‘Huyu mzee anataka nionane naye kwa
haraka,mimi na yeye tulishamalizana, na sitaki tena kazi zake...’akasema mdada na mpelelezi
akamuangalia kwa mashaka na kumuuliza
‘Ina
maana kumbe hayo unayoyafanya ni kwa ajili ya huyo mzee?’ akauliza mpelelezi akimkazia jicho
mdada, na mdada akacheka kwa dharau na kusema;
‘Sikiliza
wewe mtu, tusifuatane fuatane, mimi
siwezi kumfanyia kazi mtu kama yule, hivi unanionaje mimi, kuwa nina shida sana
ya pesa au...atanipa nini yule mzee...nilikataa aliponipa kazi ndogo kwa ajili
kumchunguza huyu mtu wako...’akasema
akinionyeshea mimi na mimi nikabakia kimya, akaendelea kuongea
‘Eti
alitaka kuhakikisha kuwa kweli huyu mtu anaweza kumuoa binti yake, na kama kuna
mambo mabaya anayoyafanya, nimuarifu kwani keshamharibu binti yake na
wamewekeana mikataba kuwa atamuoa binti yake..ni hivyo...’akasema mdada, na kabla mpelelezi
hajasema neno akendelea kuongea;
‘Na,
kwa vile ni nilishamuona mhasibu ni mtu asiye na msimamo, nikaona nimuweke
sawa, ...unaona jambo moja likazaa jingine, nimegundua kuwa anaweza kuishi na
mimi,..okey, hata kama kamzalisha huyo binti yake, lakini hiyo ilikuwa Ini
bahati mbaya, muulize huyu mtu kama hajazimia kwangu, ananihitaji mimi kama
ninavyomuhitaji yeye....’akasema
‘Sasa
huyo mzee, kaligundua hilo, akawaka, nimekutuma kazi, wewe unanigeuka,
unamuibia binti yangu mchumba wake,..nikamuambia, katika makubaliano yetu,
hatukuwahi kugusia hilo kuwa mimi na huyu mtu tusije kupendana, imetokea
tumependana kiukweli, sasa tufanyeje...’akaendelea kusema
‘Mdada...’nikawa nataka kusema lakini
akaniashiria ninyamaze, na mpelelezi akauliza
‘Okey,
sasa unataka kuonana na huyo mzee kwa ajili gani?’ akauliza mpelelezi
‘Binti
yake alinitumia ujumbe wa vitisho, kuwa nisipoachana na mchumba wake, atanifanyia
kitu mbaya, na waakti huo huo walishakaa kikao na kukatisha uchumba wake na
mhasibu, kwahiyo uchumba wao haupo tena....’akasema
‘Sasa
tuwaelewe vipi,huo ujumbe wao una maana gani,unajuawanielewe sana, hata wewe
unielewe hivyo,kuwa sipendi kutishwa, kwanza kuhusu hiyo familia, mimi...nataka
hilo swala la uchumba wao na mhasibu waliweke wazi, kama bado upo tuelewe, na
mhasibu atamke wazi ni mimi au ni huyo mshamba wao...’akasema
‘Na
pili waachane na vitisho vyao kwani mimi sio mtu wa kutishika,hata hivyo mzee
huyo namuheshimu sana nisingelipenda aje kuniona mtu mbaya kuna lolote jingine
aniambie, vinginevyo, watanijua..’akasema
mdada
‘Lakini
na wewe mdada, huoni kama unaingilia uchumba wa watu, kwanini usitafute mchumba
wao mwingine, kwani ni lazima huyu mhasibu, wanaume wapo wengi, au una ajenda
gani ya siri na mhasibu?’
akauliza na mdada akageuka kumuangalia mhasibu, huku akitabasamu kwa dharau na
akasema.
‘Hayo
hayakuhusuau na hiyo ni mojawapo ya kazi zako, tuambie tujue, kama upelelezi
wako ni pamoja na maswala ya mahusiano na ndoa za watu....’akasemana mpelelezi akatabasamu, na
mdada akiwa kakunja uso akasema;
‘Hata
hivyo, nina imani haya yatakwisha tu, ila ni lazima niionyeshe hiyo familia
kuwa mimi sio mtu wa mchezo,mimi sitishiki na ndumba au kwa lolote lile,..,
anyway, kwa vile nilishapanga nionane naye, haina shida, naona kila kitu
kimejipa kama nitakavyo...’akasema
mdada, na kuangalia saa yake huku akiwa ameshaweka mkoba wake mkononi
Mpelelezi,
naye akaangalia saa yake, na hakuonyesha dalili ya kutaka kuondoka, kwa muda
huo alikuwa akimtizama mdada, na mdada alimpomtupia jicho mpelelezi na kumuona
anamuangalia yeye, kwa haraka,akatikisha kichwa kama kusikitika akasema;
‘Natumai
tumemalizana...sitaki tena kufuatana fuatana...’akasema halafu akageuka kuniangalia
mimi, na kusema;
‘Na
wewe mtu wewe, nitakuja hotelini kwako nina mazungumzo na wewe, na wakati
naongea na wewe sitaki usumbufu na huyu mtu wako, it will be strictly business, between me and you,....umenielewa wewe mtu....’akasema akinisogelea na aliponikaribia
akawa kama ananibusu shavuni huku akininong’onezea
akisema;
‘Ole
wako urope ovyo, hakuna zaidi ya hayo niliyosema...’akasema na akawa kama ananibusu
shavuni
Mpelelezi
akawa anatuangalia huku akitabasamu, nahisi alijua ni mambo ya wapendanao,
halafu mdada akamgeukia mpelelezi na kusema;
‘Kama
una maongezi na huyu mtu mumalizane kabisa, sitaki tena nikiongea na huyu mtu
wangu wewe kuja kupiga chabo, unapenda sana kuniingilia mambo yangu...’akasema huku akitabasamu kwa dharau na
mpelelezi akawa anatabasamu tu
‘Usijali,
nitajiathidi nifanye hivyo, ilimradi na wewe uwe mkweli...lakini huyo ni mtu wa
watu, ukumbuke hilo’akasema
mpelelezi
‘Nani
kasema ni mtu wa watu, huyu mtu , ni mtu
wangu kwa ndani na nje...sasa semeni mpendavyo,mmh, najua mtasema oooh, mdada
kaiba mchumba wa mtu, hivi mapenzi yanalazimishwa jamani, kama hapendwi mtu hapendwi
tu ....’akasema
mdada halafu akanigeukia na kuniminyia jicho moja, na kugeuka kuanza kuondoka,
na mimi nikasema.
‘Mdada
hivi unavyofanya sio sahihi...’
nikasema na yeye akaniashiria na mkono kuwa ninyamaze, halafu akabenua mdomo wa
dharau na kusema;
‘You
will see...’akaanza
kundoka bila kuangalia tena nyuma
Tuendee na kisa chetu...
Mdada alitangulia kuondoka, baada ya kunipa vipande
vyangu kuwa atahitaji kuongea na mimi hotelini kwangu, na alipoondoka tukabakia
mimi na mpelelezi, mpelelezi akaniuliza;
‘Wewe
unahisi mdada anafanya hivyo kwa ajili ya nani, sidhani hayo anayoyafanya
anayafanya kwa masilahi yake binafsi au kwa ajili ya huyo mzee, huyo mzee,
hawezi kumpa kazi zake huyu binti, maana huyu binti anafahamika, haaminiki,
unahisi anamfanyia nani hiyo kazi anayoifanya?’ akaniuliza
‘Kiukweli
mimi simuelewi kabisa mdada, huwa hatabiriki, na mipango yake mingi ipo hivyo,sijui
anachofanya ni nini, na kwa masilahi ya nani, nimuonavyo mimi ni mambo yake ya
kufanikisha kazi zake, kama anataka biashara, au kutoa gari bandarini, anaweza
kumvaa yoyote ili kuhakikisha anafanikiwa,lakini alivyo, hawezi kukuambia kitu,
na ujue akikuambia hicho kitu atakuwa keshajipanga na huwezi kumpinga tena...’nikasema
‘Mhasibu
ni kwanini hamsemi ukweli kuhusu huyo mtu aliyekuwa na ndevu, mimi nimegundua
kuwa huyo mtu ni wewe, ni wewe uliyejibandika hizo ndevu, lakini nashindwa
kujua ni kwa madhumuni gani,....’akasema
‘Kama
alivyokuambia mdada, mtu kama huyu hayupo...’nikasema
‘Kama
mtu kama huyo hayupo basi ni wewe, haya niambie mlifanya hivyo kwa makusudioa
gani?’
