Inspecta
akawa sasa akitembea kuelekea kwenye hilo eneo, ilikuwa ni sehemu iliyojengwa
kwa juu kwa aina yake ip kama inaelea hewani, chini imeshikiliwa na nguzo, na
mzunguko wa kitu kama nusu dunia, ni ubunifu wa hali ya juu, ni kama vilr dunia
ipo kwenye muhimili wake, cha ajabu ukiwa chini huwezi kuiona sehemu hiyo.
Inspecta
akiwa na vijana wake wakasogelea hadi sehemu yenye ngazi za kuingilia sehemu
hiyo, hadi kwenye mlango, lakini mlango ulikuwa umefungwa, na hapo Inspecta
akawasiliana na watu kama yule mtu wa mitandao keshaweza kufanya lolote.
‘Ndio
kapewa dawa na yule mzee, inaonekana zimefanya kazi, dawa za huyu mzee kiboko, haliyake
inakwenda vyema, sasa hivi yupo kwenye
komputa akijaribu kuweka mambo sawa, ….’akambiwa
‘Ni
muhimu sana, maana tumefika kwenye mlango, umefungwa, na hatutaki kutumia nguvu
kuvunja huu mlango,nina uhakika mlango huu unafunguliwa kwa mtandao, na hatuna
uhakika kama huyu mtu anatuona au tulivyozima mawasiliano ya mitandao yake atakuwa
hawezi kutuona, …’akasema Moto,
‘Sasa
tufanyeje mkuu..’ wakauliza.
‘Mtu
wa kutusaidia kwa hivi sasa ni huyo mtaalamu wa mitandao,...sisi huku
tunajaribu kufanya utafiti, tukimsubiria yeye, nina uhakika yeye ataweza
kuufungua huo mlango, ila kama kuna simu yoyote itakayojaribikiwa kupigwa kwa
huyu mtu, au yeye kupiga sehemu yoyote mufahamishe..’akasema Moto.
Kulipita
muda kidogo, kila mmoja akijaribu kuangalia jinsi gani ya kuingia humo kwenye
hicho chumba cha aina yake, lakini ilikwa ngumu, mlango ni sehemu moja tu, ni
kila kitu kimetengenezwa kwa chuma,…na huwezi kuona ndani, hata walipojaribu
kutumia darubuni za hali ya juu, hawekuweza kuona kitu.
‘Huu
nu ubunif wa hali yajuu, maana inaonekana hata risasi hazipiti humu…’akasema
Moto
‘Mimi
naona tujaribu kuvunja, kwa risasi, pale kwenye lango, tunaweza kufanya hivyo
mlango ukafunguka….’akasema askari mmojawapo.
‘Hapana,
hiyo inaweza ikaharibu kila kitu, ngoja tuvute subira,….’akasema na mara simu
ya inspecta ikaingiza ujumbe;
‘Jamaa
anasema tayari ameshaingia kwenye anga za dunia yangu, ila amesema kwa kufanya
hivyo ina maana jamaa naye atakuwa sasa anaweza kuona kinachoendelea, je
aendelee…’akaulizwa.
‘Tunachohitaji
kwa hivi sasa ni yeye kuwezesha mlango kufunguka, pili kumzuia huyo jamaa hata
kama ataona kinachoendelea asiweze kufanya lolote je hilo linawezekana?’
akauliza.
‘Anasema,
ameshamzuia huyo jamaa kufanya lolote, kwani yeye ndiye mwenye uwezo wa kuingia
kila mahali, na kuweza kumruhusu mtu kufanya lolote kwenye mtandao wa kundi,
kwahiyo alipoingia tu, akazuia watu wote kuweza kufanya chochote ..yeye tu ndio
anaweza kufanya apendavyo….’akasema.
‘Je
jamaa huko anaweza kuona kwa kiasi gani kinachoendelea?’ akaulizwa.
‘Ataona
ile sehemu ya jengo, watu wanavyoingia na kutoka, lakini haweza kuzungusha
kuona zaidi ya hapo, na hawezzi
kuwasiliana na yoyote yule….’akaambiwa.
‘Kuna
kitu gani kingine alichokigundua ambacho kinaweza kuhatarisha maisha…?’
akaulizwa
‘Kuna
kiashiia cha bomu, ambalo limewekewa muda, anasema bomu hilo walikuwa
wameliweka kimajaribio huwa ikikaribua muda fulani, wanarudidha nyuma, lilikuwa
la majaribio tu, lakini inavyoonekana jamaa yetu huo hapo anataka kulitumia,
alishaliamrisha lije kufyatuka,…ndio anajaribu kutafuta njia ya kuongeza muda,
au ikibidi kulizima kabisa, hiyo ndio inamsumbua kwa hivi sasa….’akaema.
‘Oh,
sasa hiyo ni hatari , ina maana jamaa kazimiria kufanya unyama wa namna hiyo,
hilo bomu likilipuka, litauwa watu wangapi, na uharibifii kiasi gani….ajitahidd
awezavyo, na tunashindwa kuwaarifu watu,
ila ikibidi aseme haraka tuone jinsi gani tutawaokoa watu…..’akasema
‘Amesema
usifanye hivyo, anajua jinsi gani ya kulizuia, ni swala la muda tu…na kwa vile
vile ameshamzuia huyo mwendawazimu kufanya lolote, hakuna hatari itakayotokea,
amesema tumpe muda….’akaambiwa.
‘Je
huyo mtu ana silaha gani nyingine hapo alipo?’ akauliza Moto.
‘Hapo
alipokaa, ni mtambo wenye silaha za kila namna…lakini mtaalamu hapa anasema
ameshazizuia kufanya kazi, lakii hatuwezi kujua yeye mwenyewe anaweza akawa na
silaha nyingine ambazo hazihitaji mtandao,…amejaribu kumkagua hajaziona…..’akasema.
‘Huyu
mtu kwa hivi sasa mwenyewe yupo wapi?’ akaulizwa.
‘Yupo
kwenye kiti chake cha enzi ambacho anazunguka nacho chumba kizima, ni kama
ndege, inakwenda huku na kule, hiyo ndege ndiyo yenye hizo silaha….hutaamini ni
sehemu ndogo kwa nje, lakini ukiingia ndani utaona ukubwa wake, chombo hicho
kinaelea hewani, na akitka kutoka nacho nje, kinatoka kama ndege ya kawaida
ndogo, na kimelengwa kwenda kutua baharini, na kikitua baharini kinageuka kuwa
nyambizi,..kinazama na kutembea majini , chini kwa chini…’akaambiwa.
‘Je
anaweza kufanya hivyo,akitaka?’ akauliza moto.
‘Hawezi
kwa vile kinatumia mtandao, na jamaa keshakizuia, kwa hivi sasa kimesimamishwa
kati kati ya chumba, hakiweza kwenda kokote,…..’akaambiwa.
‘Safi
kabisa….’akasema Moto, na kutulia kidogo, haafu akauliza.
‘Hilo
bomu linasema limebakiza dakika ngapi kulipuka, na madhara yake ni kiasi gani?’
akauliza.
‘Kama
litalipuka madhara yake ni makubwa sana, litaathiri jengo zima,…likilipuka tu, hicho chombo kama ndege kitatoka na kuruka
haraka sana, kwahiyo yeye atasalamika kabisa na hatawezekana kuonekana tena, kwani nyambizi hiyo ina kazi ya hali ya
juu, jamaa anasema ameshakaribia kulidhibiti hilo bomu, tusiwe na wasiwasi…’akaambiwa.
‘Mlango
hajaweza kufungua?’ akauliza moto, akiwa na hamasa ya kuingia ndani
‘Anasema
ukifungua mlango tu, bomu lingeliweza kuongeza mwendo wa kilipuka, ndio maana
hakufanya hivyo kwanza, alichokimbilia kufanya ni kutafuta njia ya kudhibiti
hilo bomu,na kuangalia kama kuna silaha nyingine yoyote anayoweza kuitumia huyo
jamaa, akimaliza hilo ndio awafungulie mlango..’akaambiwa.
‘Na
huyo jamaa mnamuona moja kwa moja hapo mlipo, anafanya nini kwa hivi sasa
anaonekanaje?’ akaulizwa.
‘Jamaa
anaonekana kama roboti, yupo ndani ya hicho kiti chake cha enzi ambao kajivika
vifaa kama roboti, huwezi kumuona sura yake…sasa hivi anajaribu kujinasua
atoke, lakini haiwezekani tena, keshakata tamaa, na kila mara anajaribu kuwasiliana
na mtaalamu hapa, lakini haiwezekani kwa vile keshamzuia….’akasema .
‘Ok,
kazi nzuri, ngoja tumsubirie huyo jamaa amalize kazi yake, ili tuweze kuingia,….’akasema
Moto.
‘Jamaa
anasema anataka amumalize humo ndani ya chombo chake kwani alimtesa sana, na
yeye ana kisasi naye, tumejaribu kumshauri, na kakubaliana na sisi….’akasema
‘Mwambie
asije akafanya hivyo, huyo mtu anatakiwa afikishwe mahakamani na haki itendeke,
akimuua, tutakuwa hatujafanya la maana, maana kuna mengi a kufahamu , huyu mtu
ni nani, ni kweli ni yule mkuu wetu wa kazi,…’akasema Moto.
‘Ndiye
huyo huyo…..unahis ni nani mwingine, alikuwa akituchezea akili tu, sijui
ilikuwaje akabadilika hivyo, nahisi alipokutana na huyo mumiliki wa hiyo miradi
..akashawishika, na huenda, walikubaliana kuwa yeye awe mrithi wake, au wana
udugu fulani….’akasema mwenzake.
‘Hiyo
yawezekana, lakini mimi nina hisi anyingine, …na hilo tutalipaat zaidi kwenye
hichi kifaa chake anachokitafuta,….’akasema Moto.
‘Kifaa
gani hicho?’ akauliza mwenzake.
‘Kuna
kifaa cha komputa, inavyoonekana humo kuna siri kbwa sana, ambayo hakutaka
ijulikane..’akasema Moto.
‘Oh,
najua nilishasahau kuwasiliana na huyo askari niliyemtuma, kwani kilikuw ani
kifaa gani, ?’ akauliza mwenzake.
‘Hakikisha
huyo askari anakipata mapema, iwezekanavyo kabls ahuyo nesi hajamfikia huyo
jamaa, nilijua ameshakichukua ndio maana nikamwambia huyo nesi, afanye kama
alivyoaizwa, sasa unaongea kitu gani, msije mkaharibu utaratibu…’akasema moto
akijaribu kumpigia huyo jamaa aliyempa hicho kifaa akifanyie kazi, lakini simu
yake ikawa haipatikani.
‘Kwani
huyo nesi ni nani wake?’ akauliza mwenzake
‘Kwa
hivi sasa ndiye mtu aliyebakia wa kumsaidia, walikuwa na mahusiano, urafiki wa
siri, lakini kama umjuavyo jamaa huyu wetu hana rafiki wa kudumu, ukawa hana
faida kwake, anakumaliza, umeshampigia huyo askari simu….?’akasema Moto na
kuuliza
‘Ndio
anasema sasa hivi yupo hapo kwenye eneo la nyumba ya huyo jamaa, na jamaa
anaongea na mteja ndani
‘Muulize
ni mteja gani?’ akauliza.
‘Oh
simu yake haipatikani tena….’akasema mwenzangu
‘Ghoosh,….hebu
nipe namba yake..’akasema Moto
‘Una
uhakika huyo nesi hajafika sa hizi kwa huyo jamaa’ akauliza mwenzake.
