Nilipofika kazini
nikakuta wafanyakazi wamesimama kwenye ubao wa matangazo,wengine wanaondoka
wakicheka wengine wakisikitika, na mimi nikasogea kuangalia, hapo nikaona maandishi makubwa yameandikwa;
`ORODHA YA WALIOPUNGUZWA KAZI NA WATAKAOENDELEA NA KAZI. Wafuatao wafike ofisi
ya utawala, waonane na meneja utawala, kwa ajili ya kupata mkataba mpya au
kupata barua za kupunguzwa kazi.
Niliposoma maandishi
hayo mwili ukalegea, miguu ikaisha nguvu, nikageuka kuwaangalia wenzangu ambao
nao kila mmoja alikuwa akipepesa macho kusoma majina yaliyopo, hapo ni kila mtu
lake…
Nikaanza kusoma majina
moja baada ya jingine, na kila niliposogea mbele, nikawa napumua nikijipa moyo
kwa matumaini kuwa jina langu halipo, kwani nilikuwa mchapa kazi hodairi
kilichoharibu ni haya matatizo ya kifamilia na yametokea karibuni tu, hawawezi
kuchukua matatizo ya miezi kadhaa, wakasahau juhudi zangu za miaka mingi nyuma,
nikawa najipa matumaini hayo huku nikiendelea kusoma majina
Nikafika karatasi ya
mwisho, katatasi hiyo ilikuwa na majina nusu ukurasa, nikaanza kusoma la
kwanza, nikawa nashuka chini, la pili, la tatu….......
Tuendelee na kisa
chetu
***************
Nikafika jina la mwisho, macho yakashikwa na ukungu, nikawa sioni
vyema, japokuwa herufi za mwanzo zilikuwa za jina langu,…nnikafuta macho na
kuinama chini nikainua kichwa, nikasoma kwa sauti…
Kweli lilikuwa jina langu, nikakuna kichwa nikainama nikauka
kuangalia wenzangu, wengi walishaondoka, waliobakia ni kaam mimi, kila mmoja
akilalamika ndani ya nafsi yake, na baadaye wote wakaondoka nikabaki mwenyewe, sijui
ilitokea je, nikahisi kizungu zungu, na kudondoka chini.
Nilibaki pale chini kwa muda, nikajizoa zoa, na kujipa nguvu,
nikijua kuwa hayo yameshatokea na mimi ndiye muhusika mkuu, hakuna wakunionea
huruma hapo nisipowajibika picha itakwisha, …., nguvu ziliponirudia nikainuka
na kuelekea masijala ambapo kulikuwa na ofs ya meneja utawala, ili kupewa barua yangu.
‘Yah, mjumbe, umefika, au familia bado inasumbua, natumai
umeangalia orodha je jina lako lipo?’ akaniuliza kama vile hajui
‘Lipo bosi…’nikasema
‘Pole sana, ndio maisha, usikate tamaa, mlango mmoja ukifungwa
mwingine unafunguliwa, huwezi jua, albda kuna sehemu nyingine bora inakusubiria
sehemu nyingine, cha muhimu ni kujipa moyo na kupambana…’akasema huku
akinikabidhi barua yangu.
Kwa mkono unaotetemeka nikapokea hiyo barua nikafungua na kuanza
kuisoma, maelezo yaoo ya kisiasam kuwa kutokana na gharama za utendaji kuwa
kubwa kampuni imeona ni bora ipunguze wafanyakazi, na kama hali itakuwa nje
baadhi wataitwa tena, na maelezo kuwa malipo ni mwezi mmoja , na mshahara wa
mwezi huo, hakuna pesa ya usafiri maana wote wamechukuliwa kama wakazi wa
Dar-esalamu.
Nikafungua ukurasa unaonyesha mahesabu, kama nilivyotegemea, deni
nililokopa lilikatwa kwenye mafao yangu, kwahiyo sikuwa na cha kuchukua zaidi
ya kusubiri kile kinachoitwa ‘akiba ya penshion ya kustaafu au kuacha kazi.
Nayo sio nyingi kutokana na mshahara wenyewe ulivyokuwa mdogo. Nayo natakiwa
kusubiri miezi kadhaa, ili uanze kuomba, na ukiomba unaweza ukazungushwa wee,
kwahiyo pesa hiyo sio ya kutegemea kwa sasa, sasa nitaishije...
‘Vipi umeshasoma, kama tayari weka sahihi yako, na chukua karatasi
ya malipo nenda kwa mhasibu….’akasema
‘Ipo wapi hiyo karatasi ya malipo?’ nikauliza na meneja utawala
akawa anapekua pekua, siku kama alifahamu kuwa sina cha kulipwa au alijifanya
kupoteza muda
‘Mhh, naona hakuna, hebu hiyo barua yako, nione…’akasema na
akachuka ile barua akasoema, halafu akasema;
‘Haiwezekani ina maana ulichukua deni kubwa kiasi hiki, …ilikuwaje,
madeni mawili kwa wakati mmoja, …mmh, ndio matokea yake haya mkiambiwa msikope
kupita kiasi mnaona watu wabaya, sasa unaona, hakuna cha kulipwa hapa…mafao
yako ukitoa madeni unbakia bado unadaiwa na kampuni…’akasema
‘Kwahiyo mnataka kusema nini…?’ nikauliza
‘Mimi kazi yangu ni kufuata taratibu za kampuni, na kuhakikisha
zinatekelezwa, kuanzia sasa wewe
huhesabiki tena kama mfanyakazi wa kampuni hii, unachotakiwa ni kukabidhi vitu
vyote vya kampuni, na tunakutakia maisha mema....’akasema
‘Nyie watu mbona hamna huruma, ina maana nyie kukaa kwenye
madaraka mnajiona mumefika, ....sawa tu,, lakini mkumbuke mwenzako akinyolewa na wewe utie maji, mateso
haya ninayoyapata kama niliomba yanipate, basi na nyie hamtakuja
kuyapata...nashukuruni sana....’nikasema
Meneja utawala akaniangalia kwa macho ya huruma, lakini akibenua
mdomo kwa dharau na kusema;
‘Sasa wewe ulitaka mimi nifanye nini...haya sio maamuzi yangu
binafsi, ni maamuzi kutoka kwa idara yako, na ukapita mjadala wa kina, mwenyewe
umeona utendaji wako ulivyokuwa, mwanzoni ulijituma baadaye ukaona familia yako
ni bora zaidi,....’akasema
‘Lakini mika yote nilikuwa mtendaji mnzuri nimechaguliwa mfanakazi
bora mara tatu..ina maana hiyo haonyeshi kuwa nilikuwa mtendaji bora…hii miezi
mingapi ya matatizo imefanya nionekane sio mtendaji bora?’ nikauliza
‘Hayo yote yalionekana, lakini imeonekana .huna jipya,..hata kaam
ungeliachwa hali ingeliendelea kuwa hivyo, maana kama ni matatizo
yangeishaje..sana sana utazidi kuipa kapuni hasara….’akasema
‘Kwakweli tenda wema mara mia kosa moja wema wote unasahaulika
ndio hivyo….’nikalalamika.
‘Ndugu cha muhimu ni
kuhakikisha unamalizana na mambo yako ya kifamilia, ili ukipata kazi sehemu
nyingine usije ukafanya kosa kaam hili, jifunze jinsi gani ya kutataua matatizo
huku sheria za kampuni unazifuta…ni kweli wewe ni mtedaji bora, lakini
umeonyesha udhaifu mwishoni, kama umeshindwa kutatua matatizo yako ya kifamilia
je ukipewa uongozi utawezaje kuongoza, kuwajibika ili kampuni iendelee kuwepo…’akasema
‘Mimi naomba nionane na mwenye kampuni, maana kunifanyia hivi ni
kama kutaka nikafe, mtoto anaumwa sasa hivi yupo hospialini, hajiwezi, , mke
anaumwa, sina pesa,nadaiwa kodi ya nyumba, hapa sina hata akiba ya kuanzia
maisha, nyinyo leo hi mnanifanyia hivi, mumeshahau jasho langu lililomwagika
kwenye kampuni hii,.....’nikasema.
