Mahakama ilijaa
isivyo kawaida, kinyume cha matarajio , kwani kesi hiyo ilitakiwa ifanyike kimia
kimia, lakini watu walijaa utafikiri kulikuwa na tangazo kuwa leo kuna
kesi kubwa itafanyika.
Kutokana na unyeti wa hii kesi na wahusika wake,
hakukutakiwa kuwe na watu wengi, kiusalama, na mapokezi yake kwa jamii, hasa
kisiasa, lakini hilo halikuwezekana, taarifa zilisambaa kwa haraka na watu
wakaambizana, na kile aliyesikia akawa anamwambia mwenzake ikawa ni kama lamgambo la kimia kimia kuwa, asiye na
mwana aeleke jiwe.
Polisi kuona hivyo, ikabidi wafanye kazi ya ziada,
kuzuia watu kuingia eneo la mahakamani, walioruhisiwa ni wale wanaohusika na
kesi hiyo na watu wachache ambao wahusika wao wapo kwenye hiyo kesi, hali kabla
ya mahakama kuanza ikawa ni mvurugani kai ya polisi na watu waliofika kufatilia
kesi hiyo, hata waandishi wa habari walikataliwa kuingia.
Kwa vile kila mmoja alitaka kuingia, ikabidi amri
itolewe, kuwa watu wote wasiohusika waondoke eneo karibu na mahakama haraka
iwezekanavyo , la sivyo, kikoso cha fanya
fujo uone kitakuja na kuwatawanya, watu wakakaidi, na waliojitahidi,
wakasogea nji kidogo ya mhakama, na kukaa kusubiria , hata hivyo, baadaye hali
ilikuwa shwari, watu wakakubali kukaa nje ya eneo la mahakama kusubiria, waone
ni nini kitatokea.
Baadaye gari lililowabeba washitakiwa wa mwanzo
likaingia, hakuna aliyelijali hilo gari sana, labda wana ndgu wa hao washukiwa,
ndio waliojitahidi kutafuta njia angalau ya kuwasalimia, na baadaye gari lililosadikiwa
kuwa ndilo la mshitakiwa mkuu, likaingia hapo kila mtu akasimama, na kujongea
barabarani, lakini polisi wakahakikisha hakuna mtu anayekaribia eneo hilo, na
gari hilo likaingia eneo la mahakama likiwa na ulinzi mkali, likitanguliwa na
gari la askari wenye silaha za kisasa, na nyuma yake halikadhalika.
Mtu anayesadikiwa ndiye mshitakiwa mkuu, akateremka,
akiwa kafungwa pingu mikononi na miguuni, ilibidi ashikiliwe huku na huku ili
aweze kutembea, siji ni kutokana na hiyo minyororo au huenda ni kutokana na
kipigo, na kutembea kwake kulikuwa kwa shida, ilikuwa mwendo wa taratibu hadi
kufika mlango wa kingia mahakamani.
Jamaa huyo alikuwa kafunikwa usoni, sijui ni kwa kupenda
yeye mwenyewe au ni kutokana na walivyoona wenyewe wahusika, kwahiyo hakuna
aliyeona sura yake, na hili likazua gumzo, kila mmoja akisema lake, ilimradi
una mdomo, kauli ni tashi wako,.. hata waandishi wa habari waliotaka kupata
picha yake halisi walibakia kupiga picha za mtu asiyeonekana sura yake, na
swali likabakia likiulizwa na watu wengi.
‘Je huyu mshitakiwa mkuu ni nani...’
‘Wamefanya hivi kwa vile wanaona aibu,....’mmoja akasema.
‘Wanaona aibu ya nini…?’ mwingine akauliza.
‘Wewe huoni, au hujasikia, kuwa huyo muhusika ni mmoja
wa watu wakubwa wa idara ya usalama, sasa wanaona aibu kwa vile mshitakiwa ni
kiongozi wao, kiongozi wa juu wa idara ya usalama , si aibu hiyo, hebu fikiria
mtu anayetakiwa kulinda usalama leo hii inashitakiwa kwa dhamana aliyotakiwa
kuilinda ....’akasema huyo mtu.
‘Mhh, hata mimi sijiu, ndio maana nimefika , kwani
wanasema huyo mtu ni mtu wa miujiza, haonekani ovyo, wengine wanasema sio
binadam huenda ni mzuka,..yaaani hata sielewi, kwani wewe unamfahamu mtu huyo ?’
akauliza.
‘Ni mfahamu wapi,…mengine ni ya kuzusha tu, huyo
mwanzoni alikuwa ni hao askari kanzu, akapanda
vyeo hadi kufikia hapo alipo, sasa hivi alikuwa ni kiongozi mmojawapo, kutokana na unyeti wa kazi zao,
ndio maana kafichwa kama mwali..’akasema mwingine.
‘Ndio maana hawataki watu kuingia mahakamani,
...’akasema mwingine.
‘Lakini sasa ni mhalifu, unyeti, umuhim wake, haupo
tena, kavunja kiapo cha kazi yake…..’akasema mwingine.
‘Ngoja usikie, maana hapa hakna kuona tena….’akasema
mwingine.
Watu wakawa na hamasa ya kutaka kujua vyema,ni nini
kitakachoendelea, lakini hakuna aliyepata nafsi hiyo hata ya kusogea, au kusikia kinachoongelewa
ndani ya mahakama, na kesi ikawa inaendelea kimiya kimiya ndani ya mahakama
kukiwa na ulinzi mkali.
********
Ndani ya mahakama, hakimu alifika na kesi ikatajwa kama
ada, na muendesha mashitaka akaelezea mlolongo mzima wa kesi hiyo, na sasa akawa
anahitimisha muhutasari wake kwa kusema;
‘Leo kama tulivyoahidi muheshimiwa hakimu, tumemleta
shahidi mkuu, ambaye sasa ameshikiliwa kama mshitakiwa mkuu, kutokana na
ushahidi ulipatikana...’akasema muendesha mashitaka.
‘Kwahiyo huyo mtu kwa sasa ni mshitakiwa au ni
shahidi..?’ akaulizwa.
‘Ni mashitakiwa mkuu muheshimiwa hakimu..’akasema
muendesha mashitaka.
Basi mshitakiwa huyo akatakiwa kukubali au kukataa kosa,
na hapo ndipo mlolongo wa pingamizi na
kauli za kushangaza zikatokea, kiasi kwamba hata hakimu alibakia kushindwa
kuamua kwa muda huo, kwanza mshitakiwa akasema yeye hahitaji wakili,
atajisimamia mwenyewe , na ikaja swali la kukubali au kukaata kosa, mshitakiwa akasema;
‘Kwanza kabla ya yote, mshitakiwa aliyetajwa hapo na
mahakama yako tukufu sio mimi....’akasema.
‘Una maana gani kusema hivyo?’ akaulizwa.
‘Mimi sitambulikani kama mlivyotaja hapo, mimi sio mkuu wa
kitengo chenu cha usalama, nahisi kuna makosa yamefanyika, mimi ni mtu tofauti
kabisa, nahisi mumefanya makosa, na henda mliyemkamata sio huyo ambaye mlimuhitajia kwa
kifupi ...mimi sio huyo mshitakiwa mkuu mliyemtaja hapo, kwahiyo naiomba
mahakama yako tukuf iniachilie....’akasema.
‘Acha ujanja ujanja, unataka kusema wewe ni nani?’
akaulizwa.
‘Kuhusu mimi ni nani hili sio la msingi kwa sasa, la
msingi je mimi ndiye mshitakiwa mkuu kama mlivyomtaja hapo, mimi ninachotaka
kuhakikisha mbele ya mahakama hii ni kuwa mimi sio huyo aliyetajwa hapo kama
mshitakiwa, ushahidi ninao..’akasema.
‘Unataka kuhakikishia mahakama hii kwa vipi, una
ushahidi gani wakati wewe ni mkuu wa kitengo cha usalama, na umeshikwa kwa
taratibu zote,…..? ‘ akaulizwa.
‘Siku hizi kuna utaalamu wa kumgundua mtu kuwa ndiye au
siye, kuna vipimo vya DNA, naiomba mahakama yako tukufu ipime damu yangu ili
uwe ni ushahidi kuwa mimi sio huyo mtu waliyemshitakia, kwa kifupi mimi sio
mkuu wa kitengo hicho cha usalama, kufanana kwa sra isiwe ndio kigezo, mtu,
ambaye wanadai ndiye mshitakiwa mkuu, hayupo hapa kamtafuteni, lakini sio mimi,
mimi ni mtu tofauti kabisa, nataka
sheria inilinde...’akasema.
Hakimu akawa anamuangalia huyo mtu, halafu muendesha
mashitaka, hakaingialia kwa muda huo, akawa anamsikiliza muendesha mashitaka.
‘Hebu tukuulize swali, wewe siye uliyekuwa mkuu wa
kitengo cha usalama?’ akaulizwa.
‘Sio mimi nimeshawaambia….’akasema.
‘Hujawahi kufanya hiyo kazi?’ akaulizwa.
‘Nimeshawaambia sio mimi, msipoteze muda, pimeni hicho
kipimo, na mfanye haraka kumtafta huyo mtu wenu…’akasema.
‘Hujaeleweka, kwasababu wewe ndiye uliyekamatwa, ukiwa
ndani ya chumba, ambacho kinasadikiwa kuwa ni makao makuu ya kiongozi wa kundi
haramu, pili wewe ni kiongozi, mkuu wa kitengo cha usalama, inajulikana hivyo,
leo hii unakuja na hoja kuwa wewe sio kiongozi wa usalama..usitake kupoteza
muda….’ Akaambiwa.
‘Ili kuhakikisha hilo, nataka mchukue damu yangu ipimwe,
mtu hawezi kkwepa ukweli wake, kuwa ndio yeye au sio yeye kwa kupitia kipimo
cha DNA ….’akasema.
‘Mimi nawahakikishia kuwa sio mimi mliyemkamata, kuna
kosa mumefanya, pimeni haraka mtagundua kuwa kweli mumefanya makosa, huyo mkuu
wenu wa usalama sio mimi,hayupo hapa ...tusipoteze muda, wataalamu wa damu, na
vipimo vya namna hiyo waje wachukue damu yangu wapime…’akasema.
‘Na nawahakikishia, na kama kweli watathibitisha kuwa
mimi ndiye kiongozi wao , mkuu wa kitengo hicho, basi nip tayari kujibu
mashitaka hayo..lakini kama sio mimi, basi wanishitaki kama mtu baki sio huyo
mtu waliyemtaja hapo....’akasema.
Hakimu, ikabidi amuite muendesha mashitaka wakateta, na
kweli ikabidi damu ya huyo mtu ichukuliwe kwa haraka na vipimo vikafanyika na
kweli ikabainika kuwa sio yeye, DNA, ilionyesha tofauti na DNA, ya mkuu wa
kitengo cha usalama, japokuwa kundi la damu, lilikuwa ni sawa, Group O.
‘Ndugu muheshimiwa hakimu, naomba sheria ifuatwe, kesi
dhidi yangu ifutwe, na watu wa usalama waafanye kazi yao kmtafuta mshitakiwa ….’akasema huyo jamaaa.
‘Lakini tukulize, wewe siye uliyekuwa hospitalini ukitibiwa, wewe siye uliyekamatwa ukiwa
kwenye makao makuu ya kundi hilo haramu?’ akaulizwa.
‘Yawezekana nilibadilishwa na huyo mnayemtafuta , lakini
maswali kama hayo hayana msingi kwa sasa, swali la msingi, ni je huyo
mliyemshitakia ni mimi au sio…tumegundua kuwa sio mimi, hao mengine hayana
hoja, muheshimiwa hakimu, naomba sheria ifuatwe,…’akasema mshitakiwa.
Muendesha mashitaka akageuka nyuma kuangalia , alikuwa
akimtafuta Inspecta Moto ambaye kwa muda huo bado alikuwa hajafika, akasema;
‘Ndgu muheshimiwa hakimu, nahisi kuna makosa amefanyika
, lakini ttukumbuke kuwa kundi hili lina mbinu nyingi, na hii inayotokea hapa
ni oja ya mbinu zao, mwenzangu
anafuatilia ushahidi muhimu, kuna taizo limetokea, tunaiomba mahakama yako muda
..’akasema muendesha mashitaka.
‘Unahitajia muda kiasi gani, masaa au siku, …?’ akauliza
hakimu
***********
Wakati hayo yakiendelea mahakamani, Inspecta Moto alikuwa
akihangaika kumtafuta fundi wa komputa, ambaye alimkabidhi kile kifaa kwa ajili
ya kuhakikisha kuwa kinafnguka, kwani nyumba aliyokuwa akikaa hayupo, na hakuna
anayefahamu wapi kaelekea, na muda umeshakwisha, alitakiwa kuwa mahakamani.
Akajaribu kupiga simu ya huyo mtu ikawa haipatikani,
akawasiliana na mtaalamu wa mitandao kama anaweza kusaidia lolote , lakini
mtaalamu huyo akasema sio rahisi maana huyo mtu hajavaliswa, au kuwa na kitu
ambacho kinaweza kumgundua wapi alipo, na simu yake haifanyi kazi, imezimwa.
Hapo Inspecta Moto, akachanganyikiwa, na kila mara
alikuwa akipokea ujumbe kutoka mahakamani kwa muendesha mashitaka wa kutaka
kujua yupo wapi, na ushahidi aliosema anao, upo wapi, unahitajika mahakamani, lakini
alishindwa amjibu vipi huyo muendesha mashitaka.
Mara akakumbuka jambo, akamkumbuka nesi….
‘Yes, Nesi, atakuwa kafanya haya yote, ni lazima alifika
akakutana na huyu mtu akamshawishi kama alivyoelekezwa na huyu mshitakiwa,
inawezakana alimpa pesa na kukichukua hicho kifaa, ni lazima atakuwa nacho huyo
nesi, na sizani kama ameweza kumfikishia mshitakiwa,…. ni lazima nimpate huyu nesi
kwa haraka iwezekanavyo, ….’akasema na haraka akaingia kwenye pikipiki lake,
huku akipiga simu ya nesi, ambayo ilikuwa inaita tu, haipokelewi.
Alifika nyumbani kwa huyo nesi, akitarajia kumkuta hapo,
kwani jana yake Inspecta Moto alimpigia simu wakaongea, akitaka kujua kama alipitia kwa huyo fundi kama
alivyoelekezwa;
‘Ndio nilipita tu, nikafika nikakuta ana wateja,
nikasubiri, nikaona napoteza muda, basi sikuona haja ya kusubiria nikaondoka
zangu…..’akasema
‘Atakuwa wapi huyu fundi maana simu yake haipatikani…’akasema
Moto.
‘Akuwa ana wateja wengi, yupo, wewe ukipata mda kesho ,
hata leo nenda utamuona huenda akikuona wewe kwasababu anakufahamu ataachana na
wateja atakusikiliza…’akasema nesi.
‘Basi kama yupo kesho asubuhi nitampiia, una uhakika
hujakichukua hicho kifaa?’ akauliza Moto.
‘Nichukua cha nini,…sina haja nacho…’akasema nesi, na
Moo akamuamini, akijua kesho yake atapiia kwa huyo fundi, kwani askari
waliyemuma alisema alifika nyumbani kwa huyo fundi, hakumkuta, akasubiri karibu
siku nzima, lakini huyo fundi hakuonekana. Na alipoongea na nesi, akapata
ahueni kuwa fundi huyo yupo, huenda alitoka tu, kipindi askari huyo alipofika
hapo, akaweka hali ya kuamini.
Leo anafika kwa huyo fundi, fundi haonekani, ndio akajua
huenda nesi kacheza mchezo, ni lazima nesi atakuwa na hicho kifaa na huenda
anatafuta mwana wa kukifikisha hicho kifaa kwa mshitakiwa.
Inspecta alijua kuwa atamkuta huyo nesi, kwani nesi
alisema siku hiyo ni ya mapumziko kwake, hatakwenda kazini, atakuwepo nyumbani
, hata mahakamani hatafika. Inspecta akafika nyumbani kwa huyo nesi, na
akiangalia muda, umekwenda kweli, alipofika akaambiwa nesi huyo katoka muda
mchache uliopita,kaelekea mahakamani…Inspecta Moto hakupoteza muda, akaendesha
pikipiki yake hadi mahakamani.
Alipofika akajaribu kumpigia nesi, lakini simu ilikuwa
inaita tu haipokelewi, ina maana kaiweka isitoe sauti, kama yupo mahakamani,
yeye moja kwa moja, akaingia mahakamani, na hapo akukutana na yale mabishano na
akasogea kumnong’oneza kitu muendesha mashitaka, na muendesha mashitaka hakukubaliana na hoja hiyo, akasema;
‘Huyu mtu sio yeye keshatoa ushahidi wa DNA, sio yeye
kabisa, inawezekana mkuu wako katoweka, kuna sehem kajificha, fanyeni mpango
atafutwe haraka, tusipoteze muda…’akamwambia Moto.
