‘Lakini kabla ya kukuuliza hayo maswali, nataka uhakika, nataka huyo mtoto awe salama…na
wewe unipe uhakika huo…’nikasema na jamaa akataka kubisha sikumpa nafasi
nikasema;
‘Mimi nafahamu kabisa kuwa wewe ni mtaalamu unaweza kufanya
mambo yenu na hiyo mizimuikatulia…si ulipewa madawa na huyo mtaalamu, au sio,
sasa nataka uhakika huo ili tuongee kwa amani, …’nikasema na yeye akatulia
kidogo, na mara nikaona anacheza na simu, anaandika ujumbe, sijui alikuwa kama anaandika kitu kwenye simuu yake, halafu
akasema;
‘Mimii sio mtaalamu,…nilishakuambia, mimi natekeleza yale
aliyoniagiza na huyo mtaalamu, wewe uliza hayo maswali yako….hayo ya mtoto
niachie mimi, mimi ndiye baba yake nitajitahidi niwezavyo, maana haya tumekuwa tukipambana nayo muda sasa, wewe
hukuwepo….na hujui…lolote, tatizo huyu mtu,mtaalamu…’akatulia akiandika ujumbe
kwenye simu.
‘Huyu mtu unayemtumia ujumbe kwanini usimpigie simu….’nikasema
kwa lugha ya kumfanya aone na sisi tunakubaliana na yeye, na kweli kauli hiyo
ilimfanya akunjue uso, na kwa haraka akasema;
‘Ngoja bwana, hayakuhusu haya, ….’akasema akizidi kucheza na
simu yake, halafu akasonya na kusema
‘Kweli sasa yabidi nifanye hivyo,…unajua , tatizo ni kuwa nyie
mlishaanza kuleta madharau yenu,…lakini ngoja niongee naye tu, sawa kabisa, itakuwa ni vyema zaidi,….’akasema akinza
kupiga simu. Alitulia kusikiliza , lakini ilionekana hakuna mawasiliano.
‘Haiwezekani,…imekuwaje tena….huyu jamaa kaenda wapi..unajua
hii sio kawaida yake , simu yake muda wote ipo hewani…..sasa sijui leo kuna
nini…’akasema akituangalia sisi kama anatuuliza na mpelelezi akauliza
‘Ni Jamaa gani huyu..?’ akauliza mpelelezi
‘Si huyo mtaalamu mwenyewe, kwani nilikuwa nampigia nani, mwenzako
si katoa wazo kuwa tumpigie huyo jamaa
simu,…ili aweze kutusaidia, unajua , bila ya yeye mimi siwezi kuwahakikishia
hilo,…nataka ajaribu awezavyo, ..afanye juhudu zake, ili hiyo hali isijirudie
tena kwa mtoto, maana kwa jinsi alivyoniambia yeye, hiyo hali ikijirudia tena,
hata nani, hata yeye mwenyewe hataweza kufanya lolote….’akasema.
‘Kwani mtoto alipopandisha homa muda mfupi uliopitia wewe
ulifanyaje, maana hiyo ilikuwa zaidi ya mara ya nne, tuseme ukweli
hapo..’nikasema na jamaa akatikisa kichwa kama kusikitika, na mimi sikumuachia
nafasi nikaendelea kusema
‘Wewe mwenyewe ulisema ikitokea safari nyingine huwezi
kufanya lolote tena,…je mbona imewezekana,…na ilikuwa ni mara ya nne, au….sasa kumbe
wewe unaweza au ndio tuseme, umeshakuwa
mtaalamu na wewe….’nikasema
‘Unajua wewe huelewi, tatizo sio kufanya dawa, tatizo ni
miiko…kama miiko haitakiukwa, hilo haliwezi kutokea,…ndio mimi nilifanya hivyo nilivyoelekezwa japokuwa ilikuwa zaidi
ya mara nne, kinyume cha alivyoniagiza mtaalamu, kwa kubahatisha tu, sasa mimi
sijui madhara yake itakuwaje, mimi sijui, labda mimi mwenyewe naweza kudhurika,
sijui….’akasema
‘Kwahiyo sasa mtoto yupoje…?’ akauliza mpelelezi
akimuangalia mama yake na aliyejibu ni huyo huyo jamaa akasema;
‘Kwa hivi sasa mtoto hana tatizo si huyo hapio kambeba mama
yake mkague kama ana homa yoyote, ndugu zanguni, mjue tatizo kubwa ni ukiukwaji
wa miiko, munielewe hapo, najua nyie hamuamini hayo mambo, lakini yapo,…. ndio
maana hiyo hali inatokea,, …’akasema na mimi nikatabasamu tu, na kitendo hicho
kilimfanya awe kama hapendi akasemaa
‘Sijui nyie mnataka niwaelezeje ili mlielewe hili….labda
niwaulize je hayo mnayofanya , au mnayotaka kuyafanya je hayaendi kinyume na
hiyo miiko, kama nilivyokuelezea awali?’ akaniuliza akiniangalia mimi
‘Miiko gani….?’ Akauliza mpelelezi, na mimi nikadakia kwa
kusema;
‘Hiyo miiko yenu haiwezi kuizua serikali kufanya kazi yake,
hebu nikuulize, hiyo miiko yenu,….,haitaki haki itendeke…?’ kabla ajanijibu nikazidi kusema
‘Hiyo miiiko yenu inataka hii familia idhulumiwe haki
yao, hiyo miiko yenu, inataka tusijue
ukweli kuhusu hilo deni,…wewe huoni kuwa hiyo mizimu imesetiwa tu, ili watu
wasifuatilie kujua ukweli, sasa ni nani kafanya hivyo, kama sio hao….wanaotaka
kumdhulumu mjane na watoto wake, sisi tunachohitajia hapa ni kutafuta huo ukweli….je kufanya hivyo tumekiuka hiyo miiko,
hebu tuambie…?’nikasema na mpelelezi akatikisa kichwa kukubaliana na mimi.
‘Unajua mimi …..nafuata nilivyoagizwa…’akasema
‘Na nani…?’ akauliza huyo mtaalamu
‘Na huyo mtaalamu…..ni kiukweli yeye ndiye angeliweza kutupatia hilo jibu la hayo
uliyosema,…na sio yeye, ni mzimu wa kaka…ndio unaongea,…yeye anafanya mambo
yake tu, ili huo mzimu useme una tatizo gani,….sasa huo mzimu umekuja ukaingia
kwa mtoto..ndio tatizo hapo…sasa huyu jamaa ndio hapatikani kwenye simu,….yeye
ndiye angetusaidia kutupatia hilo jibu, ili tusije kuharibu tena…’akatulia
akijaribu kupiga tena.
‘Mimi naona tuendelee tu…., sizani kama hilo litafanya
mizimu ikasirike, tuomba tu isje kulete madhara mengine kwa mtoto ….na huyo ni
baba yake, anataka deni kulipwa, na huwezi kusema kwanini unamtesa mtoto wako,
kwake yeye huko alipo, haijalishi ni nani ataleta huo ujumbe, ili watu waelewe……’akasema
akijaribu kutabasamu.
Nilimuangalia shemeji, bado alionekana kuwa na uso wa
huzuni, mashaka..na alikuwa kwenye hali
ya kutaka kuondoka, nikasema;
‘Shemeji wewe kaa,
usiendelee kusimama, maana haya mazungumzo yanaweza kuchukua muda, na nia ni
kuhakikisha ukweli wote leo unajulikana,…..na baada ya hili utakuwa huru kuamua
mwenyewe kuondoka au kuendelea kukaa
kwenye nyumba yako, ukweli wote tutaubaini hapa hapa, …..’nikasema kwa
kujiamini japokuwa moyoni sikuwa na uhakika huo.
Shemeji alisita kidogo, baadaye akasogea hadi kwenye sofa
akakaa upande upande, ni kama kuturizisha tu, na mtoto wake Yule mkubwa akakaa
vyema kwenye sofa na kujiliza, alionekana naye kachoka, na haukupita muda na yeye
akalala.
