Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary', na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..pia tunakaribisha mijadala na yale yote unayopenda yawemo humu. Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu. SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthreeTuesday, September 15, 2009

MGENI MTUKUFU ANAONDOKA

Hutaamini kuwa tumekuwa na mgeni wetu kwa zaidi ya siku 20, na baada ya siku kadhaa ataondoka, na kawaida ya mgeni akiondoka mwenyeji humsindikiza,na kumsindikiza kwetu tunatakiwa tuambatane na mgeni atakayekuja baada ya kuondoka mgeni wetu mtukufu Ramadhani, mgeni huyo ataambatana na mwenzake Idd el fitry, na ujuavyo Idd-el -fitry kawaida yake hakai muda mrefu, yeye huja kuwapongeza nyote kwa kumkarimu ndugu yake Ramadhani, na mkewe Swaumu.
Mgeni tutakayedumu naye kwa masiku karibu sawa na yale Ramadhani, anakuja ili kutuweka sawa, kutusaidia tuwe kama vile tulivyoshauriwa na Mgeni Ramadhani na kama tuliteleza hapa na pale basi tunatakiwa tuwe pamoja na yeye kwa kutubia. Mgeni wetu huyu anatuomba tumpe zawadi aipendayo ya kufunga siku sita muhimu, ukizifunga hizo utakuwa umejiweka sawa kiimani ni sawa na mtu aliyefunga mwaka mzima(Ramadhani na hizo siku sita). Mungu atupe nini jamani

Naomba waungwana tutafute jina la huyu mgeni wetu huyu ambaye naye ametuletea neema.

Wakati tunatafakari kumjua huyu mgeni ambaye wengi wetu tunamsahau kumpokea kwa visingizio mbalimbali, basi hebu tuelezane nini tuanatakiwa tufanye kipindi kama hiki ambacho tupo katika pilikapilika za kumuaga mgeni wetu mtukufu Ramdhani.

Mgeni wetu huyu ni adimu, na huja mara moja kwa mwaka,lakini kila akiondoka wengi wetu tunamuaga sivyo ndivyo. Inakuwa kama mtu aliyefua shati lake jeupe halafu siku ya kulivaa akagaragara kwenye matope. Tunakosa shukurani na adabu mbele ya mgeni wetu adimu Idd-el fitry. Siku tatu zakuwepo kwake anajionea kero, kwani furaha hugeuka kuwa karaha. Ulevi, uzinzi na yale yote ambao mgeni wetu alikuwa akituusia kuwa tuachane nayo, tunayafanya mbele ya mgeni rasmi, aliyekuja kutupongeza.

Jamani, ni adabu gani tunaionyesha mbele ya mgeni wetu huyu na tutakuja kusema nini mbele ya muumba wetu, kwanini tuliamua kujizuia siku thelathini au ishirini na tisa kwa toba, halafu ghafula tunarudi kula matapishi yetu wenyewe. Inasikitisha na sijui nini hasa nini makusudio yetu, ya kuwa tutajaliwa kila mwaka kutubu na kurudia makosa yetu, je tuna miadi gani na Mwenyezimungu kuwa mwaka mwingine tutauona na kutubia zambi zetu.

Nawausia wenzangu na mimi mwenyewe kuwa Ramadhani ni chuo pekee cha imani, ndani yake tulipata darasa la maneno ya mwenyezimungu, ni nini tutanatakiwa tuwe, tufanyenini na wenzetu walifanya nini. Ndani ya chuo hiki tulijifunza mengi, ikiwemo huruma, upendo, na uvumilivu ndio maana Mwenyezi mungu alisema kuwa malipo ya funga yako yeye mwenyewe ndiye atakayetulipa,kwasababu ni nani anayejua kweli tulifunga kisawasawa. Chakula kipo ndani na ungeweza kujificha ukala ukashiba na bado ukadai umefunga,lakini unamuogopa mola wako kwani anakuona popote ulipo, na hapa ukajenga uvumilivu, na hapa ukajenga huruma kuwa ukimuona mwenzako ana njaa utakuwa mwepesi kumsaidia kwasababu unaijua njaa kivitendo.

Lakini kuna kubwa zaidi ambalo tunatakiwa kulifahamu kwa ajili ya afya zetu, swaumu ni tiba ya miili yetu. Tunakuala vyakula vilivyojaa mafuta kwa mwaka mzima, na miili yetu hujenga magonjwa kutokana na mafuta na vyakula tunavyokula, swaumu huyeyusha mafuta hayo, na kuondoa sumu na mabaki ya uchafu uliojificha ndani ya miili yetu, mwili hujikarabati na kujiweka sawa.
Kwa ujumla kuna fadhila kubwa za swaumu kwa wale wenye kuamini, kwani hata yule uliyemuona mtukutu ndani ya mwezi huu alitulia, aliacha pombe aliacha maasi akarejea kwa mola wake.

Sasa wale waliokuwa wakimuogopa Mungu sababu ya Ramadhani, Ramadhani anaondoka, wasubiri mwakani,lakini wale wanaojua kuwa Mungu yupo milele na milele, basi Ramadhani hii inapokwisha ni mahala pa kukaa na kutafakari ninini wamajifunza, na kumeongezeka nini kwenye imani zao ukilinganisha na Ramadhani iliyopita na je kama Mola atawajalia kuiona Ramadhani ijayo watafanya nini zaidi. Huyu wa mwisho ana haki ya kumsindikiza Ramadhani huku machozi yakimlengalenga, huyu ndiye aliyekuwa mwenyeji halali wa mgeni wetu mtukufu Ramadhani na anastahili kukaa na Idd-el-fitry, na baadaye ataendelea kumkarimu mgeni ambaye zawadi yake muhimu ni kufunga siku sita na mbele ya mola anataraji malipo ambayo Mola ametuahidi.
Tunawatakia kila-laheri na kumi hili la mwisho la kusamehewa madhambi
From miram3.com

No comments :