‘Ndio yeye bwana, hawa wanataka kutuchezea, hebu
akaguliwe begani kama hana jeraha la risasi, ….kama ana jeraha la risasi, ina
maana yeye pia anahusika na mlipuko wa yale mabomu, ..’akasema.
‘Lakini badi haitasaidia, maana ushahidi wa kuwa sio
yeye keshautoa…labda nipoteze muda, ili baadaye kesi ihahisrishwe, tujipange
pya,..ushahidi umekuja nao…?’ akauliza.
‘Ushahidi umepotea fundi haonekani…’akasema Moto.
‘Sasa hapa hakuna kesi,….’akasema Muendesha mashitaka
akiwa kakata tamaa,akamgeukia hakimu
aliyekuwa akiteta na watu wa baraza, akasema;
‘Ndugu muheshimiwa hakimu, huyu mshitakiwa anahusika kwa
yote tuliyomshitakiwa, kuna tatizo la huo utambulishi, hatujui kwa sasa ni
kwanini DNA, imetokezea hivyo, ila huyumtu hata siku ile ya mlipuko wa mabom
alikuwepo, na alionekana na Inspect Moto, wakati bomu linalipuliw akwenye ile
nyumba.
Inspecta Moto alimfyatulia risasi na kumjeruhi begani,
kama anabisha, tuone kama hana jeraha begani..’akaambiwa
‘Bado tunarudi kule kule..je mimi mnanishitaki kama
nani, …..?’ akauliza huyo mshitakiwa.
anayemsengenya mwenzake, ni sawa na kumla nyama huyo
unayemsengenya, tuacha tabia hiyo sio nzuri. ‘Hebu kwanza tuthibitish hilo..’akasema
muendesha mashitaka
‘Muheshimiwa hakimu, hawa watu wanafahamu sheria, lakini
hawataki kuzitumia, ninaweza nikawa na jeraha hilo, lakini sio lazima kuwa
lilitokea hapo..kuna uthibitisho gani kuwa jereha hilo nililipata siku hiyo, na
sio mahali kwingine…’akasema mshitakiwa.
Inspecta Moto akawa anatembeza macho kukagua mle ndani
kama ataweza kumuona nesi, alikagua bila mafanikio, na wakati ameshakata tamaa,
mara kwa pembeni ukutani karibu na mlango,akamuona….
Nesi akiwa kasimama, akionyesha uso wa wasiwasi,
akiangalia mahakama inavyoendelea, na alionekana kama anataka kutoka nje, na
Moto akaanza kutoka kumfuata, huku nyuma muendesha mashitaka akimuita, lakini
hakumsikiliza….
Hakimu akawa anamuangalia huyo mtu kwa mshangao, maana
yeye amafahamu, na siku zote anamfahamu kuwa ni kiongozi wa kitengo maalmu cha
usalama, lakini lao anapinga, na hata uthibitisho wa DNA, umethibitisha hivyo, kuwa
sio yeye, sasa huyo mkuu anayetakiwa
yupo wapi….’akawa anajiuliza.
NB: Samahani kwa kutokuweza kumalizia kisa hiki kwa leo
, nilitaka nisubirishe hadi nikimalizie, lakini nimeona ili siku isiishe bure
niweke sehemu hi muhimu ya mahakamani….swali je huyo mkuu kapotelea wapi, na
huyu mtu ni nani?
WAZO
LA LEO: Dunia sasa imeharibiwa na watu wenye nia mbaya , watu
ambao wanatumia kila nafasi, kuwazalilisha wenzao, ama kwa mitandao, au kwa majungu,
fitina na kuesenganya ikiwa ndicho
kigezo kikubwa. Kusengenya imekuwa hulka ya watu kila wanapukutana, utasikia
muone yule, asikuambie kitu yupo hivi, kafanya hivi, ni mbaya, nk ..na kauli
hizo zinaweza zisiwe za kweli, lakini nia ni kuchafuliana, kuharibiana,
kwasababu ya wivu, choyo na husuda. Kusengenya ni dhambi, mtu
1 comment :
Kazi nzuri mkuu, endeleza kisa usikatishe. ukikatisha utaharibu, kama watu wamechoka kivyao
Post a Comment