‘Sasa tuendelee, ila ndugu,….hakikisha huyu mtoto haumwi…hali
ya mtoto ikijirudia tena, sasa itakuwa
kazi yako mpelelezi, maana umeshaiona jinsi hali ilivyo,na ukweli kiasi,
umeshaanza kuuona, hii ndio hali halisi ya dunia ilivyo…mimi nina imani baada
ya haya maswali nitakayomuuliza, utaujua ukweli wote, na sizani kama tatizo
hili litakuwa kubwa tena, zaidi ni nyie kuchukua hatua….’nikasema na jamaa
aliposikia hivyo, akasema;
‘Lakini ….mbona siwaelezi, mimi kuhusu huyu mtoto nimejitahidi
kwa hivi sasa hana tatizo…najua nyie hamna nia mbaya, su sio…ndio maana hata
hiyo mizimu itakuwa imelewa, sioni kwamba kuna haja ya kuwa na
mashaka….’akasema halafu kwa sauti ya huruma akasema
‘Eti shemeji, kuna kitu ulitaka kukifanya kinyume na miiko,kwa jinsi ulivyoagizwa, maana ulisikia mwenyewe,
siku ile…. hawa watu hawawezi kuelewa, zaidi yetu,… sisi ndio tunafahamu maana
tulikuwepo siku hiyo, sisi ndio tunafahamu jinsi gani mtoto anateseka, hawa
hawajui…..sasa tusaidiane kwa hilo, je kuna jambo , …?’ akauliza na shemeji
hakujibu hapo hapo, ila alipoona wote tunasubiria jibu lake akasema;
‘Mimi nimeshasema nataka kuondoka, nawasikiliza nyie tu,
lakini leo hii silali kwenye hii nyumba, kama ni nyumba, ndio imefikia kutaka
kuwaumiza watoto wangu, ….haya, chukueni, …mimi nataka kuondoka…ninakwenda
kwetu….’akasema.
‘Lakini shemeji hiyo kauli yako inautata, ni nani achukue
nyumba, unavyosema ni kama vile na mimi nahusika na mambo hayo,…usiwasikilize
hawa watu, wao wanashinikiza tu,ili mwisho wa mwezi wa kinge mshahara ,…na hata
hivyo, sijamuamini …’akageuka kuniangalia
‘Shemu…hawa watu, hawajui ukweli, ukweli halisi tunaufahamu sisi,… sisi ni kitu
kimoja,….nia ni kuhakikisha roho ya kaka inatulia, nia ni kuhakikisha familia
inaishi kwa amani, hebu fikiria kama haya yangelitokea tu, na tukawa hatujui sababu ni nini,
unafikiri ingelikuwaje, mtoto angeendelea kuteseka tu….sasa shukuru tumejua
sababu ni nini….’akasema, na mimi nikaingilia na kusema;
‘Dada wewe tulia,mambo sasa yanakwenda sawia, …..kuna mambo
yanfanyika, ukweli utaajulikana, kama ni kweli au la…kama anavyodai shemeji
yako , kama kweli kuna ukweli, kwanini litokee hili, mtoto kuumwa, huoni kuna
utata…sasa subirini tuone, …’nikasema na jamaa aliposikia hivyo, nikamuona
anaangalia simu yake,akainua na kuipiga tena, …naona namba ilikuwa haipatikani,
akawa sasa uso unaonyesha hali ya mashaka, akasema;
‘Unajua tatizo ni kuwa nisipoweza kuwasiliana na huyu mtu,
mambo yanaweza kuharibika ,, na mimi sitaweza kufanya kitu,…na huyu mtu sio
kawaida yake, simu yake muda wote ipo hewani, ni lazima kuna tatizo..sio
kawaida yake….’akasema
‘Naona sasa mumepatikana..’nikasema kwa sauti kama ya mzaha,
na yeye akanitupia jicho la aina yake halafu akasema;
‘Tumepatikana, kwa vipi,i…..wewe maneno yako bwana mimi siyapendi ,kwanini unasema hivyo, kwani wewe
unanishuku nini mimi, mimi ninajaribu kufanya kile kiwezekanavyo ili kuisaidia
familia yangu, sasa hapo nimefanya kosa gani…?’ akauliza
‘Mimi naona tuendelee….’akasema mpelelezi akiangalia saa
yake.