‘Alisema
anakwenda nymbani kwake kwanza, ….’akasema Moto akijaribu kuwasiliana na huyo
askari, na alipompata akamuliza
‘Upo
wapi?’ akamuliza
‘Nipo
kwa huyu mtaalamu wa komputa…’akasema
‘Umeshaongea
naye?’ akaulizwa
‘Bado
….namgongea hafungui mlango, naona kama anaongea na mtu ndani….’akasema
‘Ni
mtu gani huyo anayeongea naye?’ akaulizwa
‘NI
mwanadada….’akasema
‘Hakikisha
huyo mwanadada hakipati hicho kifaa, ….lishaongea na huyo fundi kabla kwenye simu?’ akamuliza
‘Ndio
nilimambia kama ulivyoniagiza
‘Akasemaje?’
akaulizwa
‘Tutaongea
ukija….alisema hivyo tu,….’akaambiwa
‘Nampigia
hapatikani,….gonga kwa nguvu, ikibidi ungua mwambie polisi.ni muhimu sana….’akasema
Moto, na mara simu yake nyingine ikawa inaita akaangalia kaona hakuna namba,
akaipokea, na sauti ikasema;
‘Moto,
welcome to my world, nakusubiri kwa hamu…..’sauti ya kujirudia ikasikika
masikioni kwake, na mara ule mlango wa kile chumba ukafunguka
*********
Wakati hayo yakiendelea, nesi alifanya kama alivyoagizwa
na mtu wake, akapitia kwa mhasibu, akpewa pesa nyingi tu zikiwa ndani ya briefcase, hakujua ni kiasi gani, na
haraka akaelekea sehemu aliyoagizwa, kichwani alikuwa anashindwa kumkatalia mtu
wake, lakini hapo hapo, akili nyingine ilishamuingia, akawaza kufanya jambo
lenye manufaa mbeleni.
‘Huyu mtu sasa hivi watamkamata, wakimkamata ina maana
na mimi nitakuwa mshukiwa, kwanini nisikipate hicho kifaa, nikakitumia kama
silaha, nikatajirika na mimi zaidi, nikapata angalai moja ya kumi ya huu
utajiri wa huyu jamaa, hata akinipa hisa kidogo nikawa sina shida ya maisha, ,…..’akasema
‘Mhh, nikikipata hicho kifaa, nitamwambia huyo mtu
wangu, anipe pesa nyingi, nyumba keshanijengea, lakini nahitaji pesa zaidi
nikamilishe nyumba ya huko kijijini, nifungue duka kubwa la vifaa vya jumla,
nifungue na duka la madawa, niachane na hii kazi ya kuajiriwa….nitakitumia kwa
malengo ya kujinufaisha, ..’akawa anawaza
‘Hapo hapo akakmbuka maswala ya polisi, akasema kimoyo
moyo, ‘Hawa polisi wakikihitajia,mmmh…..sijiu, kwanza polisi watanipa, nini, hawana
pesa….nitawaambia nimeshakiharibu,au nitatoa nakala ya kuwadanganyia….’akasema
na muda huo alishafika kwenye nyumba aliyoelekezwa, akalisogeza gari lake
sehemu salama, akatoka na ile briefcase.
‘Hakuna vibaka kweli huku….’akasema lakini kwa hali
ilivyo pale hakuna mtu anayeweza kumvamia, kuna watu wengi na mishughuliko,
akaondoa wasiwasi.
Akagonga mlango, na mlango ukafunguliwa na jamaa mmoja
akiwa kifua wazi, ni kama alikuwa akipika au alikuwa kwenye kazi ya kumtoa
jasho akawa kasimama kati kati ya mlango, akasema;
‘Oh, kuna joto kweli……..’akasema
‘Wewe ndiye mtaalamu wa komputa?’ akauliza nesi
akimkagua mtu mwenyewe, kwani alikuwa haelekei kabisa.
‘Haswa…na wewe ni nani na unataka nini kwangu, una
tatizo la komputa yako, au unahitaji picha za urembo, nikikupiga picha wewe,
nikaweka kwenye mtandao utakuwa tajiri, wewe ni mrembo sana, umbo lako linavutia,
ulivyo hapo wewe ni pesa…unalijua hilo, karibu tufanye dili ya pesa, halafu utanikatia
kidogo…unasemaje, ?’ akaulizwa
‘Hapana…sijafika hapa kwa hayo, sina shida ya pesa, pesa
ninazo za kutosha,..ila kuna tajiri mmoja, ana pesa za kumwaga, hana shida ya
pesa, pesa kwake ni kitu kidogo sasa kanituma kwako,…’akasema mdada, na yule
jamaa kusikia neno pesa, tajiri… akaonekana kujilamba mdomo.
‘Pesa,..pesa mmmh,, tajiriieeh, ana pesa, mmh, hayo ndio
maneno nayataka, lakini pesa anazo kiasi gani, maana pesa thamani yake ni wingi
au sio, kwanza anataka nini kwangu?’ akauliza huyo jamaa akianza kujenga matumizi
hewani, akikumbuka kuwa muda mchache uliopita alikuwa akigombana na
mwenyenyumba aliyekuja kudai pesa yake ya pango, hajalipa mwezi wa pili sasa.
‘Ni kitu kidogo tu, ni kifaa ambacho unacho wewe,….sasa ni wakati wako wa kuinuka,
uwe na uwezo wa kuanzisha kampuni yako mwenyewe, uwe na nyumba yako mwenyewe,
huyo jamaa ni tajiri sana, atakupa pesa nyingi tu, kwanza ukimpa hicho kifaa,
kifaa chenyewe hakina thamani hiyo, lakini ni cha kwake, kilipotea, amesikia
unacho wewe….’akasema Nesi
‘Mhh, kifaa, kifaa gani hicho, na huyo mtu ni nani..hapana
nahisi umepotea, mimi sijawahi kuokota kifaa…kifaa gani hicho?’ akauliza huyo
jamaa akijaribu kuwaza ni kifaa gani hicho cha kuhitajiwa kwa pesa nyingi.
‘Kumbuka kuwa huyo ni mtu ni tajiri sana…na matajiri
huona mbali sana, unafikiri kakonaje kuwa una hicho kifaa, ..’akasema nesi,
wakiwa wameshaingia ndani, kulikuwa ni chumba chenye kitanda, feni ndogo, vifaa
vingi vya komputa vilikuwa mezani, …joto lilikuwa kali kweli, na nesi alitamani
atoke humo ndani haraka, akasema;
‘Unaona hizi pesa hapa, zote ni zako, lakini anachohitajia
ni hicho kifaaa…’akasema nesi na kufungua briefcase
iliyojazwa manoti,..na jamaa alipoona yale manoti, akajilamba, na macho
yakamtoka pima kwa tamaa, hakuamini
‘Zote ni zangu, mimi sina kifaa chenye thamani kubwa
kiasi hicho, sema ni kifaa gani, mimi nitakupa, kwa pesa kama hiyo, ninaweza kukupa
vitu vyote nilivyo navyo humu, havifikii thamani ya hiyo pesa, ni kifaa gani
hicho?’ akauliza akiwa anazikagua zile pesa na kwa mahesabu ya haraka, zinaweza
kufikia hata zaidi ya milioni hamsini….zinaonekana zimepangwa kwa milioni milioni…
‘Kifaa alichokupa jamaa mmoja anayeitwa Moto….’akaambiwa
‘Oooh, nini….oh, Moto,..sasa huo mtihani’ akasema na kukaa kwenye kiti akionyesha kuwaza na
akilini akawa akiwaza…..`lakini tangu huyu Moto afike hapa,hajarudi tena, yeye kazi yake kupiga simu, kuulizia nimfikia wapi, yeye anafikiri mimi nitaishije, ....'
Na hapo hapo akakumbuka
kuna mtu aliyesema ni askari, aliyedai kuwa katumwa na Moto, kasema atakuja kukichkua
hicho kifaa, akamuahidi kuwa kama kazi imeisha atakuja na chochote, chochote inaweza ikawa elifu kumi au hata thelethini,sasa hiyo itamsaidia nini, yeye atabakia na umasikini wake, na wakati kuna mtu kaja na mamilioni,
kwanini aikate hii bahati…...' akawa anawaza
Yule jamaa akageuka kuiangalia bahasha, ambayo
alishakiweka hicho kifaa ndani ya hiyo bahasha ili akija huyo askari amkabidhi,..yeye alipohakikisha kimefunguka, akawa hana kazi nacho, hakutaka hata kuangalia ndani kuna nini,
akakichuka na kuweka kwenye bahasha, na muda huo ndio alikuja mwenye nyumba wakaanza kuzozana, ikamfanya asahau kila kitu.
‘Kumbe kifaa chenyewe ni mali…ningelijua nikatoa hata nakala moja au nika-save kwenye kumbukumbu zangu….’akawa
anajilaumu kichwani
‘Nitakupa hicho kifaa..lakini….’akasema na kusimama na huyo nesi
akadakia, kwa kusema;
‘Nionyeshe hicho kifaa kwanza nihakikishe kuwa ni chenyewe, na
pesa hizi ni zako….’akasema nesi akilifunga lile briefcase na kulishika mkononi, na mara mlango ukagongwa kwa nguvu,
na nesi akasema;
‘Ni nani huyo….?’ Akauliza kwa mashaka
‘Hao ni wateja….usiwe na wasiwasi nao nimeshawazoea acha wagonge wakichoka wataondoka….’akasema akisogelea ile
bahasha yenye kile kifaa, tayari kumkabidhi huyo mdada, na moyoni, akipanga
kuwa huyo mdada akitoka tu, na yeye anatoka kwa mlango huo huo, acha huyo anayegonga agonge mpaka kesho, yeye akitoka tu anatafuta bajaji, anaondoka eneo hilo na
kutafuta sehemu nyingine ya kuishi, kuanza maisha mapya akiwa tajiri.
‘Huo mlango wa nyuma mbona haufunguki, hebu nifungulie nitoke huko,
kipo wapi hicho kifaa…nataka niondoke…?’ akauliza nesi,na wakati huo mlango
ukawa unagongwa kwa nguvu, na yule jamaa akawa ameshatoka kile kifaa
kumthibitishia huyo nesi.
'Ndio hiki, hii ni external hard drive, ina nguvu sana na huhifadhi vitu vingi sana,ilikuwa wamei-lock, nikafungua kwahiyo sasa unaweza kufungua bila shida, ...mimi sijiu kuna nini ndani yake.....'akasema
Nesi hakuwa na uhakika nacho, maana hajawahi kukiona kabla kama ndio hicho au huyu jamaa katumia mbinu, lakini akaamini kuwa ndio
chenyewe, akasema;
‘Kiweke humo humo kwenye bahasha,..nipe niondoke,..kama utaleta ujanja nakuapia haitapita sikuu ya leo utakuwa marehem....’akasema
na jamaa akasogezewa hilo briefcase kwa sasa ni mali yake, akiwa haamini, macho yake
yakiwa yanaiangala ile briefcase na tamaa ya matumizi ikawa imeshamteka moyoni.
‘Usiwe na wasiwasi kabisa, hiki ndicho alichonipa Moto,....kama huyo tajiri ndicho anachohitajia ndio chenyewe, labda kiwe ni kiti kingine...'akasema
'Sawa mimi nimekuamini...'akasema nesi akikipokea, na kukiweka vyema mkononi
'Sasa wewe tokea mlango
huo, na hakikisha hauonekani, mimi mwenyewe nitatokea hapo hapo, sihitaji
wateja tena….’akasema na mlango sasa ukawa unagongwa karibu ya kuvunjika, na
sauti ikasema
‘Mimi ni polisi fungua mlango haraka…..’ na yule nesi
akawa ameshafungua mlango, na kuanza kutoka nje, na jamaa naye akawa anavaa
flana yake, tayari kutoka na kutokomoe mitaani.
WAZO
LA LEO: Shida zinaweza kumfanya mtu akawa mtumwa,akauza hata
utu wake, hata kuzalilika, yote hayo ni mitihani ya kimaisha. Ndugu ukikabiliwa
na shida, matatizo sikate tamaa, na usikubali kuuza utu wako, ukarubuniwa
kwenye mambo yasiyofaa, kama ya uhalifu, au tabia chafu, kumbuka utajiri, pesa,
vyote ni vya kupita tu, lakini utu wako, na heshima yako ina thamani zaidi ya
hivyo vitu.
mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment