'Docta, huyu sio mtoto wangu, ….’akasema mdada.
‘Sio mtoto wako…! ' Akasema docta kwa mshangao, na mdada akawa kimia
'Kama sio mtoto wako, wazazi wake wapo wapi…au wewe ni nani
kwake?’ docta akauliza, akiangalia saa yake, akikumbuka anahitajika kwenda
wodini kuna mgonjwa alihitajia huduma yake.
‘Docta mimi ki-ki ukweli, s-sijui, hutaamini lakini sijui….’kauli
iliyomfanya docta aweke peni mezani, akaangalia simu ya mezani, akitarajia
kuitwa muda wowote.Lakini kwa kauli hiyo
ya mdada ilimfanya ahisi kuna jambo linakuja.
Docta akaangalia saa yake tena,….halafu akamwangalia yule
mdada, hakuweza kuona sura ya huyi mdada vyema kwani kwa muda ule huyo mdada
alikuwa kainamisha kichwa chini. Docta akamuangalia mtoto aliyebebwa na huyo
mdada, halafu akamuangalai tena yule
mdada. Docta alitafuta jambo kwa wawili hao, huku akichelea muda…!
‘Unajua sikuelewi, kama wewe sio mzazi, wewe ni nani kwa
huyo mtoto…?’ akauliza docta
‘Docta , naomba tu unielewe, mimi sijui wazazi wake wapo
wapi, mtoto anaumwa, ni huruma ..ni…huruma yangu tu….’akasema sasa huyo mdada
kwa sauti ya huzuni.
‘Sawa…lakini kwanza unielewe… ili mtoto atibiwe, eeh, si
tunahitaji maelezo, eeh….kwanza kadi yake ya kliniki unayo..?’ akauliza docta
‘Si nimekuambia mimi siwajui wazazi wake, …mimi sina kadi
yake… na hata sijui kama ana kadi….’akasema mdada
Docta akahema kama kuchoka hivi….akaangalia saa yake ya
mkononi, halafu akataka kama kusimama, akaangalia simu ya mezani…ni kama
alitaka kuitumia, au kusubiria kuitwa, akamuangalia mdada…
‘Mdada..!, sijui nikuite hivyo,...sijui kama unanielewa, na
sijui kama tutaelewana, huyu ni mtoto mdogo, unasikia sana….umempataje mimi
sijui eeh…si wewe umekuja naye, au..?’akasema docta lakini mdada alimkatisha
kwa kauli iliyomshfanya docta agwaye kudogo
‘Docta,….naomba msaada wako..!’akasema mdada.
Msaada….!
Docta kusikia hiyo kauli akilini akasema,…yah…kama nilivyowaza, yale yale….!
Lakini docta hakutaka kulichukulia hilo analoliwaza akilini kwa
haraka, kwanza akavuta subira, akawa anamuangalia yule mdada,….mdada alikuwa
kimia, bado akiwa kainamisha kichwa chini akimuangalia yule mtoto.
‘Msaada…!, unaomba msaada gani…?’ akauliza docta
Mdada aliendelea kukaa kimia,… halafu baadae yule mdada akainua
kichwa na kumtizama docta, mara moja paah…halafu akarudisha macho chini.
Docta aliyaona yale macho, yale macho yalikuwa kama yanalengwa lengwa na machozi. Hata hivyo,
docta hakuweza kumuona vyema,…Hata hivyo,Docta machozi ya wagonjwa ameyazoea!
Docta kwa uzoefu wake, akahisi kuna jambo, na hayo machozi
sio kama yale aliyoyazoea, hata hivyo,aliona avute subira, hakuwazia tena huyo
mgonjwa mwingine wa wodini,…
Kuna jambo kwa huyo
mdada na mtoto….Aliwaza hivyo!
Yule mdada sasa taratibu akainua uso, na sasa akamtizama
docta, moja kwa moja, macho ya mdada yakakutana na macho ya docta, hapo sasa
ndio docta akaweza kumuangalia vyema huyo mdada, na machoni kulikuwa kukavu,
Mhh...…. Docta aliguna hivyo kimoyo moyoni
‘Docta, ninaomba umtibie tu huyu mtoto tujue ana shida gani….hilo tu
docta….’akasema huyo mdada, kabla docta hajahitimisha uchunguzi wake wa
kuwalinganisha wawili hao kama kuna uhusiano wowote mdada aliongea hivyo .
Docta, kwa haraka akachukua peni na kuandika kitu kwenye
kadi, halafu…
Na mara simu ya mezani ikaanza kulia…
NB. Ni tukio nililokutana nalo hospitalini, na diary yangu ikaona sio vyema lipite bure.....Ni kisa cha mdada na mtoto, Je huruma yake iliishia wapi? Je kuna nini nyuma ya pazia.....
KARIBUNI SANA KWENYE SEHEMU YA INAYOFUATA
1 comment :
Your blog serves as a testament to the impact of passion and dedication in content creation.
Post a Comment