‘Sawa tutaendelea ila nilitaka uhakika kuwa huyo mtoto hali
hiyo haitajirudia tena, maana, ….sisi tunachotaka ni kujua ukweli wa hilo deni,
na tukiwa tunalifuatilia hilo, mama wa
mtoto na familia yake wawe na amani…’nikasema
‘Lakini kama maswali yako yanalenga huko, kutafuta ukweli wa
hilo deni, mimi sizani kama mimi…sijui lakini,….tuone utakavyoniuliza,….ila
kama lengo lako ni kutaka kukwepesha deni lisilipwe, hilo ni moja ya tatizo,
tukipekenyua undani wa hilo deni tunakuwa tumekiuka miiko, kwanini , kwanini,
mimi naona haina maana tena ….kwasababu deni ni kweli ni la kaka….’akasema
‘Hebu nikuulize kitu, mbona wewe ulifanya hivyo..?’
nikauliza
‘Kufanya nini…?’ akauliza
‘Wewe uliposikia kuwa kuna deni, kaka yako ana deni, ulifanya nini, si
ulihakiki, sasa kwanini hutaki na sisi tufanye hivyo,….wewe ulipohakiki, hakuna
mtu aliyeumwa, au kuna mtoto wako aliumwa,..hakuna….sasa, kwanini alipoanza kufanya hivyo shemeji, si ndio mtoto wake akaanza kuumwa,….au sio, mtoto
hakuanza kuumwa ulipoanza wewe kutafuta ukweli, ni kweli si kweli, sasa ni kwanini?’ nikamuuliza
‘Kwahiyo unataka kusema nini…?’ akauliza
‘Ndio nataka kukuhakikishia hilo,…na wewe ndiye unayeweza
kutupatia jibu hilo, ni kwanini...na nataka kulithibitisha hilo deni je kweli
ni la kaka yako au kuna ujanja ujanja hapo…na hili litapatikana kwa kupitia
maswali nitakayokuuliza wewe…..umenielewe, je upo tayari…?’ nikamuuliza
‘Wewe uliza maswali yako , tatizo lako, unanishuku mimi,
wakati mimi sijui lolote, haya uliza hayo maswali yakoo ….’akasema na mimi
nikatulia, nilikuwa nasubiria taarifa fulani kutoka kwa vijana wangu, lakini
niliona wanachelewa kunipigia,…, lakini moyoni nilijua watakuwa wamefanikiwa.
Jamaa alipoona nachelewa kumuuliza maswali akasema akimuangalia mpelelezi
‘Unaona mwenzako alivyo, hivi hayo maswali yapoje, mbona
hayaulizi,…yeye ni hivi hivi,….kwanini haulizi hayo maswali…?’ akasema akimuangalia
huyo mpelelezi, na mara simu ya mpelelezi ikalia, na akawa anaangalia simu
yake, na ndipo akasema;
‘Samahani kidogo, ….kuna simu ngoja nikaisikilize
nje….’akasema na kutoka nje, na mimi nikabakia na jamaa, jamaa, akamwangalia
shemeji yake, nilimuona jinsi gani alivyotahayari, hakusema neno, akawa
anatikisa tikisa mguu, na mimi nikasema;
‘Tukimsubiria jamaa, ngoja na mimi niwasiliena na watu wangu
kidogo…’nikasema na mimi nikatoka nje, ile simu yangu iliyopo mezani nikawa
nimeiacha pale pale… nikawa natumia simu nyingine. Nilipoongea na watu wangu,
maana pamoja na hayo kulihitajika kibali, kwani hayo sasa ni mambo ya kisheria,
na wakili wa kujitolea ndiye alikuwa anakitafuta ili sisi tutambulikane
kisheria, kwa ajili ya kazi tunayoifanya japo kwa huyo mama lakini ilionekana
kuna utata.
Kwahiyo nikawa bado nipo
kwenye njia panda, hata nikiweza kuupata huo ukweli ni nani atanisaidia,
ni huyo mpelelezi, …lakini tutakuwa tumeingilia kazi za watu, …kama tusipopata
mwanasheria wakili wa kutusaidia hilo kazi itakuwa nzito sana, nilikuwa sijajua
ni wapi mwanasheria huyo kakwama….wakati nasubiria nikaona nirejee ndani.
Wakati narejea ndani, Jamaa alionekana akiongea na shemeji yake kwa
ukali kidogo maana nilisikia sauti kama ya kukaripia, japokuwa sikuyasikia hayo
maneno, na nilipoingia nikamkuta huyo mdada akionekana kulia, ilipoona hivyo nikasema;
‘Vipi tena, kuna nini zaidi….?’ Nikauliza
‘Wewe uliza maswali yako, haya ni maswala ya ndani mimi na
shemeji yangu , hayakuhusu…wewe si uniamini bwana, mimi ni baba wa hii familia,
muulize shemeji ni nini nilichowafanyia…..mimi nimekuwa naye bega kwa bega,
niijali hii familia kama watoto wangu,lakini leo hii nafikiriwa vibaya,…sasa
sijui, ndio tulikuwa tunaongea hayo,..haya wewe uliza maswali yako hayo…..’akasema
*********
Mara simu yangu ikalia, nikasimama na kusogea dirishani,
nikawa naongea kwa sauti ya chini, ili jamaa asisikie, nikasikiliza kwa makini, halafu nikauliza
‘Kapatwa na dharura gani….sasa mumempata mtu mwingine?unasema
nini,…anahitajia malipo…oooh…mtihani….’nikasema na kusikiliza naona kuna mambo
yanaibuka kwa sasa, kwenye mali kuna mitihani yake, nikawasikiliza maelezo yao
halafu nikasema;
‘Una uhakika, ni nani, mtu wa usalama, ni nani huyo, sio
huyu huku, ni mwingine yupi….kwahiyo …tuendelee, au …kukamatwa, kwa kosa gani…usijali,…’nikasikiliza
halafu nikauliza
‘Kwani wao wanataka kibali gani….nani , polisi , kwanini..?’
Nikauliza na kusikiliza kwa muda,halafu nikageuka kumuangalia shemeji, nilitaka
aniangalie kwani hadi hapo nilihitajia msaada wake, lakini nitaupataje wakati
ndio yupo kwenye kifungo cha miiko…Jamaa alikuwa kasimama na kwenda dirishani
akawa anatizama nje, alikuwa kanipa mgongo.
Nikaendelea kuongea na simu nikasema, …’Nyie fanyeni
muwezavyo,…huku nitapambana tu,…Mungu yupo pamoja nasi…nina imani kesho itakuwa
siku nyingine, lolote lawezekana…., hata nikitoka hapa usiku tutamwendea huyo
hakimu….nina uhakika atatuelewa ongea na
huyo wakili, namfahamu sana, ni mnzuri lakini hafanyi bure….kama anahitaji malipo yatapatikana tu….’nikasema
nikiwa sina uhakika na hilo, yote hapo nacheza
bahati nasibu.
Niliwasikiliza
maelezo yao, mpaka nikahisi vibaya,….naona mambo yanaharibika, ….kuna vizingiti
vingi, vimejitokeza, na ilionekana kama kuna watu wameshaweka masilahi mbele,
na sijui ni nani yupi nyuma ya hilo, kwani huyu jamaa muda wote tunaye hapa…
‘Unasema wakili anataka kuongea na mjane,…lakini muda…’nikasema
na kusikiliza…sikulipenda hilo wazo la huyo wakili la kutaka kuongea na mjane…kwani
hakuna muda kabisa, na isingeliwezekana kwa hali ilivyo!
‘Hilo kwa hivi sasa ni gumu….mimi naliona gumu kwasababu
nipo hapa na naiona hali ilivyo….’nikasema huku nikijaribu kumuangalia huyo
mdada, kama naweza kumtoa pale nikaongee naye mahali kwingine , ili nimwambie
kinachoendelea na ikibidi awe tayari kwenda kuonana na huyo wakili mpya, lakini
niliona itakuwa ngumu sana.Nahisi jamaa ndio maana hataki kucheza mbali,….
‘Kwahiyo mnataka kusema nini….?’ Nikauliza na wakati huo
shemeji aliinua uso wake, machoni kulikuwa kumejaa machozi bado alikuwa analia,
sijui jamaa alimuambia kitu gani….nikageuka kumuangalia mpelelezi naona naye
alikuwa kwenye harakati zake, alichelewa kurudi. Kazi inaanza kuwa ngumu!
Kulikuwa na sintofahamu nyingine….,benki walikuwa
hawakubaliani na ombi letu kuwa mnada huo uahirishwe kwani wao walishafuata
taratibu zote , na amri ilishatolewa, na imetolewa na mahakama, na kama kuna watu wanazuia wanakwenda kinyume
na mahakama, ni wakosaji…tunahitajika kushitakiwa kwa kukiuka amri halali ya
mahakama, na hilo limeshafikishwa polisi ili sisi tuchukue hatua.
‘Je ni nani kawaambia hayo…?’ nikawauliza wakatoa maelezo
yao, yaonyesha kuna mtu , huenda alikuwa akiwasiliana na huyu jamaa na
kawaambia wajaribu kufuatilia uhalali wetu , sikuwa na uhakika nalo, lakini ni
nani angenishuku uhalali wetu kama sio huyu jamaa!
Hata hivyo, watu wangu walikuwa kwenye harakati ,
wakihangaika huku na kule….kuhakikisha wanazuia huo mnada wa kesho, na pili
kunapaitikana ushahidi ,lakini wakili mpya anadai mtu anayeweza kuleta huo
uzito ni mjane, ….alimuhitaji akutane naye na ikibidi waongozane naye mguu kwa
mguu hadi kwa hakimu…na pili anahitajia kuwe na ushahidi mnzito, utakaoweza
kubadili mawazo ya hakimu na polisi waweze kuingilia kati! Mambo yameharibika
mwishoni…
‘Na zaidi ya hayo kuna mtu wa usalama mkubwa kasema sisi
yawezekana ni matapeli kwahiyo tukamatwe, …’akasema mtu wangu
‘Huyo mtu wa usalam mkubwa ni nani….?’ Nikauliza na
kusikiliza!
Oh, hilo sasa ni balaa jingine, nikajua kumbe tatizo hilo sasa
lina mikono mingi, yote kwasababu ya mali , na mali yenyewe ni mali ya mjane na
yatima, watu wameshaanza kuimezea mate…. Ni kweli nyumba ikiuzwa kihalali
kutapatika pesa nyingi sana, sasa ni kiasi gani watapewa hawa wahanga na kiasi
gani kitakwenda kwa hao wapambe…dhulumati. Ni lazima kifanyike kitu, …hii si
haki kabisa
’Mungu wangu toa msaada wako…’nikajikuta nikisema huku bado nimeshikilia simu nikisikiliza
maelezo ambayo kila hatua yalikuwa yakinikatisha tamaa…sikujua kuwa jambo hili
lilikuwa limeshawahusisha watu wengi hivyo, lakini kama wakili Yule wa mwanzo
angelikuwepo,….mambo yasingelikuwa magumu hivi,….kapatwa na nini ghafla hivyo….!
‘Sasa tufanyeje….?’ Nikauliza na kusikiliza maelezo ya watu
wangu wakitoa mapendekezo yao, kwa ujumla wao walishafikia kuzuri…lakini
ushahidi waliopata unahitajia muda kuuweka sawa. Na kesho ndio kesho…! Nikakata
simu na kugeuka kumwangalia mjane na mwanae..huruma ikanitinga!