‘Nielewe ndugu haya sio maamuzi yangu binafsi , ama kwa mwenye
kampuni, yeye haya hayamuhusu, yeye katupa sisi majukumu yote, …yeye ni mtu wa
miwsho wa kuhalalisha tu, hakujui wewe, hajui utendaji wako wa kazi, anatujua
sisi washauri wake..’akasema
‘Kwahiyo nyie ndio mlimshauri kuwa mimi sifai…?’ nikauliza
‘’Utendaji wako unajieleza…nimekuonya mara ngapi, au umesahau…’akasema
‘Lakini umenionya miezi hii ya karibuni baadaya kuaptwa na mataizo
ya kifamilia, huku nyuma uliwahi kunionya, au ilikuwa ukinipa pongezi za
utendaji bora, hayo ya nyua mumeyasahau…?’ nikauliza
‘Ulimi wako, ndio umekuponza, unakumbuak..nilikuambia chunga ulimi
wako, …sasa ndio hayo,..nakupa tu kama dokezo, ukiwa sehemu ya kazi usijifanye
wewe unajua kuongea sana, kumbuka kila mtu kaja na mikono yake nyuma baraua ya
maombi mbele…hapa ndio unajua kuwa , kila mtu kaja na hamsini zake…’akasema
‘Mimi naomba nikaonane na mwenye kampuni..’nikasisitiza na yeye
akasimama na kuondoka.
Nilikaa pale kwa muda, nilipoona harudi nikatoka nikitaka kwenda
kumuona mwenye kampuni, na wakati natoka nikaona mwenye kampuni akitoka na huyo
meneja utawala, kuonyesha kuwa walikuwa wakiongea , nikaona sio vyema kwenda
oja kwa moja kwa mwenye kampuni, nikamsubiria meneja utawala, ambaye alikuja
ofisini kwake nikamuuliza;
‘Je umemueleza mwenye kampuni tatizo langu?’ nikamuuliza.
‘Amesema sheria ni msimeno , hakuna atakayependelewa kwa vile tu
ana matatizo yake ya kifamilia, tukifanya hivyo wengine watalalamika,
kwahiyo,...kasema kampuni itakusaidia nusu ya deni lako la kawaida, sio deni
kubwa,...deni kubwa kampuni imesema haitawajibika nalo, kwani haina pesa ndio
maana imefikia hatua ya kupunguza wafanyakazi, deni kubwa utalipa wewe
mwenyewe...’akasema meneja utawala
‘Lakini hata hiyo nusu ya hilo deni dogo ni shilingi ngapi, ni pesa ndogo tu ya
kunifiksiha siku mbili tatu.....’nikasema
‘Kwahiyo tukate deni lote ndivyo unavyotaka, shukuru hicho kidogo
ulichopata, nenda kanisubirie nje, nikamilisha barua yako mpya....’akasema
akienda kutayarisha barua nyingine, nikatoka hadi sehemu ya kusubiria hadi pale
nilipoitwa kuchuku barua yangu nyingine.
Haya nenda kwa mhasibu ukachukue pesa yako…’akaniambia
Mambo yameanza hapo, mke ana-mashetani, mtoto anaumwa magonjwa
yasiyojulikana , kazi sina, pesa sina…pale nilipopewa hizo pesa an kuona si
pesa kitu.nililia kama mtoto, nikarudi tena kwa meneja utawala nikampigia magoti, ili angalau
wanisamehe hilo deni, kwani nyumbani mtoto anaumwa, sina hela ya matibabu, mke
anaumwa anahitaji uangalizi, kodi ya nyumba inanisubiri…lakini meneja utawala
hakuwa yule ninayemfahamu tena, hapo kawa kama askari
‘Ondoka, nimekuvumilia vya kutosha, niwaite walinzi wakutokea kwa
nguvu….’akasema kwa hasira. Hapo nikaona sina la kufanya nikaondoka zanu huku
nikiangalia ajengo ya kampuni, nikikumbuka kuwa sisi ndio waanzilishi,
tulipigana usiku na mchana na mwenye kampuni hadi hapo ilipofikia, lakini leo
nafukuzwa bila hata thamani, nimeshasahaulika…
Nilijikuta natembea huku naongea mwenyewe kama mtu
aliyepagawa, nikielekea nyumbani, na kwasababu ya kuchanganyikiwa, nikajikuta
nipo kati kati ya bara bara bila kujijua...
Wakati natembea sikujua kuwa nimeshafika barabara kuu, nikawa natembea kati kati ya barabara,
sisikii sioni, akili yangu ilikuwa moja, …dunia sasa sio yangu….nilikuwa mbali
nikiwaza dunia nyingine isiyokuwepo, akili hafanyi kazi, sasa nikawa nakatisha
ile barabara kulekea upande wa pili.
