Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Friday, December 24, 2010

wakati ni mali, lakini...


 ‘Bwana wewe nikuambie siri moja ya maisha,…’Mzee mmoja alikuwa kaka karibu nami kwenye daladala kaniambia, tulikuwa tumekaa wote kwenye daladala na muda huo nilikuwa nimechoka, sikupenda kusumbuliwa, hamu yangu ilikuwa kupata usingizi kidogo, kwasababu najua nina zaidi ya masaa mawili ndani ya daladala hadi kufika kwangu, siunajua tena foleni.


Nikamwangalia yule mzee, alikuwa kaniangalia kuonyesha kuwa ana jambo muhimu nikaona nimsikilize na kumwambia , `Niambie mzee, huenda likanisaidia katika maisha yangu…’

‘Katika mipangilioa yako ya maisha , fanya juhudi pangilia mambo yako, fanya kazi kwa bidii na ipende dunia kama vile utaishi milele..siunaniona mimi hapa nimezeeka nina miaka sitini, lakini najihisi kama nina miaka mingine sitini mbele, sijipweteki, na kusema aah, mimi mzee basi tena, nasubiri cha kupewa, nani atakupa hivihivi dunia hii. Najitosa hivyohivyo kama vile nitaishi milele, ingawaje kwa kweli naukumbuka sana, na kuujutia ujana wangu…’ akaniangalia kwa macho makali. Akaongezea kusema `wakati ni mali, lakini wakati ni ukuta, unahitaji mipangilio…’ akatikisa kichwa na kuendelea kusema;

`Pili muabudu sana mungu wako kama vile utakufa leo, au hata sasa hivi, huwezi jua, hapa gari linaweza likadondoka, tukawa wote marehemu au nikafa mimi peke yangu, au hata bila kudondoka gari unaweza ukakauka ghafla, na ukafa. Sasa ni bora umwabudu aliye na mamlaka na hiyo roho yako kwasababu hujui muda gani ataichukua roho hiyo. Omba, muabudu mola wako kama vile hapo unapoomba ni sekunde au dakika yako ya mwisho…’ akainama chini na nilijua anamuomba mola wake!

Nilijiukuta nimelala na nilipoamuka yule mzee akawa hayupo, ina maana aliteremka kituo nyuma wakati mimi nimelala, nilijuta sana, kwani alionekana ana busara na mengi yakunieleza, lakini nimechelewa keshaondoka.

Mzee huyu namfananisha na mwaka huu, unayoyoma, ni muda mchache umebakia tutauita jina jingine, mwaka jana au sio , na tutaukaribisha mwaka mpya. Mwaka huu tulikuwa nao na tulikuwa na mengi ya kufanya, na sijui mangapi tulifanikiwa kuyafanya na mangapi hatukufanikiwa, sidhani wengi wetu tuna kawaida ya kuweka kumbukumbu hizo, sidhani. Kumbukumbu hizo tunaziona kwenye bajeti za serikali, bajetiza makazini, lakini sio bajeti ya mtu mmoja mmoja.

Mwaka huu tupo nao kwenye kiti una mengi ya kutuambia, lakini tunajifanya tumechoka, tunajifanya tupo busy…labda tungelitulia tukatafakari na kuwa nao bega kwa bega k wa mipango, huenda tungelifanikiw sana. Tumekuwa tukikimbizana na hili na lile na huenda hayo tunayokimbizana nayo haya maana, tunapoteza muda mwingi kwenye vilevi, kucheza bao, kuongea na kufanya mambo ambayo ukiangalia ni ya kupotezea muda, muda uishe ulale, siku ipite. Ndio siku inapita, umri unakwisha na mwaka huo unakwisha, tukiamuka tutaukuta haupo tena!

Tukiangalia katika maisha yapo mambo mengi yanaharibu miili yetu hasa vyakula, vinywaji, vipodozi, hasira zisizo na msingi na mambo kadha wa kadha ambayo unayaona mazuri kwa umri wa miaka hadi telathini ujanani yaani, lakini ukifikia zaidi ya umri huo, hayo hayo uliyokuwa ukiyaona mazuri yanageuka kuwa sumu mwilini mwako. Mfano vyakula vya mafuta, pombe, starehe , madawa, vipodozi na mambo anuai, ni mazuri, yanastarehesha katika umri wa ujanani, lakini ikifikia uzeeni hayo matamu yanageuka kuwa machungu, yanakuwa sumu. Tunajikuta tunaamndamwa na presha, kisukari, ugonjwa wa moyo, vidonda vya tumbo nk, kwasababu ya yale matamu tuliyokuwa tukiyafadi ujanani. Kosa hatukua na mipangilio, hatukuali kusoma na kujifunza uzuri na ubaya wa hilo unalilofanya au kula!

Sasa wakati umefika kabla mwaka haujaisha kaa na huu mwaka kabla haujaisha, kumbuka yale ya muhimu, panga matarajio ukiwa na malengo kuwa utaishi milele. Na mipango hiyo haiwezi kuja kichwani tu, chukua karatasi pata muda, hata ikibidi soma, tafuta , uliza, kaa na mkeo au mumeo, angalieni matarajio, majukumu na mambo mbali mbali ya kimaisha yapangeni vyema na jinsi gani ya kuyatatua matatizo, jinsi gani ya kupata kipato, jinsi gani ya kusaidiana na hata kama huna kitu lakini kwa kujua nini kifanyike na kipi cha muhimu kwanza inasaidia, kuliko kulala, au kunywa pombe, au kusubiri mwisho wa siku ukaanza kupiga mayowe , kurusha mawe kwenye mabati eti unashagilia mwaka umekwisha, lakini umekwishaje? Ulikuwa nawo kweli wewe au ulikuwa umelala…!

Mkumbuke mola wako, kwani imani ni kitu muhimu sana, mola wako ndiye mwenye mamlaka na mwili wako, wangapi ulikuwa nawo siku za karibuni au mwaka huu sasa hawapo, je ina maana wao walikuwa na makosa na wewe uliyebakia huna makosa. Kumbuka wangapi wapo mahospitalini wagonjwa, wengine hawana viungo, wengine wanaomba mola awachukue kwa mateso wanayopata ya kansa au mengineyo, je wao walikuwa wanjua haya, je wao walimkosea Mungu ndio maana wanapata mateso haya, na wewe ni mbora zaidi yao ndio maana leo upo mzima. Hapana, wao hawajakosa, na wala wewe sio mbora sana mbora zaidi ni yule mcha mungu, ni yule anayemuomba mungu kuwa sala yangu hii huenda ikawa ya mwisho kuwa mzima, kuwa hai…nahivyo Sali kama vile hutaiona sekunde inayofuata.

Huu ni ujumbe wangu wa Ijumaa ya leo!

Ni mimi: emu-three

5 comments :

Anonymous said...

Hapo umenena mkuu, umenikumbusha kitu cha maana sana. Silali, mimi nitamsikiliza huyu mzee(mwaka) Nataka nijitahisi niwe nao sambamba, ikifika mwishoni, nishajua yapi yakufanya yapi yakuacha,...na mbioni nitatajia kuoa, na namtaka mke wangu alielewe hili, kuishi kwa mipangilia, na kumuabudu sana mungu.
Bwana M3, NAKUPA MKONO WA PONGEZI, UMENIPA KITU MUHIMU SANA,NA UMEIGUSA SANA IMANI YANGU...NAKUSHUKURU SANA

Simon Kitururu said...

Ijumaa njema Mkuu!

Na ujumbe umenigusa sana miye huu!

Sijui niache pombe leo?:-(

Anonymous said...

KWA KWELI UJUMBE HUU MKUU NI WA MUHIMU SANA KTK MAISHA YETU YA SASA. YAANII SINA HATA LA KUSEMA,NI UJUMBE MZURI SANA. SIJUI NIKUITE 'MZEE WA BUSARA' KWANI JUMBE ZAKO NI ZA MUHIMU SANA KTK MAISHA YETU YA SASA.

NAMI SILALI NG'O MPAKA KIELEWEKE. NAMSIKILIZA KWA MAKINI HUYU MZEE MPAKA MWISHO NIPATE BARAKA ZAKE.

MUNGU AKUBARIKI SANA NA JUMBE UNAZOPUPA WADAU. KWA KWELI ZINATUFUNDISHA KITU AU VITU FULANI NA PIA ZINATUELIMISHA, KUTUFUNDISHA NA HATA KUTUKUMBUSHA MAMBO FULANIFULANI, KAMA VILE KUMCHA MUNGU WETU. UMEBARIKIWE, AHSANTE MKUU. 'BIG UP'

NATAMANI WATU WOTE WANGEUSOMA HUU UJUMBE WAKO, LABDA UNGEWAGUSA NA KUBALI MENYENDO YAO KTK MAISHA YAO YA KILA SIKU.

MUNGU WAKO UNAYEMTUMIKIA AKUINUE ZAIDI NA ZAIDI NA PIA UTAMBULIKE DUNIANI KOTE, UPATE MFADHILI WA KUKUFADHILI ILI UINUE KIPAJI CHAKO. KWA KUFIKISHA JUMBE ZAKO KWA JAMII ZIMA KWANI SIO WOTE WASOMAO BLOG YAKO, KWA HIYO MUNGU AKUFANIKISHE UWEZE TUNGA VITABU ILI WEZETU WENGINE WAPATE HUU UJUMBE.
SAMAHANI WA DAU KWA COMMMENT NDEFU. KWANI LEO MZEE AMENIGUSA SANA.

GOD BLESSED

BN

Anonymous said...

M3 UPO JUU, MKUU.

NAKUTAKIA X-MAS NJEMA MKUU, PAMOJA NA WADAU WENZANGU WOTE.

NAFIKIRI UJUMBE UMETUFIKIA.

AHSANTE SANA.

GOD BLESS U

BN

mumyhery said...

Shukran kwa ujumbe murua, na kwa vile tumeisha chelewa labda tusubiri mwaka ujao. Heri ya Mwaka Mpya!!!