbona hatumuoni sisi,hebu tuonyeshe..?’ akasema huyo wakili mwanadada.
Yule mfungwa mwanadada,akanyosha mkono kuonyesha pale
nilipokaa, nami nikageuka nyuma tena kuhakikisha, lakini sikuona mtu, nikawa
nusu nimekaa, na nusu nataka kuinuka, lakini sikuweza hata kusogeza mguu, na
yule mwanadada, alrudisha mkono wake haraka, kama vile kaogopa kuunyosha, au
kaambiwa usifanye hivyo, akageuka na kuangalia mlangoni, alipokuwa kasimama yule
askari.
‘Nikuulize tena, huyoo hapo ndiye mtu uliyetaka aje muongee
naye au sio yeye,….?’ Akauliza yule wakili mwanadada.
‘Ndio yeye, lakini….kwanini nawaona wapo
wawili…?’akasema huku akionyesha
kuchanganyikiwa, na baadaye akamwangalia yule wakili mwandada, akitaka kusema
kitu, na yule wakili mwanadada akamshika yule mwanadada mfungwa mkono, na
kumvuta kuja mbele yangu.Ilikuwa kazi kubwa, mpaka walipofika pale miliposimama, yule
mwanadada mfungwa, alikuwa akitetemeka na hata kulowana jasho.
‘Niacheni, niacheni, nyie mnataka niuwawe hamuoni hayo majitu yanayotisha ...sasa…ooh, jamani nimekoma..nimekoma sirudii tena, nimekoma nimekoma,sitamfanyai lolote tena.…..’akasema huku
anapiga ukulele.
Mimi niliona sasa imekuwa taabu, nikaona nitamke
lolote,ilimradi mambo yaishe, nikasema kwa sauti ya upole,sijui ni kwasababu ya
ile sauti, au ni ninii kilitokea, maana sauti yangu ilipotoka yule
mwanadada mafungwa alishtuka na kutulia,akageuka kuniangalia alifanya hivyo kwa muda,halafu
taratibu akanisogelea.
‘Mbona mimi nipo peke yangu hapa,…una nini wewe
mwanadada…’ndivyo nilivyosema.
Yule mwanadada aliponikaribia,...ghafla akasimama, na kufanya kama alivyofanya
mwanzoni, kwanza alitoa macho ya uwoga, halafu akapanua mdomo kamavile anataka kupiga
ukulele, na hapo hapo akageuka kwa haraka sana, na kwa vile aligeuka kwa kasi
bila kutegemewa kuwa atafanya hivyo, alimpiga kikumbo yule wakili mwanadada.Na yule wakili
mwanadada kwavile hakutegemea hilo akajikuta akidondoka chini, na yule askari
alikuwa keshajua mambo yameenda vyema, kwahiyo hakuwa kaangalia kwa makini upande wetu.
Yule mwanadada mfungwa alitoka mle ndani na kumpita yule
askari kama upepo,na yule askari, alirukakutaka kumdaka, lakini alikuw akachelewa, mwenzako akatoka huyooo, mbio sijui huko nje itakwuaje. ….
Yule askari hakupoteza muda, akatoa filimbi yake nakuipuliza, kilikuwa kitendo cha
sekunde chache wenzake walishafika an kupata maagizo kuwa yule mfungwa mwanadada
katoroka wahakikishe kuwa hatoki getini, lakini walishachelewa,….
Yule mwadada
mbio alizotoka nazo hapo, hakuna aliyeweza kumkamata, kwani hata askari wa
getini ambao hawakuwa an mashaka, maana haijawahi kutokea wafungwa kutoroka,na muda kamahuo waliachia geti wazi kwa wageni kuingia,...yule aliyekuwa karibu na mlango, alishitukia tu huyo mwanadada akimpita kwa mwendo wa kasi, na hata alipojaribu kumzuia akajikuta akila mwereka.
.
‘Wewe mbona umeacha geti wazi,huoni huyo mfungwa
kuwa anatoroka..’sauti ya ukali ikasema na mimi kwa wakati huo nilikuwa nafuatilia
kwakaribu hayo matukio. Ilikuwa kama picha ya aina yake....
‘Mbona mimi sielewi ….!’ Nikasema kwa mshngao.
‘Hakuna anayejua, hatujui kuw ailikuwani mbinu yake,au kuna
kitu kingine…lakini tutampata tu…..’akasemaaskari mmojawapo.
‘Aaah, sasa unaona kunileta huku ,matokeao yake ndio
hayo,….’nikawa namlaumu yule wakili mwanadada.
‘Kwani sisi tumefanya makosa gani,yeye ndiye aliyeagiza kuwa
uuitwe, na hakuniagiza mimi moja kwa moja, aliomba kupitia ngazi husika, na wao
wakanipa ujumbe nikufikishie, wakijua nitakupata,haya yaliyotokea sasa hivi hakuna
aliyetarajia….’akasema huyo wakili mwanadada.
‘Hata hivyo itabidi mukahojiwe , tunahitaji maelezo
yenu,..huku tukiendelea na uchunguzi, atatafutwa na ataonekana, ...wapo watu wanamfuatilia kwa karibu, atakamatwa tu,hawezi kwenda mbali….’akasema huyo
askari. Na tukakubali wito wake, na kuelekea huko sehemu ya mahojiano,
nilishukuru kuwa nilikuwa na wakili ambaye alijua nini cha kuongea, na mimi
sikuwa na kazi kubwa sana.
‘Hebu niambie wewe una nini katika maisha yako ambacho
siocha kawaida, maana kwanza uliniambi kuwa ndugu yoyote anayekujua akikuona
nakukimbia, na hilo sikuwa na uhakika nalo,mpakanilivyomuona huyo, na kwanini
iwe kwa walewanaokujua tu….?’ Akaniuliza
‘Ni kweli,lakini huyu mwanadadambona mimi simjui..sikumbuki
kabsa kumona kabla….’nikajitetea.
‘Yeye mbona ansema anakujau, na sio kukujua tu, anadai kuwa
yeye ni mke wako,..’akasema wakili mwanadada. Na kamaulivyosikia alivyosema
yule afande,kuwa aliomba kuwa akutane na mumewe,kabla hakijafanyika chochote,
na wao kwa vile wanaheshimu mambo ya mke na mume,wakafanya hivyo, na
walipoelezwa ni nani,na wapi unaweza kupatikana, …..’akasita hapo kidogo.
‘Wao ndio walijua wapi naweza kupatikana,au yeye ndiye
aliwaelekeza….?’ Nikasuliza.
‘Hapo kuna kitu….kuna kitu natakiwa nikifanyie kazi, ….maana
askari wanasema yeye ndiye aliyewaelekeza wapi unaweza kupatikana,ina maana
huyo mwanadada anakujau vyema….hadi msiha yako….’akasemahuyo wakili mwanadada.
‘Atanijuaje na mimi simjui?’ nikauliza.
‘Hilo nitalifanyia kazi,nahisi kuna kitu kimejificha hapa,
lakini ni kazi ndogo kuigundua, kwanza nikuulizie kuhusu maisha yako mengine
huna mambo mengine ambayo yaliwahi kukutokea kabla, au kuhisiwa au kuambiwa,
maana hayo yaliyotokea sidhani kuwa ni mpango, nahisi kweli yule mwanadada
atakuwa anaona kitu,…. au anatokewa na kitu kinachomuonyesha hivyo…kinachomugofya…..’akasema
huyo wakili mwanadada.
Aliposema hivyo, nikaumbuka maisha yangu ya utotoni wakati
babu akiwa bado hai, nilikuwa nimesahau kabisa maisha yangu na babu, ….sikuwa
nimeliwaza hilo kabla , na huenda haya yanayotokea kwasabaabu ya yale
aliyonifanyai babu, lakini hata hivyo sikuamini hayo, ……………
**********
‘Mjukuu wangu, kama utakuwa hivi ,karibu na mimi nitakupa
zawadi moja nzuri sana, zawadi ambayo hitolewi ovyo, maana nimekuependa sana,
….’akaniambia babu yangu tkusaidiana kupukuchua mahindi.
‘Zawadi gani babu,…?’ nikauliza nikifurahia, maana
nilishamuambia babu anitafutie manati, kwa ajili yakuwindia ndege, na mimi hiyo
ndiyo niliona kuwa ni zawadi nzuri kwangu,….’nikasema.
‘Wewe zawadi nzuri ni manati, …Hapanamimi siwezi kukupa
manati, maana sipendi hiyo tabia ya kuwaua wadudu wadogo kama ndege, ….na hiyo
zawadi nikikupa hutakiwi kuwaua ndege tena. Unanielewa kama hutaweza kufuata
hayo masharti, nimpa mtu mwingine hiyo zawadina hautakuwa rafiki yangu tena…’akasema
babu.
‘Mimi napenda zawadi ya manati,….nikiwapiga hawo ndege
nawachukua kuwafuga, akiumia nitamtibia…’nikasema. Akanishika kichwa na kusema;
‘Mjukuu wangu, hiyo zawadi kama nilivyokuambia nikikupa,
unatakiwa usiwaue ndege, au kuua wanyama wasio na hatia,ili hata ukiwa mkubwa,
usije ukawaua watu, ukiua mtu na wewe utauliwa, …sasa hiyo dawa itakusaidia
wewe watu wasikuzuru, na atakayejaribu kukufanyia ubaya, yatamkuta
makubwa,unasikia…?.’akanimbia na mimi nikakubali maana nilikuwa mtoto a sikujua
nini anachoniambia zaidi ya kuitikia tu.
Kila siku babau akawa ananimbi jambo hilo hilo, na wakati
mwingine ananichukua matembezini kwenye shamba lake, na sehemu ambazo
aliniambia ni sehemu anapoweka dawa au kutengeneza dawa zake.Babu yangu alikuwa
mganga wa kienyeji. Na ukumbuke yote hayo yalitendeka kipindi nikiwa hata
darasa la kwanza sijaanza.
Nilipofika umri wa kuanza darasa la kwanza, siku moja, babu
akanichukua tukasafiri naye mbali sana, huko alinimabi ndipo familia za mababu
zetu zilipoanzaia, na hata akanionyesha mafuvu ya hawo mababu wa mababu. Na
pale alianza kumwaga mwaag unga huku akiongea maneno ambayo sikuyajua,..
baadaye akakoka moto na kuweka chungu jikoni.
Katika moja ya yale mafuvu, alitoa unga mweupe, akauchukua
na kuchanganya na mfuta ambayo alisema ni ya simba….akavichangaya vyote hivyo
kwenye damu, aliyoichukua toka kwenye mbuzi aliyemchinja siku hiyo ,kabla
hatujaanza safari ya kuja huku mashambani. Halafu alichukau wembe akanichanja
mwilini na kunipaka huo mchanganyiko, .akanifukiza na na moshi uliotoka kwenye
mjani ambayo aliyachoma na kutoa harufu kali…
Nakumbuka baada ya kufukizwa huo moshi wenye harufu kali,
nilisikia kizunguzungu, na usingizi mzito ulinichukua, sikumbuki ilikuwaje
maana nilipoamuka nilijikuta nipo nyumbani. Sikuweza kukumbuka nini kilitokea
hata wazazi wangu sikuwahi kuwaambia, ….na hata nilipoanza kupata mambo ya
ajabu ajabu, sikuwa nakumbuka mambo hayo aliyoniafanyia babu.
Nilianza kutokewa na mambo ya ajabu ajabu, kipindi babu
ameshafariki, na sikumbuki kama abu aliwahi kumwambi baba kuwa alinifanyia hayo
aliyoniafanyia,mimi mwenyewe sikuwahi kukumbuka hadi nilipofika ukubwani, ndipo
nikakumbuka hilo tukio,…..na wala sikujua kuwa lina uahusiano wowote na hayo
yaliyokuwa yakitokea.
Nakumbuka nikiwa mdogo kuna mambo mengi yalikua yakinitokea,
kwa mfano niliweza kuwaona watu ambao watu wengine walikuwa hawawaoni, hasa
kipindi cha usiku,…na watu wengine wakasema nina karamaya unajimu, lakini mimi
nilikuwa sitaki kabisa mambo hayo,na
wakati mwingine nilikuwa kama napandisha hayo wanayoyaita mashetani, na hali
hiyo iliwafanya wazazi wangu wahangaike kwa waganga na wataalamu mmoja alisema;
‘Mwanenu anatembea na wahenga wake,….na sisi hatuwezi kufanya
lolote kuhusu hilo, na kama kuna mtu anatasema kuwa anaweza kufanya lolote
kwakwe, anawadanganya.Kwanza wahenga wake, sio watu wabaya, wao kazi yaokubwa
ni kumlinda huyu mwanenu. Na inafanyika hivyo kwasababu ni mteule katika ukoo
wenu.,…
‘Sasa mbona anatokewa na mambo ya ajabu.. kama
kuchanganyikiwa…..?’ akauliza baba.
‘Inatokea hivyo kwa sababu ni mara ya kwanza, lakini baadaye
atawazoe, na hata kama hatawazoea ,hawo watu watakuwa karibu yake, na wabaya
wake wanaweza wakawaona kama mijitu ya kutisha….’alisema huyo mtaalamu.
‘Kwahiyo mtoto wetu ataonekana kama mchawi…?’ akauliza mama.
‘Hapana ….mchawi ni mtu anayewangia watu na kuwazuru, lakini
huyu atakuwa na hawo whenga kwa ajili ya kumlinda tu, …hawatakuwa na kazi
nyingine kwake, na hawatamuingilia katika mambo yake,ila tu,sije
akaua,…..’akasema huyo mtaalamu.
Wazee hawakukomea hapo, walihangaika we mpaka
wakachoka,wakoona waniache na mambo yangu, na nikawa nimekuwa, ila kila aliyejaribu
kunifanyia ubaya alikipata cha moto,…mimi sikuwa nafuatilia nini wanakipata,
ila nilichokuwa nikiona nahawo watu kukimbia sana, na kwa vile sikufuatilia
niliishia kucheka, kwasababu sikujua ni kwanini walikuwa wakifanya hivyo, au
waliona nini kwangu. Baaaye nilianza kuna wasi wasi,maana kuna watu walianza
kuninyoshea kidole.Baadaye yakawa kama yameisha,….
Huyo wakili mwanadada akaniangalia kwa muda na baadaye
akaniuliza;
‘Je wewe kama ulivyodai walisema usimwage damu ya watu au
wanyama wasio kuwa na hatia,ina maana haijawahi kutokea hivyo,kuwadhulumu
watu,au kuwafanyia ubaya….kama hivyo ulivyokamatishwa na hilo kundi,huoni damu
ya watu ilimwagika…?’ akaniuliza huyo mwanadada.
‘Sikuwahi kumwaga damu ya mtu, na kama ilitokea hvyo, sio
kwamkono wangu,na mambo mengine nilijikuta nikiingizwa bila ya hisari yangu,
kama ujuavyo,… na nahisi hawo watu walikuwa na niambaya kwangu ndio maana
yametokea hayo yaliyotokea….;nikatulia na kukumbuka jambo.
‘Unajua Nimefikia hatua nakudhania kuwahuenda hata hawo watu
ninaokutana nao halafu wananikimbia,…inawezekana
walikuwa na lengo baya kwangu au huenda walikuwa ni washirika wa watu wenye
lengo baya kwangu, nafikiri itakuwa hivyo, ingawaje kwakweli sina uhakika na
sihitaji kuwa na uhakika….’nikasema.
‘Kwahiyo unayaamini hayo ….kuwa kweli unayo mwilini mwako, na
yanafanyika hivyo kwasababu ya mambo yaliyopo mwilini mwako…?’ akaniuliza huyo
mwanadada,
‘Niamini nisimiani,…kwa sasa nitasemaje…hebu niambie kama
wewe ungelikuwa katika nafasi yangu ungelisemaje, ….?’ Nikamwangalia kwa muda nay
eye hakujibu kitu, akawana kanitizama tu mahoni.
‘Mimi sijui kuwa ni kweli au sio kweli,na wala sijali….ndivyo
nilivyo siwezi kujidai kuwa labda najisifia au labda napendaiwe hivyo,…..hapana
kabisa, na nimeyaongea haya kwasababu umeniuliza na kunisistizia kuwa nikuambie
ukweli kwa ajili ya utafiti wako huo, …insingekuwa hivyo, nisingeliongea
lolote, kuhusu hayo…’nikasema huku nikikunja uso kwa kuwaza mbali;
‘Ni kweli nitashukuru sana kama utakuwa mkweli kwangu na
kuniambia kila jambo, …na ina maana hata baada ya mtukio yote hayo, nafsi yako
haijaguswa na kitu, kuwa una jambo ambalo sio la kawaida…?’ akaniuliza na huku
kidole chake kikiwa kimeshikilia kichwani karibu na jicho.
‘Sijawahi kufikiria hayo kwa undani, maana hayo ni mambo ya
imani…na mimi sina imani nayo …ila kwa ujumla yanapotokea, ukaona watu
wanavyobadilika,….inashangaza, na hata wakati mwingine nakuwa kama siamini, maana
mimi sioni hivyo wanavyoviona kwangu….’nikasemana kutulia kwa muda.
‘Ina maana hayo yanayowatokea hawo watu wewe huyaoni, na
hujawahi kuwaona watu wa ajabu ajabu ?’ akauliza na kuniangalai kwa mashaka.
‘Huwa ilikuwa ikitokea hivyo, hasa nilipokuwa kijijini,
nawaona watu kamili, na wengine nawafahamu kabisa ni watu walio hai, lakini
wamekuja kimazingara, ambayo watu wengine hawawezi kuwaona ,mimi nawaona kabisa
kwa macho yangu,…..’ niaksema huku naonyeshea macho yangu kwa kidole.
‘Hayo yalitokea kipindi nikiwa mdogo, na sikumbuki kutoka
hayo nilipokuwa mkubwa, sikumbuki ….sin
uhakika na kwa vile sifuatilii, naona kama hayo yalikuwa ya utotoni,..ila
wakati mwingine ,huwa nahisi tu, kama kuna mtu yupo karibu, lakinii simuoni, au
nahisi naambiwa jambo, labda nenda huku, usifanye hiki, lakini sioni mtu, au
kitu cha kutisha….’nikatulia kidogo nikiwaza.
‘Unaju amwanzoni nilidhania kuwa hawo watu au sijui mizimu,
wapo kwa ajili ya kukusaidia kwa kila hali, nilitaka nikuulize kuw a kwanini
hawakusaidii atika hali ya kimaisha kama sasa hivi huna kazi,…..”akasema na
kuangalai nje.
‘Hilo sijui, lakini kama sikose, yule mtaalamu alisema hawo,
aliowaita wahenga, kazi yao ni kunilinda tu na mabaya,sio kunipatia utajiri…..hawahusiki,
labda na wao wana mashsrti yao,mimi sijui….’nikasema.
‘Je hali kama hiyo haikusumbui, hujisikii vibaya kiafya au
kujiona kuwa katika jamii unaonekana mtu waajabu, hujisikii lolote, …na uliwahi
kusema kuwa kuna muda watu wa huko kijijini walifikia hatua ya kukunyoshea
kidolena kwa hayo au ni kwasababu ya utundu wako mwingine…?’ akaniuliza.
‘Najiskia vibaya pale tukio linapotokea, lakini baadaye nazarau,na
wakati mwingine napotezea tu kinamna, kwasababu siamini,…sijui kama unanielewa,…’nikasema
na kutulia kwa muda,halafu nikasema tena;
‘Mimi sitilii maanani hayo matukio,…lakini kama binadamu
lazima inipe mawazo fulani, hasa pale unapoona watu wananikimbia,….kwakweli hainipi
raha,na kama kungelikuwa na njia ya kuliondoa hilo wazazi wangu wangeshafanikiwa
kuliondoa, lakini kila walipokwenda waliambiwa hilo haliwezekani…..’nikawa
nimetulia na kuwaza kwa muda, halafu nikasema ;
‘Unajua hata mimi
kama ningelikuwa najali au kuyaamini hayo ningelikuwa nimeshalifanyia kazi hilo,…lakini
hayo siyaamini na wala sijapoteza muda wangu kuwazia hilo…huwezi amini hilo,
lakini kama ungelifunua moyo wangu ungeligundua hilo, kuwa mini siamini kabisa
mambo hayo ya nguvu za giza, ushirikina au…’nikasema.
***********
‘Hebu nikuulize swali kuhusu huyo mwadada tuliyemkuta huko
gerezani, huna kumbukumbu yoyote kumuon mahali, maana hata askari wanatlia
mashaka kuwa huenda unamfahau, lkini kwasababu ya kuogopa unajifanya humfahamu?’
akaniuliza.
‘Nikuambie ukweli, simfahamu,….siwezi kukuficha wewe…..na
kwanini nifiche, hata mimi najaribu kuvuta kumbukumbu ,lakini haiji akilini, na
kwanini aniite mimi mume wake, au alidanganya tu, au alikuwa na maana ya mtu
mwingine nyinyi mkazania kuwa ni mimi….’ Nikasema.
‘Hilo la kukosea , …haipo, kiujumla alikutaja wewe kwa jina
na kwa sifa, na kusema uliwahi kushikiliwa kwa muda mrefu kwa kesi hiyo
uliyokuwa nayo….alitoa vielekezo vya maneno ambavyo kila mtu aliyesikia na
anakufahamu angeubali kuwa wewe ni mke wake, lakini mke kwa vipi maana wake
zako tunwajua..’akasema na kutulia kidogo.
‘Kwani Kimwana hamjajua yupo wapi,…?’ nikauliza.
‘Hajulikani kabisa alipo…kila kons ya nchi na kila mahali
kunapojulikana kumetafutwa hajapatikana na wala hakuna anayejua habari zake…’akasemahuyo
wakili mwanadada, na kuniangalia kwamuda halafua akniuliza;
‘Kwanini umemuulizia yeye kwa sasa?’ akanitimzama machoni.
‘Maana nilitaka kusema huenda huyo mwanadada wanajuana na
huyo Kimwana na amemtumia au amejifanya kama yeye, ….kwahiyo pengine
alishaambiwa mengi kuhusu mimi,na wakatumia hiyo mbinu ili nifike huko
magereza,…’nikasema.
‘Ili iweje….?’ Akauliza.
‘Hapo sijui,labda ili apate mwanya wa kutoroka…labda ili
niingie hatiani, maana itaonekana kuwa mimi nimeshiriki kumtorosha…nashukuru
mlikuwepo hapo, kama msingelikuwepo, unafikiri ingelikuwaje…’nikasema na
kutulia.
‘Hilo halina mantiki,kuna kitu…nitakigundua tu, ngoja nipate
mudawakulifanyia kazi, lakini bado nina maswali ya kukuuliza,…’akatulia na
kuwakama anawaza jambo.
‘Uliza tu,mimi na wewe tena…’nikasema na kumwangalia,
nilimtizama kwa muda na hata akili ikawa inaanza kumfikiria yeye, na hata
kutaka kuulizia kuhusu maisha yake na mume wake amabye simjui na wala hataki
kuliongelea kwa sasa, nakaribu nimuulizie hilo swali, lakini yeye akaniwahi kwa
swali jingine.
‘Sasa tutafanyeje,maana huyo mwanadada alikuwa mtu muhimu
sana kwa huu utafiti wangu, na …na huenda tungeligundua jambo hapo,…na ikibid
itabidi nitasafiri hadi huko Kenya, nataka kutafuta wapi huyo mke wako wa
utotoni yupo,….’akasema na kuniangalia kwa makini.
‘Mimi sioni kamakuna umuhimu wowote, lakini ni vyema,
kamautakuwa na uhakika wapi alipo,na mimi kama itakuwepo nauli tutaongozana….’nikasema.
‘Hiyo naweka kama akiba,..lakini huenda mambo yote yakaishia
hapa hapa, ….cha muhimu ni wewe kutoa ushirikiano wa kuniambiakila kitu
unachokijua kuhusu hawo waliowahi kuwa wake na zako, na kama utakutana nao,
nipe taarifa haraka….’akasema .
‘Haina shida,kwangu mimi na wewe tena, haina shaka,….lakini fanya
ufanyalo, ila naomba msinirudishe tena huko mageerzani..sitaki kufika huko gerezani,na
kama inawezekana, nisingelipenda kuonana na huyo mwanadada,maana nahisi hana
jema na mimi, ….sitaki kushirikiana na watu wa namna hiyo, mtu simjui, halafu
anadai mimi mi mume wake,haiingii akilini…..’nikasema.
‘Haya tutayaangalia baadaye kwa kina,… maana dunia hii ina
mambo, unaweza ukasema haiwezekani, ukaja kuona tofauti ikawezekana, usihukumu
jambo kablahuajlithibitisha,….leo unaamuka hivi kesho vile, huwezi ona ajabu kamaulivuyosema
hujafa hujaumbika….au sio?’ akasema huyo mwanadada na mwishoni akaniuliza
kiujanja, huku anatabasamu.
‘Yaah, ni kweli hujafa hujaumbika maana matukio
yanayoniandama hata mimi sikujua kuwa ninaweza kuwa hivi leo hii, ila
ninachotaka kwa sasa ni kukwepa mambo ambayo yatanitia kwenye misuko suko,
nimepata mafundisho….na ili kukwepa hayo ni kuwakwepa watu wenye nia mbaya,
hasa Kimwana na huyo mwanadada, nitajaribu kuwakwepa kwa nguvu zote…’nikasema
na yule mwanadada wakili akaniangali kwamakini nakusema;
‘Mimi katika maisha yangu , huwa sipendi kukata tamaa, na
huwa napenda kudadisi mambo ya ajabu ajabu, ndio maana napenda kupekenyua
undani wa matatizo ya kina mama, ukiyachunguza sana unapata hadithi za ajabu
ajabu walizokumbana nazo. Na sasa hili lililotokea kwako,linanipa hamasa ya
kulijua undani wake, nataka nilichunguze nigundue kuna nini kimejificha ndani
yake,….na huenda ikawa na msaada mkubwa …hasa kwa aina mama, naomba
tushirikiane…’akasema.
‘Mimi sipendi hayo….sipendi kuchunguza chunguza watu,naogopa
sana kufanya hilo, ila nitakusaidia pale utakapohitaji msaada wangu, lakini nisichopenda
ni huko kwenda magerezani,….kama uliwahi kuingizwa huko sizani kama utatamani
tena itokee hivyo,labda wewe sio mtu kamili,…na naona ili niweze kuyashinda
hayo majaribu,…naona ni vyema nisikutane na hawa watu wanaonikimbia….’nikasema.
‘Hakuna shida tutaangalia itakavyokuwa….’akasema huyo
mwanadada wakili, na kuniacha niondoke kwenda kuhangaika, kwani alishaniahidi
kuwa atanipatia kazi kwenye ofisi yake, lakini mwakani, …kwasasa nihangaike
kivyangu….
NB. Je ni nini huyu mwanadada atakigundua…na kitanihusu nini
mimi,na je kweli hiyo miiko ya kutokukutana na hawo wanadada au kwenda magereza
itafanikiwa,..tuzidi kuwemo hata kwa
KIMIYA KIMIYA, HAINA SHIDA.
WAZO LA LEO:Katika maisha yetu tujaribu kukwepa dhana mbaya
kwa wengine,…tusipende kuwadhani wengine kuwa wapo hivi au vile , kwa ubaya, ….hebu
tujaribi kujenga dhanazilizo njema, ili tukwepe chuki, na uhasama, maana Ubaya
hauna kwao.
Ni mimi:
emu-three
2 comments :
Ndugu wa mimi upo juuuuu juuu zaidi,Mungu azidi kukufunulia, yaani zaidii.
Mmmmhh!! kweli ndugu yangu ubaya hauna kwao.
Pamoja Daima!!
Ndugu wa mm kweli ubaya hauna neema na mwisho wake ni fedheha.
Nakushukuru sana kuwa nami wakati wote. Ubarikiwe sana
Post a Comment