Kwa hali ilivyo hadi hapo mtu atakayeweza kunisaidia hadi
hapo ni huyo mpelelezi,…kwanza aniamini,
ili tu asikilize huo ukweli, …..ukweli una nguvu, na yeye sizani kama ana uwezo
wa kupingana na wakubwa zake, kwani huyu amayeleta vikwazo huko ni mkubwa wa
huyu mpelelezi!
‘Sasa huu ni mtihani…..’nikajisema nikiinua hatua kurudi
kwenye sofa…nilitingwa na mawazo mazito sasa,…hata hivyo, bado nilikuwa na
matumaini,….nilikuwa na uhakika kama huyo mpelelezi atakubali kuusikiliza huo
ukweli kwa kupitia kwenye maswali yangu ambayo nitambana huyo jamaa basi yeye
atakuwa upande wetu na kesi hiyo itakuwa na mshiko. Lakini pili awe tayari
kutoa ushirikiano, ili kuwashawishi wenzake na hasa hakimu…na kwa muda huo muhimu ni hakimu
ilii akubali ombi letu, ili huo mnada wa kesho usifanyike…miujuiza!
Sikuweza kukaa, nikawa natembea tembea nikiwaza, na
mpelelezi hajarudi, bado anaongea na simu huko nje, nilijawa na wasi wasi, ….
Nikatembea hatua chache hadi kwenye dirisha la upande wa
pili, nichungulia nje, …nilimuona mpelelezi akiongea na jamaa wawili, kumbe
kuna wenzake walikuwa nje…nilimuona akiongea kwa vitendo, yaonekana kuna kitu
kikubwa sana, kwani ishara ile ya mikono, ilikuwa kama kutokakukubaliana au
kuna kitu kimekosewa…nikazidi kuingiwa na mashaka….kuna nini…nikageuza kichwa
kumwangalia jamaa yangu, huku ndani…
Huyu jamaa alikuwa akijinyosha na nilimuona hana wasiwasi….anaonyesha
kujiamini zaidi, tabasamu mdomoni….aliponiona namuangalia yeye akasema;
‘Nyie watu,… mimi siwezi kupoteza muda wangu siku nzima
hapa, kama hamjawa tayari basi tupange siku nyingine, lakini kesho,….keshoo si
ndio mnada au…..’ akawa kama anauliza halafu akamgeukia shemeji yake na
kumuuliza.
‘Au sio shemeji……?’ akamwangalia shemeji yake aliyekuwa
kajiinamia tu, na alipoona hajibiwi akaendelea kusema
‘Kesho walisema ndio siku ya mnada… na sisi hatuna jinsi,
kama tulivyokubaliana,…..hawa jamaa hapa sizani kama wana msaada wowote, wanapoteza
muda bure, mpaka nafikia hatua siwaamini, kama wana msaada wangelikuwa huko kwa
hakimu…labda wafanye jambo, jambo lakuonyesha kuna namna ya kulipwa hizo
pesa..maana muhimu hapa ni deni lilipwe, au sio shemeji, likilipwa hatuna
maneno,…lakini hawa mmmh,nina mashaka nao …yawezekana ni matapeli tu…’akasema
kama anamnongeneza shemeji wake! Shemeji yake aliposikia kauli hiyo akainua
kichwa kidogo, akitaka kuniangalia lakini akasita,na jamaa akamsogelea shemeji
yake ili awe naye karibu akawa anaongea kwa sauti ya chini chini…
‘Sisi kama tulivyokubaliana…huo mnada ufanyike tu…maana
hakuna njia nyingine ya kuzipata hizo pesa…na pesa itakayopatikana, watachukua
deni lao itakayobakia tutajenga nyumba nyingine, sio lazima iwe kama hii… ili
roho ya kaka isiteseke au sio,….yule ni mume wako anahitajia msaada wako sana…na
jingine ni hili la mtoto, je hali ikijirudia tutafanyaje….tuwahurumie hawa
watoto….na hilo ni kwa kuondokana na hilo deni, au unasemaje shemeji,….’akasema na shemeji yake alikuwa kimia tu
‘Na hiyo ya mnada sio amri yetu, hatuna la kufanya…maana
kila kitu kipo wazi, stakabadhi zote zina sahihi ya kaka, …sasa hawa watu wanataka
nini,…. ndio maana hawataki kwenda huko benki, na huko benki hawawezi kuvumilia
tena walishaniambia iwe isiwe ni lazima wachukue chao…sasa,…. haya ngoja tuone,
….’akasema akimuangalia shemeji yake, na shemeji yake alikuwa kimia tu.
‘Na kama wewe unataka kunaondoka wewe nenda tu…, mimi
nitayasimamia mambo yote,usiwe na wasiwasi….hilo lisikutie shaka, na ikishapatikana
hiyo pesa, eneo lipo..ujenzi utaanza mara moja…nitajitahidi hata kutia nguvu
zangu, naweza hata kuuza sehemu ili mpate nyumba yenu nyingine….’akasema kwa
sauti ndogo ili nisisikie…na shemeji yake hakumjibu kitu, alikuwa kainama tu.
‘Nikuambie ukweli, hawa ni matepeli,….mwenyewe utaona,…nimeshawajua,….wanacheza
na mimi…shemeji mwenyewe utaona….ngoja usikie vumbi langu...’akasema na kugeuka
kuniangalia, na mimi nilikuwa najidai naandika ujumbe kwenye simu, yeye
alipoona hivyo akamgeukia shemeji yake akitaka kumwambia kitu, lakini
akasita,…kuna ujumbe wa simu uliingia kwenye simu yake….akawa anausoma, na alipomaliza
akasema
‘Nilijua tu…hawa ni matapeli, sasa ngoja waionje joto ya
jiwe….shemu usiwe na wasiwasi, hawa sasa hivi wanakamatwa, wewe utaona
tu…’akasema na shemu wake sasa akainua kichwa kwa wasi wasi akaniangalia ,
lakini hakusema kitu, na jamaa alipoona shemeji yake hamjibu akanigeukia mimi
na kusema
‘Sasa sijui nyie mumefanya juhudi gani kwa hilo….’akasema
‘Juhudi ya nini….?’ Nikamuuliza kama simuelewi
‘Kuhusu huo mnada wa kesho….’akasema
‘Usiwe na shaka kwa hilo…wewe mwenyewe baada ya hapa utatusaidia
kuhakikisha hilo halitendeki…’nikasema na yeye akaniangalia kwa macho ya
kushangaa, akasema;
‘Mimi….kama nani, maana hiyo ni amri ya mahakama…’akasema.
Mara mpelelezi akaingia… cha ajabu sasa alipoingia alikuwa
kashikilia pingu mkononi, ….akawa anatembea mwendo wa hatua za kuhesabu, na
anakuja muelekeo wangu, pale nilipokuwa nimekaa…akanifikia, na akawa ananiangalia
kwa jicho la kujiuliza mpaka nikahisi kuna tatizo…
NB: Ehee…sasa ni nanii hii tena,….uone mtihani wa mali
ulivyo…. tuwemo sehemu ijayo.
WAZO LA HEKIMA: Mali na madaraka ni mtihani kwetu…wangapi
wangapi wametumbukia kwenye mtihani wa mali, na madaraka, ..wakasahau kutenda
yaliyo haki , wakaupindisha ukweli, wakadhuluma wenye haki zao, kwa sababu tu ya kupata mali na madaraka…,
kisa ni nini pesa. Wangapi wangapi wameshindwa kuutetea ukweli, kwasababu ya
ubinafsi, wakataka kumfurahisha bosi wao, huku wakijua wanchofanya sio halali,…
tukumbuke jamani, Haki na ukweli havipindishwi kwa kujua kuongea vizuri,
ukaipindisha sheria….hiyo ni dhuluma,…ipo siku utaumbuka tu!
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment