Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za kimaisha, na matukio yenye mafunzo ndani yake, ndio maana nikaiita 'diary'(shajara). Pia tunakaribisha mijadala yenye kuelimisha

Na kwa kuifanya iweze kuvutia zaidi tunaandika matukio hayo kwa mfumo wa visa, hadithi au tamithilya..

Wewe ukiwa mdau muhimu, unaweza kuchangia na wenzako kwa kutoa hoja (comments). Pia unaweza kutoa maneno ya hekima, utaalamu, au dukuduku lako (kilio chako)kwa jamii ili kuweza kukidhi mahitajio yetu.

MUHIMI, SOMA , CHANGIA, NA TOA kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

TUPO PAMOJA DAIMA


Tushirikiane, Tusaidiane, Tupendane, Tuvumiliane, Tusaidiane, Tusameheane.

Kwa visa motomoto tunapatikana pia kwenye mitandao ya kijamii ya: Facebook, na Twitter, bofya hapa upate visa zaidi;

https://www.facebook.com/emu.three, na kwa ajili ya kuitangaza hii blog, ingia hapa:

https://www.facebook.com/diaryyangu/

`u-like' na pia unaweza kutwitter hapa;

https://twitter.com/emuthree



Tuesday, June 27, 2023

JINAMIZI.....Utangulizi..

Ilipoanzia....

Nilishtuka toka mawazoni, kilichonishtuka ni sauti....

Sauti ya mtu analia...nikageuka kushoto kwangu, kama vile vile...sauti kama ile ile, kiukweli niliogopa kugeuka, hata hivyo, nikafanya kama vile..

'Unalia nini..?'

Abiria yule akawa kama kashtuka, kwa haraka akanitupia jicho, macho yangu yakakutana na yake, ...akawa kama kashtuka fulani hivi...akashika mdomoni,....kama haamini, kama ....nahis hivyo, sasa  akawa kama anawaza jambo fulani, halafu akasema

'Siamini...'

Kimia kikatanda,  na niliyemuuliza akawa anajifutafuta usoni na leso, na kujifanya kama vile kuna kitu kilimuingia machoni, halafu akarudia tena kusema...

'Siamini...!' halafu akashika kichwa na kuinama kama anawaza jambo...halafu taratibu akainua uso kuniangalia, sasa akiwa katoa jicho la woga......

Mdada mrembo...sasa tulipokutanisha macho yetu,..hii ni mara ya pili, mimi sasa... nilihisi moyo kunienda mbio, mwili ukaisha nguvu.....sijui kwanini

Nilikuwa na yangu kichwani, kichwa kilikuwa kinauma kwa mawazo..
,..na kwa hili, kichwa kikazidi kuuma....kukapita ukimia fulani,...na nili-nilipoona hivyo, kwa maana sasa mdada aliinamisha kichwa chini na mimi sasa nikaona nijinyamazie tu,  nilitafakari hili jambo.

Yaliyokuwa kichwani sasa yalikuwa ni lukuki....

'Kama  hii ni kweli ni heri nife tu....'kauli ndogo ikasikika.

Hapo sasa niligeuza kichwa upande ule wa kushoto kwangu  huyo mdada....sasa akiwa kaangalia mbele tu, ni kama kazama kwenye dimbwi la mawazo.

Kimia kikapita tena...na nikaona labda yamepita, lakini haikupita muda, nikahis huyu mdada analia...

Sikuweza kuvumilia

'Samahani, ...naona hata nikivumilia sitakuwa na amani..dada tafadhali ninambomba sana...uniambie wewe ni nani...na na... niambie yaliyokusibu, huenda tukasaidiana..

'Mhh....'akaguna hivyo

'Naona unalia, na nimesikia neno aheri nife tu.....kwanini....'

Hapo akageuza kichwa kuangalia dirishani,...sasa akionyesha wasiwasi...ni kama anataka kutokea dirishani hivi... 

'Ha-ha...hamna kitu...'akasema hivyo sasa kidhahiri anaogopa, je anaogopa nini...ananiogopa mimi,...!

'Hamna kitu , wakati hali inaashiria kuna jambo....huwezi jua labda kukutana mimi na wewe kuna sababu, huenda tukasaidiana ukaja kunishukuru....tuka...'

'Wala usihangaishe kichwa chako, kuniwaza mimi....nahis hii ndio hatima yangu,...labda, ...sistahili kuishi,...niache tu....isije ikawa ni kweli.....labda ni wewe....'hapo akaendelea kulia, sasa akiwa kajiinamisha kichwa.

Niligeuka huku na kule kuwaangalia abiria wengine, labda kuna mtu anafuatilia haya mazungmzo, lakini wengi walitingwa na mambo yao, na asubuhi kama hii kila mtu ana jambo lake.

'Wale wa mnazi mmoja...'konda akanadi, nami nikajua baada ya vituo kadha nitakuwa nimefika mwisho wa safari yangu, lakini sikuwa na amani moyoni..

'Nikuulize tu....sasa unakwenda wapi?'

'Kujitosa baharini....'akasema na hapo nikashituka, 

'Wewe.....binti mrembo kama wewe unataka kujitosha baharini, kwa jipi kubwa, unajua nikuambie kitu, ujana ni pambio, na katika ujana mengi yanapita, na yatapita utayasahau,...muhimu kama kuna changamoto fulani, ichukulie kama mtihani tu...ukifeli, bado maisha yapo...

'Hahahaha.....ulisema hivyo hivyo....hahaha....nilijua ni ndoto ya jinamizi lakini ...nahisi ni kweli...nahisi...mungu wangu nifanye nini mimi, ....'akasema 

Nifanyeje....

'Sikiliza mimi nateremka posta, tukifika hapo posta, tuteremke pamoja, tukae mahali tuongee, ....

'Tuongee nini....'akasema kwa hasira

'Kuhusu matatizo yako..'

'Matatizo yangu....wakati wewe ndio chanzo cha yote...'akasema kwa hasira

'Mimi ndio chanzo cha yote kwa vipi...'

'Hahaha...unajifanya hunikumbuki sio....'akasema

'Sasa unanichanganya naona haupo sawa...'nikasema ...sasa nikitaka kuachana na huyo mdada, nilihisi huenda ana amatatizo kichwani

'Unakumbuka jana ulikuwa wapi usiku...?' akaniuliza

'Jana.!!.......'nikasema sasa nikishtuka,...ilinifanay nigeuza kichwa taratibu kuangalia huku na kule kama watu wanasikia, au kufuatilia.

'Kumbuka.....ulipoamuka subuhi, ulikuwaje..?' akaniuliza

Hapo nikagwaya...kwa maana awali nilitingwa na yangu kichwani, kwa maana nilijua ni ndoto tu, sasa mbona ...

'Mimi naenda kujiua,...lakini hutaishi salama.....'akasema

'Mimi sielewi kitu...'nikasema na .....

'Posta...posta......'konda akasema na nikajua nimeshafika mwisho wa safari yangu, ....lakini je niliache hili jambo hivi hivi, au....

'Teremka umeshafika, ...kumbuka tutakutana kuzimu,....sio ndoto ile,.....'akasema mdada

**************


Ni mimi: emu-threeH

No comments :