Nilisikia honi zikipigwa, tahamaki, nikajikuta nikipigwa na kikumbo
kikubwa, na mara nikwa napaa hewani, nikatua chini, sio chini ni kwenye kitu,
kumbe nilikuwa nimegongwa na gari, na hapo nilipotua, ilikuwa sehemu ya mbele
ya gari, .....giza likatanda, sikujua kilichoendelea baadaye.
******
Nilipozindukana nilikuwa hospitalini nikiwa nimefungwa mabandeji ,
na mwili ulikuwa unauma kila sehemu nikasikia mtu akisema;
‘Ana bahati sana huyu mtu, kwenye vipimo vya mwanzo, inaonyesha hajavunjia
mfupa labda huku kwenye mbavu, ambapo tunahitajika kusubiria vipimo vya x-rays, na pia inahitajika kupimwa utra-sound, ili tuone kama ndani kuna
madhara ...’akasema huyo mtu nahisi ndiye docta.
Na mtu mmoja ambaye nahisi ndiye dereva aliyenigonga akasema;
‘Gharama nyingine inabidi azibebe yeye mwenyewe, kwasababu kosa ni
lake yeye mwenyewe, hata trafiki wameliona hilo....anaonekana alikuwa na mawazo
mengi wakati anavuka bara bara...’sauti ikasema nilijaribu kugeuza kichwa
kuangalia huo upande walipo hao watu lakini sikuweza shingo ilikuwa imevalishwa
dude zito.
‘Mume wangu kwa hali ilivyo, ni vyema tukamsaidia tu huyu mtu,..angali
hali aliyo nayo kakonda,a anonekana hata kula hajala, mume wangu tumsaidie tu...’ilikuwa sauti ya
kike naona alikuwa mke wa huyo mtu.
‘Hiki tulichosaidia kinatosha, angalia gari lilivyoharibika kwa
sababu ya uzembe wake, unafikiri atatusaidia matengenezo yake, gari la nyuma limetugonga tulipofunga break ya haraka, sehemu kubwa inahitajia matengenezo….mimi naona
tumuache dakitari aendelee naye, tunamlipa gharama za leo, kama kuna zaidi,
tutawasiliana….’huyo mtu akasema
‘Inatakiwa muache kitangulizi cha nusu ya gharama, hiki mlicholipa
ni kidogo sana…’akasema docta
‘Tutawasiliana docta, sasa hivi hapa sina kitu utanipigia ngoja
nikaone taratibu za kulitengeneza gari,, …’sauti ikasema na hao watu wakaondoka.
Nikajua huenda kesho yake watakuja, lakini hawakuonekana tena, hata docta
alipojaribu kuwapigia simu wakawa hawapatikani, hapo docta akaaja kwangu na
kuniambia;
‘Watu wako waliokuleta, wameshakimbia mawsiliano hayapatikani, na
pesa waliotoa ni ndogo sana,..wewe huna pesa..?’ akaniuliza
‘Nilikuwa na pesa kidogo kwenye nguo zangu…’nikasema na docta
akasogea pembeni kuna nguo zangu zilikuwa zimewekwa akaniletea nikasema;
‘Angalia hapo mfukoni kuna bahasha ina pesa ndani…’nikasema, yeye
akajaribu kutafuta kwenye mfuko wa suruali akasema;
‘Mbona hakuna kitu….’akasema
‘Kulikuwa na bahasha kuna barua yangu kutoka kazini na pesa…kwani
ni nani alinivua nguo zangu?’ nikauliza
‘Mimi mwenyewe na nesi wangu, hakuna mwingine aliyegusa nguo zako…’akasema
‘Kulikuwa na bahasha na pesa zangu za mafao…’nikasema nikijaribu
kujiinua lakini nikashindwa, maumivu, nikatulia, akili sasa ikaanza kufanya
kazi, ina maana hata hicho kiodgo nilichopata nacho kimeibiwa
‘Hamna bahasha humu ndani, huenda ulipopatwa na hiyo ajali wali
walikupekua wakakuibia…ulipoletwa hapa sis hatukuwa na muda wa kukagua nguo
zako, na humu hakuna tabia ya kuibia wagonjwa, haijawahi kutokea, nawaamini
wafanyakazi wangu….’akasema docta.
