Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeThursday, December 23, 2010

Aisifuye mvua imemnyea-16

Akajiwekaa vizuri na kujiangalia kwenye kiyooo kabla hajatoka nje. Na huko nje akasikia kama watu wanongea na kukaribisha, akajua ndio huyo kaja, na kichwani alishajua nini cha kumjibu docta wa Sinza ni jibu safi kuwa kakubali haina shaka, …


   *****Je ilikuwa hivyo na iliendeleaje, hebu tuumuike kwenye muendelezo huu wa kisa hiki********

                                                         ************

Docta wa Sinza alikasirika kuona foleni haziishi , muda aliokuwa amekadiria kuwa atafika nyumbani kwake ajiandae vyema, ndipo ampitie Maua umeshapita, akaangalia saa yake na kuona kachelewa, ikabidi atafute njia za mikato, na alipofika mbele akakumbana na `trafic’ . Yule askari akamsimamisha na kuanza majibishano naye, mwishoni yule askari akatumia rungu ladola kuwa kuwa kwa usalama wake arudi nyuma hadi pale ulipoingilia , la sivyo atampeleka kituoni kwa kukatisha njia zisizoruhusiwa.

Docta akaona asiumbuke, akarudi nyuma hadi pale alipoingilia na kuanza moja, na hili likamzidishia kachelewa zaidi. Foleni ilipoisha akaendesha gari kwa haraka na mwishowe akaingia Sinza, na hakutaka kupitia kwake tena akaona aende moja kwa moja nyumbani kwa akina Mua. Alijiangalia alivyovaa, akasema haina shaka, cha muhimu ni maongezi . Akajaribu kumkumbuka maua alivyomchekea pale alipomwambia swala la harusi ya haraka.

‘Yule keshakubali, swala ni kuhakikisha hadanganyiki na mtu mwingine yoyote, mke ni wangu yule…sijui nitafurahi namna gani siku nikifunga ndoa na Maua, …’ akasema mwenyewe huku atatabasamu.

Wazo la kuwa rafiki yake anamipango kama hiyo halikuwepo akilini, yeye alichukulia kuwa rafiki yake alikuwa akimsaidia Maua kama Huruma, na kama alikuwa na mapenzi nay eye hayakuwa ya undani kama anavyohisi yeye.

‘Yule anachagua sana, na anapenda wasomi, hawezi kumchukua Maua, na kama alikuwa na lengo hilo keshachelewa yeye na alie tu, na amsubiri Rozi amalize shule …Rozi ni saizi yake kabisa, sio Maua, Maua ni chaguo langu…’ akapiga mruzi kuimba wimbo anaoujuamwenyewe wa kimapenzi.

Akaongeza mwendo na kufika barabara ya kukatisha kuingia nyumba anapokaa Maua, alipofika kwenye geti akaona gari kwa ndani limesimama. Kiroho kikamdunda, ni nani yule. Alifunguliwa mlango wa geti na kuingiza gari lake, akashuka haraka haraka huku analikagua lile gari, akagundua kuwa ni gari la rafiki yake, docta mwenzake.

‘Duuh, jamaa hajakata tamaa, ina maana kaja kumchukua Maua haiwezekani..’ akajikuta anaongea kwa sauti bila kujua kuwa yule kijana ambaye huhudumia pale mara kwa mara kamsikia. Yule kijana hakusema kitu akacheka tu.

Docta wangu alifika mapema, licha ya foleni za hapa na pale na alipofika alikutana na wazee wa pale akawaeleza nini kilichomsibu, na wao wakaelewa na kumpa pole ya majukumu, na wakawa wanaongea mambo mbali mbali ya kitaalamu na muda ukawa unakwenda. Docta alijua huenda Maua yupo jikoni anaandaa vyakula ndio maana hajaonekana akawa anatizama huku na kule bila hata dalili ya Maua, na kila akitaka kuulizia anajikuta anaulizwa maswali mengine ambayo anashindwa kuyakatiza kiheshima na inabidi awajibu na kutoa ufafanuzi wa hapa na pale.

Na wakati wanaongea mara wakasikia gari likipiga honi nje. Wazee wale wakabaki mdomo wazi, na kumwangalia Docta wangu kuwa amekuja kwa lipi, kwani Docta mwenzake kaja kumchukua Maua kwa chakula cha mchana na Docta huyu huenda ndio kaja kuondoka na Maua sasa kunaweza kukaleta kutokuelewana kati ya hawa madakitari.

‘Hivi Maua yupo wapi kwani mimi nataka ikiwezekana tuondoke naye sasa hivi, kwani nafasi ile nimepewa leo tu, kesho kama hakuonekana basi nafasi inachukuliwa na mtu mwingine. Na kazi zetuu kama unavyozijua unaweza ukajiandaa kwa hili mara simu hiyoo kuna dharaura, sasa nikiwa naye kule nii rahisi hata kama kkuna dharura nitampitisha na kumuacha huko akiendelea na mengine huku nawahi hospitalini.

‘Sawa ngoja tumuite, ile alikuwa kaalikwa na Docta wa Sinza kwa chakula cha mchana, sasa sijui haitaleta mgongano hapa, na nafikiri ndiye huyo kaja nje, …’ na kabla hajamaliza mlango ukagongwa.

Maua ndani hakujua nini kinaendela alikuwa kwenye kioo akijitizama, akiwa na ndoto ya kufanyika kwa harusikubwa, na atapambwa na kuvaa gauni zuri la harusi. Akawaza maisha atakayoishi na huyo dakitari, kuwa yatakuwa mazuri, kwani dakitari mwenyewe ana pesa, ana hospitali yake, na ana nyumba yake anamalizia. Hakuwahikuiona, lakini Rozi alifika na kuiona, anasema ni nyumba kubwa nzuri ya kisasa. Kwahiyo haoni ni kwanini aiachie hiyo bahati. Akakumbuka nyumba ya Docta wangu, ni nzuri lakini ina vituko.

Akakumbuka yale yaliyomtokea kule , akasema hayatamkuta tena, kwani hategemei kufika huko, wakae na maruerue yao. Lakini hapo akamkumbuka Docta wake, akajiskia kumkosa na hali na akatamani amuone tena, alitabasamu na kufikiria kuwa angekuwa yeye ndiye kamchumbia ingekuwa vyema, sana.

‘Docta wangu nampenda sana, lakini naona yeye labda hanipendi, ananionea Huruma tu kwa vile nimepitia maisha magumu. Kama kweli ananipenda muda wote tulioishi naye sikuwahi kumsikia akisema hivyo. Naona yule anampenda Rozi zaidi, kila mara wanawasiliana naye kwenye simui, nafikiri anapenda wasomi, ndio maana mara nyingi ananisisitizia kusoma..’ akasema kwa sauti ndogo, akijisikia uchungu kwanini hakuwahi kusoma kama Rozi.

‘Kama ningelisoma kama Rozi najua Docta wangu angenichagua mimi, naihisi kama nampenda zaidi ya Docta wa Sinza, lakini mmmh kwani kupenda ndio nini, mimi nahisi kama wote kwangu sawa, akinioa huyu au yule ilimradi tu muishi kwa amani…mmh, lakini Docta wangu jamani namuwaza sana…nampenda. ..’ akajikagua tena nguo aliyovaa

Na alipoona yupo tayari akachukua kimkoba chake na kuelekea nje, alipokuwa anafungua mlango akasikia honi nyingine ikipigwa nje, akashituka, akasema au ndio Docta wangu anakuja sasa hivi. Mungu wangu sasa kama ni yeye, nifanyeje. Akarudi nyuma na kuelekea kitandani akakaa kwanza kuwaza. Kama watafika wote na inabidi aamue ataamua kwenda kwa nani? Hapana haitawezekana kuwa hivyo…ninaweza kukosa kote, ngoa nisubiri kidogo…siwezi kuiachia harusi hivihivi…!

Huku chumba cha maongezi mambo yalikuwa yakipamba moto. Docya wa Sinza akaingia na kukaribishwa na baada ya kuwasalimia wazazi akamgeukia Docta mwenzako huku akionyesha mshanga wa kumkuta pale…

‘Halloh, Docta upo huku, mbona hukunijulisha kuwa utatutembelea, …’ akasema Docta wa Sinza, akisalimiana na Docta mwenzake, halafu akawaangalia wazee kusikia nini kinaendeela. Wazee wakaitazamana wasijue nini waseme. Na hapo Docta wangu akaona inabidi afanya jambo la maana vinginevyo, kunaweza kuzuka kutokuelewana kati yake na rafiki yake, pia wazee wa watu wanweza kujisikia vibaya.

‘Ndio rafiki yangu, nimesikia kuwa kuna mualiko wa chakula cha mchana, mimi naona tutatoka pamoja mimi na wewe na Maua, lakini awe amjiandaa kabisa, ili akitoka huko kwenye chakula cha mchana tuondoke pamoja, hana haja ya kurudi tena hapa nyumbani kwani kama unavyojua kazi, unaweza ukaamuka asubuhi ukakutana na miito ya dharura, na hata hivyo, shule niliyomsajili muda wake wa mwisho ni kesho tu, na kila kitu kipo tayari kasoro sahihi yake na baadhi ya maelezo yake, na …’

‘Kwani ni lazima asome hicho chuo au sijui shule, kama kuna matatizo mimi nitamtafutia chuo kingine, hilo lisikutie shaka rafiki yangu, vyuo au shule siku hizi zipo nyingi kwanini ung’ang’anie chuo kimoja chenye masharti mengi …’ akasema Docta wa Sinza huku anaangalia saa yake.

Docta wangu akaona sasa kunakoelekea ni kuzozana kusiko na faida, akawageukiwa wazazi na kuwauliza mawazo yao, kuwa wanaonaje, kwani yeye mawazo yake yalikuwa hayo. Na wao wakaangalina kila mmoja akimtegea mwenzake aongee, lakini mwishowe baba mwenye nyumba akasema haya;

‘Mimi naona mtihani huo tumuachie Maua mwenyewe aamue, kwani sisi kote hatuna wasiwasi nako, lakinii hata mimi naona hilo wazo ni jema, Maua ajiandae achukue vitu kabisa akitoka huko mfuatane, na kwa vile mwenzako alishafanya juhudi za muda mrefu naona tusimvunje nguvu…ngoja tumuite Maua aamue mwenyewe, kwani yeye ndiye mlengwa.’ Baba mwenye nyumba akamuangalia mkewe kama ana nyongeza, na mkewe akkasema kweli hilo ni wazo zuri, kwasababu elimu ina umuhimu sana.

Docta wa Sinza akataka kuweka pingamizi, lakini akaona hapo ni kama ukweni inatakiwa kuonyesha heshima akakaa kimya na kutingisha kichwa kuwa anakubaliana na mawazo yao ingawaje kindani alikuwa hataki kuweka kipengele kinachoweza kumpa nafasi Maua kukwepa maongezi hayo. Na akataka kumsikiliza mama mwenye nyumba naye anataka kusema nini..

‘Kwani chakula hicho nichakawaida tu, au kuna sherehe au mualiko, maana kama ni mualiko na kadi zimetolewa tunaweza kusema vinginevyo, lakini kama ni chakula cha kawaida kama ufanyavyo kila siku , basi siku nyingine sio mbaya. Lakini ngoja tumuite Maua ataamua mwenyewe..’ akasema mama mwenye nyumba.

Je maua ataamua nini, ni itakuwaje, naomba tuendelee kuwemo kwenye kisa chetu hiki:

Ni mimi: emu-three

Enhanced by Zemanta

5 comments :

Anonymous said...

Mbona picha mmmh, katoka bomba kweli, kaazima vitu vya Rozi nini, mwenyewe akija si-atamtoa nduki...!
Nimeipenda sana sehemu hii, kwani Madocta walionyesha usomi wao, ingawaje kwenye swala la kimapenzi hutaamini hasa mkuu wa nchi anaweza akafsnya sivyo ndivyo...ni hayo tu. Ahsante twasubiri maamuzi ya huyo Maua!

Pamela said...

ooooosh!! najickia kuumia hata cjui wahucka ilikuwa vp nafcni mwao...nasubiri muendelezo.

Anonymous said...

Mmmmm! Sasa kazi kwake Maua, sijui itakuaje? Lakini huyu Dr. wa Sinza anaonekana kama ana tamaa vile, na hekima yake si nzuri. Ila Dr wake kama aitavyo mwenyewe anaonekana yupo juu, lakini je, Maua atamuelewa nia ya Dr. wake?

Haya twasubiri.

BN

Pamela said...

Mama mwenye nyumba kanifurahisha saaaana kama lunch hata cku nyingine ataenda kwani ile ilikuwa lunch gani?? Maua alipata walezi wazuri sana asante m3 tujifunze na hilo pia kama walezi tuwalinde watt wetu...

Candy1 said...

Maua Maua!!! usije ukasinyaa Maua!!! Angalia kwa makini Mauaaaaaaaaaa.....hahaha...nipo tu M3...