akaniuliza na mimi nikabakia kimiya nikijiuliza kichwani sijui nimuambie ukweli
yaishe tu, lakini kwa hali nyingine nikakumbuka onyo la mdada akinikanya kuwa
hilo jambo liwe kati yangu mimi nay eye tu, nikasema;
‘Mpelelezi,
nikuambie kitu, mimi sioni kwanini upoteze nguvu zako nyingi kumtafuta mtu kama
huyo, kiufupi huy mtu hayupo, kama alivyokuambia mdada, na hawezi kuhusika na
hayo ,mauaji...’nikasema
‘Kwa
kauli yako hiyo mimi nahitimisha hapo kuwa huyo mtu alikuwa ni wewe, na
mlifanya hivyo na mdada, ili wewe usijulikane na marehemu, labda kwa usalama
wako, kwa vile wewe ulitumwa kuchukua huo mzigo...’akasema mpelelezi
na mimi nikakaa kimiya.
‘Kwa
kukaa kwako kimiya natumai tumekubaliana na hilo, ila kwa tahadhari, polisi
bado wanamtafuta huyo mtu, kwani kwa jinsi walimvyomuhoji huyo mlinzi, wanahisi
kuna jambo jingine limejificha wenye hayo mauji...’akasema mpelelezi
‘Jambo
gani?’
nikauliza
‘Kwanini
huyu mtu awepo na kutowekabila hata kuonekana, na wewe ulikuwa na nafasi zaidi
ya kumuona, kama hakuna mlango mwingine wa nyuma, na kwanini kazi aliyofanya
huyo mtu iwe sawasawa na kaziuliyofanya wewe...’akasema mpelelezi
‘Una
maana gani kusema kazi aliyofanya yeye, ni sawa na kazi niliyofanya mimi?’ nikamuuliza
‘Huyo
mtu aliongea na mlinzi, na mlinzi akampa taarifa ya huyo mgeni, yaani marehemu
na maelezo hayo hayo ndiyo uliyotupaambia sisi kuwa uliongea na mlinzi, hapo
umejinasa na polisi wanawatizama nyie wawili, kama mna ajenda fulani
inayohusiana na hayo mauaji...’akasema
‘Polisi
wanaweza kusema lolote, je wewe unahisi nini kuhusu hayo yote...?’ nikamuuliza
‘Lolote linawezekana
kwa sasa, hasa ukiwa na watu kama hao, na mtu kama mdada, mdada ni mjanja sana...lakini
nitakuja kugundua mwenyewe ni kitu gani kipo nyuma ya haya yote, nilichotaka
kukifahamu zaidi ni mazingira ya ndani ..ni nini kilitokea kabla na baada ya
hayo mauji, kipindi hicho mpo humo ndani....’akasema na kuangalia saa yake.
‘Natumai
yote umeyasikia, sizani kama unahitaji maelezo zaidi...’nikasema
‘Nikuulize
kitu, wakati upo chini, ulisema mdada, alimtupa marehemu kama kagunia kutoka
chumbani hadi bchumba cha maongezi, na halikadhalika wewe, ukaangukia karibu na marehemu, marehemu kwa
muda huo alikuwa akijaribu kujizoa zoa, kuifuatilia ile bastola, je kwa muda
huo mdada alikuwa katika hali gani?’ akaniuliza na mimi nikatulia kama nawaza
jinis ilivyokuwa
‘Nilimuona
mdada kama anayumba yumba hivi....sio kama alivyokuwa ndani, na wakati huo,
marehemu alikuwa karibu kuishika ile bastola.....na pale nikajiona napambana na maadui wawili, lakini pia nikiwa
na lengo la kumsaidia mdada, japokuwa kwa muda huo nilikuwa namuogopa, kwani marehemu
alikuwa akiiendea ile bastola, na akiishika atamua mdada, na mimi pia...’nikasema
‘Kwa
maelezo ya dakitari, na hata wanandugu waliowahi kumshughulikia mdada, ni kuwa
ile hali ya kubadilika kwa mdada, ikianza kuondoka, ili arejee katika hali yake
ya kawaida, huwa anaishiwa nguvu, kama alikuwa amesimama ni lazima
atadondoka....’akasema
mpelelezi na mimi nikawa nawazia siku ile ilivyokuwa, na kuanza kuhisi jambo
ambalo sikuweza kuliweka vyema kichwani.
‘Kama
ni hivyo basi,marehemu alikuwa na uwezo wa kuichukua ile bastola na kufanya
lolote, kwanini ...hapo sielewi,..ina maana hapo mdada, alikuwa hana nguvu tena
kama awali,kuyumba kwake kulionyesha kuwa ile hali ya ushetani ilishakwisha, au
sio, ...’nikawa
naongea
‘Hivyo
basi yeye asingeliweza kuichukua ile bastola na kumuua marehemu, atakuwa
alidondoka chini, ina maana basi hapo ni lazima kulikuwa na mtu mwingine na
huyi mtu ni lazima atakuwa ni huyo mlinzi ..huyo mtu mtu mwingine ndiye
aliyemaliza kazi, ni nani huyo...’nikasema.
‘Yawezekana
pia asiwe mlinzi, ndio maana mpaka sasa polisi wanaendelea kumtafuta huyo mtu
mwenye ndevu, ...kama mlinzi amekataa kata kata kuwa hakuwahi kuishika hiyo
bastola, na anadai kuwa mlio wa bastola aliusikia akiwa ndani,..chumbani mwa
mdada, akitafuta kitu alichotumwa na bosi wake....’akasema
‘Mhh,
hapo nashindwa kuelewa, kwanini polisi wasimlazimishe huyo mlinzi akamkataja
huyo bosi wake,...huoni hapo kuna jambo,..., huyo bosi wake ni nani?’ nikauliza
‘Inavyoonekana
huyo bosi wake ni mtu ambaye hatakiwi kujulikana, huenda ni kiusalama, nahii inadhihirisha kuwa, kifo cha
mtoza ushuru, kinaweza kuwa mchezo wa kuigiza, na haya yanayoendelea sasa ni
kupoteza muda tu, kuna wakubwa wa ndani ya idara ya usalama wanaweza wakawa
wanalifahamu hilo .....lakini hayo mimi nitayagundua tu...’akasema mpelelezi
‘Lakini
wewe ni mmojawapo, wewe ni mtu wa uslama au sio, kwanini usilijue hilo?’ nikamuuliza
‘Mambo
mengine ni ya kiujasusi zaidi, yanaweza kufanyika kwa siri kubwa, na wanaoweza
kufahamu wakawa watu wachache na wanaoaminika...hayo ni mambo ya
kintelejensia...huwezi kuyafahamu...’akasema
‘Sasa
kwanini kupoteza muda, gharama, na hamuoni kuwa mnaua watu bila kuhukumiwa, na hiyo
sio haki..’nikasema
‘Hakuna
aliyesema huyo mtu kauliwa na watu wa usalama,...na watu wa usalama hawawezi kulifanya
jambo hilo kihivyo...wana namna zao nyingi za kummaliza mtu kama wanamuona ni
tishia, kwa hilo, lilivyofanyika, sio sahihi, limefanyia kisivyo, nahisi sio kusudio
la watu wa usalama kama ni wao, kuna watu wamelifanya ionekane hivyo,nahisi
kuna jambo jingine nyuma ya pazia....’akasema
‘Wewe
unaweza kuhisi ni jambo gani hilo nyuma ya pazia...?’ nikamuuliza
‘Kuna
vitu vichache navihitaji kuvifahamu, nikiongea na mlinzi nitavijua, na pili
nyie wawili mkiniambia ukweli uliobakia, nitaweza kufikia tamati ya uchunguzi
wangu, ila mpaka sasa nimegundua jambo, kuwa mauaji haya yamepangwa yatoee kwa
mdada, kwa vile kulishaonekama kuwa kuna kutokuaminiana kati ya mdada na mtoza
ushuru, na wewe wakakutumia kama chambo....’akasema
‘Mimi
hapo sielewi unajua mpaka sasa nawaza hilo ulilosema kuwa mdada,akianza
kuondokewa na hiyo hali, anapoteza nguvu, na mimi nakumbuka kabisa alishaanza
kuyumba yumba, kwahiyo hakuwa na uwezo wa kufanya lolote, unaona hapo sasa ni
lazima awe ni huyo mlinzi aliyefanya hayo mauaji ni kweli kabisa hapo, ...’nikasema na
mpelelezi akasema;
‘Huyu
mlinzi aliingia kwa kupitia dirishani, na ndiye aliyevunja kabati la mdada,
akitafuta nyaraka muhimu, ni nyaraka gani hizi,....na kipindi hicho wewe na
wenzako mpo katika harakati za mapambano,...huyu mlinzi aliwezaje, kufanya hiyo
kazi ya kuvunja hilo kabati, na bado awe na muda wa kutoka na kuwagonga na
nyundo, na hata kumua mtoza ushuru....ukipiga mahesabu ya muda hapo, hautoshi,
naona kuna msaada wa mtu mwingine hapo...’akasema
‘Mhh,
atakuwa alipitia wapi, ukumbuke mimi nilikuwepo, na nikatoka nje, kukimbia, na
wakati natoka huku nyuma ndio nikasikia mlio wa risasi, huyu mtu atakuwa kapitia
wapi,...’nikasema
‘Nilichunguza
mlalo wa marehemu, kama hakuhangaika wakati anakata roho, basi, mpigaji wa hiyo
bastola, atakuwa upande wa...mmmh, yes, sasa nimegundua jambo, ..’akasema mpelelezi
akiinua ngumi ya kuashiria ushindi
‘Umegundua
nini mpelelezi...?’
nikamuuliza na mimi nikiwa na hamasa
‘Nitakuambia
nilikithibitisha hilo, ...ngoja niwahi sehemu, wewe tangulia kwa mzee, nitawakuta
huko, ni lazima kazi hii niifanye leo hii, hii maana kesho ndio mwisho wake,
faili lake linafungwa,...’akasema
na mimi nikataka kumuuliza lakini yeye akaendelea kuongea
‘Lakini
kuna kitu muhimu, nataka uniambie ukweli, maana nina mashaka nacho bado, kuhusu
wewe kujivika ndevu, nina uhakika ni wewe ulifanya hivyo , ni kwanini mlifanya
hivyo....’akasema
akitaka kuondoka,
‘Lakini
mimi sijafanya hivyo, na ukisema una uhakika una maana gani?’ nikamuuliza, na
mara akatoa mfuko wa plastiki na ndani mkoba wake na unionyesha ndani ya kile
kifuko cha plastiki kulikuwa na ndevu za babdia...akanionyesha na kusema;
‘Ushahidi
huu hapa....’akasema
na kabla sijasema kitu,akaondoka kwa haraka
NB: Mpelelezi kagundua nini, mzee anawahitaji hawa watu
kwa jambo gani
WAZO
LA LEO:Tunaposikia maneno, tetesi, uvumi, au kupewa taarifa
kutoka kwa mtu mwingine, tusikimbilie kuziamini kwanza, ni vyema tukajenga
tabia ya kuzihakiki hizo taarifa, au tetesi hizo, kabla ya kuchukua maamuzi yoyote yale.
Dunia sasa hivi imegubikwa na propaganda, na propaganda
nyingine zina malengo mabaya ya kuchonganisha na kuleta uhasama katika jamii kwa
masilahi binafsi, watu hao wanaochchea hizo propaganda potofu,hawajali maisha
ya watu, hawajli athari za hizo propaganda, ilimradi wao wananeemeka. Tuwe
makini .
Ni mimi:
emu-three
No comments :
Post a Comment