‘Huu sasa mkosi,…’nikasema
’Je una ndugu na jamaa zako ambao unaweza kuwasiliana nao, ili
waje kukusaidia, maana siwezi kuendelea na matibabu wakati sijui hatima ya
malipo yako, unajua hii ni hospitali ya kulipia, ilitakiwa upelekwe hospitali
ya serikali, lakini waliona sehemu ya karibu ni hii hapa…’akasema
‘Ndugu na jamaa zangu hawapo hapa Dar, na waliopo hapa hata
ukiwapigia simu hawataweza kunisaidia lolote, mimi naona nitoke tu, nitajua
mwenyewe mbele kwa mbele…’nikasema
‘Kwa hali hii siwezi kukuruhusu utoke hivi hivi, hali yako bado sio nzuri unahitajika vipimo, hatujui hukondani kupoje,…inaonekana
kuna athari ndani, tunahitaji tuchukua vipimo vya vya utra
–sound, lakini havitapimwa mpaka tuwe na uhakika wa malipo, jamaa zako
hawajafika, na hali uliyo nayo haihitajii kusubiria sijui tufanyeje…’akasema
‘Naomba msaada wako docta, nimekwama, mimi nilijua kuna pesa
kwenye mfuko wangu kama wameniibia tena, sijui hata nifanye nini, nidhamini nikipona nitajua jinsi gani ya kukulipa…’nikasema kwa
uchungu.
‘Mimi ni docta tu, sio mwenye hospitalini natimiza wajibu wangu tu, …labda
nikushauri jambo, sasa hivi kuna gari linapeleka mgonjwa muhimbili,
nitakachofanya nitakuandikia kuwa uende muhimbili, kwa matibabu zaidi,
watakuchukua …’akasema
Na kweli ikafanyika hivyo nikachukuliwa hadi Muhimbili, kipindi
hicho Muhimbili kama humjui mtu umeumia, nimefikishwa pale nikapokelewa
nikapewa kitanda, nikaandikiwa kupimwa hivyo vipimo…siku ya kwanza ya pili, ya
tatu, hakuna cha vipimo wala nini, kila docta akipita anasema nisubirie vipimo.
Ndani kwa ndani kunauma,…lakini kila siku nikawa nahisi kupungu kwa
maumuvu, na siku moja alipofika docta nikamwambia kuwa mimi najisikia nafuu
nitoke tu;
‘Unatakiwa usubirie vipimo …’akaniambia.
‘Mpaka lini, leo ni siku ya nne, sipimwi, mimi naona nitoke tu….’nikasema
na sijui ikawaje, docta akaondoka na baadaye nikachukuliwa kwenda kupata hivyo
vipimo, na majibu yakaja kuwa hakuna matatizo, ikabidi siku iliyofata nitoke.
Unajau mwili ni wa ajabu sana, siku hizo tano, mwili ulikuwa
umekwisha, nimekonda, natisha, …mpaka macho yamezama ndani, siku ile Lugalo uliponiona
macho yametoka nje, sasa hapo ilikuwa kinyume chake, ndipo utashangaa mwili wa
bindamu ulivyo. Mungu ni mkubwa
Basi nikaruhusiwa na ukumbuke siu zote hizo hakuna anyejua nipo
wapi, ajali ile ilitokea hakuna mfanyakazi aliyewahi kuniona, kwani kama
wangeliniona taaarifa ingefika nyumbani.
Nikiwa nimechoka sina nguvu, nikapanda dala dala kwa nauli na
kuomba kwa mmoja wa wagonjwa ambaye nilimuelezea matatizo yangu akanionea
huruma akanipa pesa kidogo ya nauli
Nikafika nyumbani, nilipokaribua nyumbani nikashangaa kuona watu
wamejaa , kwanza nikasimama na mawazo ya haraka yakakumbuka mtoto aliyekuwa
kiumwa, ..hapo nikavuta hatua ili nijue kumetokea nini....
NB: Jamani leo matatizo, lakini hicho kidogo kinatosha
WAZO LA LEO: Kuna watu wanakufa njaa lakini hapo hapo
kuna watu wanamwaga chakula. Kuna matajiri wa kukufuru na hapo hapo kuna
masikini waliovuka mpaka, hawajui leo watakula nini, kuna mayatima, kuna
wasiojiweza wagonjwa…wanahitaji misaada, hapo hapo kuna watu wanachukua dhaana
ya hao wenye shida na kushibisha matumbo yao na utajiri wao. Kwa hali hii, baraza katika ardhi inapungua. Kumbuka ukishiba,
ukamwanga umedhulumu halali ya watu wengine, kwanini umwage, kwanini
usimwangali jirani yako mwenye njaa, maana tunajuana..
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment