Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeFriday, September 18, 2009

Maandalizi mema ya Idd-el fitry

Tunawatakieni maandalizi mema ya Idd-el fitry, tusisahau kutoa zakatil-fitry. Hii zakatil-fitry ni kwa ajili ya kusaidiana, kwani hali zetu kivipatosio sawa. Wapo ambao siku hiyo ya Idd, hana chakula, hana nguo au hana kile chakumfanya na yeye asherehekee hii siku tukufu. Wewe ambaye umejaliwa kuwa nacho na ziada hapa ndipomahali pake pakuonyesha ile imani yako ya dini, nini ulichojifunza kwenye swaumu yako. Umejifunza upendo na kuhurumiana. Umeiona njaa jinsi inavyouma. Basi msaidie mwenzako kwa kutoa zakatil fitry.
Siku kama ya leo wenzetu wengine wapo vitandani, wengine wapo mahospitalini, na wao walitaraji siku kama ya leo wangefurahi na kuisherehekea siku hii ya Idd, lakini kwa uwezo wa muumba hawakuweza. Ni jukumu letu kuwatembelea wenzetu na kuwafariji kwakuwapamkono wa Iddi.
Tusiitumie siku hii vibaya kwa kufanya maasi kama tulivyokwisha kuelezana wakati tunamuaga mgeni wetu Ramadhani.

Namaliza kwa kusema, nawatakia kila-laheri na siku ikifika wote `TUPEANE MKONO WA IDD

Best wishes

From miram3

No comments :